SEHEMU YA THEMANINI NA SABA
ILIPOISHIA...
“Dakika zinakwisha shemeji”
Phidaya akajiinamia chini, kisha akanyanyanyua kichwa achake na kunitazama tena kwa mara nyingine pasipo kuzungumza kitu cha aina yoyote.
NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
Akamrudishia John saa yake kisha, akanyoosha mkono wake kwa John akiashiria kwamba kuna kitu anakiomba
“Nini?”
John alimuuliza Phidaya aliye baki amemnyooshea mkono mmoja pasipo kusema kitu cha aina yoyote
“Kisu”
John akatabasamu na kuchagua kisu kikubwa kiasi chenye ncha kali na kinacho ng’aa, akamkabidhi Phidaya, aliye kishika vizuri na kuanza kupigha hatua hadi sehemu niliyo lala, macho yangu yakanitoka kwani sikuelewa Phidaya anataka
kufanya kitu cha aina gani
“Eddy ninakuomba unisamehe, nafanya hivi kwa ajili ya mwanangu aliye tumboni mwangu, ninaimani nizawadi tosha uliyo nipatia mimi”
Phidaya alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake na kunitazama kwa macho makali.Machozi yakaanza kunimwagika taratibu
“Phi…d….”
“Shemeji usimsikilize huyo muue”
John alizungumza kwa sauti kali, iliyo zidi kumtetemesha Phidaya aliye changanganyikiwa
“Usipo muua ninakufumua tumbo lako hilo, kubwa hilo sasa upo tayari kupoteza maisha yako na
mwanao?”
John aliendelea kuzungumza kwa sauti ya ukali na yajuu kiasi
“Hembu jitazame wewe mwenyewe, jinsi ulivyo mzuri, mwanamke mwenye kupendeza, hadi sasa hivi sijatambua ni kwanini unapata tabu kwa ajili ya mpumbavu mmoja, ambaye sijuu mumekutana wapi?”
John aliendelea kumshawishi Phidaya kufanya anacho hisi kwao kitakuwa ni furaha
“Wifi, mbona wanaume wapo wengi tuu, utapata wanaume wazuri zaidi ya huyo mume wako, huu ni wakati wako sasa, uhai wako upo juu ya mikono yako”
Victoria naye aliamua kusema kitu juu ya Phidaya aliye anza kuchanganyikiwa na kujikuta akiwa amekishika kisu kwa mkono mmoja, taratibu Phidaya akaikutanisha mikono yake kwa pamoja katika kishikizo cha kisu, taratibu akaanza kuinyanyua juu akijiandaa kikishusha kwenye mwili wangu na wala sikujua ni wapi kitwakwenda kutua
“I say kill him”
John aliendelea kuzungumza kwa kufoka huku akimtazama Phidaya anaye mwagikwa na jasho mwili mzima, sikuwa na uwezo wa kufanya kitu cha aina yoyote kutokana mwili wangu wote imefungwa kwa kamba
“Eddy am sorry”
Phidaya akakishusha kisu kwa nguvu, kabla hakijatua kwenye kifua changu akakisimamisha na kukitupa pembeni na kuniangukia kifuani mwangu na kunikumbatia huku akilia kwa sauti ya uchungu
“Nakupenda mume wangu, wewe ni baba wa wanangu, siwezi kukuua kwani sijui nitamjibu nini
mwanangu pale atakapo uliza yupo wapi baba”
Phidaya alizungumza huku akiendelea kunikumbatia kifuani mwangu, machozi yakeendelea kunimwagika huku nikimtazama
Phidaya, Phidaya akasimama kwa hasira na kumtazama John
“Kama unataka kuniua niue tu, ila siwezi kumuua mwanaume wa maisha yangu, niliye jiapiza kwamba sinto weza kumuacha katika maisha yangu yote hadi ninaingia kaburini”
Phidaya alizidi kuzungumza kwa hasira huku akiwa amelishika tumbo lake kwa mkono wa kulia, akichechemea na kumfwata John aliye pigwa na butwaa
“Ni mangapi aliyo kusaidia rafiki yako Eddy, ni vitu vingapi alivyo kutendea Eddy, leo hii unataka kumuangamiza mbele yako, unataka kupelekeshwa na huyo mzungu wako.Kumbuka huyo sio muafrika mwenzio, kumbuka huyo ndio aliye kunyanyasia wazazi wako.Leo hii bado unaende………”
Victori akapimtandika Phidaya kibao kilicho muangusha chini, ila Phidaya akanyanyuka na kusimama, huku akiyumba yumba mithili ya mlevi.Gafla nikaanza kuona maji maji mengi yakichuruzika kwenye miguu ya Phidaya, ambaye alianza kulishika tumbo lake, huku akilia kwa uchungu mkali sana.Nikaanza kujibiringisha taratibu nikilisogelea eneo alilo lala Phidaya huku akiendelea kulia kwa uchungu
“Eddy……”
Phidaya aliita huku akilia kwa uchungu, miguu yake akiwa aimeipanua, jasho jingi likianza kumwagika
“Ba……by p..usssh”
Nilizungumza kwa kujikaza huku nikiwa sina msaada wowote kwa mke wangu, John na watu wake wakabaki wakiwa wametukodolea mimacho huku wengine wakicheka kwa dharau, Victoria akataka kuja sehemu tuliyopo mimi na Phidaya ila John akamzuia, huku akimshika mkono.
“Acha tuone watafanyaje”
John alizumngumza kwa dharau
“Push baby”
Nilizungumza huku machozi yakiendelea kunimwagika usini mwangu Phidaya akazidi kujikakamua, huku akiendelea kulia, kutokana Phidaya ni nesi kidogo kuna mbinu za uzalishaji aliana kuzitumia kwani hapakuwa na msaada wowote kwake zaidi ya mimi kumchochea kwa maneno aweze kumsukuma mtoto atoke nje
“Anakuja baby anakuja”
Phidaya alizungumza kwa uchungu huku akiendelea kuzidi kujikakamua kumzaa mtoto wetu, wazo likanijia haraka, japo ninamaumivu makali mwili mwangu ila nikajigeuza haraka na kuiweka miguyu yangu karibu na miguu, ya Phidaya aliye
zidi kujikaza katika kumleta kiumbe change duniani. Nikamshuhudia mwanangu akitoka taratibu na kufikizia kwenye miguu yangu, Phidaya akajitahidi hadi mtoto wangu wa kiume akalala kwenye miguu yangu, iliyo fungwa kamba kwa pamoja
“Duuuu hongereni sana”
John alizungumza huku akiichomoa bastola yake kiunoni
“John unataka kufanya nini?”
Victori alizungumza, huku akimtazama John aliye anza kuifunga bastola yake kiwambo cha kuzuia sauti
“Sifanyi chochote mke wangu”
John akanisogelea hadi sehemu tuliyo jilaza, akanitazama kwa muda, mimi pamoja na mwanangu aliye anza kulia
“Mwanao ni mzuri sana”
John alizungumza huku akimtazama mwanangu pamoja na mama yake aliye jilaza, akiwa ameishiwa nguvu za mwilini mwake
“Goodbye my friend”(Kwaheri rafiki yangu)
John alizungumza kwa sauti ya upole nikastukia risasi kadha zikitua kifuani mwangu na kuninyamazisha kimya katika sehemu niliyo lala
Sauti ya milio ya ndege nikaanza kuisikia kwa mbali kwenye masikio yangu, taratibu nikajaribu kuyafumbua macho yangu kuweza kuona n kitu gani kinacho endelea ila, ukungu mwingi umawa umetawala kwenye mboni yamacho yangu, jamvo lililo nifanya nisione kitu cha aina yoyote, nikajaribu kupapasa katika sehemu niliyo lala, nikagundua kwamba nimelalia kitanda cha kamba, ila sikuweza kutambua ni sehemu gani niliyopo.Muda jinsi ulivyo yoyoma ndivyo nilivyo weza kugundua kwamba eneo nililopo, kuna watu wanao zungumza lugha nisiyo ijua
“Nipo wapi?”
Nilijarivu kuzungumza huku nikijitahidi kunyanyuka kutoka katika kitanda nilicho lala ila milono ya watu si chini ya wanne wakanirudusha kulala tena kwebye kitanda.Sauti za wanaume pamoja na wanawake zikaendelea kupenya kwenye masikio yangu, nilipo anza kusikia milio ya watoto wadogo wakicheza na wengine kulia ndipo nilipo amini kwamba eneo hili ni salama kwa maisha yangu
Nikawasikia wakiendelea kunong’oneza, mara sauti ya kike ikasikika, ambayo sikuweza kuisikia tangu wà lipo anza kuzungumza watu hawa, ambao hadi sasa hivi siwezi kuwaona vizuri zaidi ya vivuli vyenye giza, vilivyo simana pembeni ya kitanda nilicho kilalia.Nkasikia wakiyazungumza maneno niliyo yasema dakila kadhaa za nyuma nikiwauliza kwamba hapa nilipo ni wapi
“Hei”
Sauti ya msichana hiyo ilinisemesha, ila sikujua anataka kusema kitu gani
“Nipo wapi, dada?”
Nliyarudia maneno yangu niliyo yazungumza hapo awali
“Unazungumza kiswahili wewe?”
Msichslana huyo aliniuliza, kwa lugha ya kiswahili jamvo lililo nifanya nizidi kufarijika moyoni mwangu na kuamini kwamva nimepata mwokozi katika wakahi huu mgunu nilio nao katika yangu maisha
“Ndio, ndio dada”
Niliitikia kwa haraka ila hata ninaye zungumza naye asibadili mawazo ya kunisaidia mimi
“Unaitwa nani?”
“Eddy, Eddy dada yangu”
Nikamsikia msichana huyo akizungumza na wezake huubakilitaja jina langu, kwa wezake ambao ninaamini hawaijui lugha ya kiswahili tunayo zungumza
“Umetokea wapi?”
“Tanzania dada yangu”
“Ulikuja huku kufanyaje?”
“Wapi, kwani hapa ni wapi?”
Kabla sijajibiwa nilicho kiuliza nikasikia sauti za watu waliomo ndani ya chumba wakisalimia kwa pamoja kwa kutumia lugha wanayo izungumza, sauti nzito ya mwanaume ikaitikia na kuwafanya watu wote kukaa kimya ndani ya chumba tulichopo
“Mumesema, ameamka?”
Mwanaume huyo alizungumza kiswahili cha kuvuta maneo, akionekana kwamba hakifahamu vizuri
“Ndio baba, na anazungumza kiswahili”
“Amesema ametokea wapi?”
“Tanzania, ila hajanitaji ni sehemu gani”
Mwanaume huyo akaendelea kuzungumza kilugha chao, baada ya muda akatoka ndani ya chumba tulichopo
“Eddy baba amrsema tukuache upumzike”
“Ndoja kwanza, unaitwa nani?”
Msichana huyo akakaa kimya kwa sekunde kadhaa kisha akajikoholesha kidogo kuliweka koo lake vizuri kisha akanijibu kwa upole
“Nitakujibu, ukiwa vizuri”
Nikamsikia akitoka ndani ya chumba nilichopo, nikajipapasa kifuani mwangu, na kukuta kitambaa kigumu kikiwa kimefungwa kuzunguka usawa wa kifua changu chote
“Ehee Mungu warehema, nisaidie mimi mja wako”
Nilizumgumza kwa sauti ya chini, huku nkihisi machozi yakinitiririka pembezoni mwa macho yangu.Kumbukumbu za maisha yangu ya nyuma nilipo kua bado mdogo zikaanza kunijia kichwani mwangu, picha ya sura ya mana yangu ikaanza kunijia kichwani na iukumbuka baadhinya matukio ya furaha aliyo kua akinifanyia
‘Eddy mwanangu jaribu kuishinda hasira yako’
Nimaneno ya mama, niliyo anza kuyakumbuka vizuei na hili tukio lilitokea kipindi nilipo mpiga mwenzangu nilipo kua chekechea hadi akapoteza maisha akiwa anakimbizwa kupelekwa hospitalini
‘Usiwe mjinga na wewe utakubali vipi kupigwa na mwanaumwe mwenzio’
Nimanenoya mzee Godwin, alipo kua akinifundisha mbinu za kupigana baada ya kupugwa sana na wezangu nilipo kua darasa la kwanza
‘Mwanaume halisi, hupambana hadi dakika ya mwisho ya uhai wake’
‘Hata ikiwezekana kutoa roho ya mtu wewe toa tu, ili mradi uwe msindi’
Nimaneno menfine ya mzee Godwin alipokua akinifundisha kadei siku zilivyokua zikienda jambo ambalo alinifanya na mimi ka katili na roho ya kinyama tangu nilipo kua mdogo.
‘Uwe unasamehe saba mara sabini, kwani Mungu anawasamehe wale wote walio mkosea’
Nimaneno mengine ya mama, alipokua akinifundisha kusoma biblia kabla ya kulala, kwani alipenda kunikuza katika mazingira ya kidini na kumujua Mungu
‘Mimi baba yako, nihodari sana wa kuua pale ninapo kua kwenye uwanya wa vita, risasi yangy moja inapo toka kwenye mdomo wa hii bastola yangu, hua nilazima imuangamize mtu’
Maneno ya Mzee Godwin yakaendelea kujirudia kwenye akili yangu, siku hii alikua akinifundisha kulenga shabaha kwa kutumia bastola take tukiwa shambani, tulipo kwenda kuwinda nguruwe pori waliokuwa wakila mihogo yetu
‘Jitahidi kumuomba Mungu mwanangu kwani yeye ndio muweza wa kila jambo, usimruhusu shetani akaitawala roho yako’
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI
KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Email: ZephilineEzekiel@Gmail.Com