SORRY MADAM (83)

0
SEHEMU YA THEMANINI NA TATU
ILIPOISHIA...
Nilijisemea mimi mwenye, kimoyo moyo, huku nikiendelea kuzitazama picha walizo piga pamoja, nikaingia upande wa namba za simu na kuanza kuandika jina la victoria na kukuta likiwa limeandikwa ‘my wife v’, nikajaribu kuipiga namba, ikaingia kwenye simu ya victoria na kutokea jina la ‘baby john’

NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU

SASA ENDELEA...
“wamejuana juana vipi?”

Ni moja ya swali lililo anza kuniumiza kichwa change, kabla sijajipatia jibu kichwani mwangu, muhudumu akarudi akiwa ameshika laptop ndogo mkononi mwake.

“chukua hii, nenda chooni, katazame kuna video nimeiiba ndani kwenye chumba cha mawasiliano”

“powa”

“fanya haraka mimi ninakusubiria hapa, nenda moja kwa moja kwenye ile kordo kunja kulia, utakuta vyoo”

Nikanyanyuka katika sehemu nilipo kaa, moja kwa moja nikaelekea katika sehemu alipo nielekeza muhudumu huyu, nikaingia kwenye choo cha wanaume, nikaifungua laptop aliyo nipa na kukuta faili moja lili andikwa video, nikalifungua

Nikaanza kuona mkanda wa video, katika ndege ya shirika la philipines, video hii imerekodiwa kwa kamera za ulinzi lilizipo kwenye ndege tulio kuja nayo, nikaanza kuona abiria wakiingia, ikiwemo mimi na phidaya.Ikanilazimu kuisimamisha video mara moja baada ya kumuona victoria akiingia ndani ya ndege hii, ila alikaa siti ya nyuma kabisa, pamoja na abiria mwengine.

Katikati ya safari nikamuona john akiwa anazungumza mara kwa mara na victoria, pia nikaona jinsi john alivyokuwa akizungumza na mimi.Hadi ndege inafika, na sisi tunatoka kwenye ndege nikaumuona john akizungumza na victoria, wakakumbatiana kwa pamoja na kila mmoja akaondoka zake

Kwa kamera zilizopo nje ya uwanja wa ndege, nikamuona victoria akiingia kwenye moja ya gari jeusi na kuondoka huku, mimi na phidaya tukiwa tumekaa katika sehemu tuliyo kuwa tumekaa na kuondoka pamoja na john.Nikashusha pumzi nyingi, nikapata kumbukumbu za haraka kuhusiana na gari ambalo aliingia victoria kwani nililiona likiwa kwenye maegesho ya hoteli tuliyo kuwa tumefikizia.

Nikaifunga laptop, na katikti yake nikaweka noti tatu za dola mia mia, ili kukamilisha malipo ya dola mia tano, kutokana tayari nilisha mlipa dola mia mbili kama utangulizi wa kazi, nikarudi na kumkuta akiwa ananisubiri.Nikakaa kwenye kiti nilicho kuwa nimekalia, wakaingia askari wawili ndani ya ukumbi tuliopo, wakatutizama kwa umakini mimi na muhudumu na kuanza kupiga hatua za kuja sehemu tulipo kaa

Nikastukia kumuona muhudumu akinishika mashavu yangu, akaanzak kuinyonya midomo yangu, huku macho yake yakiwatazama askari wanao karibia kufika kwenye meza yetu

“mmgghhh”

Askari mmoja aliguna na kumfanya muhudumu huyo kuniachia taratibu, akatabasamu na kuwafanya askari hao watabasamu, akazungumza nao kizulu

“sizibuna ukuthi kungani muna?”(mbona munatabasamu?)
“sibona lapho nabasekweni”(tunaona upon na shemeji)
“yebo, nabasemzini zakho lokhu”(ndio shemeji yenu huyu)
“siyakubongela thina kudlule”(hongera sisi tunapita)
“esizayo efanayo”(sawa baadaye)
Askari wakaondoka na ku kutuacha sisi tukiwatazama
“haita jirudia tena”

Muhudumu alizungumza huhu akijifuta mdomo wake, kwa kitambaa

“pesa yako nimeibananisha katikati ya laptop, asante”

“sawa”

Nikanyanyuka na kuondoka, nikatoka nje ya uwanja wa ndege na kuingia katika taksi niliyo kuja nayo, nikamuomba dereva anipeleke ilipo hoteli tuliyo fikizia, njia nzima moyo wangu ukawa na maswali mengi kati ya john na victoria wamejuana vipi

“ahaaa, ila inaweza kuwa ni mambo ya kidunia”

Nilijisemea mwenyewe na kumfanya dereva taksi kunitazama, tukafika kwenye hoteli, tukasimama kwenye maegesho yamagari, nikashuka kwa bahati nzuri nikaliona gari alilo ondoka nalo victoria, nikapiga hatua hadi lilipo na kuchungulia kwenye dirisha, lake, sikukuta mtu ndani.Mlio wa mbwa na tochi za walinzi zikanistua, wakaniamuru nisimame kama nilivyo huku mikono yangu nikiinyoosha juu

Wakafika katika sehemu nilipo simama na kunza kunikagua, ila askari mmoja akastuka baada ya kuniona, akawanong’oneza wezake, ambao walikuwa wameninyooshea bunduki zao, wakazishusha chini

“samahani bwana bosi”

Askari huyo alizungumza huku akijaribu kutengeneza tabasamu la kinafki usoni mwake, huku akionekana kutahayari kwa kitendo walicho nifanyia

“hii gari ni yanani?”
“ahaa, hili gari ni la mkurugenzi victoria”
“yeye yupo wapi?”
“alikuja nalo juzi usiku, ila kutokana sikuingia mchana zamu sijajua aliondoka vipi”

Nikajaribu kuuvuta mlango wa gari upende wa dereva na likafunguka.Nikaufunga mlango nikaondoka na kuwaacha walinzi wakiulizana maswali kadhaa, nikafika kwenye chumba cha kurekodia video zote zinazo chukuliwa na kamera za ulinzi.Sikuamini macho yangu baada ya kuwakuta wafanya kazi wawili wa chumba hichi, wakiwa uchi wa mnyama, wakifanya mapenzi na msichana, anaye onekana ni kahaba

Walipo niona wakastuka, na kila mmoja akasimama sehemu yake, huku msichana wanaye fanya naye mapenzi akiziwahi nguo zake zilizo kuwa juu ya meza, na kujifunika katika sehemu zake za siri.Nikawatizama jinsi wanavyo babaika, sikutaka kuwasemesha kitu cha aina yoyoye zaidi ya kwenda zilipo computer nyingi

“kuna video ninazihitaji”

“sawa sawa bosi”

Akawasha computer moja, nikamuelezea, video ninayo ihitaji ni ile ya siku nilipokuwa ninafika hapa hotelini, nikaanza kuyaona matukio yote tangu nikiwa ninaingia na phidaya sebleni, katika usiku ule nilimshuhudia john akizungumza na victoria katika sehemu ya vinywaji, baada ya mimi na mke wangu kuingia ndani ya chumba chetu cha kupumzikia.Nikawaona wakiingia kwenye moja ya chumba ambacho si kile john alicho kichukua

“mnamjua huyu?”

Nilimuonyesha john kwa kutumia kidole changu’’

“huyu ndio tunamjua, mara kwa mara huwa anakuja na mkurugenzi victoria”

Nikaona mwanamke mwengine akiingia ndani ya chumba alichokuwa john na victoria, huku akiwa amevaa baibui lililo mficha sura yake na kumbakisha macho tu

“huyo aliye ingia ni nani?”

Jamaa akairudisha nyuma video, hadi sehemu anayo ingia mwanamke huyo ambaye, ndiye aliye mteka na kumuua mke wangu.

“mlimuona kipindi akiingia ndani ya hicho chumba?”

“hapana bosi”

“iendeleze”

Jamaa akaiendeleza video, inayo onyesha watu wakiingia na kutoka kwenye vyumba vyao, kutokana  na camera hizo zimetengwa kwenye kordo ya hoteli hii.Baada ya muda nikamuona john akitoka ndani ya chumba hicho, akaondoka zake, baada ya dakika chache akatoka victoria na kuondoka, ila msichana huyo hakutoka hadi inatimu muda wa asubuhi ndipo naye akatoka, hapa ndipo nilipo ipata picha kamili kwamba kuna mchezo ambao ninachezewa na john pamoja na victoria.Nikajikuta nikiwa ninahasira dhidi ya john na victoria ambao wanaonekana wana siri kubwa sana waliyo ificha

“huyo msichana alikwenda wapi?”

Wakanionyesha video ambayo tuliiangalia muda baada ya mke wangu kutekwa na msichana huyo ambaye hadi sasa hivi sura yake sikuweza kuijua

“hembu nitolee hizo picha zake”

Jamaa akanitolea picha za msichana huyo aliye vaa baibui, kwa kutumia mashine ya ‘printing’ nikaikunja karatasi yenye picha ya msichana huyo na kuiweka mfukoni mwangu, nikatoka nje ya chumba na kurudi nilipo muacha dereva taksi, huku moyoni mwangu nikiwa ninahasira ya kwenda kutembeza kipigo kati ya john na victoria hadi waseme ukweli ni wapi alipo mke wangu.

“nirudishe kule tulipo anzia safari yetu”

Nilimuambia dereva taksi naye akatii, safari ikaanza kwa mwendo wa kawaida huku saa iliyopo kwenye simu ya john ikionyesha ni saa kumi na moja na dakika kumi, alfajiri.

“ongeza mwendo dereva tuwahi kufika”

Nilimuamrisha dereva taksi, akazidisha mwendo kasi wa gari kutoka spidi ya themanini hadi mia moja na thelathini, gafla nikastukia kumuona derava taksi akipiga kichwa kwenye mskani wa gari, huku akitoa mlio wa maumivu, makali, gari ikayumba na kutoka kwenye barabara, huku vitu vigumu vikipiga kwenye kioo cha mbele cha gari, na upande wa pembeni wa gari.

Kwa akili ya haraka nikagundua kwamba ni risasi zinazo piga kwenye gari letu, lilili poteza muelekezo na kusababisha lizunguke kutokana na miguu ya dereva kufunga breki za gafla na kuyazuia matairi yote kutembea.Nikabaki nikiinama chini, huku nikijitahidi kuushika mskani wa gari kuhakikisha gari haizidi kupoteza muelekeo.Risasi zisizo ni milio ya bunduki zikazidi kumiminika kwenye vioo vya gari tulilopo, sikujua hata zinatokea wapi.Chakumshukuru mungu, gari ikapiga kwenye mti mkubwa ulio pembezoni mwa barabara na kulisabaisha lisimame na kutulia.Mianga mikali ya taa za pikipiki nikaziona zikija kwa kasi kwenye sehemu gari lililopo

“nimepona…….?”

Nilizungumza huku nikijipapasa mwili mzima, sikujihisi maumivu yoyote kwenye mwili wangu, zaidi ya vioo vingi, vidogo vidogo vilivyo vunjwa kwa risasi, kuniangukia kwenye koti nililo livaa pamoja na suruali yangu, kwa haraka nikajirusha kwenye siti ya nyuma ya gari, jamaa wenye pikipiki wakazidi kulisogelea gari nililomo.Sikutaka kujua kwamba dereva taksi ni mzima au amekufa, nilicho kifanya ni kuufungua mlango wa nyuma upande ambao gari imepiga kwenye mti.Nikatambaa haraka hadi nyuma ya mti na kujibanza, huku nikihema sana. Nikachungulia nikawashuhudia majamaa kama sita wenye pikipiki kubwa, wakiwa wamevalia makoti, makubwa meusi, huku wakiwa na bunduki mikononi mwao zilizo fungwa viwambo vya kuzuia sauti

Wakasimama mita chache kutoka lilipo gari, na kuanza kulishambulia tena kwa risasi, na kuzidi kunipa woga mwingi.Dakika kama tano hivi zikakata kwa majamaa kulishambulia gari letu kwa risasi, nyingi, nikachungulia kidogo, nikamuo jamaa mmoja akipiga hatua za taratibu hadi ilipo gari na kuichungulia ndani, na kuonekana akistuka sana

“hayupo muhusika”

Alizungumza kwa sauti ya juu, huku akiwatazama wenzake, anaye onekena ni mkubwa wao akatoa simu, na kuminya minya na kuiweka sikioni, gafla simu ya victoria ikaanza kutetemeka mfukoni mwangu, kutokana kuweka mlio ulio katika mfumo wa mtetemeko(vibration).Nikaitoa kwa haraka mfukoni mwangu na kwabahati nzuri ikawa imesha jipokea kotokana na kuibabatiza kwenye mfuko wangu wakati ninaitoa kwa haraka mfukoni mwangu, kutokana ni ‘screan touch’ nikasikia sauti ikitoka kwenye simu iliyo pigwa ikizungumza kwa sauti ya juu kidogo

“bosi muhusika hatujampata”

Maneno hayo yanafanana na jamaa anaye piga simu hiyo, nikachungulia na kumuona jamaa akiishusha simu yake kutoka sikiooni mwake

“vipi”
“bosi azungumzi chochote”
“inakuwaje sasa?”
“hivi mnauhakika hii ndio taksi, tuliyokuwa tukiifwatilia aliyo ipanda huyo eddy?”
Mkubwa wao aliuliza
“ndio hii, hembu mpigie bosi, kwenye ile namba yake nyingine”

Jamaa mmoja alimshauri mwenzake na kuinyanyua tena simu yake na kuiweka sikioni, nikajikuta nikiitumbulia mimacho simu ya victoria nikisikilizia kuingia kwa simu hiyo.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI

KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)