SORRY MADAM (110)
JINA: SORRY MADAM Mwandishi: Eddazaria G Msulwa SEHEMU YA MIA MOJA NA KUMI ILIPOISHIA... Tukamaliza mazungumzo, nikaondoka na kuingia chumbani kwetu, nikafanya maandalizi ya kulala, baada ya muda Phidaya akaingia na kukaa kitandani "Baby ni kazi gani inayo kufanya ubaki huku peke yako" NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... Phidaya aliniuliza kwa sauti ya upole, huku akinichezea chezea kifua changu. "Yakumuua John" "Kumuua John!!?" "Ndio, nimemuona leo, na ninatambua anapo ishi." "Sa..sa sasa itakuwaje akituona, si atatuua?" "Kwa sasa hawezi kuniua" Nikaanza kumuadisia Phidaya kuanzia mipango ya harusi ilivyo pangwa, hadi kuuawa kwa Ftedy. "Kwahiyo wanaamini wewe umekufa?" "Ndio maana yake, nahitaji mutangulie nyumbani mimi niimalizie kazi hiyo ya kumuua yeye kwa mkono wangu." "Eddy kuwa makini, sihitaji kukupoteza katika hili" "Usijali mke wangu, nipo makini tena sana"…