SEHEMU YA NANE
ILIPOISHIA...
“Kwani ni saa ngapi Eddy?”
“Saa kumi na mbili kasoro”
Nikafungua mlango wa chooni nikachungulia nje,nikaona kupo salama hakuna mtu nikampiga busu Salome kisha nikatoka na kuelekee kwangu bwenini kwa ajili ya kujiandaa kwa ajili ya msomo.
NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
Nikamkuta John akiwa bado amelala sikutaka kumsumbua nikapanda kwenye kitanda changu ambacho kipo juu nikajilaza ili kuupuumzisha mwili ila nikakumbuka kuwa nimejikojole.Nikaivua suruali pamoja na boxer yangu japo kuna baridi kali ila ikanilazimu kwenda bafuni kuoga
Nikarudi na kukuta watu wengeni wakianza kuva nguo za darasani huku wengine wakiwa wanaelekea kupiga mswaki
“John vipi hembu amka kwanza?”
“Eddy mwanangu nina umwa?”
“Una umwa na nini?”
“Eddy wee acha tu mwanangu jana yaliyo nikuta nimakubwa”
Kwa jinsi ninavyo mjua John kweli nikagundua anauwmwa kwani hata kuzungumza kwake ni kwa shida
“Sasa nikufanyie mpango kwa Patroni(Mlezi wa kiume) akupeleke hospitali”
“Ndio mwanangu hapa sijielewi kabisa”
Nikavaa nguo za darasani na kwenda katika chumba cha Patron na kumueleza juu ya kuumwa kwa John.Ila Patron akaniomba nimsindikize John hospitali kwani yeye anakwenda kushuhulikia kumtafuta msichana mmoja aliye potea jana usiku.Moyo ukaanza kunienda mbio huku nikiwa na wasi wasi
“Patroni huyo msichana aliye potea ni wakidato cha ngapi?”
“Kidato cha tano”
Sikutaka kujitia mawazo kwani moja kwa moja msichana aliyelala nje ya bweni alikuwa ni Salome na kwa jinsi wasichana wanavyo lindwa huwa huesabiwa kila mara wakati wa usiku nikamuaga Patroni na kutoka kwenda bwenini kumchukua John.Nikaikuta hali yake ikiwa imezidi kuwa mbaya kwani mwili mzima ulikuwa ukimtoka jasho.Nikasaidiana na rafiki zangu wengine kumuwahisha John hospitali huku moyo ukianza kupata mashaka juu ya hali ya John.Tukafika hospitali ya shule akapokelewa na manesi na kumtundikia dripu la maji.
Wezangu wengine wakaenda darasani mimi nikabaki hospitali huku nikiwa na kazi ya kumfuta John jasho linalo mwagika huku wasiwasi ukizidi kunijaa juu ya afya ya John
“Eddy”
“Niambei ndugu yangu”
“Eddy ninakufa kaka”
“John husi kamanda wangu”
John akacheka taratibu huku akinishika mkono huka anatetemeka.Nikazidi kupata wasi wasi huku machozi kwa mbali yakianza kunilenga lenga.Dokta akaanza kumfanyia John vipimo vyote ila hakumkuta na ugojwa wowote
“Eddy jana mwenzako ni….nili…..kuwa nipo na Clau…..”
“Ndio kaka”
“Tulikuwa darasa la kule chini basi kuna ki…..tu ki….linipiga kifuani il…a siku..jua ni ni..ni”
“Ikawaje kaka?”
“Nikaja kukufwata kule ulipo ila sikukupata wakati naru…I pale darajani nikao…….oo….oo..”
Gafla John akaanza kutingishika kama mtu mwenye kifafa huku akiwa amening’ang’ania mkono wangu.Manesi wakaanza kumshika ili kuutuliza mwili wake huku nikisaidiana naye.Machozi yakaanza kunimwagika kwani hali ya John ikazidi kuwa mbaya,Puvu jingi likaanza kumtoka huku puani akiwa anatokwa na damu
“ED…….”
John akajitahidi kuniita ila kinywa chake hakikuweza kufunguka na suati yake ikakata gafla na kunifanya nizidi kuchanganyikiwa.Sikuweza kuyazuia machozi yangu baada ya kumuona John akiwa ametulia kimya kitandani huku vidole vyake vikiwa vinajifungua taratibu kwenye mkono wangu alio ushika.
“John…..John…..John kaka please wake up you can not die brother you my soujar please”(John…..John……John kaka amka huwezi kufa kaka wewe ni mwanajeshi wangu tafadhali)
Nilizungumza huku machozi yakinitoaka nikiwa najitahidi kumtingisha huku kichwa chake kikiwa nimekiweka kwenye mapaja yangu.Dokta akampima John mapigo ya moyo na nikamuona akitingisha kichwa akimaanisha John amefariki dunia
“John amka rafiki yangu nitasoma na nani mimi”
Manesi wanishika na kunitoa nje huku nikiona wakimfunika John kwa shuka mwili wake mzima.Nikazidi kuchanganyikiwa na kujua hiyo ndio safarai yangu ya mwisho ya kumuona rafiki yangu John ambaye kwangu amekuwa zaidi ya ndugu.Manesi wakanikalisha kwenye benchi huku wakiendelea kunibembeleza
Nikaana kundi kubwa la wanafunzi wa kike wa kidato cha tano likija hospitali huku wakiwa wamembeba mwenzao ambaye anaonekana kupoteza fahamu.Nikasimama na kumuona ni Salome aliye bebwa huku akionekana kuwa na hali mbaya kupita maelezo
Nikazidi kuchanganyikiwa sikujua Salome kimempata nini,Nikataka kwenda kumuuliza mmoja wa rafiki zake ila Nesi akanizuia kwa kunishika mkono.Nesi mmoja akaondoka kwenda kusaidiana na wanafunzi wa kike wa kidato cha tano na kumuingiza katika chumba cha wagojwa mahututi.Kila nilipojaribu kuyazuia machozi yangu nikajikuta nikishindwa na nikaendelea kulia hadi wanafunzi wa waliobaki nje wakanifwata kwenye benchi huku kili mmoja akiwa anahamu ya kutaka kujua ni kitu gani kinacho niliza
Nesi akanizuia nisizungumze chochote huku akiwa amenifnga mdomo kwa kiganja chake
“Jamani mwenzenu anaumwa nawaomba mkakae kule”
Nesi alizungumza na kuwafanya mwanafunzi mmoja baada ya mwengine kuondoka katika eneo nililopo kasoro Claudia ambaye anaonekana kuwa na mashaka
“Nesi Maria dokta anakuhitaji haraka”
Nesi aliyeniziba mdomo akanyanyuka haraka na kumfwata nesi mwenzake aliyekuja kumuita nikawaona wakiingia katika chumba alichoingizwa Salome.Claudi akaja kwa haraka hadi sehemu niliyokaa mimi huku naye machozi yakimwagika na akazidi kunichanganya akili kwani sikujua kinacho mliza ni kitu gani
“Eddy Salome anaumwa sana ten asana”
“Ooooh Mungu wangu naye anaumwa na nini?”
“Yaani hata sisi hatujui amekutwa ameanguka nje ya vyoo vipya kule chini huku damu zikimtoka puani”
“Ahaaa Mungu wangu ni nini hichi umefanya John naye amekufa,Salome naye aahaaa……Nakuomba Mungu usiwachkue wote”
“Eddy what are you say…..!?”(Eddy unasemaje……!?)
“John is dead”(John amekufa)
Nilizungumza kwa uchungu huku machozi yakinimwagika yakiandamana na makamasi yakinishuruzika katika pua zangu.Claudia akaachia ukulele mkali a kulia huku akipiga hatua za kwenda walipo wezake huku akiwa anakimbia.Kwa bahati mbaya nikamshuhudia Claudia akikanyaga kamba ya kiatu chake cha shule na kumfanya miguu yake kugongana na kwa kasi kubwa akaanguka chini huku kichwa chake kikipiga kwenye ukingo wa msingi wa baraza ya kuelekea katika chumba alicho ingizwa Salome na kusababisha damu nyingi kuanza kusambakaa chini kwenye mchanga.
Nikanyanyuka kwa haraka na kwenda kumuangali Claudia na kukuta akiwa yupo katika kauli ya mwisho huku akiwa ananiomba msaada nimnyanyue.Kila mwanfunzi aliyekuja katika eneo hilo nikamuoana akiondoka huku akilia na wengine wakiwa wanaziba macho yao wasione kilichotokea kwani ubongo uliochanganyikana na damu ulitapakaa chini huku mimi nikawa kama nimepigwa butwaa.
