SORRY MADAM (33)
JINA: SORRY MADAM Mwandishi: Eddazaria G Msulwa SEHEMU YA THELATHINI NA TATU ILIPOISHIA... Madam Rukia alibadilisha mada baada ya mume wake kufika katika eneo tulilopo na sikuwa na haja ya kujiuliza ni kwanini amebadilisha mada nikajua moja kwa moja ahitaji mumu wake atambue kuwa mimi nilikuwa naye porini NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... “Hivi wamesemaje kuhusiana na swala zima la shule kuendelea?” “Wamesema watatoa tangazo kwenye vyomba vya habari pele shule itakapo funguliwa ila kwa sasa wameunda tume ya madai yaliyopelekea shule kufungwa ambayo itachunguza kila kitu na wanafunzi walio kamatwa na polisi wapo wengine wanahojiwa” “Sasa hiyo tume watatumia muda gani kuchunguza hayo madai yato kwa maana siku zinakwenda mbele na masomo ndio hivyo yamesimama?” “Mimi wala sielewi ila kidato cha sita na cha nne wamesambazwa kwenye shule za jirani ili kuendelea na masomo hadi pale majengo yatakapo fanyiwa ukarabati nao ndio watarudi” “Ahaaa....” “Wewe sasa hivi …