ROHO MKONONI (5) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumatano, 6 Julai 2022

ROHO MKONONI (5)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
πŸ“– KUSOMA SIMULIZI
🎬 FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
πŸ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
πŸ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa
Mwandishi: Zuberi Maruma

SEHEMU YA TANO
ILIPOISHIA...
Sasa huyu ni na nani?!,na namba zilizo mpigia inasemekana mmiliki Ni mtu huyu?!,akatafakari na kujiuliza maswali

Mwisho akaona asijiumize kwa maswali wakati mwenye majibu yupo mbele yake.

"Unaitwa nani bwana mdogo?!"

KABLA HATUJAENDELEA NIOMBE KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media BASI INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KWA WAKATI
πŸ‘‰GUSA HAPAπŸ‘ˆ

SASA ENDELEA...
Akaanza kuhoji huku macho yake yakiwa usoni kwa mtu yule.

"Zuberi Maruma"

Mtu yule akaitikia,Butu akatabasamu,na kuandika jina lile katika kakijitabu chake.

"Una miaka mingapi Zuberi?!"

Inspekta akauliza kirafiki tu

"Thalathini na mbili!"

"Ok umeoa"

"Hapana"

"Unaishi na nani?!"

"Naishi mwenyewe"

"Umepanga"

"Hapana nimejenga"

"Wafanya kazi gani!?"

"Mwandishi wa Riwaya"

"Nyumbani unapokaa unaishi na nani?!"

"Afande nishakwambia naishi mwenyewe"

"Kwa nini?!"

"ah afande ungetaka niishi na nani?!"

"Mpaka miaka yote hiyo ujaoa wasubiri nini?!"

"Ni mipango yangu binafsi"

"Ok siku ya tukio ilikuwaje?!"

"Nikiwa nyumbani kwangu mida ya saa tatu usiku Askari walikuja na kuniweka chini ya ulinzi wakanileta hapa kituoni"

"Ulijua kosa lako?!"

"Hapana sikujua na Wala sija ambiwa"

"Uliuliza?!"

"Ndiyo,ila sija ambiwa"

"Nawe una hisi unakosa gani?!"

"Sijui"

"Kwa nini ujui?!"

"Kwa kuwa Sina kosa lolote!"

"Kwa hiyo wahisi umekamatwa bure?!"

"Inawezekana"

"Ok hii ni simu yako?!"

"Ndiyo ni simu yangu"

"Unaweza nitajia namba ya line zilizopo humu ndani"

"Tigo 0673999120 na voda 0759427653"

Inspekta Butu akaguna kidogo baada ya kusikia zile namba za voda,ni zile zile za yule mnasibu wake aloiteketeza familia yake...

"Simu yako unaitumia na nani?!"

"Peke yangu"

"Siku za karibuni ushamwachia mtu?!,au kumpa yeyote line yako?!"

"Hapana!"

Butu kuhakikisha akaingia upande wa meseji katika ile simu ila akukuta sms ilomuhusu akaenda upande wa simu zilizopigwa akatafuta namba yake ila akuzikuta,upande wa simu zilizo ongelewa pia akuzikuta.

Ina maana zimefutwa?!,akawaza pasina kupata jibu,akarudi katika simu yake na kutafuta sms ya mwisho kutumiwa akaikuta,akapiga zile namba simu ile ya Zuberi ikaita hii ikiwa na maana namba Ni zilezile akamgeukia tena Zuber sasa akiwa kakunja uso akarudia swali lake la awali!.

"Simu yako unatumia na nani,au nani ushampa simu siku hizi za karibuni?!"

Sasa alikuwa akimsogelea pale alipokaa!

"Hakuna afande huwa natumia mwenye..."

Paaaaaaaaaaaaaaaaaa

Kibao kikali kikatua shavuni kwa Zuberi,meno matatu palepale yakaacha fizi mdomo ukajaa damu.

Butu sasa alishabadilika,mishipa ya kichwa ilimsimama alidhamiria kuua kama kijana yule asingemweleza ukweli alijua lazima kijana yule hatakuwa anamjua yule alokuwa akimpigia kwa namba zile ila hakutaka kujidanganya Zuberi ndo alokuwa akiongea naye,hili alikataa kabisa.

Usilolijua....

*BUTU ANA ANDALIWA UAMISHO!,ATAKUBALI KUONDOKA PASINA KUWAPATA WABAYA WAKE?!*

*ZUBERI NAMBA ZAKE NDIZO ZILIZOKUWA ZIKITUMIWA NA MTU ANAYEMSUMBUA BUTU,JE WANA UHUSIANO GANI AU ZUBE ANAMJUA MTU HUYO NA ATAMWELEZA UKWELI BUTU?! NA NI NANI MTU HUYO?! NA NI KWA NINI ATUMIE NAMBA ZA ZUBERI?!*

Mambo bado mazito tuonane katika hatua ijayo kwa mwendelezo..

Inspekta wa jeshi la polisi John Butu bado anaendelea na upelelezi mkali kumjua muhusika wa mauaji ya familia yake,na sasa kafanikiwa kumpata mmiliki wa namba za simu zilizokuwa zikitumiwa na mtu huyo alo msevu kwa jina la 'mr x' katika simu yake,

Moyoni mwake anakataa kwamba mtu yule 'Zuberi' siyo lakini ndo mwenye namba,anaanza kumtesa vikali akitaka kujua ni nani alompa namba yake aitumie,je Zuberi atamtaja?!,na kama si yeye ni nani mtu huyo?!

Inspekta Butu akamkwida Zuberi shati! na kuanza kumfokea kwa ukali:

"Kwa hiyo utaki kunieleza siyo?,unatumiwa eeh! Utanieleza tu!"

Palepale akarusha ngumi palepale mdomoni,Zuberi akaachia yowe,

"Sijampa mtu afande unanionea bure!"

"Sasa alotuma hii meseji ni nani?,si namba yako hii au?!"

Palepale akamkabidhi Zuberi simu yake,

"Ongera afande kwa kujiokoa,ila je utaweza kuiko mboa familia yako?! Nakupa dakika kumi na tano uchague kuikosa familia yako? Au kuwa achia watu wangu nawe kuipata familia yako maamuz juu yako"

Zuberi akamaliza kusoma sms ile kutazama jina lililoseviwa ni "Mr x" kucheki namba alishtuka!

Zilikuwa ni namba zake za voda,

Mikono iloshika ile simu ikaanza kutetemeka,meno mdomoni yakaanza kugongana yenyewe.

"Hizo si ndo namba zako na ujawah mpa mtu simu je hii meseji ulo ntumia ilikuwa na maana gani?!"

"Hapana afande,siyo miye nilokutumia"

"Ndo unieleze ndo nani sasa ulo mpa simu yako akantumia mie meseji tofauti na ivyo utaya beba madhambi yake unajua alochoifanyia familia yangu?,utamtaja tu huyo kibaraka wako"

Butu aliongea kwa hasira huku akikunja mikono mirefu ya shati lake! Kilichofatia ni kipigo kikali,kipigo kilichoisha baada ya Zuberi kupoteza fahamu,askari wakaitwa wakambeba kijana yule na kumrejesha mahabusu,wakamweka huku akiwa vilevile kapoteza fahamu!

'Huyu lazima atakuwa naye ni kibaraka wa yule shetani sina haja ya kumuacha hai usiku wa leo atanieleza akizidi kuwa msiri sitosita kumchinjilia mbali"

Butu akawaza,tayari alishavaa roho ya kikatili, yeyote ambaye alihisi kwa namna moja ama nyingine anahusika na vifo vya familia yake alishahapa kumteketeza,na leo alipanga kuanza na Zuberi,ushahidi ukiwa ni namba ile!...

Maskini Butu akujua kuwa anaenda kuua kiumbe kisicho na hatia...

Ilipofika mida za saa moja za usiku akiwa na baadhi ya maaskari wenzake wakamtoa Zuberi mpaka ndani ya gari yao wakaelekea naye mpaka katikati ya msitu Tasa,palepale alipoikuta miili ya familia yake!,wakamshusha na kuanza kumtesa vikali kijana yule,wakimlazimisha aeleze ukweli,ila ukweli ni kwamba Zuberi akujua chochote kuhusu kutumika kwa namba zake,je angeeleza ukweli upi?!

Butu akamuona kijana yule ni kiburi,'Kama nilivyohaidi kumuua yeyote ambaye anausika na vifo vya familia yangu naanza na wewe,japo ujataka kunifungulia njia sawa kawafungulie wenzako njia soon watakufata mpuuzi wewe!'

Butu aliwaza huku akiwa kakunja sura na palepale akapayuka...

"Tunakupa muda wa kujitetea haya kimbia..."

Maskini pasina kujua Kwa shida Zuberi akaanza kukimbia risasi kadhaa zikaushambulia mgongo wake,nyingine zikikishambulia kisogo,wakaubeba ule mwili na kurudi nao kituoni!

Kesho yake habari zikatapakaa katika vyombo vya habari,jambazi lauwawa wakati akijaribu kukimbia mahabusu,ni yule mwandishi mahiri wa vitabu mtandaoni,kila gazeti lilikuja na habari yake,kwa majonzi familia ikachukua mwili wa marehemu na kwenda kuuzika.

OFISINI KWA KAMISHINA
Kamishna Nurdin alionekana wazi kuchukia,mbele yake alikwepo inspekta Butu!

"Najua wewe na wenzako ndiyo mlousika na mauaji ya yule mshtakiwa!"

"Ilibidi nifanye ivyo mkuu,sioni faida ya kukaa na mtu ambaye atoi msaada wa nini sasa?!"

"Ndo umuue?!,wakati unajua yule alikuwa ndo mtuhumiwa pekee ambaye angewezesha kukamatwa kwa wahusika we unaenda kumuua utawajibika kwa hili afande"

"Niliapa kumuua yeyote ntakayegundua kwa namna moja au nyingine ni mshirika wa yule alosababisha niikose familia yangu,huyu kijana namba zake ndizo zilizotumiwa na adui yangu naye kamficha sijui ndo kibaraka wake au vipi!,kifo kilikuwa ni haki yake!"

