SORRY MADAM (55)
JINA: SORRY MADAM Mwandishi: Eddazaria G Msulwa SEHEMU YA HAMSINI NA TANO ILIPOISHIA... Sikujali kama mkono wangu mmoja umevunjika kwa hasira nikamrukia Derick ambaye akanikwepa na kunisindikiza kwa teke kali la mgongoni na kujigongwa kwenye uso kwenye ukuta na kuangukia pembeni ya miguu ya mfanyakazi wa ndani ambaya mkononi mwake ameshika kisu na kitunguu. NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... Nikamuomba mafanyakazi wa ndani kisu kabla hajanipa Derick akauwahi mkono wa mfanyakazi wa ndani ulio shika kisu ikanilazimu na mimi kuuwahi mkono wa mfanyakazi kwa kuutumia mkono wangu mmoja usio vunjika.Derick akatuzidi nguvu na kumshika mfanyakazi wa ndani na kusukumia pembeni na kisu kikaanguka chini.Kabla Derick ajakiokota nikampiga teke na kuifanya miguu yake yote miwili kunyanyuka chini na akaangukia mgongo. Nikajisogeza kwa haraka na kabla sijakiokota kisu akanikanyaga vidole vya mkono wangu wa kulia nilio unyoosha kukiokota kisu.Derick akakipiga kisu mbali …