MUWASHO (4) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Ijumaa, 31 Machi 2023

MUWASHO (4)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
๐Ÿ“– KUSOMA SIMULIZI
๐ŸŽฌ FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
๐Ÿ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
๐Ÿ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa

Jina: MUWASHO
Mwandishi: Seif Jabu

SEHEMU YA NNE
ILIPOISHIA...
seif ndiye chaguo langu nimeamuwa hivyo na leo nitaenda kulala kwake nitampa chochote atakacho hitaji kutoka katika mwili wangu kwani nimeamuwa kumpa maisha, na kuanzia leo sitokuwa muoga kwa yeyote lazima nijisimamie na nifanye kile nafsi yangu inachotaka tena acha nimuandikie sms nimwambie ukweli seif

WAKATI UNAFUNGUA KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE WALAU KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UPO NJE YA APP INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Mernah alishika simu yake alatafta namba ya simu ya seif kisha akaenda upande wa SMS akatuma ujumbe mfupi wa maneno,

Seif nimefanya maamuzi kutoka moyoni mwangu na maamuzi yangu ni kuwa nimeamuwa kukupenda na kukuweka katika moyo wangu, jina lako nimeliweka katika mishipa ya fahamu ya mwili wangu ili daima nikupende seif nakupenda sitokuumiza na wewe niahidi kitu"

Seif akiwa amejilaza amepumzika kutokana na uchovu aliokuwa kuwa nao alisikia mlio wa sms kwenye simu yake iliyokuwa pembeni yake akaichukuwa na kuisoma baada ya kusoma ujumbe akaujibu kama hivi,

Mernah na mimi nakupenda sina cha kukuahidi zaidi ya kukwambia nakupenda

Mernah aliufurahishwa na ujumbe wa seif akamwandikiya sms tena seif,

"asante seif kwa ujumbe wako mzuri pia napenda kukwambia kuwa leo nitakuwa mgeni wako nitalala kwako mpaka kesho"

Seif alipata ujumbe wa sms akaujibu kwa furaha,

hata Sasa hivi ukipenda uje hapa ni kwako usipaogope"

Seif alipomaliza kutuma ujumbe gafla sms kutoka kwa Skola iliingia,

"leo usile hotel nitakuja na chakula mida ya saa mbili na kuanzia leo nitakuwa kama nimehamia kwako"

Seif alipagawa………

Seif alishitushwa na ujumbe wa Skola kwani alikuwa hajajiandaa kuwa naye siku hiyo na alijuwa hawezi kurudi siku hiyo kutokana na kutokana na kulalamika kusikia maumivu makali, seif alimtumia sms ili kumzuia asije,

"Skola sitokuwepo leo nitakuwa mjini kwa rafiki yangu wana sherehe"

Ujumbe ulifika ila haukujibiwa na skola seif akawa anajiuliza kama ameupata au laa maana hakupata ujumbe wowote wa Skola,

mbona kakaa kimya atakuwa ameupata ujumbe kweli? Au haujamfikia? Ngoja nimpigie

Seif alipiga simu ya Skola ikaita na baada sekunde kadhaa ikapokelewa,

"Skola mbona nakutumia ujumbe alafu hunijibu?"

"Sorry Mpenzi wangu"

"Ujumbe umepata?"

"Ndio,"

"Sawa baadae basi"

"Sawa,"

……………….

Masaa yalikimbia kama upepo Mernah akawa anajiandaa kwenda kwa Seif, ila wakati akijianda Skola alimuuliza,

"Unakwenda wapi mbona maandalizi hayaishi?"

"Napokwenda napajuwa Mimi,"

"Kwa hiyo Mimi sifai kupajuwa?"

"Ingekuwa lazima upajue ningekwambia,"

"Naona umeota mapembe siyo?"

"Utakavyoona wewe,"

"Unajua naweza kukuzuiya kutoka?"

"Labda siku nyingine siyo leo, leo ni lazima nitoke na nitalala ninapo kwenda,"

"Unasema Mernah?"

"Kama ulivyo sikia"

Skola alijiuliza kilichombadili Mernah ni nini ila hakupata jibu akamuwa aache kumhoji mengi kwa kuwa na yeye alikuwa na mipango yake,

Skola na yeye alivaa baada ya kumaliza kuvaa alitoka bila kumuaga Merman,

……………………..

Upande wa pili seif baada ya kujiridhisha kuwa Skola hatokuja alimtumia tena sms Mernah,

"Mernah utafika saa ngapi hapa kwangu? Naomba uwahi Mpenzi wangu"

Mernah alipata ujumbe wa seif na bila kuchelewa akaujibu kama ifuatavyo,

"nakuja baada ya dk10 nitakupa nimefika hapo kwako wewe tafta cha kuniandalia"

Seif alipopokea ujumbe wa Mernah alitoka kitandani mbio mbio kaenda kwenye kiosk cha karibu akanunu juice kisha akarudi mbio mbio mpka kwenye chumba chake ila alipoingia alimkuta kitandani Skola,

"Hheee!!! Skola mbona uko hapa?

" unachoshangaa ni nini Seif?"

"Nashangaa umefikaje chumbani kwangu?"

"Kwa hiyo sikubaliwi kuingia hapa?"

"Sijamaanisha hivyo ila si nilikwambia kuwa nitatoka?"

"Tutatoka wote kwani kuna tatizo?"

"Wewe si ulisema unaumwa ndio maana sikutaka kukusumbua,"

"Nimepata nafuu baada ya kujikanda na maji ya moto na kunywa dawa za maumivu,"

"Oky, basi nakuja kuwa unatumia juice,"

"Sawa,"

Seif alitoka nje ili kumsubili Mernah nje asije kuingia ndani akakutana na Skola,

Seif alipotokeza nje tu alikutana na sura ya Mernah akiwa anakaribia kufika mlango,

"Ohhh!!!! Mpenzi wangu karibu,"

"Asante mambo vipi seif?"

"Shwari kabisa nimefurahi kukuona nilijuwa hautokuja,"

"Kwanini nisije?"

"Unaweza kupata dharula,"

"Kwako wewe Seif siwezi kukubali dharula labda iwe dharula ya kifo tu,"

"Mernah unanifurahisha sana,"

Seif alichezesha hakili afanye nini ili kuokoa jahazi akaona cha kufanya ni jambo moja tu ni kuondoka na Mernah eneo hilo,

"Mpenzi hebu twende huku kuna sehemu nataka nikupeleke,"

"Mhh wapi tena?"

"Ni surprise Mpenzi wangu twende utapaona,"

Seif aliondoka na Mernah na moja kwa moja akampeleka katika hotel ya garama wakakaa baada ya kukakaa seif akamuuliza Mernah,

"Vipi Mpenzi wangu umepapenda mahala hapa?"

"Sana tena sana Mpenzi wangu kwani nilikuwa nikipaona kwa nje tu,"

"Basi leo chakula chetu tutakilia hapa na vinywaji tutanywea,"

"Mhh…. Asante nimefurahi sana,"

"Mernah nataka nikwambie kitu?"

'Kitu gani Mpenzi wangu?"

"Nataka nikwambie kuwa nakupenda sana, na ikitokea ukaona nimefanya kitu ambacho hakijakufurahisha naomba uniambie nijue sawa?"

"Sawa Mpenzi wangu,"

Seif alitoka akaenda kaunti kuchukua chumba baada ya hapo akarudi wakaendelea kula na kunywa ila akiwa amekaa gafla simu ya Mernah iliita na Mernah akaipokea kusikia mpigaji anataka kumwambia nini?

"Hallow Mernah unaongea na baba yako hapa, uko wapi?"

"Niko hapa hapa chuo chumbani kwangu,"

"Niko hapa nje fungua mlango,"

"Sawa baba,"

Mernah alimuangalia Seif kwa jicho la huzuni na masikitiko kwani hakufikilia kama hayo yanaweza kutokea,

"Mernah usiwe na shaka wewe twende ukaonane na Baba yako,"

"Seif nisamehe,"

"Hayo ni ya kawaida katika maisha wala usiyawazie sana,"

"Sawa basi acha nichukue tax hapo nje niwahi,"

"Sawa wewe wahi na Mimi acha nirudishe funguo za watu Niko nyuma nakuja,"

"Sawa,"

Mernah aliondoka hivyo na Seif akabaki anawaza sana dhamani ya chumba alicholipia sh.50,000 roho ikamuuma sana akaona hawezi kurudisha funguo hivi hivi akachukua simu akampigia Skola,

"Hallo Skola uko wapi?"

"Kwani wewe umeniacha wapi?"

"Bado uko kwangu hapo?"

"Sasa wewe unazani nimeenda wapi?"

"Sasa Mpenzi wangu kwanini usiende kupumzika tu maana Mimi nikilala hapo na wewe ni lazima niombe game na wewe mwenyewe unasema unaumwa Sasa nitafanyaje?"

"Kwa hiyo hicho ndio kimefanya usije kwako?"

"Ndio kwa kuwa nakuonea huruma,"

"Wewe njoo Mimi Niko vizuri tutanya tu hata kidogo,"

"Sasa fanya hivi chukua tax umwambie akulete hapa GL.Hotel tutapakutania sawa?"

"Sawa nakuja swty,"

Skola hakutaka kuuliza mengi haswa kumuuliza seif kwa alimuacha ndani peke yake? Swali hilo aliliweka kipolo ili aje amuulize wakiwa wote,

Kama alivyo ambiwa Skola ndivyo alivyofanya alichukua tax na mda mfupi tu alikuwa amefika katika eneo la GL.Hotel na kuonana na Seif,

"Karibu swty,"

"Asante,"

"Vipi mbona kama hauko sawa,"

"Niko sawa mbona,"

"Kama uko sawa basi ni vizuri twende ndani,"

Skola yeye alifuata nyuma kwani alikuwa hana analolijuwa Juu ya uwepo wake pale,

"Karibu swty wangu hapa ndipo nilipo taka tupumzike siku ya leo"

"Asante Mpenzi wangu kweli naona nimeamini unanijari,"

"Nisipokujari wewe nitamjali nani?"

