SORRY MADAM (66)
JINA: SORRY MADAM Mwandishi: Eddazaria G Msulwa SEHEMU YA SITINI NA SITA ILIPOISHIA... Nilizungumza huku nikiendea kumwagikwa na machozi mengi, malengo yangu yote niliyo jiwekea kuja kuwa daktari bingwa nchini Tanzania yametoweka kabisa, hapa ndipo nikaanza kuamini kwamba pesa haitimizi malengo ya mtu, kwani tangu nimezaliwa sikuwahi kuishi maisha ya shida kwani baba anapesa na mama ndio tajiri kupindukia, ila kwa sasa ndio wamekuwa maadui sana. NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... Sikujua baba yangu wa damu anaendeleaje, kwani sikupata hata muda wa kukaa na mama na kumuuliza kuhusiana na baba yangu aliyepo Afrika kusini Macho yangu, nikaendela kuyakaza kwenye kioo, nikiitazama sura yangu, iliyo jaa dhambi na ukatili ulio mkubwa.Sikupenda kuwa hivi, ila matatizo yakanibidi mimi kuwa hivi “Mungu, nisamehe, mimi ni mwenye dhambi tena dhambi nyingi.Ila ninaomba nimuue Mzee Godwin tuu.Ili nikifa nife kwa amani” Nilijikuta nikizungumza maneno haya ambayo sikujua…