SORRY MADAM (82)

Zephiline F Ezekiel
SEHEMU YA THEMANINI NA MBILI
ILIPOISHIA...
“ngoja noisome”
Nikaitoa simu mfukoni na kumpa john anitolee namba za siri alizo ziweka kwenye simu yake upende wa meseji kisha akanirudishia
{kaa mbali na hii vita kati yangu mimi na eddy, utaumia}

NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU

SASA ENDELEA...
Nikairudia kuisoma tena meseji kwa msisitizo, kisha nikamtazama john, huku mapigo ya moyo yakianza kunienda mbio
“nani aliye ituma hii meseji?”
“mimi wala sijui, kutoka hata namba yenyewe haionekani”
“mmmmmm, ulimuonyesha mtu mwengine tofauti yang?”
“pale ilipokuwa inaingia, ndio nikakukabidhi hiyo simu”

Nikashusha pumzi kubwa huku nikiendelea kumtizama john machoni, nikajaribu kuipiga namba iliyo tuma hii meseji ila haikenda zaidi ya kukatika.Tukafika nyumbani kwa baba, mazingira nikayakuta yamebadilika kwa kiasi kikubwa sana, kuanzia nje hadi ndani, sikumkuta yule mama wa kambo aliyekuwa akinisumbua akili yangu kipindi nilipokuja kwa mara ya kwanza

“una mpango gani, juu ya hili eddy?”
Baba aliniuliza mara baada ya mimi, kukaa kwenye moja ya sofa lililopo hapa sebleni, nikakaa kimya kwa muda kabla sijamjibu baba, kwani akili yangu ikaanza kutafakari juu ya meseji aliyo tumiwa john, inavyo onekana mtu huyo ananijua mimi vizuri ndio maana ameamua kunifanyia unyama wa kumuangamiza mke wangu

“sijajua baba”
Jibu langu, likamfanya john kunitazama kwa mashangao
“ngoja tupate ripoti ya polisi juu ya muhusika, wa tukio zima kisha tutajua nini cha kufanya”
“sawa baba”
Baba alizungumza na kuanza kupandisha ngazi kuelekea ghorofani, nikasikia sauti ya kike ikizungumza na baba, ikanilazimu kusimama kutazama ni nani anaye zungumza naye, macho yangu yakakutana na macho ya mototo wa mama wa kambo, ambaye kipindi ninakuja kwa mara ya kwanza nyumbani kwa baba, yeye alikuwa chuo akisoma

“waoooo kaka eddy”
Alinikimbilia na kunikumbatia kwa furaha, sikuamini macho yangu kwani mimi na yeye kidogo kuta tofauti zilizo tokea kipindi cha nyuma, hususani swala la mimi kumpiga mama yake
“za huku utokapo?”
“si salama”
Nikamuona john akimshangaa huyu dada yangu, akataka kumpa mkono ila akasita, ikanilazimu nimtambulishe mimi

“dada huyu ni rafiki yangu anaitwa john, na john huyu ni motto mwengine wa baba yangu”
“nashukuru kukufahamu”
John alizungumza huku akimpa mkono dada yangu
“eddy unatabia mbaya”
“kwa nini dada?”
“hadi leo hulitambui jina langu”
“ahaaa”
Nilibaki nikitabasamu tu, kwani ni kweli jina lake sikuwa ninalikumbuka vuzuri

“mimi ni victori”
“ahaaa, kama lilikuwa likinijia kwenye akili yangu vile?”
“kwenda kulee, ulikuwa hulijui”
Alizungumza kwa utani, huku akiichezea chezea mikono yangu, tukatizamana kwenye macho kwa sekunde kadhaa, sote tukajikuta tukiwa kimya
“mama yupo wapi?”
Nilimuuliza na kumfanya apooze gafla, akaniachia mikono yangu na kwenda kukaa kwenye moja ya sofa, huku machozi yakimlenga lenga, akainyanyua sura yake kidogo na kunitazama

“mama, amesha fariki”
Alizungumza kwa sauti ya upole huku machozi yakianza kumtoka, nikapiga hatua hadi alipo kaaa, nikamkumbatia, huku na mimi hisia za mke wangu kufa, zikaanza kunijia kichwani
“eddy kwa nini unalia?”
“mke wangu amekufa”
“weeee”
Victoria alistuka baada ya kusikia maneno haya
“amefariki lini?”
“leo”
“leoooo?”
“ndio”
“kwa nini?”
“amefariki kwa mlipuko wa bomu baada ya kutekwa, na mtu asiye julikana”

John akabaki akitutizama jinsi tunavyo zungumza mimi na dada yangu, victoria akanikumbatia kwa nguvu na kuanza kunibembeleza kwa hisia kali, tukaachana na stori za kufa kwa mke wangu, tukaendelea kuzungumza kuhusiana na mambo mengine, muda wa chakula ukawadia na sote tukakaa kwenye meza maalumu ya chakula, nikagundua kitu kutoka kwa john, wakati wote alikuwa na kazi ya kumtazama victoria kwa macho ya kumtamani.Tukamaliza kula mimi na john, tukaelekea kwenye chumba change

“john mbona ulikuwa unamtazama sana victoria?”
“hapana”
“mmmmm john wewe hakuna cha hapana, au umempenda nikuunganishine”
“ahaaa eddy, ila ngija kuna kitu ninakichunguza, kikikamilika nitakuambia”
“kitu gani?”

John akautazama mlango wa kuingilia humu ndani ya chumba change, akapiga hatua za taratibu huku akiniomba ninyamaze kuzungumza, akaliweka sikio moja kwenye mlango, huku mkono wake mwingine ukishika kitasa cha kufungulia mlango, akaanza kuufungua taratibu, mimi nikawa na kazi ya kumtazama jinsi anavyo fanya.Akauvuta kwa nguvu, macho yetu yote yakakutana na victoria akiwa amevalia nguo ya kulalia, inayo onyesha nguo yake ya ndani

“vicktoria vipi?”
Nilimuuliza victoria baada ya yeye kushindwa kuzungumza kitu kinacho mfanya asimame nje ya mlango wetu, akaanza kuvunja vinja vidole vyake kwa aibu, akamtazama john, ambaye hakuwa amezungumza kitu cha aina yoyote, akamshika john shati lake, kisha akamvuta karibu yake na kumpiga busu la mdomo na kunifanya nibaki nikiwa ninamshangao

“I need you john”(john, ninakuhitaji)
Victoria alizungumza huku akimsukumia john ndani ya chumba, changu, kama simba mwenye njaa victoria akamsukumiza john kitandani na kuanza kumvua shati, lake, kwa aibu ikanilazimu mimi kutoka ndani ya chumba nikawaacha waendelee na mambo yao

Nikaelekea moja kwa moja jikoni, nikachukua maji ya kunywa kwenye friji lililopo humu jikoni, kisha nikakaa kwenye kiti kirefu ambacho nacho kipo humu ndani ya chumba.Mawazo yakaanza kurudi upa juu ya mtu aliye mteka mke wangu na kumuua kinyama kwa kumlipua kwa bomu

“nilazima nilipize kisasi kwa yoyote aliye husika katika hili”

Nilijiapiza kimya kimya huku nikiyatazama maji yaliyopo kwenye glasi niliyo ishika mkononi mwangu, nikaitazama saa ya ukutani na kukuta ikionyesha ni saa sita kasoro dakika ishirini, usiku

“hawamalizi na sasa hivi”

Nilizungumza huku nikinyanyuka kwenye kiti na kutoka nje, na kuwakuta walinzi wakizunguka zunguka kaimarisha ulinzi wa jumba hili la baba yangu, sikutaka kuzungumza na mtu wa aina yoyote zaidi ya kubatazama mandhari mazuri yalipomo kwenye eneo hili

“hei”
Nilimuita mlinzi mmoja aliye kuwa anakatiza karibu yangu
“ndio bosi”
Kwa bahati nzuri mlinzi huyu alinijibu kwa kiswahili
“ninaweza pata usafiri muda huu”
“kivipi?”

“nina maanisha ninaweza kupata gari, lolote lenye funguo”
“unataka kwenda wapi usiku huu?”
“kuna sehemu ninahitaji kwenda”
“kwa hapo, ndugu siwezi kukusaidia kwani bosi hajatoa ruhusa ya mtu yoyote kutoka na usafiri, tena muda huu wa usiku”

“ahaa powa asante”

Nikaachana na mlinzi na kurudi ndani, nikafika hadi mlango wa kuingilia chumbani kwangu, nikaweka sikio la upande wa kulia, nikasikia miguno ya mahaba ikiwa inaendelea ndani ya chumba change.
“mmmm kazi kweli kweli”

Nikapata wazo la kwenda chumbani kwa victoria japo kuegesha kichwa change kidogo, hii ni kutokana na uchovu mwingi.Nikaingia na kuwasha taa, kitu cha kwanza nikakutana na mwanga wa simu ya victoria, ikionyesha ni muda mfupi kuna meseji au simu ilipigwa.Nikapiga hatua hadi kitandani ilipo, nikaichukua na kutazama, na kukuta missed call na namba ambayo haikuwa na jina lolote.Nikafungua kipochi chake kilicho kuwa pembezoni mwa simu, nikakuta noti kumi za dola mia mia

“yess, kazi yangu imeanza kukamilika”

Nikazichomoa noti hizo, na kuzidumbukiza kwenye mfuko wa jinzi langu, ambapo kuna simu ya john, aliyo nikabidhi muda wa mchana.

Nikatazama salio kwenye simu ya victoria nikakuta lipo lakutosha, nikaiweka mfukoni, nikafungua kabatini kwake na kukuta makoti mengi makubwa ya baridi.Nikachukua koti jeusi na kulivaa, nikachukua kofia ya kuzuia baridi na kuivaa, nikatoka nje ya chumba cha victoria.Kutokana ni mzoefu sana wa jumba hili la baba haikuwa, ngumu sana kwangu kutoroka pasipo walinzi kunioa, nikatoka nje ya ukuta wa jumba hili, kwa kuuruka, nikaanza kutembea kuelekea barabara kuu, kwa bahati nzuri nikapata taksi

“nipeleke kwenye uwanja wa ndege, wa ‘johannesburg’, itakuwa ni bei gani?”

“dola mia”

“sawa”

Kutokana nina kiasi cha kutosha cha pesa, sikuwa na haja ya kumbembeleza dereva huyu, japo ninatambua amenipiga kizinga, kutokana na ugeni wangu, tukatumia dakika ishirini kufika uwanja wa ndege.

“unaweza kunisubiri?”

“bili shaka”

Nikampa dereva taksi pesa yake, nikaelekea sehemu ya huduma kwa wateja, na kuwakuta dada kadhaa wakiwa wamejipanga wakizungumza na baadhi ya abiria waliopo kwenye eneo hili

“samahani dada”

“bila samahani, nikusaidie nini?”

“juzi usiku, kuamkia jana nilifika hapa na ndege ya shirika la nchini philipines, kuna kitu ninahitaji kukipata kwenye kwenye safari ile”

“kitu gani?”

Dada huyo alinijibu kwa umakini, huku akinitazama usoni

“nahitaji video zilizo rekodiwa kwenye safari nzima, kutoka philipines hadi hapa south africa

“eheeeee, kaka yangu, mbona hiyo ni kazi kubwa sana, na kwakitengo changu, mimi siwezi kukusaidia”

“unaweza, nitakupa pesa yoyo……”

Mngurumo(vibration) wa simu ya vivtoria, ukaanza kutetemesha mfuko wangu, ikanilazimu kuitoa simu yake na kukuta meseji ikiwa imeingia, nikaifungua ila nikakutana na batani nyingi zikiniomba niiingize neno la siri ili niweze kuifungua meseji hiyo

“akhaaaa”

Nilijisemea mwenye baada ya kushindwa kuifungua meseji hiyo, nikamgeukia dada niliyo kuwa nikizungumza naye, nikakuta akimalizia kumnong’oneza rafiki yake, aliye kaa kiti cha pembeni yake

“niambie sasa dada, inawez……”

Akanikatisha mazungumzo yangu, kwa kunikonyeza kwa jicho lake kubwa kiasi, akanionyeshea ishara kwa macho nitazame juu yangu, nikakuta kameta ya ulinzi ikinirekodi

“nifwate”

Alizungumza kwa sauti ya chini, akajinyanyua kwenye kiti alicho kalia, akatoka kwenye chumba walichopo nikaanza kuongozana naye kuelekea anapo kwenda yeye, tukapandisha kwenye ngazi, sikujua ni wapi ananipeleka.Tukafika kwenye moja ya ukumbi wenye viti vingi, vya kupumzikia.Akatafuta sehemu iliyo tulia na kuniomba nikae

“eheee kaka ulikuwa unasemaje?”

Nikamuelezea nini ninacho kihitaji, akaniomba nimsubiri kama dakika kadhaa atarudi na kitu ambacho ninahitaji, ila akaniomba nimpatie malipo ya awali, na tulikubaliana nimpatie dola mia tano kwa kazi atakayo nifanyia.Nikaito simu ya john na kufungua upande wa picha, nikajikuta nikistuka baada ya kuzikuta picha za john na victoria wakiwa pamoja, kwenye fukwe za bahari, ila sikujua ni nchi gani.Nikazidi kwenda mbele na kukuta picha nyingi wakiwa pamoja, hapa ndipo nikagundua kuna mahusiano ya kimapenzi kati ya john na victori

“ahaaa, ndio maana nilivyo kuwa ninawatambulisha john alistuka, kumuona victori….”

Nilijisemea mimi mwenye, kimoyo moyo, huku nikiendelea kuzitazama picha walizo piga pamoja, nikaingia upande wa namba za simu na kuanza kuandika jina la victoria na kukuta likiwa limeandikwa ‘my wife v’, nikajaribu kuipiga namba, ikaingia kwenye simu ya victoria na kutokea jina la ‘baby john’

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI

KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger

Chapisha Maoni