MUUZA CHIPS (7) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Ijumaa, 19 Mei 2023

MUUZA CHIPS (7)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
๐Ÿ“– KUSOMA SIMULIZI
๐ŸŽฌ FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
๐Ÿ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
๐Ÿ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa
Mwandishi: MoonBoy

SEHEMU YA SABA
ILIPOISHIA...
Sasa dada kuingia anamkuta chidi katulia kwenye siti huku akitafuna muhogo mbichi, dada huyo alijilaumu sana kwa kile kitendo alichokifanya muda ule, na uzuri wa chidi yeye hakutaka kubishana na mdada huyo aliekuwa mzuri wa kila aina sema ana kakiburi flani hivi ambako sio kazuri kwa jamii,

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Chidi alimaliza kula mihogo yake, aliweka mfuko wake wa nguo katika siti yake kisha akatoka nje huku yule dada anamuangalia tu, na chidi hajui kama alikuwa anatafutwa na huyo huyo dada

Chidi alienda msalani kisha akawa anarudi, mara akapishana na yule dada nae alikuwa akitoka nje, chidi akaingia na kukaa katika siti yake ile ile,.. Aliendelea kula mihogo mana hakuwa nao mmoja alikuwa nayo ya kutosha,.. Mtoto wa kiume alikuwa akila nazi na muhogo, mjanja utajua tu kinachoendelea hapo mana nazi na muhogo kuna vitamini flani vinaongezeka huko mwilini, na hapo hajapata karanga na maziwa ili dozi ikamilike vizuri….

Ghafla yule dada anaingia ndani ya gari huku akiwa kashika kamfuko keusi kana kwamba kuna kitu kaweka humo ndani, mara muda umeisha na abiria wote walikuwa wakimiminika ndani ya gari, na hatimae gari kuondoka, Safari inaanza kuelekea Arusha,… Yule dada kumbuka amekaa na mama mmoja ambae aliiacha siti yake ili kijana huyo asikae chini

"samahani mama"

Alikuwa ni yule binti akimwomba samahani yule mama aliokaa nae pale

"una shida gani"

Hata yule mama nae alianza kumletea nyodo mana kitendo cha kumkataza chidi kukaa katika siti ile kiliwaudhi baadhi ya abiria waliokuwemo humo haswa haswa wakina mama.. .

"naomba mnisamee mama angu, nilikuwa nataka nimuombe huyo kijana msamaha"

"heeeeeee we ndio wa kumuomba yule kijana msamaha"

"najuta kwani nilimkosea sana"

Yule dada alikuwa akilengwa lengwa na machozi ya hapa na pale kana kwamba kweli alikuwa hajafanya vizuri kwa kitendo kile

"sikia nikuambie wewe binti, tena ni sawa na mtoto wangu wewe,… Haya ni maisha tu watu wanapita, leo unamchukia huyu kesho kuna mahari utamkuta na utakosa msaada kwa sehemu uliyomkuta, kwahio huu uzuri wenu na haya maumbo yenu yanayowadanganya kuwabeza wenzenu kuwaona sio kitu kwasababu nyinyi mna maisha mazuri sasa wamnyasa nyasa mwenzio, sio vizuri, kwani alikutongoza huyu… Kiukweli mimi kama mzazi sijapenda tabia uliomfanyia kijana mwenzio, na hata wewe unakuja kuwa mama kama mimi, je mwanao akifanyiwa hivi utaridhika wewe,.. Ukitaka kufanya jambo, hebu fikiria na kesho itakuwaje sio ufanye tu… "

Yule binti alilia kwa haya maneno mpaka akamuegemea yule mama huku akiomba msamaha..

"wakumwomba msamaha sio mimi wala yule kijana,.. Umati woote huu ulikasirishwa na kitendo chako kibaya,.. Hivyo kama kweli unataka msamaha, Anta kuuomba umati wote humu ndani wakusamehe kisha umuombe kijana wa watu"

Kweli yule binti alijutia sana kitendo kile na alikijutia sana,

Hivyo alipoambiwa awaombe watu wote msamaha,.. Binti huyo alipiga magoti pale katikati ya njia ya siti, huku akiomba msamaha kwa kila aliekwazika na kitendo chake, huezi amini kula mtu aliukubali msamaha wake hata wamama walimuamsha na kumuambia inatosha ila haitakiwi kurudia tena kitendo cha kumuona binadamu mwenzio kama mavi vile, kisa wewe umefanikiwa kimaisha,

Binti yule alisamehewa na kila mtu aliekwazika na kitendo hicho na hata kijana chidi nae aliweza kumsamehe binti huyo ambae ni lika lake, sema kwakuwa binti wana maisha mazuri basi alijikweza na kumuona kijana chidi ni kichaa mchafu kuoga yaani hakuwa tofauti na jalala, kwa yule binti alivyomchukulia,…

Safari ilikuwa ikiendelea na abiria wengi walishuka njiani hivyo hata siti zilikuwa zipo wazi, hivyo chidi kuona siti ya nyuma ipo wazi aliona bora akatulie kule nyuma kabisa ambako hakukua na watu,..

