BABU UTAMU (14) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumamosi, 18 Machi 2023

BABU UTAMU (14)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
📖 KUSOMA SIMULIZI
🎬 FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
😂 VIDEO za KUCHEKESHA
📑 MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa
Mwandishi: Pablo Hernandes

SEHEMU YA KUMI NA NNE
ILIPOISHIA...
"Aiseee….siku hizi nikigusa tu imoo." Emmanuel alijipongeza mwenyewe na kufurahi na nafsi yake.Palepale akaanza kutema cheche na kumsifia sana mwanamke yule ambaye alikuwa akifurahi mno kwa jinsi Emmanuel alivyokuwa anamsifia.

WAKATI UNAFUNGUA KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE WALAU KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UPO NJE YA APP INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Mazungumzo yao yalichukua lisaa lizima mpigaji akiwa Sakina aliyevutiwa mno na mazungumzo ya Emmanuel aliyekuwa mjanja sana pale aongeapo na mwanamke.Baada ya kumaliza kuongea na msichana yule haraka akachukua maji na kwenda kuoga muda huo saa tatu usiku ndio ilikuwa ikisomeka vyema.

"Sasa ngojea niende kwa mama Mariamu kwanza nikale chakula halafu nipige mambo maana nimemmiss sana."Alijisema Emmanuel baada ya kumaliza kuoga lakini wakati anatoka tu uso kwa uso akaonana na Rozinta ambaye naye alikuwa akimpenda mno Emmanuel.

"Jamani Emmanuel wangu nimekumisije mambo?" Rozinta alimsalimia Emmanuel kwa sauti ya chini na Emmanuel akaitikia poa tu kisha akapiga hatua mbili kutaka kutoka eneo lile la chooni lakini Rozinta akamzuia kwa kumkalia mbele.

"Mbona siku hizi umenisusa lakini.Nakutafuta mwenzako unanitesa kama nini aaah nimemisi mikito yako yani nina n**ge na wewe acha tu." Rozinta aliendelea kutema cheche na safari hii mkono wake akaupeleka mbali zaidi na kumgusa katika mtalimbo wake aliokuwa uko ndani ya taulo.

"Kausha na wewe….nitakutafuta nikiwa free…niko bize siku hizi Rozinta."Emmanuel alijibu na kutaka kupita lakini msichana yule akamzuia tena jambo ambalo lilizidi kumtia hasira Emmanuel lakini hakutaka kulionyesha jambo lile.

"Hebu niambie kesho unarudi….saaaa…." Kabla hata Rozinta hajaendelea sauti za viatu zikielekea pande za chooni zikasikika Emmanuel na Rozinta wakataka kuuwa soo lakini walichelewa.Hakuwa mwingine aliyekuwa anawasili zaidi ya mume wake Rozinta ambaye alishikwa na ghadhabu kubwa alipoona hali ile.Hasira zikamshika na kusogea kwa kasi zaidi wakati huo Emmanuel alijifanya kujikoholesha na kumpita Rozinta aliyeinyanyua ndoo yake na kutaka kuiingiza chooni.

"Weeee Rozintaa simama hapohapo na wewe boya Imma usijefanya mjanja kujifanya kama sijakuona simama hivyo hivyo." Aliongea kishari wake mume wake Rozinta na kusababisha Emmanuel mapigo ya moyo kuenda mbio…..

"Aaah huyu demu kashanipoza yani." Emmanuel akajiwazia na kuchukia ndani ya moyo wake kwa jambo lile ambalo wala hakulisababisha yeye.Kwakuwa mume wake Rozinta aling'aka asimame akafanya hivyo kwa kujiamini na ndoo yake aliyeshika mkononi akiweka chini na kumtazama mume wake Rozinta ambaye alimpita Emmanuel aliyesimama na kumsogelea mke wake aliyemtandika kofi zito la uso mke wake yule aliyeachia ukelele mkali wa maumivu.

"Mwanamke apigwe hivyo wewe hupigwa na upande wa kanga!" Jambo la Rozinta lilimuuma Emmanuel ambaye alijikuta akitamka neno lile kwa hasira ya kilichotokea pale na kuzidi kumtibua mume wake Rozinta aliyegeuka kwa hasira.

"Unasemaje ms**e wewe unasemaje yani nikufume unamtongoza mke wangu chooni halafu namuadhibu unanipandishia unaamua nini sasa." Mume wake Rozinta aliongea kwa jazba na sauti kubwa kisha akamsogelea Emmanuel ambaye presha ilizidi kupanda na mapigo yake ya moyo yalizidi kwenda kasi lakini hakutaka kuonyesha uoga wake akasimama palepale bila ya hofu.

"Aliyekuambia nimemtongoza mke wako nani wewe boya….au umesikia nimemtongoza au aliyeshawahi kukuambia mbona tunavunjiana heshima wewe kenge." Emmanuel akasimama kiume na kuongea maneno yale kwa ukali ambao ulipelekea kuzima moto wa mume wake Rozinta aliyeanza kuona kuwa Emmanuel naye hakuwa lele mama kama alivyotegemea.

"Mke wako mwenyewe kanisimamaisha hapa na kama unavyoona yeye alikuwa mbele mimi nyuma pia alikuwa ananikumbushia mchezo nitoe hela ya mchezo ambao nacheza pamoja naye sasa wee unakurupuka tu uliza kwanza."

"Sasa msiongelee koteeee ndio mje kuongelea chooni.Hivi ndugu yangu mbona unajitoa fahamu haujui kama huyu ni mke wa mtu.Bwege wewe huyu mke wangu mke wa mtu sio wa kumzoea zoea halafu unajifanya kuwaaaka mwenyewe." Mume wake Rozinta naye hakutaka kushindwa.Aliendelea kutema cheche na kupangua majibu ya Emmanuel ambayo kiukweli yalimuingia lakini hakutaka kuonyesha kushindwa kwa hali ile.Wakati huo Rozinta alikuwa kimya chozi likiwa linamtoka na mkono wake wa kulia alikuwa ameshika shavu lake la kulia.

Majibu ya Emmanuel yalimfurahisha sana aliona ameshapata mwanya wa kumtingisha mume wake siku hiyo kwakuwa alikuwa ameshapata sababu.Wakati majibishano yakiendelea wapangaji ndani ya nyumba hiyo walishtua akiwemo mama mwenye nyumba pamoja na Mariamu na wapangaji wengine wanne ambao walikuwa mabechela ila mmoja wao alikuwa ameshatoa taarifa ya kuoa na kuleta mke wake ndani ya nyumba hiyo hiyo.Mume wake Rozinta kuongea kwake kwa jazba ndio kulipeleka awashtua wapangaji ambao walimiminika chooni kushuhudia kulikuwa na nini kinaendelea.

"Na tena nakuambiaaa usimzoee mke wangu na kama mna mambo yenu ya upate tafuta mwingine wa kuwa anakukumbusha fala wewe…na wewe Rozinta malaya wewe mchafu mambo yako ya mchezo iwe mwanzo na mwisho sitaki tena kusikia na sitaki kuongea na huyu malaya wa kiume huyu mwanangu michezo hiyoo uta*aa"

"Mwanangu mbona unaongea sana kama dada wacha maneno tuzipange!" Emmanuel akafupisha maelezo akakunja ngumi kumsikilizia mume wake Rozinta lakini alikuwa na hofu uliopitiliza.

"Heeee ngojea choko wewe." Mume wake Rozinta naye aliuchukua msemo wa kama mbwai mbwai akunja ngumi tayari kumkabali Emmanuel.Nia yake ilikuwa inataka kuthibitisha kuwa hakuwa anataka mchezo linapokuja suala ya mke wake pia alikuwa anataka kuleta heshima..

Wakiwa katika harakati za kusogeleana kwakuwa kila mmoja tayari alikuwa ameshaingiwa na uoga kutokana na kila mmoja alikuwa mbabe wa kuchezea mdomo jambo ambalo mume wake Rozinta hakuwa akitegemea ghafla wapangaji nao wakawa wameshalaki sehemu hiyo.Mmoja wa mpangaji wa kiume akawahi haraka na kusimama katikati baina ya mume wake Rozinta na Emmanuel na mikono yake akaitanua kuwazuia hata wasisogeleane.

"Aaaah ndugu zangu kausheni nyie kwani kuna nini." Maneno akayesema yule bwana na kuibua mzozo na kila mtu akawa anauliza chanzo cha mpaka wawili wale kufikia huko.

"Niaaacheniii oyaaa dogo niachie nimuonyeshe huyu fala mmoja nimemfuma amesimama na mke wangu hapa chooni halafu namuuliza anajibu kunya!" Mume wa Rozinta akatumbua jibu ambalo lilienda kuwachoma kwenye moyo moja kwa moja Mariamu pamoja na mama yake waliyokasirishwa na kuhuzunika kwa taarifa ile ila hawakutaka kuonyesha hisia zao hapo.

"Nyieee muaachieni hawezi kunivunjia heshima mke wake ndio amenisimamisha na wewe umeona halafu unanipandisha unanichukuliaje wewe unanichukulia boya kiande wewe?." Kwakuwa Emmanuel naye hakutaka aibu iangukie kwake naye akajibu mapigo na kujifanya kama anataka kuchomoka mikononi kwa waliomzuia ili akazipange na mume wake Rozinta.Hiyo ilikuwa janja janja kwake hakuwa na hata nia ya kupigana sema hakutaka kuonekana mkimya kwakuwa ukimya wake ungethibitisha maneno aliyosema mwenzake.Juhudi za kuwatuliza wawili hao wake kimya zikafanikiwa hii ni baada ya mama mwenye nyumba kuongea kwa sauti kubwa kuomba utulivu.Wote wakatii ikiwemo waliokuwa wakigombana.

"Weee! Rozinta sasa na wewe unalia nini? Hebu sogea hapa ueleze ilivyokuwa je Emmanuel alikuwa anakutongoza au la." Mama Mariamu akawa na kweli Rozinta aliyekuwa akilia akasogea karibu na mama Mariamu aliyekuwa karibu na mwanae maana wapangaji wale wanne wanaume wawili walishika Emmanuel na wengine walimshika mume wake Rozinta aliyekuwa anaitwa David.

"Wacha kuliaaa wewe malaya zungumza huko." David akajikuta akiropoka baada ya kuona Rozinta aongei chochote alikuwa akilia tu.

"Eeeeeee wewe devi acha kisokolokwinyo kama hasidi aliyekosa haya muangalie kichwa chake kama mjusi guluguja malaya mwenyewe kama mwenye nyumba nimeomba utulivu na Rozinta wacha kulia zungumza sasa." Mama Mariamu akaweka sawa na kusababisha utulivu kutoka kwa David uchukue nafasi yake.Rozinta akakohoa kwa kwiki na kuanza kuzungumza.

"Ni kweli mimi wakati nakuja hapa chooni Emmanuel alikuwa anatoka…mimi ndiye niliyemsimamisha nilikuwa nikimkumbushia kuhusu kupeleka hela ya mchezo mapema maana amebaki yeye tu.Mimi Emmanuel sijamuona muda naona yuko bize nilipomuoana hapa nimemkumbishia maana sio vizuri kumgongea mtu chumbani kwake akiwa amepumzika.Kosa ni langu na si la Emmanuel mume wangu yeye hajauliza amechukulia hasira tu.Mimi mambo haya nimeshachoka.

Ndani hatuaminiani nimechokaaa naondoka.Huu mwili sio wa kupigwa pigwa." Rozinta akaongea kwa jazba naye akagongelea mstari kile alichokisema Emmanuel na kumkandamiza mume wake maana ndio ilikuwa mtetezi wake.David likamshuka baada ya maneno ya mke wake kibao kikageuka kwake wapangaji wenzie wakiume wakaanza kumpatia somo palepale huku mama Mariamu akianza kumshusha Rozinta hasira zake za uongo na kumsihi asichukue maamuzi mabaya kwa maana mume wake anafanya vile kwakuwa alikuwa anampenda.

"Jamani nimechoka naombeni niende kupumzika." Emmanuel aliongea lakini wenzie wakamzuia na kumuomba apeane mikono na David ugomvi uishe wasemeane.Emmanuel akakubali na David naye akakubali kishingo upande lakini hakuwa na jinsi akafanya hivyo.

"Emmanuel kabla haujapumzika nakuomba uje chumba kwangu ninataka nikupe mkataba wako na kukupa nasaha juu ya wake za watu." Mama Mariamu akamwambia Emmanuel aliyetikisa kichwa chake na kuondoka eneo lile nia ya Mama Mariamu alikuwa ameshaijua hivyo alitabasamu mwenyewe kimoyomoyo…….

Maneno ya mama Mariamu akimwambia Emmanuel yakisikiwa vyema na Mariamu aliyehisi kitu.Wakati Emmanuel akiondoka eneo hilo na yeye haraka akachomoka.Mama yake alibaki pale kuwapa nasaha ya bure Rozinta pamoja na David jinsi ya kulinda zaidi ndoa yao.

"Emmanuel weee Imaa." Mariamu alimuita Emmanuel ambaye alikuwa anajiandaa kuingia chumbani kwake.

"Mariamu nambie."

"Umenisikia naomba jifungie ulale mpenzi mama hana lolote wee mikataba gani ya usiku ana lake jambo hana hata haya.Kesho asubuhi ndio umeniskia mpe…." Kabla Mariamu hajamaliza kuongea akawaona wapangaji wengine wanne wakielekea hapo pamoja na mama yake akiwa na Rozinta na David.Haraka akaua soo na kupotea hapo na Emmanuel naye haraka akaingia chumba kwake.Nusu saa ikapita hali ikawa kimya na shwari kabisa.Mama Mariamu alikuwa akisubiri ujio wa Emmanuel alikuwa ameshaoga vizuri na kanga moja tu akiwa ameivaa kwenye mwili wake ndani akiwa hana kitu.

USIIKOSE SIMULIZI INAYOFUATA

Umeyaona Matangazo?
Yabonyeze Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni