SORRY MADAM (116)

Zephiline F Ezekiel
SEHEMU YA MIA MOJA KUMI NA SITA
ILIPOISHIA...
Ikanilazimu kumtoa Pretty kwenye mwili wangu, taratibu.
"Ptetty"
Nilimuuita kwa sauti ya upole, huku nikimtazama machoni mwake.
"Mmmmm, nakupenda sana, ila ninakuomba kitu kimoja tu unisaidie kwa wakati huu"

NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU

SASA ENDELEA...
"Kitu gani?"
"Ninakuomba, uniruhusu nikaiweke familia yangu katika sehemu salama."
"Eddy nimekuzoea sana. Ninakuomba twende wote"
"No no, nitarejea mama, kwa ajili yako, ninakuomba uniruhusu katika hilo."
Pretty akakaa kimya huku akinitazama machoni mwangu, machozi yakiendelea kumwagika usoni mwake.

"Promise me"(Niahidi)
"Nitarejea mpenzi, kwa ajili yako"
"Kweli?"
"Ndio"
Ilinilazimu kutumia akili nyingi na busara kubwa kumdanganya Pretty la sivyo nisinge ondoka na hata ndege niliyo ibahatisha kwa ajili ya usafiri nisinge ipata.
Pretty akanikumbatia tena, akunibusu mdomoni, huku akilia, nikamfuta machozi kwa kutumia viganja vyangu.

"Nitarudi baby"
"Ok, safari njema"
Pretty alizungumza kwa kujikaza, kwa maana uchungu alio kuwa nao ni mkubwa sana
"Kuwa makini, Eddy"
"Na wewe pia"
Pretty akaniruhusu kuondoka, nikapiga hatua za haraka hadi kwenye foleni ya ukaguzi. Nikavua vitu vinavyo hitaji kuvuliwa ikiwemo, mkanda wa suruali, saa ya mkononi, viatu na simu yangu nikawakabidhi. Nikafanikiwa kupita salana kwenye kitengo hicho, nikachukua kila kilocho changu na kwenda kujumuika na wasafiri wengine.

Tukaingia ndani ya ndege, huku nikiwa ninafuraha sana, kwani ni muda wa kwenda kumuonyesha mama yangu, familia yangu aliyokua akiikataa kisa wao ni waarabu ambao mara nyingi alidai mke wangu ni gaidi, kumbe Sheila ni gaidi mkubwa aliye kuwa amejificha kwenye familia yake.
Nikakaa kwenye siti yangu, ambapo pembeni nikamkuta mtu akisoma gazeti kubwa, lilolo ificha sura yale huku kichwani mwake akiwa na kofia kubwa.

"Hi...!!"
Nilijipendekeza kusalimia, kwani si uungwana kukaa siti moja na mtu pasipo kusalimiana naye. Akalishusha gazeti lake chini kidogo, ndipo nilipo pata nafasi ya kuiona sura yake vizuri.
Ni mzee wamakamo aliye enda umri kidogo, anaasili ya kiarabu, huku ndevu zake zikiwa za rangi nyeupe.
"Hakunijibu kitu zaidi ya kunitazana kwa sekunde kadhaa, kisha akalirudisha gazeti lake usawa ulio kuwepo awali na kuufunika uso wake kabisa.

"Mmmmm"
Niliguna, huku na mimi nikifunga mkanda wa siti niliyo kalia, nikatoa simu yangu na kumpigia Blanka
"Vipo dogo"
"Safi kaka, huku lini?"
"Kama wiki hivi, ndio nitarudi, wapo wapi hao"
"Mlimani city, kuna vitu tumekuja chukua"
"Ahaaa, nyumba mulipata?"
"Ndio, tulipata ya kukodi"
"Poa mida"
"Hutaki kuwasalimia leo?"
"Baadaye nitawasalimia"
Nikakata simu na kuiweka kwenye mfumo wa 'Airplane mode' kisha nikairudisha mfukoni, nikaminya minya batanani za kitv kilichopo mbele yangu, nikaweka filamu ninayo ipenda na kuanza kuitazama, huku nikiwa nimevaa earphone, zinazo tumika kusikilizia sauti ya filamu hiyo, hii nikuepuka kumbuguzi mwenzako uliye kaa naye, huku tukisubiria ndege kuwashwa na kuondoka.

Taratibu mashine, za ndege zikawashwa, tukaashiriwa na muhudumu, wa kike aliyopo ndani ya ndege hii, kupitia vipaza sauti vilivyomo ndani ya ndege kwamba kila mmoja ajifunge mkanda na kutulia kwenye siti yake, kwani ndege muda wowote itaweza kuondoka. Muda mchache baadae ndege ikacha ardi ya nchi ya Brazili, jambo lililo nipa furaha kubwa kwani tukio nililo mfanyia John na mkewe wake, laiti kama ninge kamatwa ningeozea jela, maisha yangu yote
'Asante mungu'
Nilijisemea kimoyo moyo huku nikijiweka sawa kwenye siti yangu
**
Mzee aliye kaa pembeni yangu, akalikunja gazeti lake kwa haraka. akachunguli nje kwa kupitia kioo kilichopo pembeni yake, kutokana na giza hakuweza kuona chochote, akalifunga dirisha na kukiziba kioo hicho.

Akanitazama huku akionekana kuwa na wasiwasi mwingi sana. Akavua kofia lake ambalo mara nyingi hupendwa kuvaliwa na watu wanao jiita 'Cow boys'(Ng'ombe wa kiume). Akaliweka pembeni huku jasho likianza kumwagika, jambo lililo anza kunipa wasiwasi na mashaka makubwa dhidi yake.
Akaanza kuzungumza maneno yakiarabu yaliyo nipa wasiwasi, kwani maneno yake ni kama ya yule mtu aliye jilipua nikiiwa hotelini, nchini Iraque, akapelekea mimi kupelekwa kwenye hospitali, ambayo nilikutana na Phidaya kwa mara yaa kwanza, akiwa kama daktari aliye nitetea kufa na kupona, pale madaktari wezake walipokua wakihitaji kunikata mguu.

Mzee huyo akavua koti la suti yake akabakiwa na shati lililo tuna mbele, kwa haraka nikamshika na kuchana shati lake hadi vifungo vikakatika.
"Bomuuuuuu"
Nilijikuta nikizungumza kwa sauti ya juu, baada ya kukuta bomu linalo kwenda kwa kasi sekunde zake, zinazo onekana kwa rangi nyekundu, alilo lifunga tumboni mwake. Watu wote waliopo siti za mbele wakanyanyuka na kuanza kupiga kelele, huku wengine wakimuita Mungu wao. Nikataka kuondoka mzee akaniwahi kunidaka mkono, kila nilipo jaribu kuondoka, akanishinda nguvu. Nikalishuhudia bomu lilifika kwenye namba za sifuri, likiashiria lipo tayari kwa kulipuka.

"Buuuuuuuuupuuuuuuuuu"
Bomu likalipuka, na kutuchangua sote tuliomo ndani ya ndege
**
Nikastuka kutoka usingizini, huku nikihema sana, macho yangu yakatua kwenye kiji tv kadogo kalichopo mbele yangu, kikionyesha tukio la filamu hiyo, ikiwa na mlipuko wa bomu, kwenye moja ya kipande chake, niliyo kuwa nikiitazama kabla sijapitiwa na usingizi. Nikavua earphone huku ikinilazimu kumgeukia mzee aliyopo pembeni kwa haraka, nikalivuta gazeti lake alilo kua akiendelea kulisoma na kumfanya astuke huku akinitumbulia mimamcho yamshangao.

"What....!!?"(Nini....!!?)
Mzee aliniuliza, huku akiendelea kunitumbulia mimacho, nikampiga kisukusuku cha uso, kilicho mfanya akae kimya, huku damu za puani zikianza kumchuruzika. Nikamfungua vifungo vya shati lake, nikakuta hana kitu chochote alicho kifunga tumboni mwake zaidi ya msalaba mkubwa alio uvaa shingoni na kuning'inia tumboni mwakr, nikakichomoa kitambulisho alicho kichomeka kwenye mfuko wa shati lake.
Kitambulisho chake kilionyesha ni mchungaji, wa shirika la misaada duniani

"Am sorry"(Nisamehe)
Nilizungumza huku nikimuachia mchungaji huyu, niliye muona kama ni gaidi, aliye jifunga bomu. Hakunijibu chochote zaidi ya kukaa kimya, huku akizifuta damu zake puani kwa kutambaa. Tukio nililo lifanya juu ya huyu mchungaji, halikuonwa na watu wengi, kutokana na wao kalala, kwa uchovu wa safari hii.

Hamu ya kuendelea kukaa kwenye siti hii, ikanipotea kabisa, kwa maana mchungaji huyu hakuzumgumza chochote na mimi, wala sikujua kama amenisamehe au laa. Akanyanyuka na kuniomba nimpishe, nikafanya hivyo. Akaelekea maeneo ya chooni, huku mara kadhaa akigeuka nyuma na kunitazama mimi, kama mtu mwenye wasiwasi mkubwa na mimi.

"Huyu mzee vipi"
Nilizumgumza huku, nikiedelea kumtilia mashaka, moyo wangu nikaulazimisha kumuamini mzee huyu, ila ikakataa kumuamini kabisa. Nikanyanyuka na kuelekea kilipo choo. Kitendo cha kufika mlagoni tu, nikamkuta naye anafungua mlango, akanitazama kwa muda.

"Buuuuupuuuuuuuuu"
Alinisemesha maneno, nisiyo yaelewa huku akitabasamu kidharau. Nikabaki nikimshangaa, kwa jinsi alivyo nifanyia huyu mzee, kwa mara ya kwanza nilimuota ila hii ya pili ni kitu kinacho fanyika kiukweli. Nikamtazama, akielelea kwenye siti, huku nikiendelea kumyafakari mzee huyu maana ya kunifanyia hivyo ni nini, na nikwanni amenifanyia mimi peke yangu.

"Chizi nini huyu? au ni kile kisukusuku, nilicho mpiga?"
Nilijisemea mwenyewe huku nikiingia chooni.
Nikafungua zipu ya suruali yangu, kwa ajili ya kujisaidia haja ndogo. Kabla sijaanza nikahisi kuna kijimlio kikitokea chini ya sinki la kunawia mikono. Ikanilazimu kusitisha zoezi zima, nililo kua nikihitaji kulifanya, taratibu nikainama na kuchungulia. Nikakuta bomo, lililo tegwa, kama lile nililo mtegeshea John, huku likiwa limebakisha dakika mbili na sekunde kadhaa kabla halijalipuka.

"Mungu wangu"
Nikatoka chooni haraka, kila niliye mtazama ndani ya ndege, amesinzia, huku baadhi wakiwa wanatazama filamu kwenye tv zao. Sikumuona mzee niliyekuwa nimekaa naye kwenye siti moja, kwani siti zetu mbili zote zilikuwa tupu.

"Amekwenda wapi huyu mchungaji?"
Nilizungumza huku nikiendelea kupepesa macho huku na kule.
Kusema kweli, sikuwa na ujuzi wa kutegua mabomu, nilicho kuwa nikikijua katika mabomu ni kutega tu. Nikamuona muhudumu mmoja mwanadada, akimfunika shuka, mtoto mmoja, aliye lala muda mrefu.
Nikamfwata na kumuomba, anisikilize shida yangu.

"Do you speak English or Swahili?"(Je unazungumza Kingereza au Kiswahili?)
Nilimuuliza dada huyu, huku jasho likinimwagika usoni, Kwani mimi ndio ninafahamu ukweli unao endelea ndani ya ndege hii, iliyo beba watu wengi si chini ya mia mbili na hamsini, huku watoto na wamama wakiwa ni wengi ndani ya ndege, mbaya zaaidi kwa dakika chache kila kitu kitakuwa kimesambaratika hata miili yetu pia.

"Kswahili pia nazungumza"
Aliniambia huku akinitazama machoni kwa umakini. Nikamshika mkono hadi nje ya mlango wa kuingilia chooni.
"Ninakuomba unisikilize kwa umakini, kuna bomu humu chooni, na limebakisha dakika kulipuka...."
"Bomuu....Mungu wangu!"
Dada huyu alishangaa huku akinitumbulia mimacho usoni, ilinibidi kumziba mdomo asizungumze kwa sauti kuashiria watu wengine kuanza shida, zitakazo pelekea sote kupotea kwa uzembe wetu.

"Hakuna haja ya kushangaa"
Nikamvuta na kumuingiza chooni, mikamuonyesha bomu lilipo, Sote tukajikuta tunashangaa kutokana bomu hilo limebakisha sekunde hamsini na tisa, kabla halijalipuka na sote hapa hatujui jinsi ya kulitegua, na muhudumu akaanza kulia, akijaribu kunikumbatia kwani mwisho wetu umefika.

"Una chochote cha kukatia"
Nilizungumza huku nikimtoa muhudumu huyu, mwilini mwangu, kwani kukumbatiana kwetu sio suhulisho la bomu hili kuacha kuacha kulipuka. Hakunijibu zaidi ya kubabaika, kwa mawenge yaliyo mchanganya kupita maelezo. Akaanza kujipapasa huku mwili mzima ukimtetemeka kwa woga, akatoa, kikatia kucha(Nail cutter), akaitupa chini huku akiendelea kuikagua mifuko ya nguo zake alizo zivaa. Kwa haraka nikaokota kikatia kucha, nikapiga magoti chini, huku nikiwa ninajiamini kwa lile ninalo kwenda kulifanya.

Sekunde za bomu hili, zikazidi kurudi nyuma, huku zikiwa zimebakia sekunde thelathini na mbili kabla halijalipuka. Nikaanza kuzichambua nyaya nyingi ndogondogo zipatazo ushirini, zikiwa na rangi tofauti tofauti.
"Ishirini na tano"
Muhudumu aliniambia, huku macho yake akiwa ameyatumbulia kwenye bomu, linalo zionyesha sekunde hizo, zinavyo rudi nyuma.

"Mungu wangu"
Nilizungumza huku nikizidi kuchanganyikiwa, kwani sikujua ni waya upi unanipasa kuukata, ili kulizuia bomu hili kuto kulipuka.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUTUMIA AKAUNTI YAKO YA FACEBOOK, LIKE UKURASA HUU USIPITWE NA SIMULIZI NA MENGINE HUKO FACEBOOK

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII KAMA MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA

KWA TELEGRAM👇BONYEZA HAPA

Chapisha Maoni