SORRY MADAM (97)

0
SEHEMU YA TISINI NA SABA
ILIPOISHIA...
"Dada upo na hao maarusi?"
"Ndio, tupo Saloon moja inaitwa Rich Power Women au R.P.W"
"Ipo wapi?"
"Màeneo ya huku posta"
Akanielekeza walipo, akanieleza simu za Sheila na Blanka, zimezima chaji.

NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU

SASA ENDELEA...
Nikaingia kweñye moja ya gari, kwa lengo la kwenda kuzungumza na Blanka, nikafika getini nikashangaa kuona halifunguliwi na askari wanao linda.
"Vipi fungueni basi geti"
"Muheshimiwa ametuambia kwamba wewe hàuruhusiwi kutoka"
"Nini?"
"Ndio, tunafwata agizo lake, samahani kwa usumbufu muheshimiwa"
Askari mmoja, aliniambia huku akiwa ameshika bunduki yake aina ya SMG pamoja na mbwa mkubwa, na anaye onekana mkali sana.

Nikatoa simu yangu na kumpigia mama, aliye kwenda kazini, alfajiri na mapema.
"Mama ni mambo gani unayo nifanyia lakini?"
"Mambi gani?"
"Ndio umewapa amri hawa askari wako mimi nisitoke nje?"
"Ndio, utatoka kesho siku ya harusi yako tu. Hiyo sio ombi bali ni amri"
Mama akakata simu, nikabaki nikiwa nimeitazama simu yangu, huku nikihema kwa hasira. Ikaingia namba ngeni kwenye simu yangu, iliyo nistua sana moyo wangu. Taratibu nikaipokea na kuiweka sikioni mwangu.

"Haloo bwana Eddy"
Nilisikia sauti ya kiume
"Nani wewe?"
"Hauna haja ya kujua mimi ni nani, Ila nina habari njemaa sana kwako"
"Una masaa ishirini na nne, kuleta kiasi cha pesa milioni mia moja, kumuokoa mke wako na mwanao Junio, la sivyo WATAKUFA"
"Wewe ni na.....?"
Simu ikakatwa, nikabaki nikiwa nimeitazama simu yangu, mapigo ya moyo yakinienda mbio.

Nikageuza gari langu, nikalirudisha sehemu nilipo lichuku.Nikashuka haraka na kuelekea chumbani kwangu. Kitu cha kwanza kukifanya, nikachukua kadi zangu mbili za benki, nakuziweka kwenye mfuko wa jinzi niliyo ivaa. Nikachukua sweta langu lenye kofia, japo Dar es Salaam kuna joto kali, ila ikanilazimu kulivaa, hivyi hivyo. Nikasimama nje ya chumba changu kilichopo ghorofani, kila mtu nikamuona anashuhulika na mambo yake.
Kitu kinacho zidi kuniumiza kichwa ni jinsi ukuta wa jumba hili ulivyo mrefu, huku juu ukiwa umezungushiwa nyanya zilizo na umeme wenye volt nyingi sana.

"Chaji"
Nilijisemea mwenyewe, nikachukua chaji ya simu yangu. Nikatoa walet yangu mfukoni, nikaikuta ina noti mbili za dola mia pamoja na na shilingi elfu sabini. Chakushukuru Mungu, nikaliona gari lakukusanya mataka taka likiingia getini, nikashuka kwa haraka pasipo kusemeshana na mtu, nikafika sehemu lilipo simamishwa, ambapo wafanyakazi wake wapo bize kwa kukusanya matakataka yaliyopo kwenye mindoo mikubwa.

Kwa haraka nikabingiria kwa haraka na kuingia chini, ya gari hili kubwa la taka taka. Nikashikilia kwenye, bomba zilizopo chini ya gari hili. Baada ya dakika kumi, wakawa wamemaliza, tukafanikiwa kutoka getini pasipo askari kugundua kitu cha aina yoyote. Kutokana gari hili linapita kwa kila nyumba zilizopo kwenye maeneo ya nyumba za eneo hili, likasimama kwenye nyumba ya tatu kutoka lilipo jumba la mama.
Nikatoka chini ya gari pasipo mtu kuniona. Nikakodi pikipikia kuelekea benki ya posta. Niliwa njiani simu yangu ikaita, ikawa ni namba ngeni, ila ni yatanzania.

"Mmm"
"Shem mimi Blanka upo wapi?"
"Naelekea benki ya posta, upo wapi?"
"Nimetoka huku saloon nimeazima simu ili nikupigie, sijui tunaweza kuonana sasa hivi, kwa maama leo hatuto rudi nyumbani na kesho ndio harusi yako"
"Upo wapi?"
Manka akanielekeza sehemu alipo, ikanilazimu kughairi safari ya benki na kwenda alipo yeye. Ilituchukua kama dakika kumi na tano kufika alipo Blanka kwenye mgahawa mmoja ulio jificha sana, kutona na uwenyeji wa dereva huyu wa bodaboda, aliweza kupafahamu. Nikamlipa dereva pesa anayo nidai, nikaingia ndanibya mgahawa kama Blanka alivyo nielekeza, nikamuaona amekaa kwenye kona moja ya huu mgahawa ambao si rahisi mtu yoyote kumuona, kutokana na kigiza kilichopo ndani ya huu mgahawa.

"Mbona shemu umevaa hivyo?"
"Mama alikua haitaji mimi kutoka nje'
"Ahaaa sasa hapa napata picha"
"Picha gani?"
"Nilimsikia akizungumza asubuhi na dada Sheila, kwamba huto toka, sasa sikuwaelewa wanamaanisha nini"
"Ehee kabla hujaniambia ulicho hitaji kuzungumza jana, mbona umetumia namba ambayo si yako?"
"Nimehofia kutumia namba yangu kuwasiliana na wewe kutokana toka juzi namba za watu wote mule ndani zimeunganishwa na namba ya mama, zikiingia na kutoka lazima kwake zipitie"
"Mmmmm hata yangu?"

"Yako sijajua, ila nahisi pia itakua kwenye mlolongo huo huo"
"Poa tuachane na hilo, wewe na Sheila muma undugu wa kivipi?"
"Ahaaa ni story ndefu kaka yangu, ila kiufupi Sheila si ndugu yangu wa kuzaliwa wala wa ukoo"
"Sheila nilimsaidia kipindi fulani alitekwa, sasa nilimuokota porini akakaa sana kijijini kwetu Tulimuuguza hadi akapata nafuu ndipi alipo rudi huku, akaamua kulipa fadhila zake kwa kuniendeleza na masomo"
"Ahaaaa kwa maana nilikua ninajua Sheila hana ndugu"
"Kweli hana, mimi ni ndugu yake wa hiyari"
"Kitu nilicho hitaji kukuambi wewe kama kama yangu, Sheila anatabia zilizo nipelekea leo kuzungumza hichi nimacho taka kukizungumza"
Blanka akashusha pumzi na kunitazama usoni, kisha akapiga fumba la juisi yake aliyo agizia.

"Kabla hawajaja kuja huku marekani, dada sheila alikua akinilazimisha kumtoa mimba aliyo kua nayo"
"Ng....ngooja kwanza, kimba gani?"
"Hii aliyo kua nayo, kwani kipindi anakuja huko ulipo kua, alijigundua ana mimba ya ya wiki kam moja na nusu"
"Ñgoja mimba ya wiki inaweza kuonekana?"
"Ndio inategemea na maumbile ya mwanamke wengine hadi mwezi ndio wanaiona"
"Basi nilikataa kumtoa, akaniambia atajua nini cha kufanya. Alipo kuja huko sijui kama mulikutana kimwili au laa?"
Kwa upande mmoja kichwa kikaanza kunikoroga kwa hasira, huku upande wa pili ikiwa ni nafuu kwangu kuepukana na jukumu la ndoa.

"Nilikutana naye"
"Na umaamini mimba ni yako?"
"Mi sijui?"
"Kwani siku ulipo onanana naye alikuaje?"
"Mimi wala sielewi hapa nahisi kuchanganyikiwa"
"Tulia shem wangu, ila kuna kidhibitusho kingine ñgoja nikuonyeshe"
Blanka akatoa simu yake, akaminya minya na kunipa niangalie baadhi ya meseji alizo zipiga picha zikiwa kwenye simu ya Sheila zikionyesha akijibizaba na mwanaume aliye mtia mimba.
Sheila alikakua àkimlazimisha mwanaume huyo, akubali yeye kutoa mimba kwani mumewe amesha rudi.

"Huyo jamaa yake unamjua?"
"Ndio, tena ngoja nikuonyeshe"
Blanka akachukua simu yake akaminya minya baadhi ya sehemu anazo zijua mwenyewe, akanikabidhi tena simu yake.
Moyo wangu ukazidi kukosa amani, baada ya kumuona John akiwa amekbatiana na Sheila, tena wakinyonyana midomo yao

"Huyo jamaa, anadai anafanya kazi kwenye shirika la ndege la Ufilipino, na huja mara chache sana hapa Tanzania"
Mwili mzima ukazidi kunitetemeka kwa hasira kali, huku nikimtazama John ambaye hadi sasa hivi, amechukua kila kitu kutoka kwenye mikono yangu. Kuanzia mali za baba yangu hadi Sheila mwanamke niliye tokea kumuamini sana.

"Alafu hafi sasa hivi, kuna mpango ambao Sheila ameupanga na huyo jamaa yake, sasa sijajua ni mpango gani. Mara nyingi Sheila ananiambia mambo yanakaribia kuiva, tutakua matajiri sana"
”Ila shem ninakuomba usinitaje, kwani Sheila anaweza kuniua mimi"
"Hawezi kukuua, nakuomba ufwatilie huo mpango ulio jificha"
"Sawa nakuahidi nitalifanya hilo, na vipi huto jamaa unamjua?"
"Hapana?"
"Mbona anajuana sana mama, na huwa anakuja nyumbani, anadai ni rafiki yako?"
Kabla sijamjibu Blanka simu yangu ikaingia meseji kwa namba iliyo nipigia mara ya kwanza kutoka Somalia
(Jinsi unavyo kaa kimya, ndivyo jinsi unavyo karibisha vifo vya familia yako)

"Shitiii"
Nikajikuta nikiibamiza simu mezani, kabla haija anguka chini, Blanka akaiwahi kuidaka, akausoma ujumbe ulio ingia kwenye simu yangu
"Ni familia gani?"
"Nitakuambia, fanya urudi Saloon, ila usimuambie mtu yoyote chochote kuhusiana na kuonana kwetu"
"Sawa nimekuelewa shem"
"Ukiinipigia simu piga kwa namba nyingine kama vipi tafuna namba mpya"
"Sawa niyafanya hivyo shem"
Nikawa wa kwanza kutoka ndani ya mgahawa, nikakodi pikipiki hadi benki ya posta, nilipo hifadhi kiasi changu kikubwa cha pesa.

"Samahani, nahitaji kutoa pesa"
"Nilizungumza na jamaa, mmoja ambaye ni muhudumu"
"Chukua fomu ya kutolea hapo juu"
"Sihitaji fomo hiyo kwani nataka kutoa kiasi kikubwa cha pesa"
Muhudumu akanitazama kwa macho ya mshangao

"Unataka kutoa kiasi gani?"
"Milioni mia na hamsini"
"Mmmmm, ngoja nikukutanishe na meneja, nisubirie hapo"
Jamaa alaondoka na baada ya kuda akarudi na kuniomba niongozane naye, nikaingia ofisini kwa meneja, nikamueleza shida yangu niliyo nayo, akaniomba namba ya accounti yangu, nikampa akaminyaminya batani za computer yake, kisha akanitazama huku alivua miwani yake.

"Samahani, bwana Eddy hii akaunti yako imefungiwa"
"Imegungiwa?"
"Ndio na agizo hilo, hili limetoka ofisi ya waziri mkuu, masaa kama mawili yaliyo pita"
"Sababu?"
"Ahaaa tumeambiwa tuifunge kwa àgizo la waziri mkuu"
"Asante"
Nikachukua kadi yangu, na kutondoka sikutaka kuuliza nini chanzo cha akaunti yangu kufunguliwa kwani natambua mama ndio chanzo. Nikaenda benki ya bacrays ambapo, nikakutana naajibu ya kufungiwa, kwa akaunti yangu mbaya zaidi sina akaunti nyingine zaidi ya hizi mbili.
Nikaipiga namba ya simu ya Phidaya, ikaita kwa muda na kupokelewà na jamaa aliye nipigia simu muda asubuhi

"Nimazo pesa zenu, niambieni ni wapi mupo nizilete"
"Ohoo Mr Eddy, fwatà maelekezo tutakayo kupa"
"Kwanza kabla sijaonana na nyinyi, nahitaji kuzungumza na mke wangu"
"Subiri"
Baada ya dakika moja, simu akakabidhiwa Phidaya
"Eddy usitoe chochote"
Sauti ya Phidaya ilisikika, ikiambatana na mlio wa risasi kisha simu ikakatwa, nikajaribu kupiga tena huku mwili mzima ukinitetemeka ila haikupatikana tena, na saa yangu ya mkononi ikinionyesha yamesalia masaa kumi na tano tu.

Nikabaki nikiwa nimeizhik simu yangu nisijue nini cha kufanya. Nikapata wazo la kumpigia mmoja wa waongozaji wa tangazo la magari ya Ford, ambaye alitokea kuwa rafiki yangu sana
"Smith, mimi Eddy"
"Vipi kaka, mbona unahema sana?"
"Nahitaji msaada wako"
"Upo wapi?"

"Nipo Dar es Salaam, umesha rudi Marekani?"
"Hapana, bado nipo Dar, labda kesho kutwa naweza kuondoka kuna vipande vya lile tangazo, vinamapungufu, tumeamua kuvitengeneza upya"
"Ahaa mupo wapi?"
Smith akanielekeza walipo, nikakodi tena pikipiki hadi walipo kwenye moja ya godauni, ambapo wamepafanya kama studio, wakitumia 'blue screen' wakitengeneza mazingira kama ya Arusha.

"Vipi Eddy mbona kama una wasiwasi?"
"Kaka nina matatizo makubwa sana"
Nikanza kumuadisia Smith, tukio moja baada ya jengine, sikumficha kitu cha aina yoyote.
"Eddy nakuahidi hakuna kitakacho haribika, nitakusaidia kaka yangu"

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI

KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)