SEHEMU YA THELATHINI NA TISA
ILIPOISHIA...
Nikabaki nikiwa ninatetemeka kwa hasira kiasi kwamba nikajihisi michuruziko ikinitoka puani kwangu na matone baadhi yakadondoka kwenye mapaja juu ya nguo za wauguzi nilizo zivaa na kugundua kuwa ni damu ndio zimenitoka puani na sikujua zimesababishwa na nini kwani ndio mara yangu ya kwanza kutokwa na damu za puani.NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
John akanipa kiatambaa chake na kujifuta damu zinazo nitoka na askari akasimamisha gari pembeni ya barabara na wakaniomba nishuke nipigwe na upepo wa wa halisi kulilo IC iliyo tawala ndani ya gari
Nikashuka na kuinama chini na damu zikanitoka kidogo na chakumshukuru Mungu zikakata japo kichwa nikaanza kukihisi kikiwa kimetaliwa na maumivu makali
“Unajisikiaje?”
“Kichwa kidogo kina gonga”
“Noja tukakutafutie dawa”
”Hapana twendeni air port”
“Utaweza kweli Eddy?”
“John usijali kwa hilo nitaweza tu”
Tukaingia ndani ya gari na safari ikaanza upya na kwawakati huu tukaelekea uwanja wa ndege na hatukuwa na uhakika sana kama tunaweza kuwaona baba na Sheila au laa.Tukafika uwanja wa ndege na sote tukashuka kwenye gari na mimi nikawa wa kwanza kuelekea sehemu ya abiria na nikajitahidi kuyapa wepesi macho yangu katika kuwatazama watu wengi waliopo kwenye eneo hili ili niweze kuwaona baba na Sheila ila juhudi zangu zikagonga mwamba kwani sikuweza kuwaona.Kwa kupitia kioo kikubwa kinacho onyesha sehemu ndege zilipo simama na kuwashuhudia baba akiwa amemshika Sheila kiuno wakimalizi ngazi ya mwisho kuingia ndani ya ndege na kunifanya niaze kumuita Sheila huku mkono wangu mmoja ukipiga kioo ila hawakuweza kunisikia na kuwafanya askari waliopo uwanja wa ndege kunishika na kunizui kitendo kilicho nifanya machozi kunimwagika kiasi kwamba nikaanza kupata maumivu ya kiua
John na askari wa nyumbani kwetu wakanichukua na nikaishuhudia ndege waliyo panda Sheila na baba ikiacha ardhi na kupaa angani na kunifanya nishiwe nguvu na kujikuta nikianguaka chini.John na weza watu wengine wakaninyanyua na sikujua ni wapi wananipeleka na kujikuta nikiwa kwenye kitanda cha matairi na kuingizwa ndani ya gari ya wagonjwa na kupelekwa hospitali.Madaktari wakaanza kunifanyia uchunguzi na wakanichoma sindano ambayo sikujua inakazi gani mwili mwangu
Ndani ya masaa matano madaktari wanipa ruhusa ya kutoka huku wakiwa wamenifungushia na baadhi ya vidonge vya kunywa pale nitakapo tokwa na damu kwani waliniambia chanzo cha damu kunitoka puani ni kutokana na kuwaza sana kiasi kwamba mishipa yangu inayopandisha damu kichwani husindwa kufanya kazi vizuri.Askari wetu wa getini akanipeleka nyumbani kwake ambapo anaiishi peke yake kwenye chumba kimoja alicho pangisha maeneo ya mbagala rangi tatu.Na tukafika kweye nyumba iliyo jaa wasichana wengi ambao kitendo cha sisi kupita mbela yao wakaanza kunong’onezana na kucheka kwa kicheko kikubwa
“Eddy wazoee ndivyo walivyo hawa wanawake humu ndani?”
Askari wetu wa gatini alizungumza na sikumjibu kitu cha aina yoyote na sote tukaingia ndani ya chumba chake alicho kihaza viti vingi vya dhamani
“Eddy jisikie huru ndugu yangu”
“Asante”
“Hapa ninaishi peke yangu ila ni mara chache mke wangu anakuja kutokana yupo masomoni Arusha”
“Ni mwanafunzi wa sekondari au chuo?”
“Ni mwanafunzi wa sekondari yupo shule moja hivi ya bodi na miezi minne ya nyuma wamechoma shule yao ila wazazi wake wamempeleka shule ya wasichana Iringa”
“Ahaaa anaitwa nani?”
“Salome Alex Edward”
Moyo ukanipasuka na kujikuta nikimtaza askari wetu wa getini kwani Salome anaye mzungumzia ni yule miongoni mwa wapenzi wangu japo mimi na yeye tumeachana kwa katika mazingira ya kutatanisha na mbaya zaidi ametembea na mkuu wa shule na ameambukizwa virusi vya ukimwi.
