SEHEMU YA MIA MOJA KUMI NA NANE
ILIPOISHIA...
Nikamuona Tasiana akiingiazwa kwenye gari la wagonjwa na kuondoka katika eneo la uwanja wa ndege, sikufahamu wanakwenda katika eneo gani. NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
Nikashuka kwenye gazi za ndege huku nyuma yangu nikiwa nimeongozana na askari wawili. Baadhi ya waandishi wa habari walikatazwa kunipiga picha yoyote, huku mmoja wa askari akisikika akiyazungumza maneno haya mara kwa mara pale alipokuwa akisogezewa maiki za waandishi wa habari.
“HUYU JINA LAKE NI EDDY NA WALA SI GAIDI”
Maneno yake yakazidi kunipa matumaini ya kuamini kwamba kile kilichopo mbele ya maisha yangu hakita kuwa kigumu sana kwani sina hatia yoyote katika hilo. Tukaingia kwenye moja ya gari la polisi lenye rangi nyeusi, huku tukiwa na askari wawili wenye pikipiki kubwa nyeupe zenye kupiga king’ora, mmoja akiwa mbele na mwengine akiwa nyuma.
“Mbona munanipeleka kwenye mahojiano huku kukiwa na askari wengie?”
“Hii ni kwaajili ya usalama wako kwanza, ndani ya nchi hii, ugaidi umekidhiri sana, hususani kwa mtu ambaye anahitajika kutoa msaada wa kukamatisha mtu au kundi kubwa la watu wakiwemo matajiri na viongozi serikalini, bila ya kumfanyia ulinzi wa kutosha basi anaweza kuuawa”
Askari alizungumza huku nikiendelea kutazama pikipiki ya askari inayo kuja nyuma yetu. Tukafanikiwa kufika kituo cha polisi salama salmin, nikapelekwa kwenye moja ya ofisi kwa ajili ya kukutana na mkuu wa kitengo hicho cha mahojiano
“Hembu nielezee tukio zima jinsi lilivyo tokea kwenye ndege”
Mzee wa makamo alimiuliza swali hilo, huku tukiwa tunatazama machoni. Nikamuelezea kila kitu kilivyo kuwa ndani ya ndege hadi maafa ya Tasiana kuchomwa kisu nikiwa pamoja naye.
“Muuaji ulifanikiwa kuiona sura yake?”
Nikafikiria kwa sekunde kadhaa, ikanilazimu kuktaaa kwamba sikumuona sura yake. Kutokana na kinyago alicho kuwa amekivaa usoni. Ila ukweli ni kwamba ninatambua kila kitu kuhusiana na Mzee Godwin na endapo nitawaeleza ninamtambua, nitalazimika kujibu maswali mengi ambayo yangenipotezea muda wangu mwingi. Baada ya kuridhika na mahojiano yangu, wakanipeleka, hospitali kupatiwa matibabu ya majeraha yangu kisha wakanipeleka hotelini kwa ajili ya kulala, hadi kesho nitakapo endelea na safari yangu ya kuelekea nchini Tanzania.
Usiku kucha nikiwa ndani ya Hoteli sikuweza kupata usingizi hata kidogo, swali lililo niumiza akili yangu ni kwanini hadi leo mzee Godwin anachuki juu yangu. Sababu ya mimi kuwa ni mtoto wa pacha mwenzake haikuwa kubwa sana yakunifanya niwe adui yake aliye tumia muda wake mwingi katika kunisaka kila kona ya dunia ila kuiangamiza nafsi yangu.
“Kuna kitu kinacho endelea hapa, ambacho mimi sikifahamu, itabidi nifwatilie kwenye kumbukumbu za mama.”
Nilijisemea kimoyo moyo huku nikiendelea kulala kwenye kitanda, huku macho yangu yakitazama feni linalo zunguka taratibu juu ya chumba hichi.
Asaubuhi na mapema nikawahi kuamka ili kuiwahi ndege niliyo kuwa nikisafiria kwenda nayo Tanzania, kwani ililazimika ndege hiyo kuzuiwa kwa muda ili uchunguzi wa kina uweze kufanyika kabla haijaendelea na safari yake kuelekea mashariki mwa Afrika. Nikafika uwanja wa ndege nikiwa nimevalia kofia kuepuka watu wengi kunitazma tazama mimi, nikaingia kwenye kitengo cha usafirishaji ambapo nikakabidhiwa hati yangu ya kusafiria pamoja na mizigo yangu iliyo kuwa imehifadhiwa hapo.
“Ndege itaondoka muda gani?”
Nilimuuliza muhudumu wa ndege yetu, baada ya kukabidhiwa kila kilicho changu na mamlaka husika walio kuwa wamevishikilia vitu vyangu.
“Saa tisa jioni, tunasubiria kupata ruhusa ya kuondoka hapa uwanja wa ndege, kutoka katika ofisi za Interpol”
“Ahaa basi ngoja nikazunguke zunguke mjini mida ya saa saba nirudi”
“Sawa”
“Hivi yule mwenzenu, amepelekwa hospitali gani?”
“St Hellen Hospital”
“Sawa, nitamuomba dereva taksi anipeleke hapo”
“Sawa”
Nikaiacha mizigo yangu kwa muhudumu huyu wa ndege ambaye nilikuwa nikizungumza naye, nikatoka nje na kumuomba dereva taksi kunifikisha katika hospitali hiyo niliyo mtajia jina. Nikafika hospitalini nikaelekea moja kwa moja sehemu ya mapokezi ambapo nikamuomba muhudumu kunipeleka kwenye chumba alicho lazwa Tasiana. Wakanipeleka na kunionyesha chumba chake, nikaingia na kumkuta akiwa amelala. Huku akiwa amezungukwa na mashine nyingi zinazo msaidia kupumua. Nikamtazama dada wa watu jinsi alivyo mzuri, nikajikuta mchozi yakinimwagika kwani pasipo mzee Godwin sidhani kama angelala kwenye kitanda hichi kwa wakati kama huu, tana akiwa hajitambui kabisa. Nikaivua saa ya dhahabu, niliyo pewa na Pretty na kuiweka pembeni mwa kichwa chake, kama zawaidia itakayo msaidia baada ya kupata nafuu kwani saa hii ni ya gharama sana.
“Ninakuomba hii saa, akiamka muambie umepewa na Eddy”
Nilimuambia nesi huyu ambaye amevalia mavazi ya watakatifu wa kike(masista), akaniahidi kuitunza hadi Tasiana atakapo pona na ataufikisha ujumbe wangu kama nilivyo muambia. Nikaondoka na kurudi uwanja wa ndege, nikaichukua mizigo yangu na kukaguliwa vizuri, kisha nikaruhusiwa kwenda ndani ya ndege. Baada ya masaa kadhaa, safari ikaanza kuelekea Kenya kisha inamalizikia Tanzania. Muda wote ndani ya ndege nikawa ninamuomba Mungu katika kunisiaidia ili kuweza kufika nchini Tanzania salama salimi.
Hadi tunafika Kenya, hapakuwa na Tatizo lolote ndani ya ndege, tukakaa Kenya kwa masaa kadhaa, kisha safari ya Tanzania ikaanza, ambayo ikatuchukua masaa machache kuingia katika anga la Tanzania. Ndege ikatua kwenye uwanja wa Mwalimu J.K Nyerere, nikasali sala ya kumshukuru Mungu kwa kuweza kunifikish salama Tanzania. Hadi ninatoka nje ya uwanja moyo wangu ukawa umetawaliwa na furaha kubwa sana kwani ni muda wa mimi kuiona familia yangu japo Pretty aliniambia niipeleke mbali na Tanzania, familia yangu ila siwezi kuufanya ujinga kama huo.
“Hapa ndipo ninapo nilipo zaliwa, siwezi kwenda sehemu yoyote”
Nilizungumza huku nikitazama mandhari tofauti tofauti yaliyopo nje ya uwanja huu, nikamuita muhudumu kati ya wahudumu wanao zunguka zunguka ndani ya uwanja huu
“Samahani ni wapi wanapo uza lini za simu?”
”Nyoosha kulia, utaona maduka ya simu ukifika hapo utajua ni mtandao gani unahitaji kuutumia”
“Asante”
Nikaenda nilipo elekezwa, nikawakuta wadada kadhaa wakiwa wanawahudumia watu wengine, na mimi nikajichochochomeka kati ya wateja, nikaelezea shida yangu, nikatenmgenezewa lini mpya ya simu kwa bahati nzuri wakaniambia nikiweka tu salio laini hiyo itaanza kufanya kazi.
“Niwekee”
Nikatoa noti ya dola mia na kumpa dada huyo, aliye nisajilia laini yangu.
“Hapo utajua unaniwekea vocha ya kiasi gani”
Akabaki amenitumbulia mimacho akinitazama machoni kwa mshangao, akaanza kuminya minya simu yake huku akinitazama usoni mwangu kana kwamba ananifananisha na mtu fulani ila anashindwa kuniambia ni mtu gani. Akaniingizia salio la laki moja, kabla sijaondoka akaniita
“Samahani kaka”
“Bila samahani”
“Sijui nimekufananisha au laa”
“Umenifananisha na nani?”
“Mtoto wa waziri mkuu aliye zikwa miezi iliyo pita”
“Sasa dada yangu kama mtu amezikwa atatembeaje?”
“Hapana unaweza kuwa ni pacha wake”
“Hapana, kwani huyo mtoto aliye zikwa, walisema ana pacha wake?”
“Hapana”
“Basi si mimi”
“Ila naye anaitwa Eddy”
“Majina tu yamefanana”
Nikamuaga dada huyu na kuondoka zangu, nikatafuta sehemu iliyo tulia na kumpigia simu blanka
“Dogo upo wapi?”
“Home nani?”
“Acha ujinga hujui sauti yangu”
“Ohoooo kaka Eddy”
Nilimsiki Blanka akizungumza kwa furaha kubwa.
“Nisikikilize, njoo unichukue uwanja wa ndege ila usimuambia mtu kama nipo hapa”
“Nakuja sasa hivi nipe dakika kumi nitakuwa hapo”
“Powa”
Nikakata simu, kutokana nimefika mida hii ya saa sita mchana, nina amini barabarani hakuna foleni nyingi zinazo weza kumfanya akachelewa sana. Nikatafuta sehemu na kukaa. Ndani ya robo saa nikamuona Blanka akishuka kwenye gari aina ya Haria, akaanza kutazama pande zote za sehemu wanapo tokea wageni, nikamfwata hadi sehemu nilipo. Akanikimbilia na kunikumbatia kwa furaha sana.
“Eheee mbona usoni una plasta?”
“Ahaaa nilipata kajitatizo kadogo”
“Mmmmm pole”
Blanka akizungumza huku akilichukua begi langu na kulibebe, tukaingia kwenye gari na kuianza safari.
“Tunaelekea kwa mama au kwa kina Junio?”
“Kwa kina Junio kwanza. Ila mama anaendeleaje?”
“Mama kidogo ana kiunafuu”
“Mungu ni mwema atapona”
“Ni kweli”
Tukafika katika jumba ambalo ndipo ilipo familia yangu, mlinzi akatufungulia geti, nikamuona Shamsa akicheza na Junio kwenye moja ya bustani yanye majani yaliyo katwa vizuri. Walipo liona gari la Blanka, Junio akakatisha mchezo na kuja kasi kwenye gari kumpokea shangazi yake. Junio alipo niona akageuza kumfwata Blanka na kuzunguka upande wa pili wa gari ambapo, akanirukia kwa furaha. Nikamkumbatia huku machozi yakinilenga lenga kwa furaha. Shamsa naye hakuhitaji kubaki nyuma, akanikumbatia kwa furaha kubwa.
“Hamujambo?”
“Hatujambo dady”
“Mama yupo wapi?”
“Anapika jikoni”
Nikambebea Junio na kumshika mkono Shamsa, sote tukaingia ndani, Junio akaanza kumuita mama yake.
“Nini bwana, umesha anza makelele yako Junio”
Niliisikia sauti ya Phidaya ikitokea jikoni akionekana kumkemea Junio aliye kuwa akimuita muda wote.
“Shiiiiiii”
Niliwanyamazisha, nikaelekea jikoni ambapo nikamkuta Phidaya akiwa bize akikata kata nyama. Nikamnyatia kwa nyuma taratibu na kumziba macho yake. Akatulia kwa sekunde kadhaa huku akishika shika mikono yangu.
“Eddy”
Phidaya aliita kwa sauti ya upole, iliyo jaa furaha kwa mbali. Nikavitoa viganja vyangu machoni mwake, akanigeukia na kunitazama. Kwa furaha kubwa Phidaya akanikumbatia huku akiruka ruka kama mtoto. Bila hata salamu, akaniwahi mdomo wangu na kuanza kuninyonya mdomo wangu, alipo ridhika akaniachia, huku machozi ya furaha yakimwagika.
“Baby”
“Ndio mke wangu”
“Nimekumicjeee”
“Hata mimi mke wangu”
Furaha ikarudi upya kwenye maisha yangu, nikamshukuru MUNGU kwa kuweza kunikutanisha tena na familia yangu, wakiwa katika hali nzuri ya furaha na afya nzuri. Tukapata chakula cha mchana, baada ya kumaliza sikuhitaji kupoteza muda, sote tukaelekea nyumbani kwa mama. Wahudumu wa mama wakaanza kunishangaa sana, ila sikuwalaumu kutokana wanatambua kwamba mimi nimefariki. Blanka akanitambulisha kwa daktari anaye muhudumia mama.
“Hali ya mama inaendeleaje?”
“Tumuombe Mungu atamponya, huku nami nikiendelea kuhakikisha ninayaokoa maisha yake kadri ya uwezo wangu”
Dokta Angelina alizungumza huku akinitazama. Nikamuomba dokta Angelina kuingia chumbani kwa mama, akaniruhusu bili kipingamizi. Taratibu nikaufungua mlango wa chumba cha mama na kuingia ndani, nikamkuta mama akiwa amelala kitandani huku amekondeana sana. Sikuamini kama nitamkuta kwenye halii hii mbaya. Nikapiga hatua hadi kwenye kitanda chake, taratibu nikapiga magoti chini huku machozi yakinilenga lenga. Nikamshika mkono wake wa kulia, ulio chomekwa sindano ya dripu la maji, sura ya mama imebadilika sana huku imekunjamana kwa kukonda, mashavu yake yameingia ndani huku nywele zake zikiwa na rangi ya kahawia.
“Mama”
Niliita huku machozi yakianza kunimwagika taratibu, nikarudia tena kumuita ila hakuniitikia kabisa.
“Mama, mwanao Eddy nipo hapa. Nakuomba ufumbue macho yako japo unione mama yangu. Sikufa mama nipo hai, nimerudi tena nyumbani……”
Kidogo mwili wa mama ukatingishika, nikajikuta nikiwa nimemkazia macho nikimtazama machoni mwake, taratibu akayafumbua, akakigeuza kichwa chake upande wangu, akanitazama kwa muda huku akiwa amenishangaa
“Mama ni mimi Eddy, mwanao wa pekee”
Mama akaendelea kunitazama, baada ya muda akatabasamu akishiria kufurahi uwepo wangu. Nikamuunga mkono na mimi nikatabasamu huku nikitokwa na machozi ya furaha kidogo. Gafla mama akayafumba macho yake, mwili wake ukaanza kutetemeka, hali ikazidi kuwa mbaya baada ya kuanza kuirusha rusha miguu yake kwa nguvu hadi kitanda kikaanza kutingishika tingishika. Nikazidi kuchanganyikiwa zaidi baadaya ya mapovu kuanza kumtoka mdomoni, na mwili wake ukizidi kukakamaa.
“Doktaaaaa Doktaaaaa……………..!!!!”
Niliita kwa sauti ya juu, ya kuchanganganyikiwa kwani hali ya mama, ilizidi kuwa mbaya kiasi kwamba nikaanza kuhisi kumpoteza duniani mama yangu kipenzi.
Daktari akaingia haraka, ndani ya chumba tulichopo. Kwa haraka akaanza kumuhudumia mama huku akiniomba niweze kutoka nje nimuache aifanye kazi yake kiufasaha. Nikatoka nje huku machozi yakinimwagika. Phidaya akanifwata kwa haraka baada ya kuniona ninatokwa na machozi mfululizo
“Baby kuna nini?”
“Mama anakufa”
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUTUMIA AKAUNTI YAKO YA FACEBOOK, LIKE UKURASA HUU USIPITWE NA SIMULIZI NA MENGINE HUKO FACEBOOK