SORRY MADAM (118)

Zephiline F Ezekiel
SORRY MADAM (118)
JINA: SORRY MADAM Mwandishi: Eddazaria G Msulwa SEHEMU YA MIA MOJA KUMI NA NANE ILIPOISHIA... Nikamuona Tasiana akiingiazwa kwenye gari la wagonjwa na kuondoka katika eneo la uwanja wa ndege, sikufahamu wanakwenda katika eneo gani.  NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... Nikashuka kwenye gazi za ndege huku nyuma yangu nikiwa nimeongozana na askari wawili. Baadhi ya waandishi wa habari walikatazwa kunipiga picha yoyote, huku mmoja wa askari akisikika akiyazungumza maneno haya mara kwa mara pale alipokuwa akisogezewa maiki za waandishi wa habari. “HUYU JINA LAKE NI EDDY NA WALA SI GAIDI” Maneno yake yakazidi kunipa matumaini ya kuamini kwamba kile kilichopo mbele ya maisha yangu hakita kuwa kigumu sana kwani sina hatia yoyote katika hilo. Tukaingia kwenye moja ya gari la polisi lenye rangi nyeusi, huku tukiwa na askari wawili wenye pikipiki kubwa nyeupe zenye kupiga king’ora, mmoja akiwa mbele na mwengine akiwa nyuma. “Mbona munanipeleka kwenye mahojiano huku k…