MUUZA CHIPS (14) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumapili, 21 Mei 2023

MUUZA CHIPS (14)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
๐Ÿ“– KUSOMA SIMULIZI
๐ŸŽฌ FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
๐Ÿ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
๐Ÿ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa
Mwandishi: MoonBoy

SEHEMU YA KUMI NA NNE
ILIPOISHIA...
Sema mwanamke ni mjamzito mjinga zaidi kwasababu ana maamuzi ya haraka, yaan hapendagi kuumiza kichwa kuhusiana na jambo gumu, ila mwanaume ni mjanja sana kwenye maamuzi yake, ila maamuzi yetu yakilegea tu kidogo, basi na mwanamke anakuwa juu,…

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Mke au mchumba au mpenzi wa Ibrahim ambae ni kaka yake na chidi, ni mschana mzuri lakini alikuwa na jeuri kubwa sana mbele ya ibra, kana kwamba Ibrahim hawezi kuruka juu zaidi kwa mwanamke huyo, kwani kitendo tu cha kuacha elfu 30 kwa siku, tayari ni dhahiri kuwa mwanamke huyo hafai kabisa hata kwa dawa, lakini kijana Ibrahim kapenda mpaka basi, tena anampenda sana pale aliposikia kuwa mpenzi wake huyo ana ujauzito wake, yaani hapo Ibrahim ndio kachanganyikiwa kuliko kitu chochote kile,…

Lei mke wa Ibrahim alitembelewa na rafiki yake kipenzi ambae inavyosemekana alimkopa kiasi cha laki tatu, hivyo leo kaja kuichukuwa peda hio baada ya kumdanganya Ibrahim kuwa baba mwenye nyumba kaja kudai kodi ya nyumba ambayo anaishi mwanamke huyo,.. Lakini haikuwa kweli kwasababu Ibrahim akitoa pesa haitaji kukumbuka aliitoa lini, kwasababu anamuamini sana mpenzi au mke wake mtarajiwa kuwa hawezi kufanya kitu chochote kile kwasababu wanapendana sana,..

Rafiki yake huyo alimsikia mtu huyo akisema kuwa alikuwa na uja uzito, hivyo leo alimshangaa kuona hana kitu chochote kile, na anadhani kuwa labda tayari ana kichanga kipo ndani,.. Yaan atakuwa tayari keshajifungua mtoto.. Lakini ukweli ni kwamba Rehema hakuwa na mtoto kwa wakati huo, labda mimba huenda akawa nayo,

"we acha tu, uschana unasumbua, bora yako wewe mwenye mume….. Enheee afu shost kuna siku ulinambia una mimba wewe"

"ndio shost"

"lakini ilikuwa ni muda,… Afu naona kama tayari utakuwa unafua mapempasi tu"

"shost we acha tu"

"we shost, hebu niambie ukweli, ulikuwa na mimba kweliii au unazingua tu"

Dada huyo alimuuliza rehema swali hilo huku maskio yake yakiwa hewani ili kupata ukweli

"shost jasu.. Hapa ni mjini dada, hakuna shamba huku shosti"

Yalikuwa ni majibu ya rehema akimjibu rafiki yake aitwae jasu au jasmini,…

"mmmhhh basi nimeelewa, nipe changu niende"

Rehema aliingia ndani na kutoa kiasi cha laki 3 na kumpa jasu,…. Jasu anaondoka huku akiwa kama anasikitika ila haikujulikana kitu alichokuwa akikisikitikia kwa wakati huo,..

"wenzio wanaomba mungu wapate mwanaume anaejiweza kimaisha, afu wewe unamchezea na kumuona hana thamani,… Ama kweli mahindi humuotea mwenye pengo"

Jasu Aliongea hayo huku akitembea zake tena alikuwa peke yake,…

"shost jasu… Hapa ni mjini dada.. Hakuna shamba huku shost"

Aliyakumbuka maneno alioyasema rafiki yake,…

Tukija huku kwa chidi kijana mchakalikaji wa maisha,.. Ghafla simu yake inaita, kucheki jina alikuwa ni kaka yake Ibrahim,

"haloo kaka sema"

"Aisee chidi hebu fanya mpango wa kutuma elfu 30 hapo kwa wakala"

"Elfu 30"

"ndio, fanya haraka bwana… "

"ok sawa… Lakini nairusha kwa nani, mana kama ni wewe si bora nichukue toyo mara moja nije hapo"

"we peleka tu pale kwa wakala, anajua namba ya kutuma"

"ok sawa, wacha nipeleke"

Chidi alihudumia wateja wake kisha akaenda hapo kwa wakala, kisha akatoa elfu 30 na kumpa wakala

"asee kaka Ibra kaniagizia utume hii pesa, ila kasema number unaijua"

"aaahhh ok ok, naijua hakuna shida"

Chidi alirudi kazini kwake na kuendelea na kazi,… Ikiwa ni mida ya saa 10 hivi jioni wanafunzi walikuwa wakitoka na kupitia kwenye chipsi, kila mmoja alikuwa akipenda kutembea huku akipata chipsi, na wengine walikuwa wakila hapo hapo,…

"chidi mambo"

Chidi alikuwa hajaskia, kwasababu alikuwa akiweka chipsi kwenye karai la mafuta, hivyo ilimfanya asisikie…

Sasa kutokana na kutosikia salamu hio, yule mwanafunzi alimsogelea kijana chidi na kumtekenya huku akisema,

"unajifanya husikii salamu yangu, au kisa mi sio naniii"

Chidi alishtuka na kugeuka,…. Alikuwa ni rafiki yake na saumu, mmoja wapo kati ya wale waliokuwa wakiongea mida ya saa nne leo, anaitwa fatu,..

"weee ungenidondosha kwenye mafuta huku, mbona una michezo ya hatari…. Haya sema wataka chipsi za shilingi ngapi"

"wala ata staki chipsi, nilikuja kukuona tu mana nimekumisi"

"eeee ni hilo tu"

"ndio"

"ok poa asante"

Chidi aliligeukia karai la chipsi na kuendelea kugeuza geuza chipsi,…

"afu leo kama umechoka, kama vile jana hujalala"

Fatuma au fatu alianza kumchokoza kijana chidi, mana si alisimuliwa na rafiki yake saumu, kuwa jana alilala na kijana chidi, hivyo fatuma anaanza kujiunga na kundi la mapenzi kwa kijana chidi..

"aaahh kuchoka tu, si unajua kazi zenyewe hizi zilivyo"

Aliongea chidi huku akiendelea na kazi yake ya kuchoma chipsi….

"mmmhhh chidi we muongo jamani, si useme ukweli tu"

"kweli vile.. Nimechoka tu kikawaida"

"nikuambie kitu chidi"

"kitu gani hicho"

Tukija huku kijijini kwa akina chidi, baba wa chidi alikuwa hana hali mbaya sana, kwani hata kupata chakula alikuwa anakula tofauti na mwanzo,… Mke wa chidi ndio alikuwa beneti kwa kuzifanya kazi zote za kumhudumia baba wa chidi,

"salma mwanangu, huna hakiba hapo, mana kule hospitali nimemaliza pesa yote"

Alikuwa ni mama yake na chidi akiongea na salma kama ana chochote alichokuwa macho ili wakanunue dawa, mana walipokuwa hospitali waliitumia ile elfu 70 kwa kumuuguza mzee king,.. Na hata hivyo hospitali kule walitoka kwa kukosa pesa ya kuendelea kukaa kule mana hawakuwa na pesa ya kuendelea kukaa hospitali,

Salma alikuwa ni wife Material tena kapitiliza na Material yake,… Salma alikuwa na shilingi elfu 20 alioachiwaga na kijana chidi ambae ni mume wake,..

"mama, kwani wataka nini tukanunue tu"

"dawa,… Hukumbuki dokta alisema tununue dawa"

"aaahhh mimi pale nilikuwa sipo na ndio mana sijui"

"ni hivyo tu, na dawa zenyewe zinauzwa ghari sana"

"haina shida mama, kikubwa baba apone tu,… Nipe hio karatasi niende duka la dawa"

Salma alipewa karatasi waliopewa na dokta kwa ajili ya kwenda kununua hio dozi inayotakiwa kwa ajili ya mzee huyo,.. Salma alikimbia mpaka duka la dawa na kununua dawa hizo zenye thamani ya shilingi elfu 12, hivyo alibakiwa na kiasi cha elfu 8 katika kibindo chake,…

Tukija huku kwa akina sarah na rafiki yake miriam, waliokuwa wakipiga stori za hapa na pale wakiwa kwenye gari,..

"Enhee Jana ulisema utaenda kwa jambazi, ivi ulienda"

"ndio nilienda, lakini sikuwakuta wote"

"hujawakuta… Kwani si anaumwa huyo mtu"

"mmhhh mi ata sijui ni kwanini hawapo"

"ulienda saa ngapi"

"kama saa moja hivi"

"Ehehehehe Ehehehehehe"

"sasa wacheka nini miriam"

"hao wameenda kuiba, ndo muda wao huo"

"mschiuuuuu… (msunyo) yaani unavyoniuzi we Miriam"

"aaaaaa ahahahahaha… Aaaaahahahaha, kupenda jambazi yataka moyo shost"

Walikuwa wakitaniana hapa na pale huku wakifurahi wote,

Tukija huku kwa kijana chidi akiwa ndio kwanzaa yupo bize kwa kugeuza chipsi zisiungue,…

"nikuambie kitu chidi"

"kitu gani hicho"

"naomba nikusaidie kugeuza chipsi"

"hapana… Kama umependa kuniseidia, we nioshee hivyo viazi tu"

Fatu aliweka begi ndani kisha akaanza kumseidia kijana chidi, anaziosha vizuri kisha anaziweka katika ndoo safi,…

Wakati huo huku shule, saumu alikuwa bize na kuandika somo ambalo lilimpita muda fulani hivi, hivyo alikuwa akimaliza, na nia yake ya kuchelewa ni ili atoke na chidi ili kama vp warudie mchezo,… Bila kujua huku fatu nae alikuwa na mpango aliokuwa nao saumu,…

Masaa yalisogea na hatmae chipsi zikawa zinaisha, ila ilikuwa kagiza ka saa 12 kalianza kutawala,… Wakati huo huku shule saumu ndio anatoka ili ampitie chidi wake warudi wote nyumbani,..

"chidi jamani, mbona hufungi Twende"

Aliongea Fatuma huku akifikicha vidole vyake,

"heeee ivi kumbe unanisubiri mimi tuondoke wote"

"ndio.. Mi naogopa kutembea mwenyewe afu nimechelewa daladala"

"Eeeehh mungu wangu eee… Ngoja basi nikupe buku ya kupanda toyo"

"staki, mi nataka tutembee tu"

"mi namsubiri… "

Kabla hajamaliza kusema kuwa yeye anamsubiri kaka yake waondoke nae, Fatuma alijua chidi anasema mimi namsubiri saumu hivyo kabla hajamaliza kusema… Fatuma alimkatiza na kusema

"najua, ila leo tuende na mimi, naogopa kwenda mwenyewe"

"nakupa pesa ya pikipiki"

"mmmh mi naona hutaki… Naomba uje unimulikie nichukue begi langu"

Waliingia ndani mana siku hio umeme ulikatika hivyo palikuwa na kale kagiza ka saa moja kasorobo jioni…

Sasa chidi akachukuwa tochi,.. Sasa ile anaiwasha tu, tochi ilishikwa na ikazimwa, hajakaa vizuri kavutwa na kukalishwa chini,…. Huku fatuma akisema

"hakuna mwanamke asiependa mapenzi matamu,.. Kwanini niumie juu yako chidi"

Aliongea fatuma huku akimsogezea chidi mdomo

"we nani kakuambia mi najua mapenzi"

Chidi nae alitupa swali huku akilegea na kajoto ka fatuma,.. Kama unavyojua wanafunzi walivyo na joto kali kuliko hata naniii

"kukuona tu… Ghafla tu nikakupenda"

Chidi alikuwa anataka aulize swali lingine lakini alichelewa,… Kwani kinywa cha fatu kilishafika kwenye kinywa cha chidi,.. Huku fatu akimfosi chidi amshike matiti, ili zimpande za haraka……

"Chidi jamani, bado upo mpaka saa hizi… Afu mbona kuna giza hivi humu ndani"

Alikuwa ni saumu ndio aliokuwa akiuliza huku akiwa yupo ndani, sema hajawaona kwakuwa kulikuwa na giza……

Chidi hakupatwa na mshtuko wowote baada ya saumu kuingia, mana alijua kwa sehemu waliopo hawezi kuona kwasababu hakukuwa na umeme kwa wakati huo,…..

"Huoooooooooooooo"

Zilisikika sauti za watu wakiushangilia umeme uliorudi muda huo….

Kiukweli mapenzi hayajaribiwi na wala hayatangazwi, kosa la saumu kiwatangazia wanagunzi wenzake kuhusu mpenzi wake chidi, sasa yamtokea puani, Aliwasimulia rafiki zake wengi sana lakini walioguswa na simulizi hio ni Fatuma na Zaituni,…. Kumbuka kuwa, mwanamke ana nafasi kubwa sana ya kumpata mwanaume, lakini mwanaume hana nafasi kubwa ya kumpata mwanamke… Nikimaanisha kiwa, mwanamke akimtaka mwanaume, ni rahisi sana kumpata, kuliko mwanaume kumtaka mwanamke.. Yaani wanawake ni kwamba sio desturi yao kutongoza wanaume lakini wanaweza na tena kwa asilimia 90… Na yote hio ni kuyokana na udhaifu wa wanaume ulivyo, mana takwimu zinaonyesha kuwa, wanaume ndio wanaosikia hamu zaidi kuliko wanawake,.. Mwanaume hata kama katoka kusex sasa hivi, lakini akikutana na mschana mwingine mpya, basi nae hua mpyaaa utafikiri hajagusa kitu, hivyo ndio mana wanaume ni wadhaifu sana kwa wanawake, hata iweje lazima utulie mtoto wa kiume, iwe unapita au unakaa, lazima utulie

Sasa kosa la saumu la kuwasimulia wenzake jinsi alivyofanywa na kijana chidi kwa kugeuzwa geuzwa kama samaki, kumbe mmoja kati ya hao alitamani naye ageuzwe kama saumu, na hakuchukuwa muda, Kutokana na udhaifu wa mwanaume kwa mwanamke, Fatuma alifanya kila mbinu mpaka akafanikiwa kumnyaka kijana chidi,… Tena bila kuchelewa alifanya juu chini mpaka akamnyonya denda,

INAENDELEA...

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni