ROHO MKONONI (4) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumatano, 6 Julai 2022

ROHO MKONONI (4)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
πŸ“– KUSOMA SIMULIZI
🎬 FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
πŸ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
πŸ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa
Mwandishi: Zuberi Maruma

SEHEMU YA NNE
ILIPOISHIA...
...Butu akaingia ndani ya gari yake tayari kurudi nyumbani akiacha zogo huku nyuma kati ya inspekta Jona na mkuu wake
***
Inspekta Butu aliwasili nyumbani kwake akaliweka gari lake na kutoka nje ambapo alielekea mpaka kwenye

KABLA HATUJAENDELEA NIOMBE KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media BASI INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KWA WAKATI
πŸ‘‰GUSA HAPAπŸ‘ˆ

SASA ENDELEA...
Ile gari aloelekezwa akafunguliwa mlango wa nyuma akapanda gari,akiwa ndani ya gari alisachiwa baada ya kutokutwa na silaha gari ikaondolewa,ndani ya gari hapakuwa na mtu aliye ongea wote walikuwa kimya,safari yao iliishia palipo na msitu mdogo ujulikanao kama pori tasa,walielekea mpaka katikati ya msitu huo,ghafla gari likasimama na taa za mbele ya gari zikawashwa Butu akuamini alichokiona mbele yake,haraka akafungua mlango na kutoka akaikimbilia familia yake ilokuwa imelala chini katika madimbwi ya damu!

Kitendo cha kushuka tu ile gari ikawashwa na kuondoka kwa kasi ikipita pembeni yao kidogo,Butu wala akuangaika nayo,macho yake yalikuwa kwa familia yake mkewe na wanaye wawili walilala pasina uhai,tena walikufa vifo vibaya waliharibiwa macho na kutandikwa risasi,nguvu zilimuisha Butu sauti ikakata baada ya kulia sana,huku akiwa kapiga magoti ghafla giza likamjia akajikuta naye akienda chini!

Tayari alishapoteza fahamu!.
*****
Usiku ule maneno aloambiwa na Inspekta mwenzake kiukweli yalimuumiza roho,japo hakuwa tayari kufatwa kama agizo alilopewa ila Jona aliwapa ishara maaskari wenzake watatu walokuwa zamu usiku ule,wakafunga kituo nao kuingia ndani ya kitara cha polisi na kwa siri sana wakaanza kumfatilia John Butu,baada ya kuona anaelekea mtaa alokuwa akiishi wakiwa mtaa wa nyuma walisimamisha gari wakashuka na kutambaa pembezon mwa barabara,ghafla kwa mbali waliliona gari limepaki,wakasimama palepale kujificha kuto onekana hata na walioko kwenye lile gari...

Wakiwa pale katika ficho lao walishughudia Butu akitoka katika jumba lake akaifata ile gari akaingia na gari kuondolewa waliiangalia ikiondoka wakaiacha mpaka ikatoka kwenye mtaa ule ikakata mtaa wa pili kushoto nao haraka wakarudi kwenye gari yao wakaingia na kuitoa kwa spidi wakamaliza mtaa ule na kuingia huo mtaa wa pili nao wakakata kushoto ila hawakuweza kuiona ile gari, wakanyoosha na hiyo barabara wakaingia lami,kwa kuwa kulikuwa na gari nyingi awakufanikiwa kuiona ila kwa mawazo yao tu wakaona wachukue barabara iendayo pori tasa,kwa kuwa ndo pori linalosifika kuwepo kwa majambazi,na pori hili ndilo linalotekewa watu na kuteswa,safari yao iliendelea hatimaye wakaingia katika pori lile,saa sita za usiku ndipo walipofanikiwa kuikuta miili ile barabarani,inspekta Jona akamjulisha mkuu wao,wakafanya uchunguzi,wakachukua vipimo haraka wakapigiwa simu madaktari usiku ule ule askari na madaktari wakawasili katika pori lile uchunguzi ukaendelea

Mihili ikabebwa na kupelekwa hosptalini kwa uchunguzi zaidi!

Macho yalikuwa mazito kufunguka, kichwa kikawa kikimuuma, akayafungua , harufu ya madawa ndiyo ilo mpokea,ndani ya chumba kile taa ziliwaka kumjulisha ni usiku akagundua yupo hosptal,

Kafanyaje sasa?!,akajaribu kuvuta kumbukumbu ndipo alipoikumbuka familia yake,pale pale akajikuta akipiga kelele na kuinuka,hasira ghadhabu zilishampanda,alichohitaji ni kimoja tu kujua ukweli je ni kweli familia yake imekufa?!

Madaktari kadhaa wakiume na baadhi ya maaskari ndio walokuja kumtuliza na kumchoma sindano nyingine ya usingizi,

"Itahitajika apatiwe daktari wa saikolojia awe hapa karibu asubuh akizinduka tu awekwe sawa tofauti na hivyo itamchukuwa muda akili yake kutulia"

Daktar alokuwa zamu usiku ule alizungumza kwa upole,ni wazi alimuonea huruma askari yule na si yeye tu hata na maaskari walokuwepo pale wakiongozwa na Jona wote walimuonea huruma kijana yule!.

Asubuhi aliwasili kamishna Nurdin na viongozi wengine wa jeshi la polisi pia aliwasili daktari Samson Semkiwa huyu ni daktari bingwa wa magonjwa ya akili na saikolojia,yeye alienda moja kwa moja kwenye kitanda cha Butu akisubiri azinduke kusudi aianze kazi yake rasmi,kamishna yeye alielekea mochwari kuiangalia miili ya familia ya Butu ukweli wote walisikitika baada ya kuiona miili ile ikiwa imeharibika vibaya...

Hatimaye baada ya nguvu ya dawa alopewa kupitia sindano alochomwa kumuisha hatimaye taratibu akafumbua macho yake mbele yake akapokewa na tabasamu jepesi la mtu alokaa pembeni yake...

"Pole sana kijana unajisikiaje sasa?!"

Mtu yule kwa sauti ya upole akauliza huku bado tabasamu lake likiupendezesha uso wake!

"Najiskia vizuri,kwani nimefanyaje na hapa nipo wapi?!"

Ni wakati alipouliza swali lile wakati akijilazimisha kukumbuka Samson akamuwahi

"Hapa ni hosptal ulipata mshtuko wa ghafla ila familia yapo ipo salama!

"Hapana!,imekufa,nani kawaua,kwanin lakin...

Palepale Butu akaanza kulia,SAM alikuwa na wakati mgumu sana kumuweka sawa ila mwisho alifanikiwa sasa akawa akipokea pole,akaenda kuiangalia familia yake,waandishi nao awakubaki nyuma kuripoti swala lile...magazeti ya mchana yakajaa habar hizo,televisheni zikarusha mubashara tukio lile wengi wakimpa pole,mkuu wa polisi IGP SULTAN BOZI akatoa ahadi ndani ya masaa 48 kuwatia mkononi wahusika wa tukio lile,baada ya uchunguzi inspekta akakabidhiwa maiti ya familia yake kuzizika...

Watu wengi akiwemo Raisi wa Jamhuri ya muungano walikwepo msiba ule ulitikisa taifa,baada ya mazishi inspekta Butu akala kiapo mbele ya makaburi ya familia yake,kuhakikisha anaua wote walohusika na vifo vya familia yake,tena atawaua kikatili,aliapa kutenda ivyo!

MASKINI!,KUMBE AKUJUA WALOFANYA IVYO NI WATU WA NAMNA GANI,AKUJUA FIKA!

Na laiti angejua?!,asingekuwa na mawazo ya kuwafatilia watu hao,ila ndo usilolijua ni sawa na usiku wa kiza!...

Inspekta wa jeshi la polisi John Butu anakula kiapo mbele ya makaburi ya familia yake kulipiza kisasi kwa kuwa angamiza wote walohusika katika kuiteketeza familia yake,mbaya zaidi akujua anaenda kupambana na watu wa aina gani!,ni vita inayohatarisha maisha yake ungana na mtunzi Zuberi Maruma uburudike na riwaya hii ilojaa upelelezi,na ujasusi ndani yake

SURA YA PILI
Inspekta Butu aliwasili ofisini akaweka saini mapokezi ile anaelekea ilipo ofisi yake ghafla akaitwa nyuma yake na sauti nyororo,

"Samahani afande mkuu kasema ukija kabla ujafanya chochote ukamuone"

Ilikuwa ni sauti ya askari mwenye cheo cha Konstebo alokuwa mapokezi muda huo!

"Sawa Fatma hiyo aina tabu!"

Butu akajibu na kugeuka kuelekea ilipo ofisi ya kamishna Nurdin Kyango.

Alifika akabisha hodi mara moja kabla ya kusikia sauti ya kukaribishwa akaingia na kupiga saluti mbele ya mkuu wake!

"Kwa niaba ya jeshi la polisi nikupe pole sana afande kwa yaliyokukuta ni ajali katika kulitumikia taifa lako,na barua hii...

Nurdin aliongea huku akimkabidhi Butu barua,Butu akaipokea na kuifungua palepale na kuanza kuisoma!

Alikuwa na maana yake kuisomea pale,na kama alijua barua ile ni ya kumpa likizo ya mapumziko ya mwezi mzima kusudi akili ikae sawa!

"Hapana mkuu,sipo tayari kwenda likizo nahitaji nishirikiane na mwenzangu kuchunguza juu ya walohusika na vifo vya familia yangu,kivipi nikae nyumbani hali ya kuwa wakatili wa familia yangu wanaishi nishahapa nitawaua wooote"

Butu aliongea kwa uchungu huku akiwa kakasirika.

Nurdin akatingisha kichwa,

"Butu wewe kuua ni kwenda kinyume na sheria,kwa sasa akili yako ijakaa sawa yakupasa ukapumzike,acha sisi tutalisimamia swala lako na wote walohusika tutawakamata na kuwapeleka mbele ya sheria wakapate adhabu inayostahili!,kwa sasa wewe upaswi kufanya chochote unaongozwa na hasira utadhuru hata wasousika..."

"Hapana mkuu,sitoweza kutulia bila kuwakamata makatili wangu!"

Palepale akageuka na kuufata mlango akaufungua na kutoka,huku nyuma Kamishna alishika mkonga wa simu na kumpigia

"Alooh mkuu Butu kakataa kwenda likizo,kahaidi kuisimamia kesi ya familia yake na yeyote atakayemgundua anamuua sijui tufanyaje mkuu!"

"Ok! Ahsante kwa kunijulisha wacha nimuandalie uhamisho ntampa kijana wangu alete"

"Ok mkuu!"

Nurdin aliitika na kukata simu,alishapoteza raha,ghafla akaingia kwenye mawazo!

Mawazo juu ya inspekta John Butu...

kivipi?!
***
Butu alitoka ofisini kwa bosi wake huku akiongea mwenyewe tena kwa kunung'unika,akiwa kakunja sura,ni baada ya kupewa barua ya likizo ya mwezi mmoja!

Katu akujua anaandaliwa barua ya uamisho,taratibu akaelekea zilipo mahabusu akafungua mlango

"Zuberi nakuhitaji"

Akaongea na kugeuka....

Mahabusu pale aliinamia magoti kijana mmoja , baada ya kusikia akiitwa akanyanyua uso wake macho yalovimba kwa kulia yakaonekana,kijana yule akanyanyuka na kumfata inspekta mpaka katika ofisi yake.

Huyu alitambulika kwa jina la Zuberi Maruma,alokamatwa siku chache zilizopita na Inspeka Jonathan,Ni baada ya Inspekta Butu siku ile kupigiwa simu na mtu asiye mjua akitumia namba 0759427653 na kumpa vitisho kwamba awaachie watu wake pamoja na mzigo wake wote tofauti na ivyo ataiteketeza familia yake, palepale Butu akaituma ile namba kwa Kpl 001 kitengo cha mawasiliano sambamba na kwa mkuu wake,kamishna Nurdin akamruhusu kwenda nyumbani kuicheki familia yake akihaidi kuchunguza zile namba,ndo pale Butu alipochukua pikipiki kuwahi kwake ambapo aliikuta familia yake aipo aka amua kurudi kituoni na kuwa achia wale watuhumiwa!...

Kamishna naye usiku ule alimpigia kpl 001 kitengo cha mawasiliano kuomba taharifa za namba hiyo!

"Usajili wa namba hizi jina ni la Zuberi Maruma,mkazi wa hapa hapa jijini dar anapatikana maeneo ya temeke maghorofani block 2 ana miaka 35 kazaliwa tarehe 15 mwez wa pili mwaka..."

"Inatosha..."

Nurdin akamkatiza,usiku ule ule kamishna akampigia simu Jonathan na kumpatia kazi ya kwenda kumkamata Zuberi kweli Jona na askari kadhaa usiku ule ule wakaingia katika kitara mpaka walipoelekezwa,wakamkamata huyo kijana na kumpeleka kituoni.

Akaswekwa ndani.

Kabla ajaojiwa ghafla Butu aliwasili usiku ule na kuwatoa wale vijana watano!.

Ndivyo ilivyokuwa.

Ivyo wakati wa msiba na uchunguzi wa miili Zuber alibaki ndani pasina kuulizwa chochote!,mpaka siku hii Butu akiwa na hasira akaenda kumtoa na kumswaga mpaka katika ofisi yake.

Akampa ishara aketi mtu yule akaketi.

Butu akamwangalia kwa dakika kadhaa na kumtathimini,moyoni mwake alijikuta akikataa kuwa yule si alokuwa akiongea naye kwenye simu,mwenye sauti ya majivuni!,mmiliki wa vijana wa madawa ya kulevya alowakamata uwanja wa ndege!.

Sasa huyu ni na nani?!,na namba zilizo mpigia inasemekana mmiliki Ni mtu huyu?!,akatafakari na kujiuliza maswali

Mwisho akaona asijiumize kwa maswali wakati mwenye majibu yupo mbele yake.

"Unaitwa nani bwana mdogo?!"

USIIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUTUMIA AKAUNTI YAKO YA FACEBOOK, LIKE UKURASA HUU USIPITWE NA SIMULIZI NA MENGINE HUKO FACEBOOK

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE TAZAMA VIDEO HII KAMA MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA

KWA TELEGRAMπŸ‘‡BONYEZA HAPA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni