SORRY MADAM (104)
JINA: SORRY MADAM Mwandishi: Eddazaria G Msulwa SEHEMU YA MIA MOJA NA NNE ILIPOISHIA... Shamsa akanyanyuka, kitandani mwangu, akapiga hatua hadi mlangoni akafungua na kutoka. Nikabaki nikiwa nà msongo wa mawazo, nikiiwazia familia yangu. Kijiusingizi kikaanza kunipitia taratibu, kila nilipo jaribu kuitazama saa ya ukutani, masaa yalizidi kuyoyoma pasipo Madàm Mery kutokea.Mida ya saa sifa usiku, nikasikia mlango ukigongwa taratibu. NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... Nikanyanyuka, nikiwa nimeishika bastola yangu, iliyopo chini ya mto. Nikasimama pembeni ya mlango. "Nani?" Niliuliza kwa sauti ya chini, ambayo mtu aliyopo nje ya chumba ataisikia vizuri. "Mery" Ilikua nisauti ya Madam Mery nikashika funguo, iliyopo kwenye kitasa nikaizungusha tatatibu, huku nikiwa makini kwa lolote litakalo jitokeza. Nikaufungua mlango, nikakuta Madam Mery akiwa amevalia baibui jeusi, bila ya salamu kaingia ndani. Nikachungulia nje kwenye kordo, hapakuwa na…