SEHEMU YA THENAMINI NA NANE
ILIPOISHIA...
Maneno ya Mzee Godwin yakaendelea kujirudia kwenye akili yangu, siku hii alikua akinifundisha kulenga shabaha kwa kutumia bastola take tukiwa shambani, tulipo kwenda kuwinda nguruwe pori waliokuwa wakila mihogo yetu
‘Jitahidi kumuomba Mungu mwanangu kwani yeye ndio muweza wa kila jambo, usimruhusu shetani akaitawala roho yako’
NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
Mana alijitahidi kadri ya uwezo wake kunishawushi kuwa kijana mwema. Maumivu makali yaliyo changanyika na uchungu moyoni mwangu, yakaanza kunitawala, hapa ndipo nilipo gundua, maisha yangu yameharibika kwa kufwata maneno ya baba, na kuyaacha maneno ya mama, ambae siku zote alinihasa niwe kijana mwema, mbaya zaidi baba niliyekua nikimuamini kwa kila alicho niambia, mwisho wa siku amekuja kya adui yangu namba moja, hii ni baada ya kugundua kwamba mimi sio mtoto wake, bali ni wapacha mwenzake
Siku zikasonga mbele nami ndivyo nilivyo zidi kupata unafuu wa machi yangu, pamoja na kifua changu ambacho kilipigwa baadhi ya risasi na rafiki yangu John, ikafika kipindi macho yangu yakapona kabisa kutokana na kutibiwa kwa dawa za kienyeji zilizo nipa uponyaji huu, hapa ndipo nikaruhusiwa kutoka njie ya nyumba ya nyasi niliyo kuwa nimekaa kwa kipindi kirefu kidogo, mazingura ya wanakijiji yakanishangaza kwani mavazi waliyo yavaa, yametengenezwa na ngozi za wanyama, hususani wanaume, vinguo vyao vya chini, ni ngozi ili juu ya vjfua wapo vifua wazi.
Nikiwa ninaendelea kuwashangaa wanakijiji hawa, ambao nao pia wanaonekana kunishangaa kwa jinsi nilivyo, jamaa mmoja mwenye misuli mikubwa na mweusi akanifwata na kwaishara akaniomba nimfwate nyuma, sikuwa mbishi nikaanza kumfwata huku tukikatiza kwenye mitaa tofauti ya kijiji hichi chenye nyumba nyingi, zilizo tengenezwa kwa udongo na kuezekwa kwa nyasi juu ya mapaa yao.
Tukafika kwenye moja ya jumba kubwa lililo zingirwa na wanaume wenye vifuavyenye miraba miine, wengine hasi miraba sita, mikononi mwao wakiwa wameshika mikuki lamoja na ngao, na muda wote wakiwa makini na kila iangiae katika jumba hili, lililo jengwa kwa aina yake
Tukaingia kwenye moja ya ukumbi mkubwa ambao nikakutana na wasichana wengi walio vifua wazi, hiku sehemu zao za siri zikiwa zimefunikwa kwa vijingozi vidogo, mikononi mwao wameshika mikia ya simba, na farasi ambayo wanaitumia kumpepea kila anaye ingia sehemu hiyo.
Jamaa akanionyesha sehemu ya kusimama, akaniacha hapa na kuondoka zake, niliwa ninaendelea kusimama sauti nzito ya mwanaume nikaisikia ikitokea kwenye nyumaa ya pazia lililopo kwenye ukumbi huu ikiniita jina langu, akatoka mwanaume wa makamo, aliye valia ngozi ya chui, mwilini mwake huku kwenye bega la kushoko kukiwa na kichwa cha chui huyo,
“Unaonekana sasa unaendelea vizuri sio?”
“Ndio kwa sasa ninaendelea vizuri kiongozi”
“Safi ila mimi siitwi kiongozi bali ninaitwa chifu Kambute”
“Chifu KAMBUTE?”
“Ndio, karibu uje kuketi hapa karibu yangu”
Nikapiga hatua hadi kwenye kiti chaje kilicho tengenezwa kwa miti migumu sana, nikakaa pembezoni mwa kiti cheke kama alicyo niamuru kufanya.
“Kwanza pole kwa yaliyo kukuta bwana Eddy”
“Asante sana chifu Kambute”
“Vijana wangu walikuokota kwenye moja ya mto, ambao naji yake, yanakwenda kwa mfumo wa maporomoko, ulikutwa ukiwa na hali mbaya walikuchukua na kukuleta hapa nikawaamuru wakujenge kibanda chako, ili waganga wangu waweze kukufanyia huduna hadi leo ukapona”
“Asante sana chifu Kambute”
Nilizungumza huku nikipiga magoti chini, kama ishara ya kumshukuru kwa alicho nifanyia. Akaniruhusu ninyanyuke na kukaa kama nilivyo kaa mwanzoni
“Nilifurahi sana kusiki kwamba unajua kuzungumza kiswahili fasaha, na pia nilifurahi kusikia umetokea Tanzania”
“Kwa nini Chifu Kambete?”
“Mwaka 1975, baba yangu alinipeleka nchini Tanzania, kwenda kusoma,ambapo alibikabidhi kwa rafiki yake Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kipindi hicho alikua ni raisi wa nchi ya Tanzania”
Ilinibidi nimshangae chifu huyu, kwani ninaimani anaitambua vizuri Tanzania, japo hadi sasa hivi sijijui nipo wapi
“Kipindi hicho cha makaburu hapa nchini Afrika kusini, hakiwaruhusu watu wengi kupata elimu, na ukibagatika kupata elimu basi ni yamasharti makubwa inayo fundisha utamaduni wao. Baba yangu alinipeleka kule kisuri, kutokana alikua ni chifu katika kijiji hichi cha Kambute, Nilikaa Tanzania kwa Miaka zaidi ya kumi na tano, ambapo, nilibahatika kuzaa na mwanamke mmoja, alikua akiitwa Maria”
Sauti ya chifu kidogo, ikapungua uzito wake, huku machozi yakianza kunlenga lenga usoni mwake,
“Maeia alikufa, kipindi mwanangu akiwa na umri wa miaka mitatu, ilinilazimu kurudi naye huku, ambapo nilimkuta baba akiwa katika hali mbaya sana, naye hakukaa sana alidariki dunia kutokana na magonjwa yawakumbayo wazee wengi.”
Kijistori cha chifu kilinisisimua mwili wangu sikujua ni kwanini ameamua kuzungumza maneno mengi kwangu.
“Pole sana chifu”
“Nimesha poa”
Chifu Kambute, hakuendelea kuzungumza kitu cha aina yoyote zaidi ya kuondoka na kuagiza nibadilishiwe mavazi nivae kama walivyo vaa wao. Japo kwangu ni ngumu sana kuvaa nguzo za wanyama kama nguo ili ilinibidi kufanya hivyo.Taratibu nikaanza kuyazoea mazingira ta watu wa hichi kijiji, chifu akaniomva niingie kwenye jeshi la kijiji hichi, ambapo nikaanza kufundishwa taratibu jinsi ya kutumia silaha za asili katika kupambana, ikiwemo kutumia majambia makali. Nilistushwa na makofi ya mtu yakitokea nyuma yangu, baada ya kufanya vizuri katika mapambano yangu na jamaa mmoja miongoni mwa askari katika eneo la kufundishiwa kupigana
“Hongera sana”
Sauti ya msichana huyu haikuwa ngeni sana kwangu, kwani niliisikia kipindi nilipo kua bado ni mgonjwa wa macho. Msichana huyu ni mrefu kiasi, huku umbo lake likia limekaa kimazoezi sana, japo ni mrembo kisura ila mazingira aliyo kiweka ni tofauti sana na mazingira wanayo jiweka wasichana wanao jijua wai niwarembo, msichana huyu akachomoa upanga wake, akashuka kwenye farasi aliye mpanda na kuja katika eneo nililo simama, askari wote wakatuzunguka.
Gafla msichana huyu akaanza kunishambulia kwa haraka kwa kutumia upanga wake nkali ni mrefu kiasi, ikanilazimu na mimi kujitetea kwa upanga wangu. Kila nilivyojaribu kujikinga na upanga wangu ila msichana huyu anaonekana hodari sana katika kutumia upanga, nikastukua akinipiga mtama na kuanguka chini, huku ncha ya upanga wake ikielekea kwenye koo langu
“Vipi unahitaji kuendelea kupambana?”
Aliniuliza huku akihema sana na jasho lilimwagika kwani mapigano tuliyo yafanya nimajali kupita maelezo. Kutokana na kuchoka sana sikuwa na haja ya kuendelea kupambana naye, akanipa mkono na kuninyanyua juu
“Ninaitwa Lutfia”
Alijitambulisha jina lake, nikataka kuzungumza jina langu akanizui
“Unaitwa Eddy, ulisha niambia jina lako”
“Wewe ndio yule uliye, zungumza nami siku ya kwanza?”
“Ndio mimi, ila unahitaji kufanya sana mazoezi, ili kuwa askari mzuri”
Lutfia alizungumza huku akimpanda farasi wake
“Jioni tutaonana nina mazungumzo na wewe”
“Wa…..”
Tatari Lutfia alisha ondoka na farasi wake na kuniacha nikiwa nimeshangaa.Nikarudi katika kibanda changu ninacho ishi, nikakaa kwenye kitanda changu cha kamba, huku jasho likinimwagika, nikajichunguza msili wangu nikagundua kuna mabadiliko makubwa sana kwani kifua changu kimekua kikubwa na kugawanyika kama askari wengine, hii nikutokana na mazoezi magunu niliyo patiwa kwa kipindi kirefu tangu afya yangu ilivyo tengemaa
“Kuna haja ya kuondoka, siwezi kuendelea kuishi kwenye mazingira haya”
Nilizungumza mwenyewe, nikaletewa chakula kama kawaida ya mama huyu anà ye niletea chakula.Nikamaliza kula na kuelekea kwenye mto ambao tunautumia kuoga askari wa kijiji hichi kila ifikapo jioni. Nkawakuta baadhivya askari wakioga, nikavua kinguo cha kingozi changu, amoja na upanga wangu ambao muda wote ninatembea nao, nikaingia kwenye mto na mimi nikaanza kuoga.
Kwa mbali nikamuona Kutfia akiwa amesimama kwenye moja ya kilima kilichopo karibu na mto huu, nikawatizama askari wote wanao oga nikawaona wapo bize na stori zao, Lutfia akaniita kwa ishara, nikatoka ndani ya mto na kuvaa kingozi changu, nikazuga zuga na kuondoka pasipo askari wezangu kustukia kitu chochote. Nikapandisha hadi eneo alipo Lutfia, akaniomba nilande kwenye farasi wake, sikusita sana, nikapanda na kukaa nyuma yake na kuondoka katika ene hili, akanipeleka kwenye moja ya msitu akamsimamisha farasi wake, sote tukashuka.
“Nifwate?”
Tukaingia ndani zaidi ya msitu, ulio tulia sana ukiwa hauna kelele za viumbe wengine zaidi ya kusikia hatua zetu tunazo tembea.
“Huku ni wapi?”
Lutfia hakunijibu zaidi ya kugeuka na kunitaza, akapiga hatua hadi sehemu niliyo simama, akanitazama usoni mwangu kwa muda, akaipitisha mikono yake shingoni mwangu, akauleta mdomo wake karibu na mdomo wangu ila nikaukwepesha, mdomo wangu, na taratibu nikaichomoa mikono yake, shingoni mwangu. Nikatoa upanga wangu na kuanza kupiga hatua za taratibu, kuelekea mbele tulipo kua tunakwenda kwani kuna kitu nilihisi.
Gafla nikastukia kusikia kelele za Lutfia, nikageuka nyuma haraka nikakuta akiwa ameshikwa na mijitu minne yenye nguvu huku sura zao zikiwa zimechorwa, kadri nilivyo zidi kuishangaa ndivyo ilivyo zidi kuongezeka na kufika ya mijtu kumi na saba huku akiwa na marungu makubwa mikononi mwao.
Nikaushika upanga wangu vizuri, nikijiandaa tayari kwa mashambulizi dhidi ya hii mijitu, iliyo tisha. Tararibu ikaanza kunizunguka, huku ikiwa imeshika marungu yao kwa umakini.
“Mungu nusaidie”
Nilizungumza kimya kimya huku nikiendelea, kuushikilia upanga wangu ambao una urefu kiasi. Gafla majitu hayo yakaanza kunishambulia, kutokana na uzoefu nilio upata dhidi ya kutumia upanga, haikuniwi ugumu wowote katika kujibu mas uh ambulizi ya kijitu hii, inayo onekana haiña mbinu kabisà za kupambana, kwani ninajikuta nikiimaliza kijinga kwa kuikata vichwa vyao.
Kwa bahati nzuri, Lutfia akapata nafasi ya kujitoa kwenye mikono ya mijitu iliyo mkamata, likawa ni zoezi moja tu, lakuhakikisha tunaishambulia mijitu hii hadi tunaiua yote, kutokana na uhodari wetu wakupambana, tukafanikiwa kuiua yote, jambo lililo tupa uhakika wa sisi kuishi.
“Eddy umechoka?” Lutfia aliniuliza
“Hapana sijachoka”
“Tuondoke hili eneo si salama”
Tukapanda kwenye farasi, na kuindoka katika eneo tulilo kuwa. Tukà fika karibu na kijiji, nikashuka kwenye farasi na kumuacha Lutfia atangulie kududi, ili kuepusha hisia mbaya zitakazo jengwa miongoni mwa wanakijiji, dhidi yetu.
Nikafika kwenye kijumba changu, sikuingia ndani nikatafuta mti uliopo karibu na kijumba changu nikapanda, kutokana ni usiku sikuhitaji nilale ndani, kwani bado nimapema.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI
KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Email: ZephilineEzekiel@Gmail.Com