SORRY MADAM (40)

0
SEHEMU YA AROBAINI
ILIPOISHIA...
Nikajinyanyua tararibu kitandani na kukaa kitako huku Salome naye akiliingiza begi lake la nguo na kuliweka pembeni na taratibu akakaa kwenye sofa lililopo ndani ya na kuanza kuminya minya vidole vyake vya mkononi huku sura yake akiwa ameilekezea chini akionekana kujawa na aibu kubwa ikanilazimu kuanza kumsalimia

NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU

SASA ENDELEA...
“Mambo”
“Powa vipi?”
“Salama za huko utokapo?”
“Mmmm....?”
“Za huko utokapo vipi?”
“Nzuri tu”
“Karibu mbona unaona aibu?”
“Eheee walaa Jose yupo wapi?”
“Ahh amesafiri kikazi”
“Mungu wangu sijui itakuwaje?”
“Iakuwaje nini?”
“Mmmm hamna mwaya”

Nikanyanyuka kitandani huku nikiwa ninawenge la usingizi kidogo na nikaanza kuvinyoosha viungo vyangu huku nikipiga miyayo na kama kawaida ya wanaume wengi walio kamilika kimaumbile pale wanapo amka ni lazima koki zao husimama kuashiria ni siku mpya hii na ndivyo ilivyo kwangu jambo lililo mpelekea Salome kuyagandisha macho yake kwenye koki yangu pasipo kuyapepesa hata kidogo.Nikawasha redio na kuifungulia sauti ya kawaida kisha nikarudi kukaa tena kitandani na Salome akatoa simu yake aina ya Samsung Galax na kuanza kuiminya minya kisha akaiweka sikioni

“Jose jamani upo wapi?”
“Sasa utarudi lini wakati mimi nipo kwako nilikuja kukufanyia supriz naona supriz yenyewe imeharibika”
“Nimpe simu nani?”
“Haya........Eddy ongea na Jose simu ipo hewani”
“Mmmm vipi kaka Jose”
“Safi.....sasa huyo bibie ndio hivyo kaja bila taarifa”
“Ndio”
“Basi ninakuomba ukatafute hata sehemu ya kujishikiza kwa hizi siku ambazo nitakuwa sipo na yeye aishi ndani humo hadi nitakapo rejea”
“Ahaaa powa kaka”
“Hakikisha unafanya hivyo bwana....Huyo ni Malkia wangu muache ajitanue ndani kwangu”
“Sawa mzee......Chukua simu yako”
“Eeehe baby”
“Ahaa ataondoka eheee”
“Haya kazi njema”
“I love too mwaaaaa”

Salome akakata simu na kuachia tabasamu pana ila kwa upande wangu nikajikuta roho yangu ikiwa inauma kupita maelezo kwani kitendo cha kuambiwa kuondoka kikabaki kikiniumiza na sikuwa na jinsi ya kufanya.Nikanyanyuka kiustaarababu na kuzitoa ndala chini ya uvungu nilizo kwenda kuogea jana usiku na kuzivaa vizuri na kusimama kwenye kioo kikubwa na kujitazama jinsi sura yangu ilivyo jaa ndevu zisizo na mpangilio na kunifanya nionekane kama mzee wa miaka 70 na zaidi kumbe ni kijana mdogo tu wa miaka ishirini naa.

“Nawatakia maisha mema wewe na mchumba wako”
“Eddy unakwenda wapi?”
“Sijajua ila ngoja niondoke”
“Eddy...”
“Salome wewe tayari umesha mpenda mtu mwengine kuwa na mimi hilo litakuwa ni ngumu”
“Powa nenda”

Salome akajibu kwa dharau na kunifanya nimtazame kwa muda huku machozi yakianza kunilenga lenga na kuyakumbuka mambo mema niliyo mfanyia Salome kuanzia siku ninampa pesa ya matumizi kipindi tupo shule na alipo poteza pasa yake hadi siku ninamkuta na mkuu wa shule wakitoka kwenye mlango wa chumba cha Hotel kisha taratibu nikashika kitasa cha mlango
“Salome naamini unaijua afya yako ila ni bora ukamueleza ukweli Jose kuliko kumuua pasipo yeye kujua”
“Nashukuru kwa ushauri wako ila ukweli ni kwamba sijaadhirika kama unavyo dhania”
“Sawa kama ni hivyo”
“Powa nenda usije ukanivunjia ndoa yangu na mume wangu mtarajiwa....Ila umeachwa nini na mpenzi wako mbona umechakaa hivyo kipindi kile nilivyokuwa nikikuomba msamaha ukawa unanidharau haya pole mwaya”

