SORRY MADAM (36)

0
SEHEMU YA THELATHINI NA SITA
ILIPOISHIA...
Sheila akasimama na kwenda kumuita daktari aliye kabidhiwa kwa kuniangalia kwa ukaribu sana.Sheila akaanza kumuelezea dakatari hali ninayojisikia na kumfa ya daktari kutoa agazo kwa wezake wanifanyie uchunguzi zaidi.

NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU

SASA ENDELEA...
Wakanipeleka kwenye chumba cha X-reys na wakaniweka kwenye mashine kubwa iliyokaa kama mfumo wa jeneza na kunipitisha kwenye mitambo yao na kutokea upande wa pili wa sehemu hiyo na wakanitoa kwenye kifaa chao na kunirudisha wodini na kumuomba Sheila kubaki na madaktari kwa mazungumzo zaidi.Baada ya muda Sheila akaingia huku akiwa na sura ya unyonge iliyo anza kunipa wasiwasi kiasi kwamba nikajikuta ninaaza kupata wasiwasi na mimi
“Sheila wamekuambiaje?”

Badala ya Sheila kunijibu akaanza kulia na kuzidi kunichanganya na sikujua ni nini kinacho mliza.
“Eddy ninakupenda sana mume wangu”
“Sawa hata kama unanipenda ila niambie kitu kinacho kuliza”
“Eddy sitaki kukupoteza mume wangu bado hatujafikia malengo yetu”
Sheila akazidi kunichanganya kiasi kwamba nikataka kunyanyuka ila kutokana na maumivu ya kifua changu nikajikuta nikurudisha kwichwa changu kwenye mto nilio uegemezea kichwa.
“Eddy madaktari wanasema maisha yako yapo hatarini kupotea....siku yoyote”
Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio kiasi kwamba nikajikuta ninazidi kuchananyikiwa huku jasho likinimwagika

“Eddy kumbe ulisha wahi kupigwa risasi kwanini hukuniambia hadi leo madaktari wameniambia kuwa kidonda chako cha risasi hakikupona kikamilifu na jinsi askari waliyo kupiga imesababisha damu kuvilia kwenye mapafu na kuanza kujenga uzo kwenye moyo wako”
Nikazidi kuchanganyikiwa na kujikuta nikitokwa na machozi na kumzidisha Sheila kulia kwa uchungu
“Sheila kwahiyo mimi ndio nitakufa?”
“No Eddy huwezi kufa mume wangu.....usizungumze hivyo kumbuka wewe ndio mwanga wangu we....”

Kabla Sheila hajamaliza kuzungumza akaiingia daktari mkuu na akasimama kwa muda akitutizama huku akwa ameshika kikaratasi mkononi mwake
“Binti umemuambia?”
Sheila akaitikia kwa kutingisha kichwa akimuashiria daktari kuwa ndio amenimbia
“Binti nilikuambi usimuambie hii itamsababishia matatizo zaodi kwani moyo wake kwa sasa unaweza kushindwa kufanya kazi yake muda woote kuanzi sana na inaweza ikampelekea kifo”
Sikujua daktari kama akili zake zimekamilika vizuri au laa kwa maana kitu anacho kizungumza mbele yangu kikazidi kunichanganya zaidi ya alivyo niambia Sheila na isitoshe amemkataza Sheila kuniambia kiitu kama hicho na yeye ndio anakizungumza.

“Sasa hapa kuna karatasi unatakiwa usaini ili tukamfanyie upasuaji mume wako”
“Ngoja kwanza dokta ni nani munataka kumfanyia upasuaji?”
“Ni wewe kwani maisha yako yapo hatarini”
“Nyinyi si ndio wale mulio mpasua mgonjwa wa mguu kichwa na wakichwa mguu”
“Hilo sio jukumu lako na mimi ni mgani.....Binti siani kwa ajili ya kuyaokoa maisha ya mume wako na kama upo tayari kumpoteza basi itakuwa hivyo”
Sheila alachukua katatasi mikononi mwa daktari na akaifungua na kabla hajaandika chpchote nikamuomba nanionyeshe ili nipitie na mimi.

“CHOCHOTE KINAWEZA KUTOKEA IKIWEMO KIFO”
Maandishi madogo yaliyomo kwenye karatasi yakanichanganya sana na kujikuta nikimtazama Sheila ambaye amaeshika peni mkomoni kwa kusaini kwa niaba yangu.Sheila akasaini na kumkabidhi daktari karatasi yake na daktari akatoka kwenye chumba
“Eddy nakuomba ujikaze mume wangu”
“Kwenye kufa Sheila hakuna kujikaza hawa madaktari mimi sina imani nao kabisa”
“Usijali kwa hilo mume wangu”
“Kwani hiyo oparesheni ninafanyiwa lini?”
“Leo hii mida na yamebaki masaa kama mawili”
“Sasa imekuwaje na wewe ukasaini pasipo kuniambia kama ninafanyiwa leo kwa maana hapo kwenye hiyo karatasi kumeandikwa chochote kinaweza kutokea ikiwamo kifo sasa unaona ni haki kweli?”
“Eddy acha kupanic”
“Sio kupanic......Wewe kwanini usaini si uneniambia kuwa yamebaki masaa mawili nisinge kubali kufanyiwa ningesubiria hadi mama apatiakene ili hata nikifa nife vizuri”
“Eddy usitake unilize sasa hivi mume wangu hembu tulia madaktari wanajua ni nini wanafanya”

Baada ya masaa wawili wakaingia amadaktari wawili akiwemo yule daktari wa familia akaonekana kushangaa kuniona ndani ya chumba,Hakunisemesha akatoka ndani ya chumba na sikumfwatilia sana kwani manesi walianza kuniandaa kwa kunpeleke kwenye chumba cha upasuji huku wakinibadilisha nguo na kunivisha vazi maalumu kwa ajili ya upasuaji.Wakamaliza na kuniweka kwenye kitanda cha matairi na kuanza kukidukuma huku Sheila akiwa pembeni yangu na machozi yakaanza kumwagika tena

Nikastukia nikamuona daktri anaye sukuma kitanda akisukumwa na kuanguka chini na macho yangu yakakutana na macho ya baba yaliyojaa hasira hadi yakawa mekundu.Akanishika kifuani na kunivuta na kunitupa chini na kuanukia mgongo na kusababisha maumivu makali kuzidi kunitawala kwenye mwili wangu hususani kifuani mwangu.Madaktari wakataka kumsogelea baba ila akachomoa bastola yeka na kuwafanya madaktari kusita.Mguu wa baba ukatua kifuani kwangu huku ukiwa umevalia buti lake la jesi kisha bastola yake akaikoki tayari kwa kunifyatulia risasi

Nikastukia baba akitoa ukulele na kuanguka chini na kumuona Sheila akiwa ameshika kipande cha mbao kinachoonekana kimechomolewa kwenye benchi huku kikiwa kinavuja damu kwenye sehemu ambayo ilitua kichwani mwa baba.Sheila akaanza kutetemeka baada ya kumuona baba akiwa anavujwa na damu za kichwa,Madaktari wakaninyanyua na kunirudisha kwenye kitanda huku hali yangu ikizidi kuwa mbaya na mamcho yangu yakaanza kutawaliwa na ukungu na kwambali nikamuona Sheila akishikwa na askari wawili na wakaanza kumtoa enje akiwa ananililia kwa uchungu.Kitanda nilicho kilalia kikaanza kusukumwa taratibu na jinsi ninavyo isililizia hali yangu yenye maumivu makali ya mwili nikajikuta macho yangu yakitawaliwa na ukungu mwingi na sikujua ni kitu gani kinacho endelea
***
Baridi kali ikaanza kunisumbua mwili wangu na kujikuta nikianza kufumbua macho yangu na kujikuta nikitazama sehemu ya juu ambayo kwa haraka haraka sikujua nipo wapi.Mwili wangu ukawa umebanwa kidogo na na kwa haraka haraka nikagundua kuwa nipo kama nilivyo zaliwa kwani kiwamgo cha baridi kilitawala mwili wangu mzima,nikajariu kujigeuza ila nikajikuta nikishindwa na nikaanza kujisukuma na kumbukumbu za akili yangu ikagundua kuwa sehemu niliyopo ni katika majokofu ya kuhifadhia miili ya watu walio fariki dunia.Nikajaribu kuita ila sikusikia msaada wa mtu wa aina yoyote wala kitu kikitembea nje ya majokofu hayo,Nikazidi kujitahidi huku miguu yangu nikiigonga gonga kwenye sehemu ya chini ya jokofo ambapo ndipo miguu yangu ilipo elekea na kujikuta sehemu niliyo ilalia ikienda mbele na kufunguka.Nikaendelea kujikaza huku nikizisidi kujitahidi kujitoa ndani ya jokofu hili na chakumshukuru Mungu nikafanikiwa kulifunua kwa uwazi mdogo ulio niruhusu kuitoa mikono yangu kwa nje na kujivuta na likafunguka na kupata uwezo wa kukaa na kitako na kuanza kushangaa

