SEHEMU YA MIA MOJA NA TANO
ILIPOISHIA...
Japo sifahamiani naye, na wala sina kumbukumbu ni wapi nilionana naye.
"Jamani huyu ndio yule jamaa aliye okoa familia ya balozi wa Marekani nchini Afrika kusini."
Wanajeshi wengine wakaanza kutabasamu na kunipa mikono ya pongezi hata wale walio nisemesha kwa kifaransa, wakazungumza kingereza japo, kifaransa ninakijua kidogo.
NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
Nikatoka na mkubwa wao aliye jitambulishwa kwa jina la Jonson, tukafika lilipo gari letu. Tukapanda wote watatu. Tukaingia getini, bila ya kukaguliwa kutokana tupo na mkubwa wao huyo mwenye nyota tatu begani mwake.
Tukafika sehemu ya kitengo cha wanao pokea misaada, inayo letwa ndani ya kambi hiyo. Tukatambulishwa, na kuwakabidhi misaada yetu. Nikawaomba waniangalizia jina la Junio na Phidaya, katika orodha ya wakimbizi walio pokelewa kipindi cha hivi karibuni. Mama anaye husika na kutunza kumbukumbu za majina ya wakimbizi, akawasha computer iliyopo ndani ya ofisi hii. Akaandika jina la Junio
"Junio nani?"
"Junio Eddy"
"Yeah wametokea saba hapa"
Aliniita na kunionyesha majina hayo ya kina Junio Eddy yakiwa saba yamejipanga vizuri.
"Hembu andika jina la Phidaya"
Akaandika haraka, ila computer, ikaonyesha hakuna jina kama hilo. Nikajaribu kuandika mwenyewe ila pia jibu likawa ni moja, kwamba Phidaya hayupo, kwenye orodha hiyo.
Tukaondoka kuelekea kwenye mahema ambayo, wanaishi wakimbizj na pis tunaweza kuwapata Junio, hema la kwanza, tukakuta Junio huyo ni mtu mzima, mwenye umri zaidi yangu. Kila Junio tunaye onyeshwa si mwanangu, kwani wote wamezidi umri wa Junio wangu. Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio, baada ya Junio sita nilio onyeshwa na sio mwanangu. Tukafika kwenye hema ambalo walidai tutampata Junio huyo mwengine waliye nieleza ni mtoto mdogo.
Tukakuta watu wengi kiasi wakiwa wamekusanyika nje ya hema hilo, huku wakiwa na huzuni machoni mwao. Muhudumu mmoja kati ya wanne tulio ongozana nao, akamfwata muhudumu, anaye onekana ni daktari aliye kuwepo nje ya hema hilo akizungumza na watu. Waka non'gonezana, na daktari huyo akatutizama, kisha akawaomba watu wanao msikiliza, wamsubiri kidogo azungumze nasi.
"Huyu ni dokta Martin, ndio mganga mkuu wa hii kambi"
Jamaa, alitutambulisha kwa dokta huyo, mwenye asili ya Uingereza na anaumri mkubwa kiasi.
"Walikua wakimuulizia Junio Eddy"
Dokta akakaa kimya kidogo, huku akinitazama machoni, Shamsa akanishika mkono wa kulia vizuri, kutonana na yeye kuchoka kwa kuzunguka kwenye kambii hii kubwa, huku jua kali likituchoma, ipasavyo.
"Ohhh Junio Eddy, tunetoka kumzika masaa mawili ya nyuma"
"Nini doktar?"
Mstuko wangu, uliwafanya hata watu walio kua wakimsikiliza doktar huyo kunigeukia mimi.
"Ndio, tulimkuta na maambukizi ya ugonjwa wa Ebola, na yeye ndio mtu wa kwanza kuugua ugonjwa huo ndani ya kambi hii. Na hapo nilikua nikitoa mafunzo kwa watu wengine endapo wataona mtu mwenye dalili hizo watufahamishe haraka iwezekanavyo."
Sikuweza kuyazuia machozi yangu kunimwagika, Shamsa akawa wa kwanza kunikumbatia kwa nguvu huku akinibembeleza.
"Mwanangu amekufa kabla sijamuona"
"Hapana Eddy ni kazi ya Mungu, jikaze usilie mbele za watu"
Shamsa alizungumza huku, akinibembeza, Shamsa akanishika mkono, tukaondoka huku nikimuacha Jonson akizungumza na daktari huyo pamoja na wahudumu, tulio kuja nao, wakionekana kustushwa na ugonjwa huo ambao ni hatari sana duniani.
"Eddy jikaze, wewe ni mwanaume. Usilie kila mmoja akajua unamatatizo"
Shamsa aliendelea kunifariji, huku tukizidi kutembea kurudi getini. Kundi kubwa la watoto, wenye umri kama miaka kumi hivi, tukalikuta limekusanyika kwenye moja ya mti, huki wakishangili watoto wawili wanao rushiana makonde. Nikajifuta machozi na kwenda walipo watoto hao, nikapita katikati yao, na kumkuta mtoto mmoja akiwa amelazwa chini, na mwenzake amwe nguvu kumpita yeye.
Nikawatennganisha, nikamnyanyua mtoto aliye chini, ambaye sura yake kidogo imevimba, kutokana na kichapo hicho.
"Musipigane sawa, watoto wazuri"
Nilijikaza tu, kuzungumza hivyo. Sikutaka kuwataza machoni watoto hawa, ili wasigundue kwamba ninalia. Nikapita kati kati yao, nikabaki nikimshangaa Shamsa, akiwa ameduwaa, akiwatazama watoto hao.
"Shamsa twende"
"Eddy ngoja"
Shamsa alizungumza, huku akipiga hatua akipita katikati ya watoto hao. Akamfikia yule aliye pigwa, anaye onekana kuvimba sura yake. Akamtazama vizuri, kisha akanitazama na mimi.
"Eddy"
"Mmmm"
"Huyu ni mwanao"
Shamsa alizungumza, huku akimtazama mtoto huyo, niliye anza kumtazama kwa umakini.
"Mtoto unaitwa nani?"
Shamsa alimuuliza mtoto huyo, ambaye na mimi nikaanza kupata mashaka naye, japo sura yake imevimbishwa kwa ngumi za mwenzake na kuifanya iumuke kiasi, ila anafanana kidogo na mimi.
"Jack"
Kulitaja jina la Jack, maumivu ya kufiwa na Junio wangu yakarudi upya, kwani hakuwa Junio wangu.
"Jack nani?"
"Mama hajaniambia baba yangu anaitwa nani"
"Mama yako, yupo wapi?"
"Yupo kule, ninapo kaa"
"Twende ukatuonyeshe"
Shamsa akamshika Jack mkono na kuongozana naye.
"Eddy twende, umashangaa nini?"
Shamsa aliniambia kwa sauti ya chini, nikawafwata kwa nyuma, huku nikimchunguza vizuri mtoto huyu kwa nyuma. Sikutaka kuwema asilimia mia kwamba ni mwanangu, kwani tayari amesha nichanganya, kwa jina lake la Jack. Tukaona moshi mwingi, ukienda juu. Ukitokea kwenye mahema ya mbele yetu, Jack akajichomoa mikononi mwa Shamsa na kuanza kukimbia kuelekea moto ule unapo tokea. Ikamlazimu, Shamsa naye kumkimbiza kwa nyuma, mimi sikuwa na hata nguvu za kukimbizana nao, zaidi yakuwafwata kwa nyuma. Wakawahi kufika kwenye mahema yanayo ungua kwa moto. Nikafika na kumkuta Jack akilia huku akimuita mama yake, ambaye anahisi yupo ndani ya hema hilo. Huku watu wengine wakiendelea kuzima moto kwa kutumia mchanga, kwani hapakuwa na moto wa kufanyia hivyo.
"Jack, Jack"
Sauti ya msichana, ilisikika nyuma yangu, kabla sijageuka, kumtazama dada huyo nikajikuta nikipigwa kikumbo kwa nyuma, dada huyo akanipita na kukumbatia na Jack, huku dada huyo akinipa mgongo, na sikuiona sura yake. Tukabaki tukitazamana na Shamsa, huku mimi nikiwa sina la kuzungumza.
"Ulikuwa wapi mwanangu"
Sauti ya dada huyu, ikazidi kunipa ushawishi wa kutaka kumgeuza, ili kuiona sutmra yake kwani inaendana na sauti ya Phidaya, japo imejaa mikwaruzo mingi, kama mtu ansye ugua kifua kikali.
"Nilikua na hao hapo.'
Jack akanyoosha kidole kwangu, na kumfanya mama yake anigeukie. Phidaya, akanitazama kwa mshangao mkubwa, huku machozi yakianza kumlenga lenga. Kukondeana kwa Phidaya, kumembadili sana, muonekano wake. Mashavu yake yameingia ndani, akionekana kukosa lishe bora kwa muda mrefu. Mavazi aliyo yavaa, yanechakaa, sana na yanazidi kumuonyesha anamatatizo mengi, nywele zake za ndefu, zimejaa masponji mengi, ya godoro alilo lalia. Kiufupi Phidaya amechakaa sana kwa shida alizo pitia.
Taratibu Phidaya akasimama, akanisogelea huku machozi yakimwagika. Nikataka kumkumbatia, ila akanizuia, nisifanye hivyo.
"Phida.."
Kofi zito kutoka kwa Phidaya likatua shavuni mwangu, lililo mfanya Shamsa kustuka. Phidaya akaachia msunyo mkali na kumshika mkono Jack.
"Junio tuondoke"
Phidaya alizumgumza kwa hasira, na kuanza kuondoka na mwanaye, wakijichanganya katikati ya watu walio kusanyika hapa.
Sikuhofia kukatiza katikati ya watu, kuwafwata Phidaya na mwanagu Junio. Furaha moyoni nwangu ikawa imezaliwa upya kuiona familia yangu. Iliyo nigharimu maisha yangu katika kuitafuta hadi leo kuitia machoni kwa mara ya pili, ukiachilia siku ya kwanza Junio alivyo zaliwa mbele ya macho ya watu wengi akiwemo Shatani John na Victoria.
"Phidaya, Phidaya"
Nilimuita Phidaya niliye mkaribia, kumfiki. Akasimama na kunitazama kwa macho makali sana, yaliyo jaa hasira huku machozi yakimwagika taratibu.
"Unakwenda wapi mke wangu, kumbuka nimehangaika kwa ajili yako, nimejitolea maisha yangu kwa ajili yako na mwanangu. Kwa nini unanikasiriki, kosa langu ni nini haswa?"
Nilizungu huku machozi yakianza kunitiririka.
"Nimekua muuaji kwa ajili yako, nimefanya kila niwezalo kufanya kwa ajili yako, ila umaona yote hayana dhamani si ndio?"
"Eddy nyamaza. Nilikuomba usioe, ila kwa nini ulioa. Umeniacha nahangaika, naishi maisha ya kitumwa na mwanangu. Tumekua watu wa kubadilisha majina kwa ajili yako. T...."
"Phidaya mimi sijaoa mwanamke yoyote, nilijitoa kufa na kupona kuwakomboa nyinyi mukiwa kwenye maroli kwenda kuuzwa nchi za nje. Nimefanya kosa?"
"Eddy acha uongo, haukuwa wewe, uliye tuokoa, Umemuoa mwanamke aliye nidhalilisha na kuniita mimi malaya, mimi?"
"Phidaya, achana na hayo maneno. Njoo tukamlee Junio. Twende tukaishi kwa amani na upendo. Unatambua ni mazingira gani ulimzaa Junio, huku na mimi nikiwa kwenye tabu gani."
"Junio sio mwanao, ni mwanangu peke yangu. Junio twende zetu"
Phidaya alizungumza huku akimshika mkono Junio, na kumvuta waondoke ila Junio akagoma kwenda popote.
"Mama uliniambia mtu, akiniuliza baba yangu ni nani, nimuambie simjui. Ila Eddy ni baba yangu, mara ngapi ulikua ukimpigis simu. Anamapenzi ya dhati na sisi. Mama nimechoka kuishi maisha haya ya ukimbizi. Mpe baba nafadi yake, aonyeshe ni jinsi gani anavyo tupenda."
Japo Junio kiumri ni mdogo, ila maneno aliyo yazungumza huku akilia yakanifanya mwili wangu kusisimka. Phidaya akamtizama Junio kwa macho ya mshangao, kisha akanitazama na mimi.
Nikafungua vifungo vya shati langu, nikakivua na kumpa Shamsa anishikie.
"Majeraha yote haya, nikwaajili ya kuiokoa familia yangu. Mwili wangu haukua na dhamani juu ya kuziokoa nafsi zenu. Msikilize anacho sema mwanao. Anahitaji malezi yetu sote. Tafadhali mke wangu, rudi mikononi mwangu au unataka mwanangu aendelee kuishi maisha haya ya shida. Tazama jinsi sura yake ilivyo umuka kwa kupigemwa na wezake. Je unataka awe hivi kila siku?"
Nilizungumza kwa uchungu, huku nikipiga magoti chini, sikujali ni idadi ngapi ya wagu walio tuzunguka wakitushangaa. Junio akamshika mkono mama yake.
"Mama, unanifundisha niwe mpatanishaji kwa walio gombana. Mshike baba mkono anakupenda"
Phidaya aliendelea kulia kwa uchungu, sura yake yote ikabadilika na kuwa na uwekundu fulani, kutokana na kulia kwa uchungu sana.
"Nakuomba mama, patana na baba anakuhitaji bado"
Maneno ya Junio yakamlainisha Phidaya. Taratibu Phidaya akarudi sehemu niliyo piga magoti, na yeye akapiga magoti chini, huku akilia. Kwa nguvu akanikumbatia. Nikamvuta Junio wangu, naye nikamkumbatia huku sote machozi ya furaha yakitumwagika. Watu walio tuzunguka wakaanza kupiga makofi, yafuraha. Shamsa akabaki akinikonyeza huku akitabasamu.
"Nakupenda mume wangu"
"Nawapenda wote"
Tukaendelea kukumbatiana kwa furaha.
"Eddy muda"
Shamsa alininong'oneza baada ya kuona tunakumbatiana sana.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI
KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Email: ZephilineEzekiel@Gmail.Com