SORRY MADAM (83)

Zephiline F Ezekiel
SORRY MADAM (83)
JINA: SORRY MADAM Mwandishi: Eddazaria G Msulwa SEHEMU YA THEMANINI NA TATU ILIPOISHIA... Nilijisemea mimi mwenye, kimoyo moyo, huku nikiendelea kuzitazama picha walizo piga pamoja, nikaingia upande wa namba za simu na kuanza kuandika jina la victoria na kukuta likiwa limeandikwa ‘my wife v’, nikajaribu kuipiga namba, ikaingia kwenye simu ya victoria na kutokea jina la ‘ baby john ’ NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... “wamejuana juana vipi?” Ni moja ya swali lililo anza kuniumiza kichwa change, kabla sijajipatia jibu kichwani mwangu, muhudumu akarudi akiwa ameshika laptop ndogo mkononi mwake. “chukua hii, nenda chooni, katazame kuna video nimeiiba ndani kwenye chumba cha mawasiliano” “powa” “fanya haraka mimi ninakusubiria hapa, nenda moja kwa moja kwenye ile kordo kunja kulia, utakuta vyoo” Nikanyanyuka katika sehemu nilipo kaa, moja kwa moja nikaelekea katika sehemu alipo nielekeza muhudumu huyu, nikaingia kwenye choo cha wanaume, nikaifungua laptop aliyo ni…