Ndani ya gari kuna katoto kalikuwa kanalia kanataka kukojoa, hivyo gari ikasimama na mtoto huyo kutoka kwenda kujiseidia, na hata wengine pia walishuka,…

Ghafla kijana chidi anaskia sauti ya upole iliomuomba wakae wote

"samahani, naweza kukaa nawe"

Chidi alivyonyanyua macho na kumuangalia huyo aliesema anataka wakae wote,.. Alikua ni yule binti aliomwambia haogagi, chidi alitamani alipize lakini hakulelewa hivyo,.. Alimkubalia na binti yule akakaa huku akiwa kashikilia kamfuko keusi, na kalikuwa kananukia kuku wa kuchoma..

"samahani kaka, naomba upate chakula"

Kweli chidi alikuwa anakitamani lakini hakutaka kukichukua

"hapana asante dada angu"

"lakini nilikinunua kwa ajili yako, mie nishakula"

"hata mimi nimeshakula"

"mihogo mibichi"

"ndio, kwani mihogo sio chakula"

"ni chakula but ni kwa imejensi tu sio kila mara"

"ok, nimeshiba hio hio mihogo"

Dada hakutaka kumbembeleza sana, alikirudisha kile chakula kisha akarudi kuketi nae pale pale nyuma ya gari,.. Chidi alikua kajiinamia kwenye siti ya mbele huku tumbo likimkoroga kwa kula mihogo mibichi,.. Yule dada tatizo alivaa kanguo kafupi sana, afu mbaya zaidi ile sketi yake ya juu, ilikuwa ikionyesha haswa, na kusababisha chupi ya dada huyo kuonekana kutokana na uwepesi wa ile sketi alioivaa, Chidi alianza kujikunja kunja pale kwenye siti mara anyoishe miguu mara akunje miguu,… Yaan alikuwa hatuliii kijana huyo kutokana na muonekano wa huyu binti,… Yule binti aligundua swala hilo, na kujisemea tu moyoni mwake kuwa

"kweli vikuku vya kienyeji vina tabu, yaan kuona tu mapumba anateseka hivi, sasa je akiona mchele itakuaje"

Alijisemea huku akitabasam mwenyewe kisha akakimbia kuelekea mbele, aliporudi, alikuwa keshajifunga kanga, yaani kajifunga kanga kwa juu na ile hali ya kukaa nusu uchi ikapotea…

"hapo je"

Alimuuliza chidi huku akijiangalia jinsi alivyofunga hio kanga,

"hapo sawa"

"kwani mwanzo ulikuwa unanionaje"

Aliuliza dada huyo, bila kujua chidi ni mzee wa kuropoka pale anapoulizwa

"nilikuwa nakuona kama changudoa tu"

"Whaaaat?.. Yaani mimi nafanania na changudoa???"

Yule dada alianza kukasirika upyaaaa kama kachochewa kuni za moto… Heee spati picha itakuaje hapo, mana mwanadada kavimba haswa.

Chidi alikua akikwepa kumuangalia dada huyo, mana vazi alilovaa halikuwa la kistaarabu kabisa, yani hakuwa tofauti na wale wanaokesha usiku kucha, ile hali ilimsumbua sana kijana chidi, lakini hakuwa na la kumwambia, alibaki tu kuangalia chini ili kuukwepa mwili huo asiweze kuuona kwa umakini mana ukiangalia sana mwishowe waweza patwa na hisia zingine tofauti kabisa, Sasa yule dada aliona kabisa hii hali haipendezi kabisa…

"sasa hapo ndio umevaa nini"

Chidi alijikaza na kumuuliza mana anaona anateseka tu moyoni mwake,

"hii si sketi hiii au huzijui,… Ni toleo jipya kwa wasichana kama sisi"

"Ennghhh, toleo jipya eee?.. Na hii ya ndani nayo vp, mana niliskiaga kuwa chupi chupi hua zinakuaga za siri sana hasa hasa kwenu nyinyi wanawake,.. Sasa kwanini mimi na hao tuione, na wakati ni siri"

Maneno yale yalimchoma sana yule dada na kuona aibu huku akinyanyuka katika siti na kuelekea kwenye ile siti ya mwanzo alipokuwa kaketi,… Chidi alimsindikiza kwa macho tu huku akiona kinguo cha ndani kikimpagawisha,… Na dada huyo kweli alikuwa sio haba, kwenye sura humtoi, kwenye umbo ndo kabisaaa, ila tatizo wanajiharibu wenyewe..