Woga ukaanza kunitawala na baada ya kujikuta nikiwa nimeshonwa katikati ya kifua changu na kitu kingine kilichoizidi kuniogopesha ni miili mingi ya watu walio lala chini huku wakiwa wamefunikwa malailoni yanayo waonyesha vizuri huku miili yao ikiwa imeharibiwa sana huku wengine vichwa vyao vikiwa vimepasukwa na kurudishiwa rudishiwa kiasi kwamba wanatisa kwa muonekano wao.Nikashuka kwenye jokofu nililo kuwepo na taratibu nikaanza kuutafuta mlango wa kutokea katika chumba hichi na kabla sijauona nikastukia taa za chumba zikizima na giza kali likazidi kutawala
Nikajikaza na sikutaka kuuruhusu woga kutawala katika mwili wangu kwa wakati huu,Nikapapasa papasa ukutani kwa dakika zaidi ya mbili na kufanikiwa kukuta mlango na kabla sijaufungua nikasikia watu wakizunumza kwa nje

“Muambie huyo Mudi awashe hilo genereta la upande huu kuna maiti tunataka kuziingiza humu”
“Kwani hao nao wametokea wapi?”
“Kuna basi limeanguka na kuua watu ishirini”
“Sasa huku ndani si kumejaa hadi maiti nyingine tumeziweka chini tutafuta ustaarabu wa kuwatoa kesho wakazikwe na manispaa kwa maana hata ndugu zao hawajitokezi”
“Hawa tutawaweka hivyo hiyo bwana kwani hatuna seemu nyingine ya kwenda kuwaweka na hospitali zote za wilaya mochwari zao ni ndogo”

Watu waliopo nje wakaendelea kujibishana nikataka kupiga kelele za kuomba msaada ila roho yangu ikasita na kujua ni lazima watu waliopo nje wataogopa na kukimbia na ningelisitisha zoezi zima la wao kuingiza maiti wanazo zizungumzia,Taa zikawaka na mlango nikausikia ukifunguliwa na baada ya dakika kakika moja mlango ukafunguliwa
“Hembu shika huko vizuri usije ukamuachia”

Gafla umeme ukakatika na kuwafanya watu walio ibeba maiti wanayo taka kuuingiza kuanza kutukana matusi mazito na kwakupitia uwazi mdogo wa mlango nikastukia kuona wakiondoka kwa hasira huku maiti wakiwa wameilaza chini na sikujua ni wapi wanapo elekea,Nikachungulia nje na kukuta kuna giza ila mwanga wa mbalamwezi uliweza kunisaidia kuona baadhi ya majengo na kungundua bado nipo sehemu ya Muhimbili.Nikaanza kuoiga hatua za haraka na kutoka ndani ya chumba cha kuhifadhia maiti na nikafika kwenye jengo ambalo nikakuta kamba nyingi zikiwa zimeanikwa makoti meupe ya madaktari.Nikalishusha moja kwenye kamba na kulivaa kwa haraka kisha nikachukua suruali nyepe na kuivaa na muonekanao wangu ukawa kama wauduzi wa kiume kwenye hospitali hii.Nikaanza kutembea kuelekea getini huku miguuni nikiwa nipo peku peku na nikafanikiwa kutoka pasipo walinzi kunitilia mashaka ya aina yoyote.Nikatafuta sehemu na kukaa huku akili yanu ikianza kufikiria ni kitu gani kilicho wafanya madaktari hadi wakanipeleka kwenye chumba cha kuhifadhia maiti.Nikajikuta nimejishika tama na kugundua mashavu yangu yamejaa ndevu nyingi na kwaharaka haraka nikagundua ni kipindi kirefu nimekaa hospitali kwani ndevu zangu huchukua muda mwingi sana katika kuota na kuwa ndefu kama nilivyo zikuta sas

Nikapata wazo la kwenda nyumbani kwa Sheila japo ni mbali sana na sehemu niliyopo nikaona sina budi kufanya hivyo.Nikapiga moyo konde na kunyanyuka sehemu niliyo kaa na kuanza kutembea japo njaa kali inanisumbua tomboni kwangu ila nikajitahidi kwenda kutembea kwa haraka ili niweze kufika, Nikatumia kama masaa mawili na kufika nyumbani kwake na kukuta ukimya mwingi ukiwa umetawala ila kitu kingine kilicho anza kunipa wasiwasi ni nyasi nyingi na ndefu zilizo oto nje ya geti lake na kwaharaka nikajua Sheila hayupo ndani ya nyumba yake kwa maana kama angekuwepo kusingekuwa na nyasi nyingi huku geti lake likiwa lemetawaliwa na vumbi jingi.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI

KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)