MAHABA NIUE (23)

0
Mwandishi: Emmanuel F. Kway

SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU
ILIPOISHIA...
"lile shati hali kumtosha vizuri, sasa kaka yangu nili kua nataka nilirudishe hapa kwako,"
"sija kuelewa vizuri"
"yaani nime leta lile shati lako, sito linunua tena"
"dada sikia. hilo halitowezekana hata kidogo, sifanyi biashara izo hapa, ivi mfano dada angu, wateja wote wange kua kama wewe una fikiri ingekuaje"?

KABLA HATUJAENDELEA NIOMBE BURUDIKA NA VIDEO HII

SASA ENDELEA...
"Sio ivyo , ndo maana nika kuomba"
"hilo hali towezekana, tafuta ela ya shati ulete nikupe simu yako, embu muache makusudi basi"

Ramsey aliongea vile huku akimuacha martha akiendelea kuta fakari, hakutaka kuongea nae tena sababu kitendo kile ana chokitaka asinge kubali kuki fanya,
"dada katafute iyo hela,"
"sawa"
Martha aliongea huku akitoka nje.

waliongea na prosper stori za hapa na pale , baadae ilipofika jioni Ramsey alimuacha Prosper na kumwambia yeye anaenda kumuona doreen alafu atarudi kulala kwake,

kweli alitafuta bajaji usiku huo na kumtafuta Doreen kwenye simu.
"nili kua nipo chumbani Ramsey, njoo baby alafu nisha kumiss tayari"
"poa ndo nipo njiani, "
"njooo baby wangu, nime kumic kuna kitu nataka nikwambie uwahi kuja"
"kitu gani hiko tena"?
"wewe njoo uki fika nita kwambia, embu kata simu nasikia kuna mtu ana gonga ngoja nikafungue alafu nita kupigia tena, sawa mpenzi wangu?! nakupenda mwaa mwaa"

Ramsey alikata simu na kumsihii dereva yule wa bajaji azidishe mwendo, kweli mwendo ulizidi ila foleni za hapa na pale zili wafanya wacheleewe kufika,

walifika kwa warioba na kukunja kona ambapo alizidi kumuelekeza ila kabla ya kukunja kona gari aina ya PICKUP Ina funga breki za ghafla na kutimua vumbi.
"we fala nini endesha bajaji vizuri hiyo"
aliongea dereva wa pickup ile kwa jazba sana na kumfanya Ramsey atoe kichwa nje kuchungulia.
"samahani broo"
"una gongwa nini, "

dereva huyo aliachia misunyo mikali na kumtukana dereva huyo wa bajaji huku akitoa gari mbio bila Ramsey kujua kuwa ndani ya pickup ile alikua DOreen ametekwa nyara na anaenda kuuliwa.

baada ya kufika nje ya geti la Doreen ana mlipa dereva yule na kutoa simu yake mkononi akija ribu kumtafuta hewani,
simu ya Doreen iliiita bila kupokelewa, aliipiga tena bila mafanikio,
"mmh, huyu viipi tena?"

aliongea Ramsey mwenyewe huku akijaribu kufungua geti la nyumba hiyo ambapo lili funguka na kuingia huku akinyata taratibu kwa taadhari,

alitembea na kukuta mlango wa mbele uko wazi hauja fungwa.
"Doreen, DOREEN, punguza masihala yako, nime sha fika naku pigia simu yako hupokei, toka huko chumbani"

Ramsey aliiongea huku akiwa amesimama,

ila bado aliona kimnya alipiga tena simu ya Doreen na kuisikia ikiita chumbani,
alitembea taratibu na kuufungua mlango wa chumbani na kuikuta simu ile ipo kitandani,

bado haku taka kuridhika aliingia bafuni na hakuona dalili yoyote ya Doreen. aliendelea kuita bila mafanikio,

alivyoona hali iyo aliamua kuondoka na kumpigia simu Prosper akimwambia kuwa ana kuja ivyo asifunge mlango,
alichukua tena Bajaji akiwa na mawazo mengi sana juu ya Doreen.

huku akija ribu jaribu tena namba ile bila kupokelewa na mtu yoyote yule,
"labda ata kua ame toka ghafla tu, nita mcheki kesho"
alijisemea kimoyo moyo huku akijikpa moyo,

licha ya kujipa moyo lakini anahisi moyo wake ni mzito sana na moyo kumuuma sana kutokana na Doreen hakua na tabia ya kutoka ghafla wakati wana miadi ya kuonana tena bila kumpa taarifa yoyote ile.
" oyaa, nime kwambia magomeni mapipa, sasa huko unaenda wapi"?
"huku kuna shotkati moja napita huko foleni kaka"
"ahaaa sasa ndo useme,"
"samahani"

Ramsey alikua akiongea na dereva huyo wa bajaji wakielekea magomeni mapipa maeneo anayoishi Prosper, kwa kuwa alikua ana pajua haikumpa shida kufika,

baada ya kufika alimpa dereva huyo pesa na kushuka na kunza kutembea kwa miguu,

dakika tatu alikua tayari kesha fika kwa prosper na kupokelewa kwa furaha sana na rafiki yake huyo.
"bafuni wapi kwanza nikaoge Prosper"?
"njoo huku . bafuni ni hapa uki maliza uta ingia humu uta badili nguo"
"poa poa"

Ramsey aliingia na kuji mwagia maji ambapo baada ya kutoka alienda seblen na kukuta prosper kesha nunua chips mayai na wote kuanza kula.
"prosper ume jitahidi sana, hii nyumba yako"
"kuji tahidi wapi Ramsey, vyumba viwili tu, yaani hapa bado namalizia malizia kui karabati hii nyumba,"
"sasa shemeji yuko wapi"?
"hahahahaha, nani Magreth"?
"huyo huyo"
"yupo chuo, ndo maana yaani nafanya juu chini hii nyumba niimalize kabla yeye hajamaliza chuo ili akimaliza nimuoe kabisa kaka."
"kaka hauna masihala , sio mbaya lakini mimi bado nipo nipo"
"hahahahaha, ivi Ramsey, hivi nipe siri ya kuwa pata watoto wazuri , hivi una tumia dawa, maana kila ukigusa yumo. nili kukubali ulivyo mpata yule mama yule, mtasha, hapo ndo nika kupa saluti zako"

swali lile lili mfanya Ramsey amuangalie vizur Prosper na kuchukua kipande cha kuku huku akikiweka mdomoni.
"ngoja nikupe siri moja, ya kuwa kamata watoto wa kike, kwanza sina dawa wala kizizi, kitu kimoja jiweke smati kwanza, watoto wa kike wana penda mtu smati, alafu kuna mambo mawili mwanaume una takiwa uwe nayo"
"enheeee niambie bratha"
"una moto,. mtoto wa kiume ukitaka uku balike au umpate mtoto wa kike, kuna mambo mawili una takiwa uya jue au uwe nayo, moja uwe na pesa, mtoto wa kike ana hitaji matunzo ujue, sio kidogo na usiwe bahili"
"duuu, jambo la pili"?
"sikia sasa, kama huna pesa, kitandani uwe mzima, una jua Prosper, ngoja nikwambie kitu, kufanya mapenzi na demu au mwanamke sio kukojoa tu, una takiwa umridhishe yaani una hakikisha ana ridhika alafu ndo una ridhika wewe, ndo ivyo yaani, yaani una hakikisha kesho ana rudi na hajuutii tena, yaani muda wote ana kua ana kuwaza wewe"
"aiseee, nilikua sijui"
"hahahaha, sasa wewe una dhani yule mama nina pesa gani ya kumu honga, sina hela mimi ya kumuhonga yule mama, yaani ni kumpa viuno viuno tu"

waliongea mengi siku hiyo na prosper na baada ya hapo, alioneshwa chumba cha kulala kutokana na usiku mnene kuingia, Ramsey aliingia chumbani na kulala.

.....

asubuhi ya siku ina yofuata Ramsey na Prosper wali amka na kunywa chai aliyo nunua Ramsey na baada ya hapo walita futa bajaji wakielekea mjini kufungua duka.

walifika na prosper kufungua duka wote walianza kufanya usafi, ila baada ya muda kidogo Ramsey ana muona Martha akija kwa mbali na kuingia,

alimkabidhi pesa nusu ya shati lile ambapo alimuambia kuwa kesho yake ange mmalizia upande wa RAmsey hakutaka kutoa simu ile mpaka ata kapo maliziwa pesa yake kamili,

kweli alikomaa na kuto kuonesha sura ya mzaha hata kidogo.

siku hiyo ilipita na jioni kufika na kufunga duka hilo la nguo,

siku hiyo kweli usafiri ulikua ni wa shida sana kupita maelezo, watu walikua wengi sana hata bajaji na boda boda zilikua haba sana.

hakukuwa na jinsi zaidi na kuelekea stendi ya big bon ili watafute dala dala ili waweze kuelekea magomeni. baaad ya kufika kituoni hali ina kua ile ile ngumu sana.
"usafiri wa leo nishai Ramsey"
"duu, hii ya leo kiboko sana"
"tupige kwata , tutembee mwanangu"
"aaah Prosper huni tembezi,"

takribani nusu saa ili pita huku giza likianza kuingia hapo stendi, bado usafiri wa dala dala ulikua tabu sana.

gari ya kifahari aina ya VOLKS wagen, lili simama pembeni ya stendi hiyo ya big bon huku kila mtu akili kodolea macho na kutaka kujua nani atakae shuka, hata kwa Ramsey na Prosper pia macho yao yali ganda juu ya gari hilo,

alishuka mwanamke mnene kiasi mweupe, nyuma akiwa amebinuka huku akiwa amevalia kimini, kilicho fanya mapaja yake yaweze kuonekana,

na kuzidi kufanya watu wa pale hasa wana ume wazidi kumtolea macho, ila kwa Ramsey aliweza kumtambua alikua ni jOsephine.

haku taka kumuangalia aligeuza shingo yake pembeni hasa baada ya kumuona Josephine ana kuja usawa wake.
"prosper tusepe"

aliongea Ramsey huku akimvuta Prosper ila ana zuiwa baada ya Josephine kumshika mkono wake wa kushoto.
"nini tena?"
alihoji Ramsey akiwa makini sana na kumwangalia josephine machoni,
"Ramsey,naomba twende kwenye gari"
"uende na nani"?
"Ramsey nakuomba baba, please come with me, tutaongea tukiwa ndani ya gari, please please"
"nenda tu, sitaki"
"bratha, twende tu"
aliongea Prosper huku akimsihi waingie ndani ya gari,

"mmmh lile zali la mentali, dogo vipi yule ana zingua"

ili kua ni sauti ya mtu wa jirani yao akiongea vile aliye kuwa akisikia maongezi yale.

kweli RAmsey baada ya kumsikiliza Prosper ana jikuta anaenda huku pembeni akiwa na Prosper, waliingia ndani ya gari.

ila Josephine haku taka kuendeesha gari alimpisha Ramsey upande wa dereva ili aweze kuendesha.
"ramsey but hili gari hali tumii funguo"
"kumbe lina washwaje sasa?"
"sikia kanyaga breki hapo, alafu bonyeza iyo batan hapo pembeni, lita waka"

Kweli Ramsey alifuata maagizo hayo na gari lile kuwaka ambalo lilikua jipya, aliwasha hendiketa kuashiria kua ana ingia bara barini ivyo anaye kuja nyuma yake aweze kujua,

na tayari kuingia barabarani akiwa makini juu ya usukani, aligeuza shingo kwa pembeni na kugandisha shingo yake huku akiwa anaendesha gari. hii ni kutokana na kumuona ESta demu wake ame simama na mwana ume tena ame mshika kiuno huku akiwa ana ongea nae kimahaba maeneo ya stendi ya faya.


Kweli aliya gandisha macho yake kwa Esta na kuha kikisha kweli alikua ni yeye, bila kujali alikua na Josephine pembeni yake tena kushoto huku yeye akiendesha gari upande wa kulia ambapo usukani ndipo uli pokua,
aliingiza mkono mfukoni na kutoa simu yake kwa kuwa alikua na namba ya ESta kichwani haiku mpa shida, aliweka namba za Esta juu ya skrini ya simu, na kuipiga ambapo baada ya kuipiga alikua akimuangalia kupitia kioo cha nje side mirror,

kutokana na gari izo kusimamishwa na trafic ivyo aliweza kumuona vizuri Esta ambae alikua akiangalia huku na kule akiwa na simu yake mkononi bila kuipokea na kukata,

Ramsey aliendelea kuipiga simu ile na ESta kuipokea,
"mmmh uko wapi"?
Ramsey alianza kuuliza tena bila ya salamu yoyote ile
"aaah jamani Ramsey, mimi nipo mbona"
"ndio najua upo . ila upo wapi?"
"nipo nipo nipo, nyumbani"
"mmh una fanya nini sasa hivi"?
"nipo ndo nataka nianze kupika hapa mwenzio. alafu hata sijui nipike nini Ramsey wangu, kwani wewe upo wapi?"
"pika tu chochote, aah mimi nipo mbali kidogo, nipo kibaha"

ESta alizidi kukaanga uwongo wakati Ramsey alimuona kila kitu na ki ukweli hakuwa nyumbani alikua stendi kasimama na mwanaume mwingine, kila alikua ana ongea Ramsey alimuona kwenye kioo cha nje cha gari, ila hakutaka kumwambia chochote kwa wakati huo.
"poa baby naomba nikate simu, nataka nianze kupika"
"aya bwana poa poa ukimaliza kupika niambie"
Ramsey alitabasamu kidogo kutokana na uwongo ule wa Esta
Foleni zilianza kutembea na Ramsey kuanza kucheza na usukani,
"nani ulikua una mpigia simu:?"

USIIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUTUMIA AKAUNTI YAKO YA FACEBOOK, LIKE UKURASA HUU USIPITWE NA SIMULIZI NA MENGINE HUKO FACEBOOK

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE TAZAMA VIDEO HII KAMA MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA

KWA TELEGRAM👇BONYEZA HAPA

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)