“Yule dogo ninampenda sana hadi imefiki hatua mimi ninamlipia ada ya Advance”
“Yupo kidato cha ngapi?”
“Kidato cha tano japo sasa hivi anadani kuwa nimuache asome ndio tutaendelea na mapenzi imenilazimu nimsomeshe kwani familia yake ni duni sana”
“Mmmm pole sana ndugu yangu”
“Kwa nini unanipa pole”
“Jukumu la kumsomesha mtu ni kubwa sana na ikitegema ndio hivyo wazazi wake hawajiwezi kiuchumi”
“Ndio ndugu yangu si unajua mwanaume unatakiwa kujikaza na tumeubwa kupambana na ile pesa uliyonipatia kidogo ilinisaidia kumlipia ada na matibabu hospitalini”
“Alikuwa anaumwa na ugonjwa gwani?”
“Waliniambia kuwa ni mstuko wa moyo”
“Ahaa ndugu yangu hongera sana”
“Asante ndugu yangu”
John akanionyesha nguo za kuvaa nikitoka kuoga kutokana ni uswahilini ikanilazimu kutoka na kindoo cha kuogea huku nikiwa nimeshika kopo lenye sabuni na John akanionyesha bomba la maji na nikakuta kuna kindoo kimekigwa ikanilazimu kusubiri kwa muda na kuna wamama wawili wapo pembeni wanapika vyakula vyao kwa ajili ya jioni wakaanza kunong’onezana taratibu
“Eheeee OSAMA BIN LADEN ameingia mbagala jamani....mabomo yasije yakalipuka tena”
“Shosti sema wewe Obama nikisema mimi Bush nitaambiwa ninakiherehere”
“Mmmm na hayo mandevu sasa unaweza kusema kama kama paka aliye mwagikiwa na mchuzi wa moto”
Moja kwa moja nikajua wananisema mimi kotokana na jinsi nilivyo na ndavu nyingi ambazo zimenifanya kuonekana na sura ya kutisha.Nikabaki nikiwa nimewatazama kwa jicho la hasira mpaka wakajistukia.Nikaona nikiendelea kusimama katika bomba watanikera zaidi na nilicho kifanya ni kuyamimina maji yaliyopo kwenye kindoo nilicho kikuta na kuyaweka kwenye ndoo yangu na kabla sijaondoka mama mmoja akasimama na kunifwata kwa haraka huku akubwatuka
“Wee wee usijifanye muhuni rudisha hayo maji sehemu ulipo yatoa”
“Kwani si nimekikinga kindoo chako si kitajaa?”
“Koma mwanaume mzima ovyoo unazani pale nimekalisha makalio yangu bure...Nimekaa ili kindoo changu kijae maji”
“Samahani kama nimeuudhi”
Nikayamimina maji niliyo yatoa kwenye kindoo cha huyu mama ambeye sikujua ni kwanini amenichukia pasipo kuwa na sababu maalumu kwani ni siku yangu ya kwanza kufika atika nyumba hii ila wanaonekana kunichukia sana”
Nikakikinga kindoo changu hadi kikajaa na kwenda nacho kweye bafu alilo nionyesha askari wetu ambaye hadi sasa hivi nilisahau jina lake kani nilisha zoea kumuita afande.Nikaoga na kumaliza na kurudi ndani kwangu na kumkuta askari wetu akivaa nguo nyingine za kazini
“Unaondoka?”
“Ndio kaka hapa nimepigiwa simu ninahitajika lindo si unajua nilitoaka pasipo kuaga inanilazimu kwenda kufidi muda niliokuwa sipo kazini”
“Ahaa sawa ndangu yandu ila mbona hawa mama humu ndani wamekuwa watu wa maneno ya chini chini?”
“Hao wamama huwa wanapenda kumpima mtu....hata mimi kipindi nilipokuwa ninakuja walikuwa wanavimaneno vya chini chini hadi kuna siku kuna mama nilimzaba makofi ndio wote wakaniheshimu”
“Wana waume?”
“Ndio wana waume zao ila waume zao nao ni wanaume suruali”
“Wanaume suruali kivipi?”
“Wanawategemea wake zoa wao kila ikifika asubuhi hukaa maskani hadi mida ya kula ndio utawaona wakirudi mmoja mmoja”
“Mmmm ndio maana wake zao wanakuwa na dharau?”
“Ndio hivyo ndugu yangu”
“Kaka hivi unaitwa nani?”
“Eddy ina maana siku zote hulijui jina langu?”
“Silijui ndugu yangu?”
“Mimi ninaitwa Afande Josephat”
Josephat akanipa elfu kumi kwa ajili ya kununua chakula cha usiku kisha yeye akaondoka na mimi nikavaa nguo zake alizo nipa nizivaa kisha nikaenda kununua chipsi kwenye kibanda kisicho mbali na sehemu ya nyumba yuliyopo na nikarudi na kabla sijaingia mlangoni nikakutana na msichana ambaye sikuwahi kumuona akiwa anagonga mlango wa chumba cha Josephat
“Mambo vipi kaka?”
“Salama vipi?”
“Safi tuu Jose nimemkuta?”
“Hapana amekwenda kazini”
“Hawezi kurudi leo?”
“Sijajua”
“AHaa mimi ni mgani wake ameniambia kuwa nije je nimsubiei huku kwake?”
“Mmmm amekuambia saa ngapi?”
“Ahha..si....sijana”
Dada alizungumza huku akiwa anajing’ata ngat’ata kiasi kwamba sikuwa ninamuelewa ni kitu gani kilicho mleta na akapita dada mmoja na akaropoka neno lililo muudhi dada niliye simama naye
“Wewe Asha ngedere usione chaka mavi yanakubana utakuja kufa nyoo mwanamke kila ukimuona mwanaume kidubwasha chako kina kuwasha”
“Koma na wewe sura mbaya kama kwapa la bibi kizee”
“Wee wee tena utaifananisha sura yangu na hilo sura lako kama ku** ya changudoa aliye kosa mteja”
Maneno yao makali yakawafanya wapangaji waliomo kwenye yumba vyao kutoka wakiwa wanashangaa majaibizanio yao,Sikutaka kuwaingilia nisije na mimi nikavurugwa bure nilicho kifanya ni kuingia ndani na kufungua mlango na nikasikia masufuria yaliyo pangwa kwenye kordo yakianguaka huku watu wangine wakishangilia na nikagundua wanapimana lishe na nilicho kifanya nikufungulia redio yenye spika kubwa hadi mwisho na sikuzisikia sauti zao wakigombana
Baada ya muda ugomvi wao ukaisha kisha na nikapunguza sauti ya redioa na kuanza kula nilicho kinunua huku nikiwa siamini kama ipo siku nitaishi maisha kama haya ninayo yaishi na mipango ya kwenda ikulu ikaanza kujipanga taratibu kichwani kwangu na lengo zima ni kwenda kujua ni jinsi gani wataweza kunisaidi juu ya kumpata mama.Kwa msongamano wa mawazo mengi nikajikuta nikipitiwa na usingizi kwenye sofa moja lililopo kwenye chumba hicho kilicho jaa vitu vingi na mbaya zaidi kina dirisha moja tuu
Nikastushwa na mlango unao gongwa huku nikiisikia sauti ya Josephat ikiita nje ya mlango.Nikanyanyuka na kwenda kumfungulia mlango na akaingia huku akionekana kuwa na haraka sana
“Kaka nimepata safari ya kikazi naelekeaa Kagera”
“Kuna nini tena?”
“Ni maswala ya kikazi tu na ninaweza kukaa hata wiki hapo nimekuja na wezangu wananisubiria hapo nje”
“Ahaaa kwani ni saa ngapi saa hizi?”
“Nane usiku”
Afande Josephat alizungumza huku akidumbukiza nguo zake kwenye begi na la mgongoni kwa haraka akachukua vitu vyake muhimu kisha akatoa elfu hamsini na kunipatia kisha akaiiandika namba yeke ya simu pembeni na kuniambia endepo nitapata tatizo lolite nitafute simu kwa ajili ya kumpigi.Akatoka na mimi nikarudi kitandani na kujibwaga na kutokana na uchovu mwingi usingizi ukanipitia tena wa safari hii ulizidi usingizi wa mwazo
Kwa mbali nikahisi mlango ukifunguliwa nikayafumbua macho yangu na kugundua mwanga wa juu ukiwa umetawala ndani ya chumba changu ikiashiria kumesha pambazuka.Nikayapeleka macho yangu mlangoni kumtazma mtu anaye usukuma sukuma mlango na akaingia kwa haraka
“SAPRAIZZZZ BABY JOS........”
Macho yangu yakakutana na Salome ambaye alishindwa kuimalizia sentensi yake na sote tukabaki tukitazamana kwa mshangao huku yeye akionekana kunishangaa zaidi
Nikajinyanyua tararibu kitandani na kukaa kitako huku Salome naye akiliingiza begi lake la nguo na kuliweka pembeni na taratibu akakaa kwenye sofa lililopo ndani ya na kuanza kuminya minya vidole vyake vya mkononi huku sura yake akiwa ameilekezea chini akionekana kujawa na aibu kubwa ikanilazimu kuanza kumsalimia
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI
KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Email: ZephilineEzekiel@Gmail.Com