Maneno ya Salome yakaniumiza kiasi kwamba nikajikuta nikitokwa na machozi kisha nikafungua mlango na kutoka nje na mtu wa kwanza kukutana naye ni yule mama wa jana aliye ninyang’anya maji yake na baada ya kuniona akaanza kucheka kwa kicheko cha kejeli
“Heeeheee Osama na wewe pia unalia makubwa haya”
Nikasimama na kumtazama kwa macho makali na akaendelea kujichekesha kitendo kilicho anza kunipandisha hasira na nikapiga hatua za haraka hadi alipo simama na sura yangu nikaisogeza karibu na sura yake huku ndevu zangu zikiwa zinamgusa kwenye mashavu yake na akakaaa kimya kiasi kwamba akaanza kutetemeka
“NITAKUUA”

Nilizungumza kwa hasira huku nikijitahidi kuizuia hasira yangu ambayo siku zote ni mbaya na taratibu nikageuka na kuondoka zangu.Na nikafika kwenye moja ya maskani na kuwasalimia watu wote nilio wakuta na mimi nikatafuta sehemu nikakaa huku nikiwasikiliza mabishano yao ya mpira dhidi ya timu za afrika zinavyo fanya vibaya kwenye kombe la dunia la mwaka huu na jinsi mabishano yao yanavyo endelea nikajikuta hasira yangu ikipungua
“Alafu wewe jamaa ni mwera(polisi) nini?”
“Kwa nini?”
“Kwa maana umekuja hapa umesalimia na kuvamia vamia kijiwe cha watu usije ukawa unatuchunguza?”
“Hapana jamani mimi mtu wa kawaida sana”
“Sio kawaida usije ukasababisha pira(gari la polisi) likaja hapa ni kutunyanyua”

Jamaa mmoja aliye jazia kifua akanisogelea huku akiwa na kipisi cha bangi mkononi huku kikiwa kinawaka kisha akavuta fumba kubwa la moshi na kuinama na kunipulizia usoni jambo lililo nikasirisha sana na kujikuta nikinyanyuka na kumtandika kichwa cha pua na akayumba nyumba na kuwafanya wezake wapatao wanne kunivamia na kuniangusha chini na kuanza kunishambulia kwa mangumi na kujikuta nikimdaka mmoja sikio lake na kumng’ata kwa nguvu zangu na kumfanya atoe ukelele mkubwa huku akisema anakufa na nikamuachia kumng’ata na akanyanyuka huku damu zikiwa zinamwagika kwenye masikio yake na gafla vumbi jingi la gari lililo funga breki za gafla likasimama na watu walio nishambulia wote wakakimbia na kuniacha nikiugulia kwa maumivu.

Nikastukia askari wawili wakiwa wakininyanyua huku wakinipiga na virungu vya miguu na wakanisukumia kwenye gari lao walilo kuja nalo.Kwa wenge la maumivu sikujua ni wapi wananipeleka.Gari likasimama kwenye mtaa mwengine na kuwakuta askari wengine wapatao wanne wakiwa na bunduki mikononi wakiwaamrisha watu wapatao nane waliokuwa wamelala chini huku mikono yao wameiweka kichwani na wanavyo onekana ni wavuta bangi.Watu hao wakaamrishwa kuingi ndani ya gari hili la polisi na watu wengi tumezoea kuyaita ‘Defendar’ na sote tukajikuta tukiwa tumetosha na askari wote wakapanda na likaondoa kwa kasi.Ndani ya dakika kadhaa tukawa tumesimama kwenye moja ya geti ambalo kwa haraka nikafahamu kuwa ni gereza la Keko.

Gari ya polisi ikaingia ndani na sote tukaamrishwa kushuka na kupanga mastari mmoja huku tukiwa tumechuchumamaa na tukaanza kuhesabu namba huku na mimi nikiwa namba tano kati ya watu tisa tuliopo kwenye eneo hili na tukasimama huku mikono tukiwa tumewekeana kwenye mabega na kunyoosha mstari mmoja na tukaaza kutembea huku tukiongozwa na askari wa magereza hadi kwenye chumba kimoja cha mahabusu na sote tukaingia ndani na mlango wake ukafungwa.Nikatafuta sehemu yangu na kukaa huku nikijutia kitu kilicho nifanya nikae kwenye ile maskani ni nini.
“Hata nikiwaambia kuwa mama yangu ni waziri haina tija”

Nilijisemea mwenyewe kimoyo moyo na sikuwa na uwezo huo kwa jinsi ninavyo wajua askari wangeniambia mambo ya dharau ambayo yangenikera zaidi na kunisababishia matatizo mengi zaidi.Hadi jioni inaingia sikujua ni kitu gani kinacho endelea juu ya chakula.Usiku mzima sikuweza kulala kutokana na baridi kali kwenye sakafu isitoshe tumbo langu tangu jana usiku halikuuingiza chakula cha aina yoyote.Mawazo ya jinsi nitampata mama yangu yakaanza kunitawala kichwani kwangu kwani kwa maelezo ya John aliniambia kuwa mama yangu yupo South Africa akiwa anaumwa na amelazwa.

Hadi inatimu asububuhi sikuweza kupata usingizi na kengele kubwa likagongwa na milango ikafunguliwa na wezangu wakatoka kwa haraka na mimi ikanibidi nitoke kwa haraka na kuwafwata kwa nyuma na tukafika kwenye sehemu na kuwakuta wafungwa wengine walio valia sare wakinganyanyiana mabakuli yaliyo tengenezwa na alumuminiam na nimachafu ndani ya maji yaliopo kwenye karo na anayepata chombo chake anakimbilia kwenye sehemu unapotolewa uji.Nikabaki nikiwa nimesimama na kutokujua ni nini nifanye kwani nikahisi endapo nitakunywa uji wao ninaweza nikatapika kwani una harufu mbaya sana.
Watu wakakanywa uji kisha sisi tulio tolewa kwenye chumba tukaamrishwa kurudi kwenye chumba tulicho toka.

“Oya wewe ni mtoto wa mama nini?”
Jamaa mmoja alizingumza na nikabaki nikiwa nimemtazama pasipo kukjibu kitu cha aina yoyote huku akininyooshea kidole
“Oya wewe chok* si nanikuuliza wewe ni mtoto wa mama?”
“Kwani wewe umezaliwa na mbwa?”
“Ahaaa dharau sasa hizo”
“Sio dharau unavyoniambia kuwa mimi ni mtoto wa mama ina maanisha wewe umazaliwa na mbwa tena mbwa koko”
“Oya dogo inakuwaje anakuita mbwa koko alafu na wewe unakubali kirahisia rahisi”
“Na wewe yasiyo kuhusu isiyaingilie ua na wewe unataka kuitwa mbwa koko?”

Jamaa aliye ingilia mada akanifwatwa huku kifua chake akiwa amekitunisha na mimi nikasimama kwa haraka na akanisukuma kidogo na kurudi nyuma na kwanguvu zangu zote nikamrukia kwa kutumia bega langu na likatua kwenye tombo lake na kumsukuma hadi ukutani na kuanza kumshindilia mangumi na kuwafanya watu wengine kushangilia kwa nguvu.Jamaa naye hakuwa nyuma katika kuyajibu mashambulizi yangu na kusema ukweli ngumi zake ni nzito kiasi kwamba nikaanza kuona nyota nyota na kwa bahati mbaya akanisukuma na kichwa changu kikagonga kwenye nondo ya mlango na kujikuta nikianguka kama mzigo na kupotaza fahamu

***
Nikastuka na kujikuta nipo kwenye kitanda cha hospitalini huku mkono mmoja nikiwa nimefungwa pingu na pembeni yangu amesimama askari wa magereza.Nikajishika kichwani kwangu na kukuta nikiwa nimefungwa na bandeji kubwa
“Unajisikiaje?”

Askari aliniuliza na kunifanya nikae kimya nikiwa nikimtazama kwa macho ya unyonge.Askari akafungua mlango na kumuita nesi kisha na yeye akarudi kukaa kwenye sehemu aliyokuwa umekaa hapo awali.Nesi akaingia huku akiwa amebeba kisinia chenye vifaa vingi na kukiweka pembani kwenye meza iliyopo karibu na kitanda nilicho lala na kuanza kunitazama kwenye jeraha lililopo kichwani kwangu
“Amesha kula?”
“Bado hajakula”
“Ina bidi tuweze kumpatia chakula ili aweze kunywa dawa”
“Hapa ni wapi kwenye kibanda ambacho ninaweza kumnunulia chakula?”
“Ukitoka kwenye geti hapo utaweza kuona kibanda cha wauza chipsi na unaweza kumnunulia chakula”
“Sawa”
“Akimaliza kula ninaomba uniite”
“Sawa”

Nesi akatoka na kukiacha kisinia chake na askari akanyanyuka na kutoka nje na nikapata wazo la haraka nikaanza kutafuta kifaa kidogo kinachoweza kuingia kwenye shimo la funguo la pingu na kuchukua kijikifaa kidogo kilichopo kwenye sinia na sikujua kina kazi gani na kuanza kuifungua pingu niliyo fungwa kwa utulivu wa hali ya juu na chakumshukuru Mungu ikafunguka kisha nikashuka kitandani japo mwili umetawaliwa na maumivu makali ila nikajikaza na kuufwata mlango wa kutokea kwenye chumba nilichopo na kuwaona watu wakiwa wanaendelea na mishe zao.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI

KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)