SORRY MADAM (44)

0
SEHEMU YA AROBAINI NA NNE
ILIPOISHIA...
HAKUNA aliye lijibu swali la daktari zaidi ya kukaa kimya kimya na tukageukiana na kuendekea kutazama na kadri tulivyo zidi kutazamana ndivyo nilivyohisi ukweli wa maisha yangu juu ya baba yangu kwani kuanzia macho pua midomo na sura hakuna kilicho pishana na mwenzake kiasi kwamba machozi yakaanza kunilenga lenga huku moyoni mwangu nikijihisi amani na furaha iliyo kuba tofauti na ninavyo kuwa na baba yangu gaidi.

NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU

SASA ENDELEA...
“Jina lako ni nani kijana?”
“Eddy”
“Eddy nani?”
“Godwin”

Nikastukia mzee akinikumbatia kwa furaha huku akicheka kwa kicheko kikubwa cha furaha na akaninnyanyua juu kidogo na kuanza kunizungusha kisha akanisimamisha na kunitazama tena usoni huku machozi ya furaha yakimwagika na mimi nikajikuta nikiachia basabu pana
“Dokta nahitaji vipimo vya DNA na huyu kijana”
“Sawa ila inabidi na yeye aridhie”
“Eddy upo tayari kwa hili?”
“Ndio mzee”

Sikuweza kumuita baba moja kwa moja japo tunafanana kwa asilimia 99(tisini na tisa) ila nikahofia endapo majibu yatakuwa siyo sijui sura yangu ningeiweka wapi.Tukaingia kwenye maabara nzuri na yakisasa kisha tukachukuliwa damu na kuombwa kusubiri nje.
“Eddy mimi ninaitwa Godfrey nani Mtanzania japo sasa hivi nina uraia wa hapa Arfrika kusini hii ni kutokana na kuishi miaka mingi hapa Afrika kusini”
“Ahaa sasa ni kwanini uliondoka Tanzania ilikuwaje?”
“Ni historia ndefu sana iliyo nipata hadi kufikia hapa ni vikwazo na mambo mengi nilipitia ila ninamshukuru Mungu hadi leo hii nipo salama”
“Ni kitu gani kilicho kupata?”
“Ni mambo mengi sana yaliyo nipata na hapa sio wakati muafaka wa kulizungumzia hilo”

Kabla sijamuuliza swali jengine mlango wa chumba cha maabara kikafunguliwa na akatoka daktari aliye tuchukua vipimo vya damu na kutuomba twende naye ofisini kwake ambapo akatupa mikono huku usoni mwake akiwa na furaha
“MAJIBU NI ASILIMIA 100 DAMU ZENU ZINAFANA”

Ikawa ni habari mpya yenye furaha maishani mwangu kwani siku zote kilio changu ni kuhusiana na baba yangu.Baba akanyanyuka kwa fauraha na kunikumbatia huku mkono wake mmoja akiupiga piga mgongoni mwangu,machozi ya furaha yakanibubujika na hata wazo la mama kichwani mwangu kwa wakati huu likafutika kidogo.Baba akatoa simu yake na kupiga namba fulani
“Andaa tafrija kubwa na waalike watu wangu wa karibu kwani nina kitu cha kuzungumza nao”
“Fanya hivyo na ndani ya lisaa nitakuwa hapo nyumbani”
“Waambie ni saa mbili usiku”

Sikujua baba anatoa maagizo kwa mtu gani kisha akatoa kitabu kidogo cha kuchukulia pesa na kuandika kiasi anacho kijua yeye kisha akampatia daktari na nikaondoka huku nikiwa nimebeba baasha yenye majibu yetu ya DNA.Tukatoka nje na kulekea eneo la maegesho ya magari na dereva aliye valia suti nyeusi akafungua mlango wa gari aina Astorn Martin na kidogo dereva akawa ananishangaa.Safari ikaanza huku kila nilipo tazamana na baba tukajikuta tukitabasamu ikiashiria ni furaha iliyotawala kati yetu

Geti kubwa likajifungua na mbele yangu kwa mbali kidogo nikaliona jumba kubwa midhili ya ikulu na kuna eneo kubwa lenye kila aina ya kitu cha kuburudika pamoja na bustani kubwa zenye maua ya kupendeza sana
“Karibu nyumbani mwanangu”
Kwa wingi wa walinzi walioo kwenye eneo hili hadi nikaanza kuogopa japo ni baba yangu ila sikujiamini sana juu ya usalama wangu
“Karibu sana nyumbani Eddy”
“Asante baba”

Tukashuka kwenye gari huku macho yangu yakitazama tazama pande zote za sehemu tuliyupo.Mlango wa kuingilia ndani ukafungulia na macho yangu yakakutana na seble inayoendelea kupambwa na wafanyakazi na akashuka mama mmoja wa kizungu kwenye ngazi na kuja kumkumbatia baba kisha akambusu mdomoni na mama huyo akabaki akinishangaa
“Huyu ni nani?”
“Mwanangu”

Mama wa kizungu akanipa mkono kwa dharau kisha akaondoka huku akionekana kukasirika kwa uwepo wangu katika nyumba hii hadi nikajihisi vibaya
“Eddy mwanangu karibu na jisikie upo huru na mwenye amani kwa maana hapa ni kwako”
“Asante baba yangu”
Niliitikia kwa sauti ya kinyonge ila moyoni mwangu nikaanza kuhisi kuna mapambano yatakayo endelea kati yangu na huyu mama wa kizungu.Tukaongozana hadi kwenye chumba kikubwa chenye mali nyingi za dhamani na baba akanikaribisha kwenye moja ya kiti kilicho tengenezwa kihalisi na yeye akakaa kwenye sehemu nyingine

“Una hitaji kinywaji?”
“Hapana”
“Sawa Eddy kwanza ninakuomba unisamehe kwa kile ulicho kiona pale mlangoni”
“Bila samahani kwani yule ni nani?”
“Yule ni mke wangu wa ndoa ambaye nimefunga naye ndoa miaka mitano iliyo pita”
“Aaaahaa sasa mbona ameonekana kuchukizwa baada ya kuniona?”
“Ahaa nahisi hakutegemea kuupata ujio wako leo kwani hata mimi sikuwahi kumuambia kuwa mimi nina mtoto”
“Sawa na yeye ume zaa naye?”
“Hapana na sina mtoto mwengine zaidi yake japo yeye naye ana mtoto wa kike hayupo hapa yupo Johnsburg anasoma chuo”
“Mama yako hivi hajambo?”

“Siwezi kujiu kama hajambo au anaendeleaje kwa maana alikuwa yupo hospitalini na amatekwa?”
“Ametekwa na nani?”
“Ametekwa na baba?”
“Ina maana kaka Godwin anaweza kumteka mke wake?”
“Baba hiyo ni historia ndefu sana,na chanzo kikubwa cha mimi kuja huku ni yeye kwa maana alikuwa amelazwa kwenye ile hospitali uliyo nikuta”
“Duu kweli malipo ni hapa hapa duniani?”
“Kwa nini baba?”
“MAMA YAKO NI KATILI SANA TENA ZAIDI YA SANA JAPO USONI MWEKE NI MWAMA KUPITILIZA”

Maneno ya baba yakanicha mdomo wazi huku nikishangaa nisijue ni kwanini amesema mama yangu ni katili sana

Nikaendelea kumtazama baba kwa macho ya mshangao
“Mama yako ni katili sana kiasi kwamba aliyaaribu maisha yangu kwa kiasi kikuwa....Kipindi ambacho wewe bado hujazaliwa tulikuwa tunapendana sana na kaka yangu na kwajinsi tulivyokuwa tunapenda tuliamini kwamba hakuna kitu amaco kitaweza kutuchonganisha...Ila ninanakumbuka kipindi baba yaka anaingia jeshini mimi nilifeli majaribio kutokana kipindi kile nilikuwa ninaumwa na ugonjwa wa miguu”

“Basi baba yako akaja kukutana na mama yako na kutokana kipindi kile sisi tulikuwa ni fukara sana na wazazi wetu walisha fariki ikabidi kaka ambaye nilisha zoea kumuita kurwa aliniomba nihamie kwa mama yako amaye kwa kipindi kile alikuwa ni daktari ila kwao walikuwa ni matajiri sana kwahiyo swala la pesa kwake lilikuwa ni la kawaida......Nakumbuka ilikuwa ni mwaka 1991 ambapo mama yako alianza kujiingiza kwenye mambo ya vyama kwa maana uchaguzi ulikuwa unaelekea miaka ya mbeleni.....Mambo mengi sana akawa ananishirikisha kama mtu wake wa karibu sana kiasi kwamba ikafikia kipindi tukaanza mahusianao ya kimapenzi pasipo kurwa kujua na yeye kwa kipindi kile ilikuwa ni ngumu sana kuweza kujua ukweli kutokana alikuwa yupo kambini kwenye kambi ya jeshi Morogoro na sisi tulikuwa tunaishi Dar es Saalam”
“Kuseme kweli mama yako alimpenda sana kurwa na mimi alinichukulia kama kituliza nafsi.....Ninazungumza ukweli ili uweze kumjua mama yako vizuri na yale yote aliyo nitendea”
Nikabaki kimya huku nikiendelea kumsikiliza baba hata mat yenyewe mdomoni hayakuweza kupita sikujua ni kwanini

“Basi kipindi alipo gundua amepeta mimba yako na ilipo kuwa na wiki mbili akaanza kutengeneza chuki juu yangu na kipindi kile kwa Tanzania masimu yetu yalikuwa ni yale ya mezani hazikuwepo kama hizi za siku hizi,Alipiga simu kambini na kumuomba kaka kuja nyumbani.Basi baada ya kaka kuja akaanza kuniumiza moyo kwa kufanya mambo yao hadharani huku mimi nikiwashuhudia....... Kitendo cha mama yako kutuchanganya kiliniuma sana na nikaapia ipo siku nitamwambia Kurwa kila kitu kinacho endelea ila kitu ambacho ninakijutia hadi leo ni kwajinsi nilivyo anza kumuambia mama yako kwamba nitamwambia kurwa ukweli wote wa mambo tuliyo yafanya na kipindi hicho tayari ujauzio wake ulisha anza kukua”

“Kitu alicho anza kukifanya mama yako ni kuanza kufanya vitisho vya kutaka kuniua na akaniomba niweze kuondoka Tanzania kama maisha yangu ninayapenda.....Ila kutokana alikuwa na damu yangu tumboni nikawa ninavuta subra niweze kumuona mwanangu amabaye ni wewe....na nililikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke mwengine ambaye alikuwa amenihifadhi na baada ya mama yako kutambua kuwa ninamwanamke mwengine akatua matu na wakatuvamia sehemu ambayo sisi tunaishi na yule mwanamke....Wa...walimuua kwa kumuingiza chupa sehemu zake za siri na kumkata maziwa na kitendo hicho kilifanyika mbele yangu”

Baba akatulia kimya huku machozi yakianza kububujika kiasi kwamba na mimi kwa mbali machozi yakaanza kunilenga lenga
“Na mbaya zaidi yule mwanamke alikuwa na ujauzito wangu wa mwezi mmoja na nusu na akafariki na mwanangu tumboni na mimi wakanichoma sindano ya sumu kiasi kwamba sehemu hii yote ya chini ya mwili wangu ikawa haifanyi kazi,pamoja na kinywa changu kikawa kimepinda kwa na sikuweza kuzungumza kitu cha aina yoyote...Basi ninakumbuka kuna daktari wa kizungu alikuwa ni rafiki yangu sana aliweza kunisaidi na kwake kulikuwa ni huku Africa kusini....basi nilipo muelezea kuhusiana na yaliyo nikuta akaamu kunileta kuhu Afrika kusini ambapo nilifanyiwa upasuaji na ikawalazimu kunikata miguu yote miwili na kutokana yule mzee alikuwa na pesa sana akaamua kunichongeshea miguu ya bandia ambayo ni kama hii unayo iona”

Baba akanifunulia suruali yake na kuiona miguu yake ya chuma ikifanana kama ya mwanariadha maarufu Afrika kusini ambaye naye ana miguu ya namna hii,machozi yakaanza kunimwagika huku yakiambatana na maumivu makali ya moyo.
“Basi nilianza kufanya kazi kwa yule mzee na kipindi anafariki hakuwa na mtoto wala ndugu na mali zake zote aliniridhisha mimi na ndio maana unaniona nina mali nyingi kiasi hichi.....Hayo nileyo kueleza ni machache ila kuna mengi sana ambayo mama yako alinifanyia ila kutaoka upo hapa nitakuwa ninakuadisia kila muda utakavyo kuwa unakwenda”

Baba akatoa kitambaa mfukoni mwake na kunipatia na kuanza kujifuta machozi ambayo yananimwagika na nikabaki nikiwa sina cha kuzungumza kwani sikuweza kuamini kama mama anaweza kumfanyia ukatili mtu aliye mbebea damu yake tumboni.Baba akasimam na kuisogelea meze iliyo jaa mizinga ya pombe kali kisha akachukua mzinga mmoja na akamimina kiasi cha kidogo cha pombe kwenye glasi kisha akapiga fumba moja la pombe hiyo huku akiikunja sura yake akionekana kuwa kitu anacho kinywa ni kikali sana kisha akaviweka mezani na kurudi sehemu aliyokuwa amekaa kisha akashusha pumzi nyingi

“Eddy nilikutafuta sana mwanangu kupitia sehemu mbali mbali hususani mitandano ya kijamii ila kitu ambacho kilikuwa ni kigumu ni kuto kulifahamu jina lako.”
Nikaanza kuyaamini maneno ya baba kuwa mama anaroho mbaya kutokana na jinsi alivyokuwa akimkataa Manka na kutaka kumsweka gerezani kwa kunipiga risasa na kitu kingine nilicho kikumbuka ni maneno ya yule dereva taksi ambaye nilipata naye ajali

“HAAA HUYU MAMA NAYE YUOPO.....KWELI MUNGU HAPENDI DHAMBI KUNA SIKU BWANA ALIKUWA NA DEREVA WAKE SASA KWA BAHATI MBAYA NIKAMCHOMEKEA KWA MBELE ILE BARABARA YA KUINGILIA K.C.M.C NILIKUWA NAMUWAHISHA MGONJWA HOSPITALINI.AHAAAA ALIKWENDA KUNILAZA POLISI HADI SIKU ANAONDOKA ARUSHA NDIO WAKANIACHIA......TENA HAO WATEKAJI KAMA WANAJUA WAMFANYE WA KWANZA KUFA KWA MAANA YULE MAMA ROHO MBAYA SANA”

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI

KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)