SORRY MADAM (108)
JINA: SORRY MADAM Mwandishi: Eddazaria G Msulwa SEHEMU YA MIA MOJA NA NANE ILIPOISHIA... "Ehee niambie zile damu ulizitoa wapi?" "Tutazumgumza kitandani" "Sawa" Tukamaliza kuonysha vyombo na kuvipanga vizuri, tukawaaga watoto wetu na kuingia chumbani wao wakaendelea na mambo wanayo yafanya. NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... Phidaya akapitiliza bafuni kuoga, baada ya muda akarudi na kujirusha kitandani. "Nasubiria hayo mazungumzo" Nikashusha pumzu huku nikimtazama Phidaya anaye hitaji nimuambie ni nini kilicho nikuta. "Nina tatizo mke wangu" "Tatizo! Tatizo gani?" "Kipindi fulani nilipo kua Afrika Kusini nilifanyiwa uchunguzi na kubainika nina ugonjwa wa hasira ambao, nikikasirika sana damu puani hua zinanitoka, pamoja na mwili kushikwa na kizungu zungu" Nilimfinya Phidaya juu ya ugonjwa wa saratani(Canser), ambao niligundulika unaninyemelea. "Mmmm leo ni nini kilicho kukasirisha?" Ni…