Kamishna hakuwa na la kuzungumza zaidi,kikubwa alisubiria barua ya uamisho ya kijana huyo ifike katika meza yake mtu yule aondoke,hakukuwa na msaada mwingine zaidi ya huo akampa ishara Butu atoke!

Butu akapiga saluti,na kugeuka kwa hatua zake ndefu akaufikia mlango akaufungua na kutoka...

Wakati akiwa katika korido moja ndefu akipita ofisi mbalimbali ghafla simu yake ikaita,haraka akaingiza mkono mfukoni kuitoa!

Namba alizokutana nazo ilibakia robo,simu ingemponyoka na kwenda chini,ila akawahi kuukaza mkono,

"MR X"

Ndo jina alilolisoma katika kioo cha simu yake,chini ya jina lile pakiwa na zile zile namba 0759427653 haraka kwa uwoga akapokea ile simu...

Ni sauti ile ile nzito,ilo msaliti na kumuulia familia yake hata baada ya kuwaachia watu wake na mzigo wake wote "ha ha ha ha pole sana askari kwa misiba ilokupata,pia nasikia umeua kiumbe kisicho na hatia kisa tu kumshukia na yeye kutumia namba kama zangu ukasahau kabisa kuwa kuna ku ack namba,pili binafsi nisingeweza kukupigia kwa kukutumia namba zangu hivyo nikafanya mautundu yangu nika ziunganisha hizo namba nanyi bila kufikiria mkamkamata mtoto wa watu na mwisho kumuua kwa akili zako ndogo ulijua kijana mdogo kama yule ataweza miliki mzogo wote uloukamata?!,kwa maisha yale ya kale ka jumba cha vyumba viwili?!,apumzike kwa amani,hili silo lililonifanya nikakupigia,nasikia eti wantafuta ok usijali nakupa nafasi ya kuonana na Mimi leo saa tatu usiku katika Bar ya Kivulini,uje mwenyewe asante....

Palepale simu ikakata

Butu alibaki kaduwaa,akuamini kile alichokisikia kwanza alishtushwa na mawili cha kwanza kumuua kijana wa watu asiye na hatia ,kilicho mshangaza Ni kitendo cha Mr x kuhitaji kuonana naye usiku katika Bar ya kivulini.

Je Ni mtego gani aloandaliwa akajikuta uwoga ukimvaa ila itakavyokuwa na iwe akaapa usiku aelekee kivulini akakutane na huyo mtu!

"Amuue yeye au afe yeye..."

Butu alibaki kaduwaa,akuamini kile alichokisikia kwanza alishtushwa na mawili cha kwanza kumuua kijana wa watu asiye na hatia ,kilicho mshangaza Ni kitendo cha Mr x kuhitaji kuonana naye usiku katika Bar ya kivulini.

Je Ni mtego gani aloandaliwa?!

Akajikuta uwoga ukimvaa ila itakavyokuwa na iwe akaapa usiku aelekee kivulini akakutane na huyo mtu!

"Amuue yeye au afe yeye..."

Baada ya mtu yule kukata simu,Butu akaingia katika tanuri la mawazo,moyo wake ukayavaa majuto makubwa kwa kile alichokifanya,akajilaumu kwa kutojipa muda wa kutafakari hapo awali,akili yake akaiendesha kwa hasira mpaka kumuua mtu asiyehusika!.

Na sasa muhusika wake anahitaji waonane,anajiaminije?!,lipi lengo lake kwake?,je arejee ofisini kwa bosi wake kamishna akamueleze kuwa ile namba imempigia tena na wakati huu imemuomba waonane?!

Hapana!

Akapingana na wazo hilo baada ya kugundua kuwa atazalisha lawama nyingi ikiwa mkuu wake atagundua kamuua kiumbe asiye na hatia!.

na anaweza pia kushtakiwa!...

Akazikumbuka lawama alizotoka kuzipokea muda mchache ulopita,hapo mkuu wake alijua yule ni mmoja wa walohusika,je sasa akagundua kijana yule mwandishi wa hadithi akuhusika ila ni namba tu zili akiwa?!...

Hapana!,akaona aifai ibaki siri yake naye aendeleze upelelezi wake wa chini kwa chini!

Akaelekea mpaka mapokezi,akahitaji maaskari watatu wa kiume kwa maongezi maalumu!.

Dakika kadhaa zilizofatia watu wa nne walikwepo ndani ya chumba kidogo cha ofisi yake

"Ma afande nyinyi mkiwa kama watu wangu wa karibu,wasiri wangu nadhani mengi tumefanya tukiwa pamoja,kwa taharifa tu yule mtu tulomuua msitu Tasa hakuwa na hatia!"

USIIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUTUMIA AKAUNTI YAKO YA FACEBOOK, LIKE UKURASA HUU USIPITWE NA SIMULIZI NA MENGINE HUKO FACEBOOK

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE TAZAMA VIDEO HII KAMA MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA

KWA TELEGRAMπŸ‘‡BONYEZA HAPA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni