SORRY MADAM (107)
JINA: SORRY MADAM Mwandishi: Eddazaria G Msulwa SEHEMU YA MIA MOJA NA SABA ILIPOISHIA... Nikasubiri kama dakika tano, mwili kidogo ukapata nguvu za kutembe. Nikamshukuru mlinzi, nikavuka barabara na kwenda kwenye duka nilipo waagiza Phidaya awachagulie wanae viatu. Nikawakuta wakiendelea kuchagua chagua viatu wanavyo vipenda. "Mbona umelowa kichwani?" NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... Phidaya aliniuliza huku akinigusa gusa kichwani mwangu. "Kichwa kidogo kilikua kinaniuma, ndio nikanawa kichwani" Ilinibidi kumdanganya Phidaya kwa maana vita yangu na John, nitaka niimalize mimi nwenyewe japo Phidaya naye alihusika katika mateso yote tuliyo sababishiwa na John. "Hiii damu nayo imetoka wapi?" Aliniuliza huku akinishika kwenye kifua changu akinionyesha matone kadhaa ya damu. "Dady hapo je, nimependeza?" Junio alisimama mbele yetu, huku akiwa amevalia viatu aina ya Supra , huku akiwa ameshika miwani iliyo endana na viatu ali…