Kila siku mwanamke unaomba uolewe, bila kujua wewe mwenyewe unajizibia milango ya kuolewa, nani aliwambia kuwa wanaume wanapenda kuoa wanawake wahuni, nani aliwambia kuwa wanaume wanaotaka kuoa wanataka waone vyupi vyenu au mapaja yenu, au thamsing flani.. Sasa kwa taarifa yako Mwanaume yeyote yule, hawezi oa mwanamke ambae yeye mwenyewe hajiheshim, kwanza jiheshim ndio uheshimiwe,… ustake kumkufuru mungu bure na wakati wewe ndio chanzo cha kutoolewa mapema…

Ghafla yule binti anatokea akiwa kafunga kanga, chidi alipomuona sasa hapo ndio kamuona kama mwanamke halisi….

"hapo je"

Alimuuliza chidi huku akijiangalia jinsi alivyofunga hio kanga,

"hapo sawa"

"kwani mwanzo ulikuwa unanionaje"

Aliuliza dada huyo, bila kujua chidi ni mzee wa kuropoka pale anapoulizwa

"nilikuwa nakuona kama changudoa tu"

"Whaaaat?.. Yaani mimi nafanania na changudoa???"

Yule dada alianza kukasirika upyaaaa kama kachochewa kuni za moto… Heee spati picha itakuaje hapo, mana mwanadada kavimba haswa..

Chidi aliona kuwa kamuuzi sana, lakini kwakuwa ni kweli alikuwa na muonekano huo hivyo hakukuwa na budi ya kukubaliana na hilo,

"What, What nini… Ina maana ulikuwa unaonekana mzuri pale, sema walishindwa tu kukwambia tu kuwa hujavaa vizuri

"mmmhhh ok, for now unanionaje"

Huyo dada aliuliza baada ya kuona maneno alioambiwa yalikuwa ni machungu mno,…

"hapo sasa nakuona kama mwanamke mzuri tena zaidi ya Princess fulani hivi…"

Wanawake wanapenda sana kusifiwa yaan huyo dada kuskia tu ana muonekano wa zaidi ya Princess flani hivi, alijikuta anataka kumu waoo, sasa akawaza huyu jamaa ni wa kijiji tu hivyo hawezi kukubali waoo yake, ikabidi avunge tu lakini alifurahi kupita kiasi

"kwahio mimi nina muonekano wa Princess"

"kwa kuvaa hio kanga vizuri, basi ni zaidi ya yeye"

Yule binti alionekana kupenda kauliza za kijana huyu na kuondoka pale alipo, yani alijikuta anatekwa na kijana chidi Taaratibuu, gari ilikuwa inakaribia kufika usa river,… Na usa ndio maeneo mdada huyo anashuka, dada huyo alibakiza kilometa chache tu kugika kwao,.. Ila chidi bado mpaka mjini kabisa,..

Ghafla dada huyo anakuja pale kwenye siti ya nyuma na kumpa kijana chidi ujumbe kwenye karatasi,… Sasa chidi anaifungua karatasi hio, kwanza anakutana na jina la dada huyo, na wakati huo kumebaki kama mita miatano hivi dada huyo ashuke

"naitwa saumu, nashukuru kwa ukarimu wako, na nilikuwa na vingi vya kuongea sema muda hautoshi,.. But yote 9.. Kumi ni kwamba naomba unisamehe kwa yale nilioyafanya mwanzo… Nimekiri kosa langu kwako,… Natamani niwasiliane nawe, lakini nimeona aibu kukuomba namba ya simu lakini naomba tuwasiliane kwa namba hii ni yakwangu, Please usinisahau"

Sasa chidi ile anataka aandike hata namba yake amjibu, ndio anamuona huyoo anashuka kwenye gari,.. Chidi alitaka ampe namba yake hata kama hana simu, mana anaenda mjini na hawezi kukosa hata simu ya kutumia, lakini chidi aliona sio mbaya kwasababu namba zake anazo hivyo hakukua na kitu kilichoharibika.. Mwanadada anampungia chidi mkono, hata chidi haamini kama katoto kamekuja chenyewe, Chidi nae anampungia mtoto wa watu huku anaburuza begi lake na kuita toyo, kisha huyoo anapelekwa sehemu husika,… Chidi alibaki na tabasam tu mdomoni huku akiiangalia sana ile karatasi yenye namba za saumu, na chidi nae hajabikiza umbali mrefu kutoka USA mpaka Arusha mjini, ambako ndipo alipotakiwa kushuka, . Namba zile aliziandika kwenye ki notibuku ili asizisahau au kuzipoteza,..

INAENDELEA...

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni