SORRY MADAM (25)

0
SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO
ILIPOISHIA...
Salome kapiga hatua hadi sehemu niliyo kaa na nikanyanyuka taratibu na kufungua waleti na kutoa noti mbili za elfu kumi na kumpa Salome
“Nenda zako shule na sihitaji nikuone hapa”
“Wewe utakuja?”
“Hilo halikuhusu wewe nenda zako”

NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU

SASA ENDELEA...
Salome akaondoka huku akiangalia angalia nyuma akapanda bajaji na kuondoka,Sikuwa na hata hamu ya kula nikarudi ndani ya hospitali na kukuta manesi wakisukuma kitanda kutoka katika chumba alicho lazwa Sheila.Nikakimbia na kuwapata na kumkuta Sheila akiwa amewekwewa mashine ya gesi huku macho yake ameyafumba na uzuri wake ukazidi kuongezeka.Wakamuingiza kwenye moja ya chumba na kilicho tulia huku na mimi nikiwa ninafwatia kwa nyuma kisha wakamuweka juu ya kitanda tulicho kikuta humo na kumzifunga mashine za upumuliaji vizuri

“Nesi atapona kweli mke wangu?”
“Usijali kaka kwa maana hapa risasi imetolewa na uzuri zaidi risasi haikumdhuru kitu chochote ndani ya mwili wake”
“Sasa nesi unataka kuniambia hadi kesho atakuwa ameshapona?”
“Kaka nakuomba uwe mvumilivu na utulie kutokana mgonjwa wako hali yake ni nzuri hapo amelala kutokana na sindano ya nusu kaputi aliyo chomwa kwa ajili ya kufanyiwa oparesheni.Cha msingi nikuendelea kumuombea kwa Mungu”
“Sawa nesi”
“Ila uanatakiwa usipige kelele na kama una simu yako iweke silence ili isije ikamsumbua mgonjwa”
“Sawa nesi…..Naruhusiwa kulala humu humu?”
“Hapana kutokana hichi chumba ni chawagonjwa mahututi ila tunakuomba utoke nje kuna mavazi malumu ya kuvaa ili uweze kuingia humu ndani”

Tukatoka na manesi hao na tukaingia kwenye moja ya chumba wakanivalisha nguo maalumu amabazo nimezivaa juu ya nguo zagu kisha nikarudi ndani ya chumba alicho lazwa Sheila
“Kaka tunakupa dakika kumi na tano za kukaa na mgojwa wako”
“Sawa nesi”

Nikasimama pembeni kwenye kitanda alicho lazwa Sheila na kujikuta machozi yakianza kunimwagika kwa uchungu.Kumbukumbu ya maisha ya nyuma aliyo nisimulia Sheila nikaanza kuikumbuka na maisha magumu aliyo yapitia na nikajikuta ninazidi kuhuzunika na machozi yakazidi kunimwagika
“Ohhh Mungu wangu najua kuwa wewe ndio kimbilioa langu.Natambua mimi ni mtenda dhambi ila ninakuomba unisamehee mimi na huyu mpenzi wangu Sheila.Nakuoma umpe nafasi nyingine ya kuishi……Risasi hii nilistahili mimi na sio yeye nakuomba umpe mwangaza wa kuona tena….”

Nilijikuta nikizungumza huku machozi yakinimwagika kiasi kwamba mwili mzima ukapoteza nguvu na kujikuta nikikaa kwenye kiti kilichopo pembeni na kitanda na taratibu kichwa changu nikakilaza pembeni na mwili wa Sheila huku nikiendelea kulia kwa uchungu.Taratibu usingizi mzito ukanipitia. Kwa mbali nikaanza kuisikia sauti ikiniita jina langu nikaipotezea na kadri muda ulivyo zidi kwenda ndivyo ikaendelea kuniita ikanibidi nifumbue macho taratibu na kutazama ni nani anaye niita
Nikamkuta Sheila akiwa analia taratibu huku akiniita kwa sauti ya hini nikanyanyuka na kukaa karibu yake huka nikimtazama kwa huruma na sote tukajikuta machozi yakitumwagika kiasi kwamba hakuna aliye weza kuzungumza chochote kwa wakati huu.Mwanga wa jua metawala ndani ya chumba chetu ukiashiria asubuhi imesha fika

“EDDY KWANINI UMENISALITI MPENZI WANGU?”
“No Sheila sijakusaliti na siwezi kukusaliti”
“Eddy unaniongopea….Unajua ni jinsigani ulivyo uchoma moyo wangu ehee”
“Sheila usizungumze kwa sauti ya juu utajitonesha kidonda”
“Eddy acha nitoneshe kidonda na jua hii risasi nimepigwa kwa ajili yako.Eddy ni nini nilicho kufanyia baba yangu hadi umeamua kunisaliti”
“Sheila nakuomba unisamehe mke wangu ila tambua mimi pia ninakupenda na siwezi kufanaya ujinga kama huo”
“Eddy wewe ni muongo”
“Sio kweli mke wangu nakuoma unielewe kwa hilo”

Sheila akatabasamu huku machozi yakizidi kumwagika kwa uchungu na kunifanya na mimi nizidi kumwagikwa na machozi mengi
“Eddy niahidi huto nisaliti?”
“Nakuapia kwa MUNGU wangu sinto kusaliti”
“Sawa baby…..Gari ipo wapi?”
“Nimeiacha hotelini nimeshindwa kuiwasha”
“Pole baby nenda kaingize namba za siri ni mwaka wangu wa kuzaliwa na wakwako”
“Umeujuaje mwaka wangu wa kuzaliwa?”
“Kipindi pale hotelini unazungumza na yule jamaa nilikikuta kikadi chako cha bima ya afya kikiwa na mwaka wako wa kuzaliwa ndio nikabadilisha na kuweka na namba ya miaka tuliyo zaliwa”
“Wewe mwaka gani?”
“1991 na mbele utaweka mwaka wako”
“Je sauti itakuwaje?”
“Nimebadilisha mmfumo wa uwashaji na kuweka huo wa kuingiza namba za siri”

Sheila alijikaza kuzungumza kwa sauti ya chini sana kutokana sauti ikiwa kubwa anaweza kujiumiza kidonda,Kabla sijatoka nesi wa jana usiku akaingia na tukasalimiana naye
“Jana usiku nilikuja nikakukuta umelala nikaona nisikusumbue”
“Kweli nesi kidogo nilikuwa nimechoka”
“Dada unaendeleaje?”
“Salama japo maumivu yapo mengi kifuani”
“Ohoo pole utapona mwaya hapa namsubiria dokta kuna dawa atakuja kukuchoma ya kukausha vidonda”
“Baby nikuchukulie chakula gani?”
“Mmmm baby sijisikii kula”
“Kaka usimletee chakula kutokana hapa hospitalini tunatoa huduma ya chakula na huyu itambidi apatiwe chakula maalumu kwa jinsi ya ungojwa wake ulivyo”
“Ahaaa baby mimi ngoja nikalichukue gari lisije wakalichukua bure”
“Eddy njoo”

Nikarudi na Sheila akaniomba nimbusu kwenye shavu nikafanya hivyo na kutoka nikaingia kwenye chumba nilicho vaa nguo maalumu za kuingilia kwenye chumba cha wagonjwa mahututi kisha nikatoka nje ya geti la hospitali.Nikajikuta nimesimama kwenye moja ya kibanda cha magazeti na kutazama gazeti moja lililo andikwa kwa maandishi makubwa meusi
‘HEAD MASTER AUA KISA MAPENZI’

Ikanibidi kutoa pesa mfukoni na kulinunua,kutokana nina haraka nikalikunja na kukodisha pikipiki ikanipeleka hadi hotelini na kumlipa muendeshaji huyo wa pikipiki na moja kwa moja nikaelekea kwenye maegesho ya magari na kulikuta gari letu likiwa kama nilivyo liacha jana usiku.Nikaingia ndani ya gari na kuziingiza namba alizo nimbia Sheila na gari likawaka na nikalizima.Nikakumbuka kuna begi langu la nguo kwenye chumba tulicho kodisha jana.Nikapandisha gorofani kwenye chumba chetu na kulikuta likiwa salama,Kutokana chumaba tumekodisha kwa siku mbili sikuona haja ya kulichuku.Nikachukua wallet ya Sheila yenye kadi zake mbili za benki pamoja na pesa kiasi.Nikiwa ninashuka kwenye ngazi za kushuka chini muhudumu mmoja wa kiume akanisimamisha

“Samahani kaka jana wakati ugovi ulipokuwa unatokea kuna hichi kitambulisho kilidondoka”
Jamaa akanionyesha kitambulisho cha Salome ambacho ni chashule
“Nakiomba”
“Ahaaa kaka sio kirahisi rahisi hivyo kuna polisi walikuja kukagua ila nikaibania nikijua utarudi tu”
“Kwa hiyo wewe unataka nini?”
“Japo ya maji ya kunywa si unajua sote vijana”
“Powa”

Nikatoa elfu hamsini na kumpa jamaa kisha na yeye akanipa kitambulisho na tukaagana na mimi nikaelekea kwenye gari.Nikajifikiria kwa muda ni wapi nianzie nikaona ni bora niende shule kukipeleka kitambulisho cha Salome isije ikatokea polisi wakanihitaji tena kituoni na kunikuta na kitambulisho hicho na kumuingiza Salome kwenye matatizo hayo.Nikawasha gari na kuondoka nikaingia kwenye moja ya sheli nikajaza mafuta ya kutosha kwenye gari na safari ya kwenda shule ikaaza.Nikafika getini na na walinzi wakanifungulia geti na wakaonekana wakinishangaa,Nikaachana nao na moja kwa moja nikafika kwenye maegesho ya magari katika endeo la shule na kushuka na baadhi ya wanafunzi wa vidato vingine wakaendelea kunishangaa hadi nikawa ninajiuliza kinacho wafanya wanishangae mimi ni nini

Nikakutana na Madama Mery akitoka ofisini huku akiwa ameongozana na madama Rukia na wote walipo niona wakanifwata na kila mmoja akaonekana kunifurahia ila kwa Madam Mery nikaanza kumuona anamabadiliko katika mwili wake
“Eddy mpenzi wangu unaendeleaje?”
Madam Mery akashindwa kuficha hisia zake hadi machozi yakamlenga lenga
“Salama sijui wewe?”
“Mimi nipo powa…..Mbona umekuja hivyo na nguo za nyumbani hurudi tena shule”
“Narudi mbona kama tumbo limekuwa kubwa?”
“Madam Mery akainama chini na kuanza kuvichezea vidole vyake nanikaona pete ya ndoa kwenye kidole chake cha mkono wa kushoto
“Eddy nimeolewa”
“Hongera”

Nilizungumza huku nikilitazama gari la shule linalo simama na kumouna mkuu wa shule akishuka huku akiwa na mkewe wakicheka kwa furaha na kwabahati mbaya hakuniona.Nikapiga hatua za haraka hadi alipo simama mkuu wa shule na kumgusa bega kitendo cha yeye kugeuka na kuiona sura yangu akastuka na kwa kasi ya ajabu mkono wangu wa kulia nilio ukunja ngumi ukatua kwenye shavu la mkuu wa shule na kumfaya ayumbe kwa nguvu na kumkumba mke wake na wote wakaanguka chini

Madam Mery akaniwahi kunishika shati na kuanza kuniomba niache vurugu,mkuu wa shule akanyanyuka kwa hasira na kunisogelea na kunizaba kofi lililopelekea nikazidi kupadwa na hasira,Madam Mery akaendelea kuning’ang’ania kwa nguvu zake zote ila kutokana na nguvu nilizo nazo nikajitoa mikononi mwa madam Mery na kumfwata mkuu wa shule na kuanza kumrushia ngumi zisizo na idadi na uzuri zaidi kipindi nipo mdogo baba yangu alikuwa akinifundisha mbinu za kuweza kupigana kiasi kwamba hadi ninakua mkubwa swala zima la kupigana kwangu ni lakawaida.Waalimu wa kiume waliopo eneo la shule wakaja kutuzuia japo kuwa mkuu wa shule ni mzee kidogo ila na yeye alijitahidi kunipa makonde kadhaa yaliyo niingia vizuri sehemu mbali mbali za mwili wangu
“Eddy nakuomba uwe mpole kumbuka hapa tupo shule”

Madam Mery alizungumza kwa upole huku nikiondolewa eneo la tukio na waalimu wapatao wanne na kwajinsi nilivyo na nguvu na iliwalazimu kutumia nguvu nyingi katika kunizuia kwenda kuendeleza ogomvi na mkuu wa shule
“Wewe kijana mshenzi sana hujafunzwa huko kwenu hadi unapigana na mume wangu na nitahakikisha shule huna wewe mpumbavu mkubwa weee”

Mke wa mkuu wa shule alizungumza maneno yaliyozidi kunipandasha hasira laiti angejua mumewe kitu alicho toka kukifanya jana usiku wala asinge zungumza ujinga anao uzungumza
“Sawa waalimu wangu nimewaelewa ngoja mimi niondoke zangu naombeni muniachie”
Nilizungumza kwa upole na kuwafanya waalimu wa kiume walio nishika kuniachia taratibu na huku wakiniomba niondoke sehemu ya eneo la shule.

Kwa haraka nikamsukuma mwalimu wa mbele yangu akaanguka chini nikapata nafasi ya kukimbilia eneo alilopo mkuu wa shule na nikamchomoa katikati ya watu wanao mpa pole na kumpiga kabali moja takatifu iliyotupeleka hadi chini ardhini na watoto wa mjini wenyewe tunaiita kabala ya mbao na kuwafanya walinzi na waalimu wa kiume kuanza kuushika mkono wangu na kuanza kuuvuta kwa nguvu ili kuyanusuru maisha ya mkuu wa shule. Wakafanikiwa kunichomoa huku mwili wangu ukiwa umejaa jasho jingi huku misuli ya mwili mzima ikiwa imetuna kiasi kwamba mtu aliyezoea kuniona kwenye mazingira ya kawaida atabisha kuniona kwenye hali ya hasira niliyo nayo sasa na atasema sio mimi

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI

KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)