SORRY MADAM (103)
JINA: SORRY MADAM Mwandishi: Eddazaria G Msulwa SEHEMU YA MIA MOJA NA TATU ILIPOISHIA... "Ila sijajua kama yatatimia tena" "Kwani una umri gani?" "Miaka kumi na saba" "Unataka kusoma?" NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... "Ndio" "Basi tumuombe Mungu" Siku nzima tukashindia kunywa soda, hapakuwa na chakula chakupika. Shamsa akanisaidia kunisafisha majeraha yote mwilini mwangu. Akanipaka dawa nyingine aliyo ichukua kwenye kabati moja humu ndani "Hii inakausha vidonda, haraka. Nakumbuka baba alikua akinipaka hii kipindi nikipata majeraha" "Baba yako alikua anafanya kazi gani?" "Yeye alikua daktari na mama pia alikua dajtari, walikua wakifanya kazi kwenye shirika la msalaba mwekundu , hadi wanakutwa na mauti walikywa wanatoka kazini" "Pole sana" "Asante. Asili yangu mimi ni bara la Asia , ila mama alikua msomali . Walikutana na baba kwenye kazi yao ya udaktari ndipo w…