SORRY MADAM (55)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA HAMSINI NA TANO
ILIPOISHIA...
Sikujali kama mkono wangu mmoja umevunjika kwa hasira nikamrukia Derick ambaye akanikwepa na kunisindikiza kwa teke kali la mgongoni na kujigongwa kwenye uso kwenye ukuta na kuangukia pembeni ya miguu ya mfanyakazi wa ndani ambaya mkononi mwake ameshika kisu na kitunguu.NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
Nikamuomba mafanyakazi wa ndani kisu kabla hajanipa Derick akauwahi mkono wa mfanyakazi wa ndani ulio shika kisu ikanilazimu na mimi kuuwahi mkono wa mfanyakazi kwa kuutumia mkono wangu mmoja usio vunjika.Derick akatuzidi nguvu na kumshika mfanyakazi wa ndani na kusukumia pembeni na kisu kikaanguka chini.Kabla Derick ajakiokota nikampiga teke na kuifanya miguu yake yote miwili kunyanyuka chini na akaangukia mgongo.
Nikajisogeza kwa haraka na kabla sijakiokota kisu akanikanyaga vidole vya mkono wangu wa kulia nilio unyoosha kukiokota kisu.Derick akakipiga kisu mbali kido na eneo ambalo nililo angukia akanipiga teke la mbavu lilinifanya nijikunje huku nikigumia kwa maumivu makali.
“Derick utamuua mtoto wa watu”
Madam Mery alizungumza huku akimwagikwa na machozi na mikpono yake ikiwa imejaa damua na vitu vyeupe vyeupe na kugundua kuwa mwanangu amepasuka kichwa chake.Nikanyanyuka huku meno yangu nikiwa nimeyang’ata kwa nguvu.Nikajaribu kuuyanyua mkono wangu wa kushoto ulio vunjika na kuufanya kuuma kwa maumivu makali yaliyonifanya nitoe ukelel wa kuumia kwani kuna kitu kinanichoma kwa ndani.Derick akayashusha macho yake hadi kwenye mkono wangu kisha akayarudisha machoni mwangu na kwa haraka akanitisha kama ananipiga teke kwenye mkono na kuufanya niukinge mkono wangu kwa kugeuka na kumpa mgongo na kushtukia akininyanua miguu yangu na kuivuta na kuanguka kifudifudi huku mkono ulio vunjika nikiwa nimeulalia
Derick akanikalia mgongoni na kuishika mikono yangu yote miwili na kuivuta kwa nyuma.Maumivu ninayo yapata sikuwahi kuyapata tangu nizaliwe.Madam Mery akauweka chini mwili wa mtoto wetu na kukimbilia sehemu tuliyupo na kumsukuma Derick na akaanguka kwa mbele yangu.Sikuwa na uwezo wa kunyanyuka kuokana na maumuzi makali na kubaki nikilia kwa uchungu.
“Ni binadamyu gani usiye na huruma wewe,umenilia mwanangu kikatili ila bado unataka kumuu huyu kijana wa watu”
“Niliapia ni lazima nimuue huyu kijana pamoja na wewe na leo ndio mwesho wenu”
Derick alizungumza huku akinyanyuka kwa haraka na akamshika madam Mery nywele zake na kumbwaga chini kwa nguvu na kumfanya madam mery kutoa ukulele wa kulia kwa maumivu
“Shemeji mikono yako nyoosha juu”
Niliisikia sauti ya mfanya kazi kwa nyuma yangu na kunifanya nigeuke nyuma na kumkuta akiwa ameshika kisu huku mwili mzima ukimtetemeka.Derick akacheka kwa dharau na kumfwata mfanyakazi kwa kasi na kupiga kabali ya gafla na kumpokonya kisu na pasipo kuwa na huruma Derick akamchoma mfanya kazi wa ndani kisu cha tumbo na kumtupa chini.Derick akanisogelea huku kisu chake kikiwa kinavuja damu za mfanyakazi,akaniinamia na kunitazama kwa umakini huku akicheka
“Nilikuumbia siku nikikutia mikononi mwangu nilazima nikuue”
Maneno ya Derick hayakuhafikiana na moyo wangu kuyakubali kiharaka na kirahisi kama anavyo fikiria.Kwa haraka nikainyanyua miguu yangu kuikaba shingo ya Derick na kwa nguvu zote.Madam Mery akamuwahi kumshika Derick mkono ulio shika kisu na kumpokonya,Kila nilipo kumbuka jinsi mwangu alivyo anguka chini ndivyo jinsi nilivyozidi kumkaba Derick shingo yake ambaye akaanza kunishindilia ngumi za mbavu na akaubana mkono wangu uliovunjika na kuzidi kunifanya niachie ukele mkali
“Madam nisaidieeeeeee”
Madam akabaki akiwa ameshika kisu asijue nini afanye,Nikamuomba tena anisaidie ndipo akastuka kama yupo sehemu ya tukio la hatari,akatutizama tena kwa umakini na kwaharaka kisu akakishusha na kikatua kwenye bega la Derick na kumfanya aniachie na kunyanyuka kama mbogo na kumsukuma Madam Mery ambaye akaangukia mwili wa mtoto wetu na kutulia chini
“Nitaendelea kukusaka”
Derick alizungumza huku akiingia ndani kwa haraka na kutoka akiwa na begi la kuburuza na akanitazama kwa muda kisha akanipiga teke la kichwa na kizunguzungu kikali kikanitawala kikiambatana na giza kubwa lililo tanda kwenye macho yangu na nikatulia tuli
***
Milio ya ndege pamoja na mwanga mkali vikanistua na kujikuta nipo kwenye chumba chene kitanda kimoja tuu.Pembeni ya kitanda kuna meza ndogo pamoja na kiti,Kila ninapojaribu kuitadhimini sehemu hii ninashindwa kujua ni wapi.Mbaya zaidi sehemu hii haifanani na hospitalini kwani kitanda nilicho lala kinaukubwa zaidi ya kitanda cha hospitalini.Nikajichunguza vizuri na kuukuta mkon wangu ukiwa umefungwa bandeji gumu(P.O.P.O).Nikashuka kitandani na kwenda dirishani na kufungua dirisha nikaona migomba mingi nikstukia kwa nyuma mlango ukifunguliwa na akaingia mama mmoja mtu mzima
“Umeamka mwanangu?”
“Shikamoo”
“Marahaba,unajisikiaje?”
“Vizuri tuu”
Akanishika mkono na kuugeuza geuza kisha akanitazama usoni huku akiwa ameachia tabasamu pana
“Mimi ninaitwa Mama Natujwa na hapa ulipo ni Moshi”
“Nimefikaje?”
“Umeletwa na rafiki yangu anaitwa Mery na tangu uje hapa huna hukuwahi kuyafumbua macho yako na ulikuwa ni mgonjwa mahututi sana”
Ikanibidi kurudi kitandani na kukaa kwani niliaza kuhisi kizungu zungu,Mama Natujwa akakaa pembeni yangu huku akinishika shika kichwa changu na kunigeuza huku na huku
“Mimi ni daktari wa mifupa ninamiliki hospitali yangu hapa Moshi,na kipindi Mery alipo kuleta nilikufanyia oparesheni hospitalini kwangu na tukakulaza kule kwa kipindi cha mwezi mzima huku tukikulisha kwa mipira maalumu.Nilipo kuleta hapa nyumbani kwangu tatizo lililo kuwa kubwa ni wewe kurudi katika hali yako ya kawaida”
“Ni kipindi gani kimepita?”
“Unakwenda mwezi wa tatu sasa,Japo Mery alikata tamaa ya kudaidi kuwa huto weza kurudi katika hali yako ya kawaida”
“Na yeye sasa hivi yupo wapi?”
“Yupo Arusha anaendelea na kazi...tena ngoja nimpigie simu nimjulishe kuwa umezinduka?”
Nikamzia mama Natujwa kumpigia simu Madam Mery
“Kwa nini unanizuia?”
“Sihitaji alijue hili sawa”
“Je akija?”
“Nimekuambia sihitaji aweze kugundua jambo hilo”
Akili na wazo juu ya mauaji ya mwanangu likanijia kichwani mwangu,Picha niyingine ya jinsi nilivyo teseka kwenye pango nchini Afrika kusini likanijia kichwani mwangu na sura ya baba yangu mkubwa Mzee Godwin ikanijia kichwani huku ikifwatiwa na sura ya Derick.
“HII KAZI NITAIFANYA MIMI MWENYEWE”
Nilizungumza kwa sauti ya chini na kumfanya mama Natujwa kuniuliza ninasemaje
“Hapana sijazungumza kitu”
Nikaka nyumbani kwa mama Natujwa kwa wiki moja,Nilipo ridhika afya yangu ipo kamili nikamuomba ruhusa ya kuondoka na akanikubalia ila kwa kipindi chote sikumuomba asizungumze chochote kwa Madam Mery,Nikapanda basi hadi Dar es Salaam na sikufikizia nyumbani kwetu nikelekea nyumbani kwa Sheila na kukuta geti lake likiwa wazi na gari yake ikiwa imesimamishwa nje.Nikapata matumaini ya uwepo wake na moja kwa moja nikaufungua mlango wake na sikuamini macho yangu baada ya kumkuta akiwa ananyonyana denda na mwanaume mwengine ambaye kwa haraka nikamtambua ni Derick mume wa madam Mery
Sheila akastuka sana kuniona nikiwa nimesimama mbele yao,hata Derick ambaye mimi na yeye ni maadui kama paka na paya akakastuka sana na wakaachiana.Macho yangu kwa hataka nikayazungusha katika enoe la chini kutafuta kitu kizuri ambacho ninaweza kupambana nacho ila sikuona.Nikatazama nje nikaona kupande cha mbao kilicho chongonga vizuri na kina unene mkubwa kiasi.Nikakifwata kwa haraka na kurudi ndani na kumkumba Derick ambaye alikuwa anakimbilia kuufunga mlango kwa ndani,akaanguka vibaya na kunipa nafasi ya kuanza kumshambulia kwa haraka.Kwa nguvu zangu zote nikakitulisha kipande cha mbao kwenye magoti yake na kumfanya anguke chini akitoa ukulele wa maumivu makali.
Sheila akaanza kubabaika kwani siku zote ananijua nikiwa na hasira ninakuwa ziadi ya mnyama mkali,kwa kutumia kigoti ya mguu wa kulia nikakitulisha kwenye kidevu cha Derick na kumfanya arushwe juu kidogo huku meno kadhaa yakidondoka sakafuni
“EDDY UTAMUUA.....”
“Wewe Malaya funga bakuli lako”
Derick akajaribu kurusha teke,nikalidaka huku nikimtazama kwa hasira.Nikamsukuma na akajigonga kwenye kabati lenye Tv na redio kubwa.Derick akaanza kutokwa na machozi akijaribu kuniomba msamaha ila sikumuelewa kabisa kwa kitu anacho niambia.Kwa kutumia gongo nikaanza kumshambulia kwenye miguu yake,nikitumia nguvu zangu zote kuiamiza kwa kipande cha mbao na kuzidi kumpa maumivu Derick.Sheila akanidandia mgongoni akijaribu kunizuia,Nikageuka na kumshika Sheila kichwa chake na kumtazama kwa macho makali.Nikampiga kichwa kichwa cha uso na kumfamya ayumbe kama tiara,nikampiga buti nililo muangushia kwenye sofa na kuanza kulia kwa maumivu kalali.
Nilipo hakikisha miguu ya Derick haifanyi kazi yoyote,nikaingia jikoni na kuchukua kishoka cha kukatia nyama chenye makali,kabla sijatoka nikaona kamba ikiwa kwenye mfuko.Nikavichukua kwa pamoja na kutoka sebleni na kumuona Derick akijiburuza akijaribu kwenda nje huku akilia.Nikaishika miguu yake na kumburuza hadi alipo Sheila,
“Eddy mpezi wangu,nakuomba unisamehe....nisikilize nakuomba”
Sikuwa na haja ya kumsikiliza Sheila,nikamshika Sheila kichwa chake na nikachukua vipande vya vitambaa vya masofa na kumkandamiza navyo mdomoni na kumfanya ahangaike agaike,Nikamfunga kwenye mikono na miguu.Derick wakati wote anakoroma kwa kulia na maumivu.Nikatoka nje na kulifunga geti na kurudi ndani na kuufunga mlango wa kuingilia
“Sheila naamini mimi kwako si wakusimuliwa,ninaroho ya binadamu na Shetani.....leo nahitaji unijue mimi ni nani?”
Nilizungumza kwa hasira na sauti nzito iliyo jaa mikwaruzo mingi.Nikamshika Derick mkono wake wa kulia,kumbukumbu ya mwanangu alivyompiga chini ikapita kwa haraka kichwani kwangu,nikanyang’ata meno yangu kwa hasira.Nikachukua kishoka na vidole vya Derick nikavilaza sakafuni huku nikivikandamiza kwa kutumia mkono wangu wa kushoto
“No...Usinifa.......”
Nishoka kikatua kwenye vidole vyake na kuvitawanyisha kwenye sakafu,Dericka akatoa ukulele mkali ila nikamzaba ngumi ya shavu na akabaki akigugumia.Sheila akabaki akiwa ameyatoa macho kama amepigwa mshale wa mgongo.Nikavikunyanya vidole vyake vyote na nikaviweka kwenye meza ya kioo.
“Derick leo utakufa kifo cha taratibu kama mwanangu ulivyo mfanya.”
Nikavua tisheti niliyo ivaa,nikaingia jikoni na kuchukua sahani na kurudi nayo ndani sebleni.Nikamfunga Derick akamba za miguu,Nikamsokomeza vitambaa na yeye kwenye mdomo.Nikauchukua mkono wake wa kushoto ulio na vidole vyake kamili.Nikamtazama machoni kwa macho ya dharau,kisha nikaupitisha katikati ya miguu yangu na akabaki akinitazama,Nikaizungusha miguu yangu na kuusababisha mkono kutoa mlio wa kuvunjika mifupa iliyopo kwenye mkono wake.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI
KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Email: ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni