SORRY MADAM (110)

0
SEHEMU YA MIA MOJA NA KUMI
ILIPOISHIA...
Tukamaliza mazungumzo, nikaondoka na kuingia chumbani kwetu, nikafanya maandalizi ya kulala, baada ya muda Phidaya akaingia na kukaa kitandani
"Baby ni kazi gani inayo kufanya ubaki huku peke yako"

NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU

SASA ENDELEA...
Phidaya aliniuliza kwa sauti ya upole, huku akinichezea chezea kifua changu.
"Yakumuua John"
"Kumuua John!!?"
"Ndio, nimemuona leo, na ninatambua anapo ishi."
"Sa..sa sasa itakuwaje akituona, si atatuua?"
"Kwa sasa hawezi kuniua"
Nikaanza kumuadisia Phidaya kuanzia mipango ya harusi ilivyo pangwa, hadi kuuawa kwa Ftedy.

"Kwahiyo wanaamini wewe umekufa?"
"Ndio maana yake, nahitaji mutangulie nyumbani mimi niimalizie kazi hiyo ya kumuua yeye kwa mkono wangu."
"Eddy kuwa makini, sihitaji kukupoteza katika hili"
"Usijali mke wangu, nipo makini tena sana"
Tukakumbatiana na Phidaya. Akaingia bafuni akaoga, kisha akarudi kitandani na kujilaza.

"Unajua mama anaweza akapona?"
"Ataponaje?"
"Sisi madaktari, tunambinu za kuwafanya watu walio paralaizi, kuweza kutembea tena"
Maneno ya Phidaya yakanipa matumaini mapya juu ya uwezekano wa mama yangu kupona.
"Mjkienda Tanzania, kuna mtu atawapokea"
"Atatujua?"
"Ndio picha zenu anazo"
"Sawa ila nakuomba Eddy, urudi"
"Nitarudi mke wangu. Tena ngoja nimpigie uzungumze naye"
Nikachukua simu ya mezani na kumpigia Blanka.

"Ndio kaka"
"Hali ya mama inaendeleaje?"
"Kidogo anaonyesha matumaini, japo si sana"
"Msalimie wifi yako"
"Anajua kiswahili au ndio kuch kuch hotae?"
"Anajua mbona, tena zaidi yako"
Nikampa simu Phidaya akazungumza na Blanka, kisha Phidaya akanirudishi simu.

"Ehee kesho kutwa watakuja Tanzania. Watafutie nyumba maeneo ya Masaki au Mbezi beach mimi nitarudi wiki moja baadaye"
"Kaka pesa sina kwa sasa"
"Watakuja na pesa zao wenyewe"
"Poa kaka Eddy sasa nikawapokee Ubungo au wapi?"
"Kwa akili zako hujajua hii namba inatokea nchi gani. Kama ni yatanzania kawapokee Ubungo, kama ni ya nchi za watu wakukute uwaja wa ndege"
"Haaaaaa haya mwaya kaka"
Nikakata simu nikimuacha Blanka akicheka kwa jibu nililo mpa.

Usiku mzima ukawa ni usiku wakuwaza jinsi gani nimuue John pasipo mimi kutiwa hatiani, na kujisababishia matatizo mapya. Nikamuacha Phidaya peke yake kitandani akiwa amepitiwa na usingizi, mimi nikaelekea sebleni. Kitendo cha mimi kukaa kwenye kochi, Shamsa akatoka chumbani kwake.

"Mbona hujalala, hadi sasa hivi?
"Nimekosa tu usingizi, baba"
"Kichwa bado kinauma?"
"Hapana, kichwa hakiniumi, ila kuna jambo linaniumiza sana akili yangu"
"Jambo gani?"
"Nikuhusiana na hiyo kazi unayo hitaji kuifanya. Naomba na mimi niwepo"
"Noo Shamsa, hii vita ni yangu na yule John niliye kuadisia"
"Sawa Eddy, ila nahitaji kuwa karibu nawe kutokana wale wezangu wananitafuta kila kona ya dunia hii"
"Kwa nini wanakutafuta?"
"Huwa kwenye kundi lile mtu akitekwa basi nilazima atafutwe popote alipo, kuhofia kutoa siri zao"
"Mmmmm"
"Na mbaya zaidi, wanashirikiana na Al-Kaida ambao nilisha wahi kufanya kazi kwenye kundi hilo zaidi ya mara nane"
Nikabaki nikimshangaa Shamsa kwani hii habari anayo niambia ni ngeni kwenye masikio yangu na niyahatari kupita zote nilizo wahi kuzisikia kwenye maisha yangu. Kwani kundi la Al-Kaida, linatafutwa na nchi kubwa hususani Marekani. Je vita ya mimi peke yangu nitaiwezaje.

"Nikiwa na familia yako, ninahofia kuitia matatizoni kwa ajili yangu, na wale wanavyo jua ni kwamba umeniteka"
"Picha za zenu mulizo ziweka Facebook nahisi ndio chanzo?"
"Hizo ndio zilizo niharibia mimi kila kitu, najuta kuziweka. Wanenitumia ujumbe facebook"
"Upo wapi?"
Shansa akanyanyuka na kuingia chumbani kwake, akarudi akiwa ameshika laptop. Akaiweka mezani na kuufungua ujumbe alio tumiwa ambao umeandikwa kwa maandishi ya kiarabu.

"Yana somekaje?"
"Wanasena hivii. MIKONO YAO INAVUJA DAMU, ILIYO SABABISHWA NA WEWE. TUTAKUTAFUTA DUNIA NZIMA. DAMU YAKO ITAKUWA KINYWAJI CHETU."
Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio, huku wasiwasi mwingi ukiwa umenijaa moyoni mwangu. Nikamtazama Shamsa jinsi alivyo poteza raha.

"Tutafanyaje Eddy na huu ujumbe ni wakwako?"
Sikujua hata nimjibu nini Shamsa zaidi ya kumtazama tu machoni.
"Eddy hapa nilipo raha yote imetoweka moyoni mwangu, sijui hata tunawakimbiaje?"
"Fanya hivi, ifute hiyo account"
"Alafu?"
"Nitajua ni jinsi gani ya wewe kwenda Tanzania. Natambua kuwa kule mutakuwa mupo salama zaidi"
"Una uhakika?"
"Ndio ninao uhakika huo. Ila nakuomba uandamane na familia yangu"
Shamsa akakaa kimya kama dakika tano, huku akiwa amesongwa na msongamano wa mawazo kichwani mwake.

"Nitakwenda nao kuhakikisha wanafika salama"
"Asante Shamsa"
"Wewe je, usalama wako utakuaje?"
"Hilo musilihofie sana, nilipo toka nimbali sana"
Nikamfwata na kumkumbatia Shamsa. Nikamruhusu arudi kulala. Mimi nikaendelea kukaa sebleni nikiwa sina amani moyoni mwangu kabisa, huku mawàzo mapya ya Al-Kaidah yakinitawala kichwani
***
Muda wa sherehe ya Junio ikawadia, tuliamua kuialika familia ya jirani yetu. Ambaye alikubali kujumuika nasi, akiwa na mke wao na mtoto mmoja. Ili kuinogesha sherehe, tukaimba wimbo wa siku ya kuzaliwa unao tumika kuibwa katika siku za kuzaliwa.

¶Happy birthday to you×2¶¶
¶Happy birthday ni ya Junio, Happy birthday to you¶¶
Junio akaizima mishumaa iliyopo juu ya keki kwa kuipuliza kwa nguvu. Mama yake akaanza kukata vipande vidogo vidogo vya keki. Baada ya kumaliza Junio akaanza kutulisha mmoja baada ya mwengine.

"Jamani kuna kitu nahitaji nikifanye, mbele yenu"
Nilizungumza huku nikitabasamu, nikawafanya watu wote kukaa kimya wakisubiria kitu hicho ninacho taraji kukifanya. Taratibu nikamfwata Phidaya alipo, nikapiga magoti huku nikitoa kisanduku kidogo mfukoni mwa suruali yangu, kilicho hifadhi pete ya dhahabu, niliyo inunua siku tulipokua tukifanya manunuzi ya vitu vya Junio, pasipo mtu yoyote kujua hilo.

"Phidaya, upo tayari kuwa mke wangu?"
Nilizungumza kwa sauti ya unyonge na kumfanya Phidaya kuanza kumwagikwa na machozi yafuraha.
"Ndio Eddy"
Nikauchukua mkono wa kushoto wa Phidaya, na kuivisha pete kwenye kidole kinacho paswa kuvishwa pete ya uchumba. Watu wote wakapiga makofi ya furaha, huku jamaa tuliye mualika akichukua picha za video kwa kamera yetu. Phidaya akaninyanyu na kunikumbatia kwa nguvu huku akilia kwa furaha sana.

"Nakupenda Eddy mume wangu"
"Nakupenda pia mke wangu"
Hatukujali uwepo wa watu waliopo ndani ya seble yetu, tukajikuta mimi na Phidaya, tukinyonyana midomo yetu, kwa hisia kali za kimapenzi, zilizo changanyika kwa furaha nzito.

"Mmmm sasa tusherekee"
Shamsa alizungumza huku akiwasha redio kubwa iliyopo sebleni hapa. Kusema kweli japo ni sherehe ya watu wachache, ila ilitupa furaha kubwa sana mioyoni mwetu, huku kila mmoja akionekana kuridhika kwa matukio yote yanayo endelea katika sherehe hii.
Hadi inafika jioni kila mmoja akawa amechoka kwa kucheza mziki. Nikatoka na jamaa, niliye mualika kwenda nje kupunga upepo huku Phidaya akibaki na mke wa jamaa, aliye jitambulisja kwa jina la Jordan, pamoja na watoto wetu

"Nimefurahi sana kaka Eddy kunialika kwenye sherehe hii ya leo, kusema kweli ipo boma sana"
"Hata mimi nafurahi kwa kuja kwako, hivi wewe ni mwenyeji wa wapi?"
"Florida Marekani. Wewe je?"
"Tanzania"
"Safi sana, alafu kama nilisha wahi kukuona kwenye matangazo ya magari ya Ford yaliyo zinduliwa mwaka huu?"
"Ndio mimi"
"Du kumbe nipo na mtu mkubwa"
"Kawaida hivi unajishuhulisha na nini?"
"Mimi ni mzalishaji wa movie Hoolywood"
Tuliendelea kuzungumza mambo mengi na jamaa hadi majira ya saa tatu usiku tukarudi juu gorofani. Tukajumuika na familia zetu kupata chakula cha usiku, kisha wao wakaondoka na kurudi vyumbani mwao.
***
Mipango ya kukata tiketi za ndege katika shirika la KLM kwa kupitia mtandao likakamilika usiku. Muda wa ndege kuondoka ni saa tano asubuhi, ikatulazimu kufika uwanja wa ndege saa nne asubuhi, ambapo, nikakabidhiwa tiketi tatu nilizo zikata usiku wa jana. Nikawakabidhi kila mtu tiketi yake pamoja na namba za Blanka niliye mpa taarifa juu ya kuupokea ugeni wa familia yangu.
Nikamkabidhi Junio na Shamsa kila mmoja kiasi cha dola elfu ishirini, wazitunze na zitawasaidia kukiwa na tatizo lolote. Nikamkapa Phidaya dola laki moja na nusu za kumsaidia.

"Nakuomba hizo pesa uzitumie vizuri, japo kwa Tanzania ni pesa nyingi sana, ila kuwa nazo makini"
"Sawa baba Junio"
"Walinde wanangu"
"Nitawalinda, nakuomba na wewe ujilinde mume wangu ninakuhitaji zaidi ya chochote kwenye maisha yangu"
"Sawa mke wangu"
Nikamkumbatia Phidaya, kisha nikamfwata Junio.
"Mlinde mama sawa?"
"Sawa dady"
"Nakuaminia wewe ni mwanaume"
Nikamkumbatia Junio na kumpa tano. Nikamfwata Shamsa aliye onekana muda wote macho yake yakiwa juu juu.

"Vipi?"
"Hakuna, kitu baba"
"Ok kuwa makini na familia nzima. Ninakuamini huto niangusha. Mlinde mdogo wako na mama yako"
"Sawa dady"
"You call me dady again?"(Umeniita baba tena?)
"Ndio, unanipa mapenzi bora kama niliyo kua nikiyapata kwa baba yangu.Mungu akubariki"
"Asante kwa kulitambua hilo"
"Nakutakia kazi njema dady"
"Nanyi pia nawatakia safari njema"
Nikawakumbatia wote watatu, nikawaacha waelekee kwenye foleni ya mizigo yao kukaguliwa. Mimi nikaondoka, nikachukua taksi iliyo nifikisha kwenye maduka ya urembo. Nikanunua ndevu bandia.

"Jamani nimepungukiwa na dola kumi nisaidieni tu kuipata hii pochi"
"Hatushushi bidhaa zetu, bei ni hiyo tu, chukua pesa yako uondoke dada"
"Lakini jamani kuweni na utu, katika hili. Dola kumi pia munashindwa kunipa hii pochi"
Niliyafwatilia mazungumzo ya muhudumu na dada mmoja aliye shika pochi, aliyo onyesha kuipenda sana. Nikatoa dola mia na kumpa muhudumu huyo anaye bishana na dada huyo anaye onekana ni muongeaji sana.

"Chenchi itakayo baki utampa huyo dada"
Nilimuambia muhudumu huyo, huku nikiwatazama machoni. Nikachukua mfuko wangu nilio nunua vitu ndani ya duka hili ikiwemo sura ya bandia. Nikatoka nje ya duka na kutazama tazama uwezekano wa kupata usafiri wa taksi.
"Naitwa Prety wewe je?"
Dada niliye mlipia pochi dukani, alizungumza huku akiwa amesimama pembeni yangu. Huku akiwa amebeba jifuko kubwa lenye vitu vingi ndani yake.

"Eddy. Taksi"
Niliita taksi inayo katiza pembeni yetu.
"Hapana wewe nenda"
Prety alimruhusu dereva wa taksi hiyo kuondoka jambo lililo anza kunikera.

"Mimi nina gari yangu, ile pale nyekundu"
Alinionyesha kagari kadogo, kanako fanana na gari la mchekeshaji maarufu duniani Mr bean.
"Lile ndio gari lako?"
"Ndio twende tukapande"
Prety akanishika mkono hadi kwenye kagari hako. Akanifungulia mlango nikaingia, kisha yeye naye akaingia.
'Mungu wangu hiki kikipata ajali hatutoki humu'

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI

KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)