SORRY MADAM (59)
JINA: SORRY MADAM Mwandishi: Eddazaria G Msulwa SEHEMU YA HAMSINI NA TISA ILIPOISHIA... “Tuachane kwanza na hayo,mume wako yupo?” “Nimeachana naye?” “Umeachana naye,kisa ni nini kilicho wafanya muachane?” “Wee acha tuu.Ila kila kitu wewe unakijua?” “Mimi,mbona kama sikumbuki?” NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... “Eddy usinikumbushe ya nyuma” “Kweli? Ok labda nikutokana na kupoteza kwangu kumbukumbu” Nilizungumza kwa sauti ya upole kwa kumtega Madam Mery. Ukimya wa dakika kama tatu ukapita huku kila mmoja akiwa atamtazama mwenzake “Mery” “Una nipenda?” “Ehee?” “Unanipenda?” “Mimi?” “Wewe,ndio?” “Ndio” “Kwa nini umeamua kutembea na rafiki yangu?” “Ehee.....ahaaa uun....ajua” “Najua nini?” “Wewe.....wewe ulikuwa umepotelea wapi sijui?” “Hujanijibu swali langu” “Ahaa Eddy tuachane na hilo bwana” “Sawa. Nataka kuliona kaburi la mwanangu” “Eheee” “Hivi hizo Eheee zako ni za nini, Mimi sizipendi bwana” “Eddy, Sikumzika mwanao” Nikakaa kimya nikimtazama ni nini anataka kuniambia “Ila i…