SEHEMU YA THEMANINI NA SITA
ILIPOISHIA...
Madam Merry alizungumza kwa sauti ya juu, yenye uchungu ndani yake.Akalitupa chini panga lake alilokuwa amelishika.Machozi mengi yakaanza kumbubujika usoni mwake, John na Vivtoria wakabaki wakimtazama madam Mery, ambaye taratibu alianza kupiga hatua za kuelekea kwenye gari lake alilo kuja naloNIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
“Madam Vipi?”
John alizungumza huku akimwafwata madam Mery kwa nyuma
“John ninakuomba uniache”
Madam Mery aluzungumza huku akiunyanyua mkono wake mmoja akimzuia John asimfwae anapo elekea
“Ila madam haya sio makubaliano yetu”
“John sipo sawa nimekuambia usinifwate”
Madam Mery alizungumza kwa sauti ya ukali, huku machozi yakiendelea kumchuruzika usoni mwake.
“Sasa Madam tumfanye nini Eddy?”
Madam Mery akageuka kwa hasira, hadi John akastuka kidogo, akanitazama jinsi machozi yanavyo nimwagika, akayafumba macho yake kwa sekunde kadhaa, akionekana akifikiria kitu cha kufanya juu yangu.
“Kesho nimkute akiwa hai”
Madam Mery alizungumza kwa sauti ya upole, kisha akaelekea lilipo gari lake, akafunguliwa mlango na mlinzi wake, akaingia ndani ya gari na wakaondoka zao.John akalisindikiza magari ya Madam Merry yanayotoka kwenye geti kubwa la Godauni, lilipo fungwa taratibu John akanigeukia, akanitazama kwa macho ya dharau huku Victoria akiwa amejichokea, kwani ninaamini mipango yao waliyo kuwa wameipanga dhidi yangu imeharibika.John akamfwata Victoria sehemu alipo simama, wakanong’onezana kwa muda kasha wakamtama Phidaya ambaye muda wote, amejilaza chini huku machozi yakimwagika kwa uchungu.
“Mchukueni huyo Malaya mumrudishe mulipo mtoa”
John aliwaamrisha watu wake, wakamnyanyua Phidaya na kumbeba juu juu, japo anajitahidi kujitoa mikononi mwa watu walio mbeba, huku aikiliita jina langu kwa sauyti ya juu, ila hakuifanikiwa kujitoa mikononi mwao John akapiga hatua hadi katika sehemu nilipo fungwa, akanitazama kwa muda, huku macho yake yakiwa yamejaa dharau kubwa, akanitemea mate ya usoni, akiyasindikiza kwa kofi zito lililo tua kwenye shavu langu la kushoto
“Mmmmmm Eddy, unajisikiaje?”
John alizungumza huku akivifikisha viganja vyake, na kuvipuliza taratibu taratibu.Akanishika sikio langu la upande wakulia, akaanza kulivuta kwa nguvu zake zote, nikaendelea kuugulia maumivu ndani kwa ndani, sikutoa sauti yoyote kwenye kinjwa changu
“Waooo, unajifanya komandoo usikii maumivu eheeee?”
John alizungumza, huku akiliachia sikio langu.Akaanza kunitandika vibao mfululizo kwenye mashavu yangu, hasira ikazidi kumiliki nafisi yangu.
“John, tumpeleke kisimani, hapo unajisumbua bure”
Victori alitoa wazo ambalo John alilikubali, wafanyakazi wao wakanishusha kwenye meza, majamaa wawili wakanibeba kwenye mabega yao. kama wawindaji walio beba swala waliye muua kwenye mawindo yao.
Tukaingia kwenye moja ya ukumbi mkubwa wenye mwanga hafifu, unao pita kwa kutumia madirisha machache yaliyopo juu yake.Wakanibwaga chini, na kunifanya nitoe mguno wa maumivu kutokana na kujiumiza sehemu ya paja langu, nililo pigwa risasi Taa kubwa zenye rangi nyeupe zikawaka na kulifanya eneo zima la ikumbu kuponekana vizuri, kuna mashimo makubwa mawili, kwa haraka nikatabua ndio hivyo visima wanavyo vizungumzia, mabaunsa walio kuwa wamenibeba, wakaufunga mwili wangu kwa kamba ngumu aina ya manila.
“Eddy utakufa kifo kibaya sana”
John alizungumza huku akiwa ameniinamia
“Usiombe nikatoka, kwenye mikono yeno, utajuta”
Nilizungumza kwa kujiamini sana, John akaanza kucheka kwa dharau, huku akinipiga piga mashavuni mwangu
“Eddy huwezi kutoka mikononi mwangu, nakujua wewe vizuri sana.Huwezi fanya chochote dhidi yangu.Muda wako umekwisha kaka”
“Angalia wakwako ndio utakuwa umekwisha”
John akaanza kunipiga mateke mfululizo kwenye mbavu zangu, nikaendelea kutoa sauti ya maumivu ila John hakunionea huruma zaidi ya kuendelea kunipiga kwa nguvu zake zote
“Mchukueni na mukamdumbukize kwenye kisima”
John aliwaamrisha watu wake, wakanibeba, kabla hawajaondoka na mimi, Victoria akawazuia.Akapi ga hatua hadi sehemu tulipo simama
“Eddy nakupenda kaka yangu, kwaheri”
Victoria alizungumza huku akinibusu shavuni mwangu, akawarusuhu watu kuonipeleka kwenye kisima kilichopo kwenye huu ukumbi, kwa jinsi walivyo nifunga kamba mwili wangu sikuweza kufanya kitu cha aina yoyote zaidia ya mwili wangu kunyooka moja kwa moja, mithili ya mtu aliye fariki dunia.
Wakanifunga kwenye kamba nene, tartibu wakaanza kunishusha kwenda chini, taratibu.Giza jingi lililo tawala ndani ya shimo hili, likazidi kuniogopesha na kunifanya nizidi kuchanganyikiwa.Nikastuykia nikigusa chini, kwenye shimo hili lenye futi zaida kumi na mbili. Gafla nikaanza kuhisi vitu vidogo vidogo vikinitambalia mwilini mwangu, nikastukia mwili wangu ukianza kupata maumivu maklali yaliyo tokana kung’atwa na wadudu wadogo ambao sikujua ni waduudu wa aina gani, jambo lililo
nifanya nitoe ukelele mkali sana
Wadudu wenye meno makali, wakazidi kuushambulia mwili wangu jambo lililo nifanya nizidi kuchanganyikiwa na kuanza kukiona kifo kikisimama mbele yangu, nilicho kuwa nikikisubiria ni pumzi yangu kukatika name niesabike kama mfu kati ya mamilioni ya watu walio tangulia mbele za haki, masaa kadri yalivyo zidi kukatika ndivyo jinsi nilivyo zidi kupata maumivu makali yasiyo mna kikomo, ikafikia kipindi kelele na maumivu yangu hayakupata msaada wa aina yoyote kutokwa kwa mtu yoyote
“Eheee Mungu ninakuomba unisaidie”
Niliamua kumkumbuka Mungu wangu, kama kuna uwezo wowote ambao anaweza kunipatia, kwa wakatui huu, sikua na ubishi wa aiana yoyote kwani ndio tayari nipo kwenye shimo la kifo.Giza likaanza kutoweka taratibu na mwanga mkali wa jua ukitokea juu ya paa lililo funguliwa muda mchache uliopita ikiashiria kwamba asubuhi nma mapema kumepambazuka, hapa ndipo nikagundua aina ya wadudu wanao nishambulia kwamba ni ng’ee wadogo wadogo wenye meno kali sana.
Nguvu za mwili wangu zikaanza kuniishia kadri ya muda unavyo katika, mwili mzima wote umevimba kwa maumivu makali niliyo yapata. Nikaanza kuzisikia kelele za watu wakizungumza ndani ya ukumbi huu, huku kutikana na umbali niliopo kwenda chini kwenye kwenye shimo sikuelewa ni mazungumzo ya aina gani ambayo wanayanzungumza, taratibu nikaaza kuvutwa kwenda juu, na nikatolewa ndani ya shimo na watu walio niiingiza ndani jana.
“Duu huyu jamaa ana roho yap aka, bado yupo hai”
Jamaa mmoja alizungumza huku akinitazama na kunigeuza geuza kwa mguu wake alio valia kiatu kigumu sana, na kila alipokua akinmigusa katika mwili wangu, kwangu ilikuwa ni maumumi makali yasiyo elezeka
“Si bora tumuue tuu”
“Tukimuua unadhani bosi atatuelewa?”
“Sasa mtu ameumuka kiasi hichi unadhani
kwamba atapona huyu?”
“Sina uhakika ila tusubiri hao mabosi wetu wakija
watoe uamuzi juu ya hili”
Jamaa waliendelea kushauriana huku wakiwa wamenizunguka, katika sehemu waliyo nilaza huku kamba waliyo izungusha mwilini mwangu ikiendelea kubaki kama walivyo nifunga, jamaa mmoja ajachukua ndoo ya maoja na kutoka nje, wakabaki jamaa watatu wakiwa wamenizunguka. Huku wakiwa wanavuta sigara zao.Jamaa aliye toka na ndoo akarudi na kuisimamisha pembeni
yangu
“Umeweka nini humo?”
“Kuna maji ya yabaridi nahitaji kumuogesha huyu mwehu”
Jamaa pasipo kufikiria mara mbili ni maumivu ya aiana gani nitayapata, akaanza kunimwagia kuanzia juu hadi chini huku akiungana na wezake katika kunimwagia maji hayo, yaliyo zidi kuviumiza vidonda vyangu.
“Cheki jinsi anavyo babaika”
Mmoja alizungumza huku akininyooshea kidole, wakinicheka jinsi ninavyo garagara chini na kulia kwa maumivu makali ninayo yapata mwilini mwangu
“Bosi anasema mumtoe, mumpeleke kule kwenye godauni”
Jamaa mmoja aliye ingia muda si mrefu aliwapa wezake ujumbe walio anza kuutekeleza ndani ya dakika moja mbeleni, nilidhani watanibeba kama walivyo fanya jana walipokua wakiniingiza ndani ya ukumbi huu. Wakaanza kuniburuta huku wakiwa wanaivuta kamba waliyo nifunga nayo.Tukafika kwenye godauni la jana, nikamkuta John akiwa na Victoria wamesimama wakitungojea tutokee katika sehemu tuliyo simama
“Habari za asubuhi Mr Eddy”
John alizungumza huku akinizunguka zunguka katika sehemu niliyo lazwa, hata kinywa changu hakikuwa na nguvu ya kufunguka kutokana na maumimu makali niliyo yapata kutoka kwa wadudu walio nishambulia usiku mzima
“Ninaimani leo inakuwa ni siku ngumu sana kwako”
John aliendelea kuzungumza huku akiwa amesimama pembeni yangu akinitazama chini, sukuamini Yule John niliye kua nikimsaidia mambo mengi kipindi tunasoma leo hii ndio mtu anaye nifaniyia ukatili wa aina hii
“Mtoeni Yule Malaya”
Walinzi wao wakatii agizo walilo ambiwa na mkuu wao ambaye ni John, ndani ya dakika kadhaa wakarudi wakia wameongozana na mke wangu Phidaya, ambaye amechakaa kwa kiasi kikubwa huku nywele zake zikiwa zimechanguka kama mwenda wazimu, uzuri wake wote umepotea kwenye sura yake, sura yake imejaa alama nyingi za vidole ikishiria kwamba kuna mtu au watu walimpiga muda mchache ulio pita
“Eddy ninakumbuka kipindi tunasoma kombi ya
PCB, ulikua unapenda sana kuwapasua vyura kuona ni kitu gani kipo ndani ya matumbo yao, sasa leo na mimi ninahitaji kumpasua mke wako nione ni kitu gani ambacho amekibeba ndani ya tumbo lake hadi likawa kubwa kiasi hichi” John alizungumza huku akianza kuvaa gloves nyeupe, macho yangu yakakutana na macho ya Phidaya ambaye muda wote anabubujikwa na machozi mengi usoni mwake, akaanza kutingisha kichwa pasipo kutambua ni nini maana ya yeye kukitingisha kichwa chake
“Ohhh naona wifi anahuzuni sana, ila John nimepata wazo”
Victoria alizunguimza huku akimtazama John anaye chagua chagua kisu kikali kwenye moja ya meza fupi iliyomo ndani ya godauni hili
“Wazo gani mke wangu”
“Mimi ninaona tumpe uchaguzi wifi yangu kipenzi”
“Ehee endelea mama”
“Mimi ninaona achague kati ya haya mambo mawili, kumfanyia upasuaji na ukitoe hicho kiumbe cheke au amuue mume wake kwa mikono yake yeye mwenyewe”
Nikamuona jinsi Phidaya alivyo stuka na kuzidi kumwagikwa na machozi mengi usoni mwake, nikamtazama Phidaya ambaye amechanganyikiwa kwa mambo aliyo ambiwa na Vicvtoria
“Yeee hilo ni wazo zuri mpenzi, yaap Shemeji, uamuzi upo mikononi mwako, una dakika mbili za kujifikiria, wewe kuondoka duniani, au wewe kumuondoa mume wako duni ani”
John akaivua saa yake ya mkononi na kumkabidhi Phidaya, akimuomba afanye kama alivyo agizwa.Phidaya akanitazama mimi kwa macho yaliyo jaa uchungu kisha akamtazama John anaye piga mluzi, ulio jaa dharau.
“Dakika zinakwisha shemeji”
Phidaya akajiinamia chini, kisha akanyanyanyua kichwa achake na kunitazama tena kwa mara nyingine pasipo kuzungumza kitu cha aina yoyote.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI
KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Email: ZephilineEzekiel@Gmail.Com