Madaktari wawili wakaja tulipo simama huku wakishangaa ni kitu gani kimetokea,Mmoja akaniuliza swali ni kipi kilicho mpata Claudia sikuwa na chakumjibu kwani mdomo wangu haukuweza kufunguka.Nikaanza kupata wasi wasi na kwa mwendo wa haraka nikaenda katika chumba cha wagojwa mahututi nikaufungua mlango kwa nguvu na kumstua nesi anayemalizia kumfunika Salome shuka kichwani kwa shukanla kijani….Nesi akajaribu kunizuia huku akiniomba nitoke nje nikajikuta ninamsukuma na kwenda kwenye kitanda alicho lazwa Salome na kumkuta mwili wake umekuwa wa baridi huku macho yake yakiwa yamejifumba.Nikamtingisha huku nikikimuita
“Salome mpenzi na wewe unakufa ni nani atabaki na mimi eheee amka mpenzi tafadhali”
Salome hakunijibu kitu chochote zaidi ya kukaa kimya kama nilivyo mkuta nikarudia kumtingisha ila sikupata jibu.Nikaanza kulia huku nikilitaja jina la Salome
“Salome Salome nakupenda mpenzi wangu yaani penzi letu limedumu kwa masaa please baby amka basi hata nione kicheko chako”
Maneno yangu hayakuwa na nguvu ya kumrudisha Salome dunia,Nikastukia kitu chenye ncha kali kikinichoma mgongoni,nikageuka taratibu na kukuta nesi akichomoa bomba lenye sindano na taratibu macho yakajawa na usingizi na kichwa changu nikakiangushia kwenye kifu cha Salome
***
“Wewe fala Eddy”
Nikastuka huku nikinyanyuka kwa hasira nikitaka nimpige mtu aliye nitukana na kumkuta ni John,Moyo wangu ukanipasuka na kunifanya nianze kurudi nyuma huku nikiwa nina muogopa
“Eddy jana umepiga bao ngapi best hadi umeshindwa kurudi bwenini?”
John aliendelea kunisemesha na kunifanya nizidi kuchanyanyikiwa na kuanza kujiuliza kama nipo peponi mbona John mwenzangu amevaa nguo za shule na sote tupo bwenini isitoshe kama kawaida yake anatukana kiasi kwamba amenikasirisha
“Eddy mwangu saa hizi saa moja kamili wewe bado umelala tena unaota unatupigia kelele za kumtaja Salome wako hapa…….Kumbe Eddy na ujanja wako wote unaweza ukamuota demu?”
Jonh akaanza kucheka huku akinitazama nikayazungusha macho yangu chumba kizima nikamuona John peke yake,Nikajitazama nguo nizizo zivaa nikastuka kuona ni nguo za jana nilizozivaa prepo na sehemu niliyo kaa ni juu ya kitanda changu
“John nipo wapi?”
“Eheee wewe Eddy leo hii unaniuliza upo wapi kwani rafiki yangu wewe unavyohisi au unavyo ona upo wapi wewe?”
“Nina maana yangu kukuuliza nipo wapi?”
“Best upo kwenye Air Force One ya Obama”
John alizungumza huku akizidi kucheka hadi akakaa kwenye kiti kilichopo ndani ya chumba chetu
“Aisee Mzee bado munajichekesha chekesha hapa tokeni nataka kufunga milango”
Patron alizungumza huku akiwa ameshika funguo nyingi kwenye mkono wake wa kushoto
“Patroni tunaomba dakika kumi jamaa avae nguo”
“Nakwenda mabweni ya O level nikirudi nisiwakute”
“Sawa Patron…….Oya Eddy hembu hamsha ke**e zako hapo juu tumeshachelewa assemble”
Nikashuka kitandani na kusimama chini na kusogelea John na kumgusa mkono nikaona ni John kweli kwani hana mabadiliko yoyote ikanibidi kutoka nje kuangalia mandhari nikayakuta ni bwenini na mbaya zaidi nikamuona mwalimu wa zamu akiwafukuza wanafunzi wa vidato vyengine ili wawahi mstarini huku akiwa anawachapa
“Oya John mfumuko huyo anakuja”
“Yuko wapi?”
“Bweni la form four kule”
“Oya mwanangu hembu vua basi hizo nguo zako fasta tuondoke na jamaa lilivyo na mijisifa lile litatucharaza bakora humu humu”
Ikanibidi nikubaliane na hali halisi kuwa John hajakufa nikaanza kuivua surualia yangu haraka haraka huku John akifugua begi langu la nguo na kunitolea nguo za shule
“Alafu Eddy mwanagu umelimwaga eheee?”
“Kwanini?”
“Wewe huoni suruali yako ilivyo chora mchoro hapo mbele sijui ni ramani ya kuendea wapi”
“Mwanangu wee acha tu yaliyonikuta jana mmmmmm……”
“Alafu jana ninakuja kukustua kwenye vyoo kule mwangu upo na huyo demu wako ukanikaushia”
“Unajua wewe ndio chanzo cha kunifanya nirudi hapa saa kumi na mbili”
“Weee umerudi saa kumi na mbili?”
“Ndio jana dogo alizimia”
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI
KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Email: ZephilineEzekiel@Gmail.Com