SORRY MADAM (105)
JINA: SORRY MADAM Mwandishi: Eddazaria G Msulwa SEHEMU YA MIA MOJA NA TANO ILIPOISHIA... Japo sifahamiani naye, na wala sina kumbukumbu ni wapi nilionana naye. "Jamani huyu ndio yule jamaa aliye okoa familia ya balozi wa Marekani nchini Afrika kusini." Wanajeshi wengine wakaanza kutabasamu na kunipa mikono ya pongezi hata wale walio nisemesha kwa kifaransa, wakazungumza kingereza japo, kifaransa ninakijua kidogo. NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... Nikatoka na mkubwa wao aliye jitambulishwa kwa jina la Jonson, tukafika lilipo gari letu. Tukapanda wote watatu. Tukaingia getini, bila ya kukaguliwa kutokana tupo na mkubwa wao huyo mwenye nyota tatu begani mwake. Tukafika sehemu ya kitengo cha wanao pokea misaada, inayo letwa ndani ya kambi hiyo. Tukatambulishwa, na kuwakabidhi misaada yetu. Nikawaomba waniangalizia jina la Junio na Phidaya, katika orodha ya wakimbizi walio pokelewa kipindi cha hivi karibuni. Mama anaye husika na kutunza kumbukumbu …