"Mhh asante Seif,"

Seif moyoni alikuwa akimuwazia Mernah kama amefika salama au laa kwani toka ameondoka alikuwa hajaongea naye,

Mernah atakuwa amefika kweli!? Inabidi nitafte mwanya wa kidogo nimpigie nijue kama amefika

"Seif asante kwa surprise yako nzuri na ya kufurahisha,"

"Na wewe pia asante kwa kuifanya ikamilike,"

"Sawa, ila naomba nikuulize kitu Mpenzi wangu,"

"Uliza tu uko Free kwa chochote,"

"Kwanini uliondoka bila kuniaga ukaniacha chumbani kwako?"

"Nilifanya hivyo ili kuja kuandaa hii surprise,"

"Seif masaa yote hayo?"

"Ndio,"

"Mbona hii karatasi ya bili inanesha ulipewa masaa mawili yaliyopita?"

"Skola kwa hiyo hujafurahia hii surprise?"

"Siyo kwamba sijaifurahia ila nimeuliza tu, kama nimekuboa nisamehe,"

"Skola nilipita nikiwa na rafiki yangu baada ya kuacha ndio nikakupigia simu wewe?"

"Mmmhh oky nimekubali,"

Skola alikuwa kama anashitua kitu furani hivi kwa Seif japo mshituko wake haukuwa wa uhakika na jambo alilohisi,

"Skola nakuja kidogo ngoja nikaweke oda ya chakula nakuja,"

"Si uwapigie simu si naona simu ya mkononi ipo na namba hizo hapo,"

"Kuna mpishi nataka nimuone mwenyewe nimuelekeze chakula nachohitaji,"

"Sawa,"

Seif alitoka mbio mbio mpaka nje alipofika gorofa ya chini alitoa simu akampigia Mernah,

"Haloooh Mernah?.

Seif aliita Mernah ila akaduwa simu ilipopokelewa na mwanaume,

"Hallow wewe nani?"

"Seif hapa,"

"Sikia wewe paka kuanzia leo ukome kuwa unapiga simu za wapenzi wa watu usiku sasa hivi ni mda wa kupumzika,"

"Bro ungeniambia vizuri siyo kunitukana,"

"Ndio hivyo shika adabu yako,"

"Sawa asante,"

Seif alichanganyikiwa hata chakula hakukumbuka kuagizia tena bali aliwaza mengi kuhusu Mernah,

ni wapi nimekosea mpaka anifanyie hivi Mimi jamani? Mbona kama siamini? Mernah ni wa kufanya haya mambo ya mchanyo?

Seif hakuamini ila ilimbidi aamini tu japo roho ilimuuma kwani Mernah ndiye binti aliyekuwa anampenda kuliko wote,

"Vipi mbona umerudi kama mtu mwenye mawazo sana kulikoni?"

"Kawaida tu,"

"Au chakula unachopenda kimekwisha?"

"Hata sijafika huko,"

"Mhh kulikoni?"

"Nimeona nije nitumie simu maana sijamkuta huyo mpishi,"

"Sawa,"

Kabla seif hajapiga simu, simu yake iliita na mpigaji alikuwa ni Mernah.

Seif aliangalia simu yake akawazia apokee au aache ila wakati anawaza Skola alimwambia,

"Seif si simu yako inaita hiyo?"

"Ndiyo naisikia naifikilia kwanza,"

"Kuifikilia nini!?"

"Niipokee au niache,"

"Kwanini!?"

"Nina sababu zangu mie mwenyewe,"

"Sawa,"

Seif alipokuwa anaongea na Skola simu ilikatika ila Skola alionesha hakupendezwa na kile tendo kwani alihisi huenda simu ile ilikuwa ni ya mwanamke wa Seif,

Wakiwa kimya waote ukimya ulivunjwa na simu Skola ilipoita na kuipokea,

"Hallow,.

" mhhh niambie Mpenzi wangu Monica? "

"Mimi nipo boadi tu hapa kwangu mume wangu sikuoni,"

"Kuna sehemu nimeenda Mpenzi wangu,"

"Ukirudi pita kwangu basi,"

"Usihofu nitapita,"

"Sawa,"

Skola baada ya kuongea na rafiki yake alimsogelea Seif na kumkumbatia ila seif alikuwa amekasirika,

"Mpenzi wangu mbona kama umekasirika hivi?"

"Siyo kama nimekasirika kweli,"

"Kwanini?"

"Utaanzaje kuongea na simu wakati tupo faragha,"

"Nisamehe Mpenzi wangu,"

"Mimi nilipoacha kupokea simu sikuwa mjinga nilikuwa na akiri zangu, mtu unaweza kupigiwa simu ukapewa taarifa za ajabu ukakuta sitarehe zote zinasimama,"

USIIKOSE SIMULIZI INAYOFUATA

Umeyaona Matangazo?
Yabonyeze Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni