
SEHEMU YA MIA MOJA HAPA
ILIPOISHIA...
Nilizungumza huku nikizidi kuchanganyikiwa, kwani sikujua ni waya upi unanipasa kuukata, ili kulizuia bomu hili kuto kulipuka.
NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
"Kumi na tano"
Nikashika nyaya moja nyekundu na kuikata, chakushangaza, bomu likaendelea kurudisha sekunde zake nyuma.
"Nane"
Nikazidi kuchanganyikiwa, na kukata wanya mweusi, hali ikawa ni ile ile.
"Tano"
Mikono yote, ikazidi kutetemeka hadi nikaangusha kikatia kucha, nikakiokota kwa haraka, hata kukaa mkononi vizuri, nkawa ninashindwa kukishika.
"Tatu"
Nikamuona muhudumu, akipiga ishara ya msalaba akiashiria mwisho wetu ndio unakaribia, nikashika waya wa rangi ya kijani, sekunde ikawa imebaki moja, nami nikawa nimeukata. Sekunde hiyo ikasimama hapo hapo na bomu kuzima. Nikashusha pumzi nyingi, huku mwili wangu wote ukiwa umesha vuja jasho lakutosha hadi shati nililo livaa, likawa limelowana kabisa. Kumtazama muhudumu nikamkuta akiwa ameyafumba macho yake huku jasho likimwagika shingoni nwake.
"Tumefanikiwa"
Nilizungumza kwa sauti ya unyonge huku nikimtazama usoni muhudumu, akayafumbua macho yake taratibu, huku akihema. Akalitazama bomu nililo lichomoa na kulishika, akabaki akiwa ameduwaa. Akanishika mkono taratibu na kuninyanyua, akanikumbatia huku akilia kwa furaha.
"Asante Mungu, kweli wewe ni mwema. Hakuna kama wewe"
Alizungumza huku akiendelea kulia, nakunifanya na mimi machozi kunimwagika kwani sikutarajia kama nitaweza kufanikiwa kulitegua bomu hili, taratibu akaniachia, huku akijifuta machozi usoni
"Unaitwa nani?"
"Am Tasiana, from Arusha Tanzania"(Mimi ni Tasiana natokea Arusha Tanzania)
"Mimi pia natokea Tanzania, ila A leve nilisoma Arusha"
"Waooo, nashukuru kukufahamu"
Tasiana akanikumbatia kwa mara ya pili, akawasiliana na marubani wa ndege hii, kupitia kijisimu kidogo wanacho kitumia kuwasiliana, wakamuomba tuelekee kwenye chumba walipo, tukiwa na bomu hilo, ila tuhakikishe hakuna abiria atakaye liona, ili kuto hatarisha amani ya walio wengi.
Tasiana akachukua mfuko mtupu, mweusi. Akaliweka bomu, nikaongozana naye hadi chumba cha marubani. Tukawaelezea hali halisi juu ya tukio zima na jinsi mchungaji Frank, alivyo nipa vitisho nikiwa ninapishana naye kwenye mlango wa chooni.
"Hakuna aliye toka ndani ya ndege, ngoja tukifika Afrika kusini, tutafanya upelelezi kabla watu hawaja ruhusiwa kushuka kwenye ndege"
Rubani mmoja alizungumza huku akilitazama tazama bomu hilo nililo mpatia.
"Ukimuona si utamkumbuka?"
"Ndio, nilikuwa nimekaa naye ila simuoni kwenye siti yetu"
"Ulikaa siti gani?"
Nikamtajia rubani, huyo herufi ya siti niliyo kuwa nimekaa, akatazama mkanda mzima, kwenye kiji tv chao kidogo unao rekodiwa na kamera zilizo tegwa kila kona ya ndege. Tukamuona mzee huyo akiingia kwenye moja ya chumba walicho dai ni stoo, chenye gazi za kushukia chini, kunapo hifadhiwa mizigo mikubwa mikubwa.
"Ngoja nimfwate"
Nilizungunza kwa kujiamini, huku nikiwatazama marubani hawa wapatao wanne, huku wawili wakiwa niwasaidizi.
"Itaweza kumkamata?"
"Nitahakiksha nalifanikisha hilo"
Wakanitazama machoni, mkuu wao akanipa ruhusa.
"Tuongozane"
Tasiana aliomba tuongozane pamoja.
"Wewe baki, ngoja nikajaribu kulifanya na hili kama nitafanikiwa"
"Tafadhali twende pamoja"
Tasiana aling'ang'ania kwenda, ikanibidi nimkubalie tu. Tukaongozana hadi kwenye chumba hicho, pasipo wasafiri wezangu kuelewa kitu gani kinacho endelea, hakikuwa chumba kikubwa sana, kwani kina ngazi zakushuka chini kulipo na mizigo mikubwa. Tukafanikiwa kushuka chini, kwa wingi wa mizigo iliyo fungwa kwenye mifurushi mikubwa, ilitufanya tubaki tukiwa tumesimana na kuduwaa.
"Atakuwa wapi?"
Tasiana aliniuliza kwa sauti ya chini, huku tukiendea kupepesa pepesa macho yetu kila kona ya eneo hili lilolo kubwa.
"Nifwate nyuma na kuwa mkimya"
Tukaanza kupita kwenye vinjia, vilivyo tenganishwa kwa maburungutu makubwa ya mizigo. Nikaanza kupata wasiwasi, baada ya kukuta shati alilo kua amelivaa mzee yule, likiwa chini. Tasiana akataka kuliokota ila nikamzuia asifanye hivyo.
"Kwa nini nisiliokote?"
Nikatingisha kichwa nikimuashiria Tasiana asifanye chochote dhidi ya shati hilo.Tukalipita, hatua kumi mbele, tukakuta suruali aliyo kuwa ameivaa.
Kwa kutumia mguu nikaisogeza kuitazama kama kuna kitu kimefunikwa, ila hatukuona kitu.
Arufu ya moshi wa sigara, ukaanza kuingia kwenye pua zetu, ulitokea upande wa pili wa sehemu ilipo mizigo hiyo. Tukapiga hatua za tahadhari hadi sehemu inapo tokea harufu ya moshi huo wa sigara, tukakuta kipande cha sigara kikiwa chini, kikiendelea kuteketea taratibu.
"Yumo humu humu"
Tasiana aliniambia huku akitazama tazama kila kona ya hili eneo. Nkakikanyaga kipande cha sigara hadi kikazimika. Nikapiga hatua mbili mbele, nikastukia kitu lizito kikinipiga kifuani mwangu na kuniangusha chini, nikaamka kwa haraka kutazama ni nini kilicho nipiga.
Mtu aliye valia nguo nyeusi tupu akawa amesimama mbele yangu, huku amevalia kinyago kilicho ificha sura yake, mkono wake wa kulia, ameshika chuma kifupi alicho toka kunipiga nacho muda mchache ulio pita.
"Buuuuuuuupuuuuuuuuuu"
Alizungumza maneno kama aliyo niambia mzee yule nilipo kuwa nikipishana naye mlangoni mwa chooni.
"Rudi nyuma"
Nilimuambia Tasiana, naye akafamya hivyo. Taratibu nikavikunja vidole vya mikono yangu, na kugeuka kuwa ngumi.
"Hahaaaaaa"
Mtu huyo alicheka, kwa dharau kubwa huku akiendelea kunitazama machoni mwangu. Nikarusha ngumi kadhaa, ila akazikwepa zote na kunitandika chuma cha mgongo kilocho nifanya nitoe ukelele mkali wa maumivu.
Nikajipanga tena kufanya mashambulizi kwa mtu huyu, kila nilivyo zidi kupambana naye, ndivyo jinsi alivyo nizidi kwa mbinu za kupigana.
Akakitupa chini chuma chake alicho kishika na kukunja ngumi, akiashiria tunapigana kwa mkono, sikukata tamaa ya kupamba naye, baadhi ya ngumi na mateke niloyo mpiga, kidogo yakanipa matumaini ya kuamini nitamudu. Ila naye hakuwa nyuma katika kurusha makonde mazito tena yaliyo shiba kwa ujazo mzuri tu wa ngumi, kwani akinipiga konde moja nilazima nilisikilizie kwa sekunde kadhaa.
"Eddy utakufaa"
Tasiana aliniambia huku akinitazama jinsi ninavyo vuja damu, zikitokea chini kidogo ya jicho la kushoto baada ya kupigwa ngumi nzito, niliyo jitahidi kuizuia kwa mikono yangu, ila ilipita hovyo hiyo na kunipasua sehemu hiyo.
"Kama humuwezi tuondoke"
Nikamtazama Tasiana jinsi anavyo zungumza kwa wasiwasi, nikatingisha kichwa kuashiria kwamba bado sijashindwa. Nikaitazama miguu ya mtu huyo jinsi inavyo irusha rusha kwa haraka akinifwata, nikatambua anatumia upiganaji wa kichina unao itwa 'kung fu' na mimi sikuwa na mfumo maalumu wa kupigana ndio maana nikajikuta nikipigwa kizembe, kiasi hichi.
'Mtu anaye pigana kung fu, wewe tazama miguu yake na mikomo yake kabla hujafanya shambulizi lolote kwake'
Niliyakumbuka maneno ya mzee Godwin, kipindi akinifundisha utotoni, hadi mtu huyu ananikaribia nikawa nimemtazama kwa umakini, anavyo kuja kwa kasi. Akarusha mateke kazaa, nikaweza kuyakwepa na kumpiga ngumi ya tumbo iliyo mrudisha nyuma na kumfanya ajipinde kiasi.
Tukaanza kuyumbishwa, hii ni baada ya ndege kuanza kutua, kwa bahati mbaya Tasiana akateleza na kuangukia sehemu aliyopo mtu huyo. Akamkamata Tasiana na kukichomoa kisu chake na kumuwekea Tasiana shingoni.
Katika kurupushanani za ndege kutua kwenye ardhi, Tasiana akafanikiwa kumtoa mtu huyo kinyago cha usoni mwake, sikuamini kumuona Mzee Godwin, kwani muda wote nilivyo kua nikipambana naye nilihisi kuwa ni yeye, hii nikutokana na mapigo aliyo kuwa akiyatumia kushambuliana na mimi, ila sikuwa na uhakika kama ni yeye. Nikiwa nimeduwaa kumtazama Mzee Godwin, aliye endelea kujitazama kwa macho makali, nikastukia kumuona Tasiana akianguka chini, huku amechomwa kisu cha tumboni.
Mzee Godwin, akanifanyia ishara ya kunichinja kwenye shingo kisha akaondoka, na kumuacha Tasiana akiendele kuugulia kwa maumivu makli. Nikataka kumfwata mzee Godwin, ila Tasiana akaniita kwa kuhitaji msaada wangu, ili kuyaokoa maisha yake yaliyopo hatarini kupotea.
"Eddy nisaidie ninakufaa, mimi"
Nikakimbia hadi sehyemu alipo angukia Tasiana, kwa haraka nikamuweka vizuri huku kichwa chake akiwa amekilaza katika mkono wangu wa kulia, huku mkono wangu mwengine ukiwa na kazi ya kuzizuia damu zilizo kuwa zikimwagika kuto kuendelea kutoka katika jeraha lake alilo chomwa na kisu.
“Eddy ninakufa mimi”
“No huwezi kufa Tasiana”
Niliendelea kumfariji Tasiasa, huku nikiwa ninaendelea kusubiria ndege kuweza kutua kwenye ardhi, kwani sehemu tuliyopo ilinilazimu kuweza kuegamia moja ya mzigo ili tusianguke. Kwa kutumia kijiisimu kidogo alicho kuwa anakitumia Tasiana, nikaweza kuomba msaada kutoka kwa wahudumu wengine. Hadi ndege inasimama kabisa ardhini, hali ya Tasiana kusema kweli haikuwa nzuri kiasi cha kumfany ayafuyafumbe macho yake, huku mapigo ya moyo yakimuenda taratibu sana. Tukasaidiana na wezake kumpa huduma ya kwanza. Nikiwa ninaendelea kutafakari ni nini cha kufanya huku nikizunguka zunguka sehemu tuliyopo. Nikauona mwili wa mtu, ukiwa umelala chini na umesukumizwa chini ya moja ya mzigo mkubwa huku miguu yake ikiwa imetokezea kwa nje.
Nikamuita mmoja wa polisi kati ya polisi wanne walio ingia sehemu tulipo, kwa kusaidiana naye tukamvuta na kumtoa nje, sikuamini kumuona yule mchungaji akiwa ameuawa kikatili huku macho yake yakiwa yamepasuliwa na inavyo onekana ameminywa kwa vidole vigumu hadi yakapofuka.
“Unamjua huyu?”
Aliniuliza kwa lugha ya kingereza, nikamtazama machoni askari kisha nikatingisha kichwa kwa kumuashiria kwamba ninamfahamu mtu huyo. Akawaita wezake kuja kulishuhudia tukio hili la kinyama.
“Inabidi twende kituoni kwa mahojiano zaidi”
Askari mmoja alizungumza huku akinitazama machoni.
“Sawa, ila kwa sharti moja tu”
“Lipi?”
“Nahitaji kubadilisha hizi nguo zimejazana damu kama ninyi munavyo niona”
“Kwa hilo hakuna tatizo”
Kilicho niokoa dhidi ya hawa askari kuto kunichukualia mimi kama muhalifu, ni kwa jinsi marubani walivyo waeleza juu ya tukio zima la kutegua bomu lililo kuwa limetegwa ndani ya ndege hii. Nikatafutiwa nguo nyingine, nikazibadilisha na kutoka sehemu ya juu ambapo nikakuta baadhi ya abiria wakiwa wameketi kwenye siti wakisubiri safari iiendele, huku wengine wakiwa katika mlolongo wakishuka na kukaguliwa.
Nikamuona Tasiana akiingiazwa kwenye gari la wagonjwa na kuondoka katika eneo la uwanja wa ndege, sikufahamu wanakwenda katika eneo gani.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUTUMIA AKAUNTI YAKO YA FACEBOOK, LIKE UKURASA HUU USIPITWE NA SIMULIZI NA MENGINE HUKO FACEBOOK