SORRY MADAM (103)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA MIA MOJA NA TATU
ILIPOISHIA...
"Ila sijajua kama yatatimia tena"
"Kwani una umri gani?"
"Miaka kumi na saba"
"Unataka kusoma?"
NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
"Ndio"
"Basi tumuombe Mungu"
Siku nzima tukashindia kunywa soda, hapakuwa na chakula chakupika. Shamsa akanisaidia kunisafisha majeraha yote mwilini mwangu. Akanipaka dawa nyingine aliyo ichukua kwenye kabati moja humu ndani
"Hii inakausha vidonda, haraka. Nakumbuka baba alikua akinipaka hii kipindi nikipata majeraha"
"Baba yako alikua anafanya kazi gani?"
"Yeye alikua daktari na mama pia alikua dajtari, walikua wakifanya kazi kwenye shirika la msalaba mwekundu, hadi wanakutwa na mauti walikywa wanatoka kazini"
"Pole sana"
"Asante. Asili yangu mimi ni bara la Asia, ila mama alikua msomali. Walikutana na baba kwenye kazi yao ya udaktari ndipo walipo oana."
Shamsa alizungumza mambo mengi juu ya familia yake, hapa ndipo nikatambua hakupaswa kuwa katika hali kama hii. Usiku kucha sikulala, ila Shamsa yeye alipitiwa na usingizi. Nikamlaza vuzuri kwenye sofa. Nikaanza kukagua picha moja baada ya nyingine. Zilizo bandikwa kwenye kuta za seble hii. Nyingi ni za Shamsa alizo piga na wazazi wake. Nikaingia kwenye vyumba vinee vilivyopo humu ndani, vyote nikakuta vina usalama wa kutosha na hapakuwa na mtu aliye jificha kama, hisia zangu zilivyo kua zikinituma.
Asubuhi kulivyo pambazuka, nikamuamsha Shamsa, akaingia bafuni kuoga na kuvaa nguo nyingine. Alizo dai ni za mama yake, kwani zakwake zilikua ndogo kwake. Tukachukua kila kilicho chetu, tukaondoka na kwenda mjini talipo makao makuu ya umoja wa mataida kwenda kuitazama familia yangu. Ikatuchukua takribani masaa manne kufika Mogadishu, tukaingia kwenye moja ya hoteli. Tukala chakula, kuyaweka matumbo yetu sawa kisha tukaendelea na safari yetu
"Eddy kwenye hayo masañduku kuna nini?"
"Pesa"
"Pesa!!?"
"Ndio"
Ilimlazimu, Shamsa kushangaa, kwani sikumueleza chochote kuhusiana na pesa hizo. Akasimamisha gari pembeni, kutokana yeye ndio dereva tangu mwanzo wa safari, kutokana na yeye kuwa mwenyeji katika nchi hii.
"Pesa za nchi gani?"
"Marekani"
"Mmmm itabidi, tutafute sehemu tuzihifadhi"
"Kwanini?"
"Endapo tutakamatwa nazo, zitachukuliwa na serikali, na sisi tutaingia mikononi mwa jeshi la polisi kwa ajili ya mahojiano"
"Sasa itakuaje?"
"Hata mimi sijui kwani, tunapo kwenda nilazima tukaguliwe, ili kuruhusiwa kuingia kwenye hiyo kambi ya wakimbizi, inayo lindwa na wanajeshi wa umoja wa mataifa"
Ushauri wa Shamsa ukaniingia kisawa sawa akilini mwangu. Nikabaki nikiwa nawaza ni wapi kwa kuziweka hizi pesa kutokana ni nyingi sana, japo sijazihesabu. Nikafikiria nimtafute Smith, anisaidie katika hili, ila pesa haina urafiki na anaweza kunibadilikia, ikawa ni tatizo jengine.
"Kuna benki ya bacrayse hapa?"
"Ndio, imefunguliwa wiki mbili za nyuma"
"Nipeleke"
Tukaghairi safari, Shamsa akageuza gari na kunipeleka kwenye banki ya Bacrayse. Nikaingia na masanduku yangu, huku nikiwa ninajiamini. Tukafika mapokezi kabla sijazungumza kitu nikastukiwa nikiguswa bega kwa nyuma. Nikageuka na kukutana na sura ya Madam Mery, akiwa amevalia suti yeusi huku akiniwekea tabasamu pana usoni mwake.
"Za masiku mengi Eddy"
Alianza kunisalimia, nikabaki nikiwa nimemkodolea macho nisgindwe kumjibu chochote. Nikameza fumba zito la mate huku Shamsa akibaki akinitazama.
"Eddy"
"Mmmmm za kwako"
Nilimjibu huku nikijenga tabasamu la kinafki usoni mwangu.
"Bosi kile kikao kimebakisha dakika kumi na tano kabla hakijaanza"
Muhudumu mmoja wa kike aliye valia sare, pamoja na kitambulisho cha benki hii, alimuambia Madam Mery.
"Sawa, kisogeze muda nina mgeni muhimu hapa wakuzungumza naye"
"Sawa madam, nisogeze muda kiasi gani?"
"Fanya lisaa"
Mfanyakazi huyo aliondoka, madam Mery akaniomba twende ofisini mwake. Nikamtazama Shamsa, akakubali tuongozane naye, pasipo kujua ni uadui gani uliopo kati yangu na Madam Mery ambaye kidogo umri umesha anza kumsogea. Tukaingia ofisini kwake, na kukaa kwenye viti vilivyopo kwenye ofisi yake, yenye kibao kidogo kilichopo kwenye meza yake ya kisasa kilicho andikwa, 'Chief Exacutive Mery J.Shirima'
Inamaana yeye ni meneja mkuu, wa benki hii. Madam Mery akanitazama kwa muda, huku akikoaa cha kuzungumza, taratibu nikaanza kukichomoa kisu changu kilichopo kwenye soksi ya mguu wa kushoto, kwa ajili ya kuikata shingo ya madam Mery aliye, nifanyia ukatili mkubwa, akishirikiana na washenzi wezake John na Victoria.
Shamsa akanishika mkono, ulio kua ukichomoa kisu kutoka katika soksi. Akanikonyeza huku akinionyesha camera ya ulinzi, iliyopo kwenye moja ya kona ya ukuta wa ofisi hii. Nikakirudisha kisu nilipo kitoa. Nikabaki nikimtazama madam Mery kwa macho makali, yaliyo jaa hasira.
"Eddy ninatambua kwamba una hasira na mimi"
Madam Mery alizumgumza na kukaa kimya huku, akiyakwepesha macho yake kutazamana na macho yangu.
"Sikupenda kufanya kile walicho kufanyia John na nwenzake. Roho yangu iliniuma sana pale nilipo sikia kwamba umekufa."
Madam Mery alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake. Shamsa akasimama na kupiga hatau hadi mlangoni.
"Eddy nipo nje ninakusubiri"
Nikamuitikia Shamsa kwa kutingisha kichwa kumuashiria kwamba nimekubali yeye kutoka nje ya ofisi. Madam Mery akatoa kitamba kwenye pochi yake na kujifuta machozi yaliyo tapakaa usoni mwake.
'Huyu mnafki kweli"
Nilijiseme kimoyo moyo huku nikimtazama madam Mery usoni mwake.
"Eddy moyo wangu ulikosa amani, nilijaribu kutafuta japo kaburi lako, nije nipige magoti nikuombe msamaha"
"Ila sikuweza kufanikiwa katika hilo, ila nilikuka kupta amani pale nilipo kuon kwenye tangazo la magari, ndipo nilipo tambua kwamba upo hai"
Madam Mery alizumgumza huku alinyanyuka kwenye kiti chake na kuja nilipo. Akapiga magoti chini, na kuushikilia mguu wangu wa kulia, huku aliendelea kulia kwa uchungu.
"Eddy ninakupenda sana, ndio maana nilikupa nafasi ya kuishi tena duniani"
"Nakuomba unisamehe, ninakuomba unipe nafasi ya msamaha wako, ili niweze kuishi kwa amaani"
Suti ya uchungu, na yamajozi ya Madam Mery ikaanza kuilainisha hasira yangu, iliyo ganda kama barafu. Nikamnyanyua na tukasimama, akanikumbatia kwa nguvu huku akiendelea kutoa kilio cha kujutia makosa aliyo yafanya. Japo hasira bado inanisukuma niweze kumfanyia madam Mery jambo la ukatili, ila nikazidi kujitahidi kuweza kuepukana na kufanya tukio lolote baya.
"Eddy nisamehee'
Madam Mery aliendelea kuzungumza huku akilia kwa uchungu.
"Ni...mekusamehe"
Nilijitahidi kukifungua kinywa changu, kujibu nilicho mjibu Madam Mery, japo muda sote kinatetemeka kwa hasira kali. Taratibu Madam Mery akaniachia, na kunitazama machoni mwangu. Tukabaki tukiwa tumetazamana kama dakika tatu, hisia kali ya mapenzi iliyo pelekea kuyakumbuka matukio kadhaa ya nyumà dhidi ya penzi letu, na madam Mery. Zikanifanya mwili mzima kusisimka, taratibu ñikaupelekà mdomo wangu, ulipo mdomo wa Madam Mery ila akaukwepesha usikutane na mdomo wangu.
"Eddy sio sasa"
Madam Mery akanichia na kurudi, kilipo kiti chake, nikabaki nikiwa nimemtazama kwa mAcho yaliyo jaa matamanio mengi.
"Umetuletea pesa nini?"
"Eheee!"
Nilibaki nikiwa nimemshangaa Madam Mery, huku hisia za mapezi, zikiupelekea mwili wangu kuishiwa kabisa na nguvu. Taratibu nikakaa kwenye kiti changu.
"Eddy sio kwa sasa, hiyo kamera hapo juu ukutani inarekodi kila kitu kinacho endelea humu ndani."b
Madam Mery alizungumza huku, akinionyeshea kamera iliyopo ukutani.
"Ni pesa ulizo beba?"
"Eheeee"
"Una akaunti ya benki hii?"
"Ndio"
"Hembu nitajie"
Nikamtaji madam Mery namba ya akaunti yangu, akaiingiza kwenye computer iliyopo hà pa mezani mwake. Baada ya muda akanigeuzia kioo cha çumputer hii, aina ya 'DELL'. Nikaona taarifa za benki yangu, ikiwemo picha na jina langu kamili.
"Ila inaonyesha kwa Tawi la Tanzania umefungiwa, kwa nini?"
"Ahaaa ni mama, ndio alinifungia"
"Sawa, ngoja nimpigie simu muasibu"
Akampigia simu muasibu wake kwa kupitia simu ya mezani. Tukiwa tunamsubiri muà sibu madam Mery akanipatia kokadi chenye namba ya simu yake.
"Mimi nitakwenda kwenye kikao, kama utaondoka pasipo kuonana na mimi basi utanipigia kuniambia ni wapi ulipo"
"Sawa"
Akaingia jamaa mrefu, mweusi kiasi aliye valia suti, nikatoka naye ofisini na kwenda kwenye chumba chenye mashine za kuhifadhia pesa.
Zoezi la kuzihesabu pesa likaanza, halikuchukua muda sana tukawa tumepata kiwango cha pesa ambacho ni dola za kimarekani milioni saba. Sawa na bilioni kadhaa kwa pesa ya tanzani. Nikatoa dola laki moja na nyingine zilio salia zikaingizwa kwenye akaunti yangu.
"Eddy hatuwezi kwenda kwenye kambi ya wakimbizi muda umesha pita"
Shamsa alizungumza huku tukitoka kwenye mlango wa benki.
"Kwani ni saa ngapi sasa hivi?"
"Saa tisa mchana na muda wa kuingia pale, ni kuanzia saa nne asubuhi hadi saa nanechana"
"Sasa itakuaje?"
"Ni hadi kesho"
"Nasi tutafute sehemu ya kulala"
"Sawa, ila kama ukihitaji iwe rahisi sisi kuingia ndani mwa kambi tunaweza kununua vitu kama mifuko ya mchele, sabuni, mafuta ya kupikia. Tukifika pale tunawaambia sisi tunatoa msaada"
"Wee dogo una akili sana"
Kila wazo alilo litoa Shamsa, sikulipinga. Tukaanza kazi ya kutafuta alivyo sema. Ikatulazimu kununua na nguo ambazo zitatufanya tuonekane kweli ni watoaji msaada. Ikatulazimu pia kununua gari, jengine aina ya pickup lililo tuwezesha kubeba mizigo hiyo. Tukakodi vyumba viwili kwenye hoteli moja kubwa yakitalii, iliyopo katikati ya mji wa Mogadishu, ambapo usalama wake kidogo ni wa uhakika
Mida ya saa mbili, usiku nikampigia simu madam Mery simu, nikamuelekeza sehemu nilipo. Akaniambia nimpe dakila kadhaa atafika sehemu tulipo.
"Una uhakika utalala naye?"
Shamsa aliniuliza swali mara baada ya kuksta simu.
"Kwa niki umeuliza hivyo?"
"Kwa maana yule mama nina mjua vizuri sana"
"Ana nini?"
"Ni mke wa waziri wa fedha hapa nçhini. Na mumewe ni mmoja wa watu hatari hapa Somalia"
"Nisinge penda kukuona unajiingiza kwenye matà tizi ambayo hayakuhusu. Wewe kwa sasa jaribu kuiangalia familia yako"
Shamsa alizungumza maneno, yaliyo nifanya nibaki kimya nisijue nini cha kujibu.
"Usiku mwema nakwenda kulala, ila nilicho kueleza kiweke akilini. Tutaonana asubuhi"
Shamsa akanyanyuka, kitandani mwangu, akapiga hatua hadi mlangoni akafungua na kutoka. Nikabaki nikiwa nà msongo wa mawazo, nikiiwazia familia yangu. Kijiusingizi kikaanza kunipitia taratibu, kila nilipo jaribu kuitazama saa ya ukutani, masaa yalizidi kuyoyoma pasipo Madà m Mery kutokea.Mida ya saa sifa usiku, nikasikia mlango ukigongwa taratibu.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI
KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Email: ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni