MUUZA CHIPS (9) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Ijumaa, 19 Mei 2023

MUUZA CHIPS (9)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
๐Ÿ“– KUSOMA SIMULIZI
๐ŸŽฌ FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
๐Ÿ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
๐Ÿ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa
Mwandishi: MoonBoy

SEHEMU YA TISA
ILIPOISHIA...
"naitwa rashidi"

"ooohh kumbe ni muislamu si kweli ee"

"ndio"

"ok, mie naitwa Sarah"

"mmmhhh nashukuru kukufahamu"

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Sasa cha ajabu ni kwamba dada huyo hakuwa tena anataka kuondoka, na haijulikani ni kwanini ameendelea kuganda na alikuwa tayari kwa kuondoka,

"dada samahani muda wa kukaa na mgonjwa umeisha"

Alikuwa ni dokta wa kike aliomwambia sarah kuwa muda wa kuwepo na wagonjwa umeisha,…

"ok sawa natoka, nipe dakika tano tu"

"sawa"

Ukiwa na pesa hakuna kinachoshindikana kwenye hii dunia,..

"samahani chidi, naweza kupata namba yako, ili nikupigie asubuhi nikuletee chai na nini"

"heeeeee…. Afu siiioni mfukoni ujue"

"huioni"

"ndio"

"au utakuwa umeisahau kwenye gari"

"labda huenda ikawa… Ngoja nikaichukue"

"ah ha wewe ni mgonjwa lala hapo mie nikuleteee"

Chidi alikubali kulala huku, sarah akipiga hatua za madoido kwwnda kuleta simu,.. Sarah anaonekana tayari keshampenda kijana chidi sema kwa maadili ya kiafrika ni ngumu mwanamke kumtaamkia mwanaume kuwa anampenda,..

Sasa ile sarah anafungua tu mlango wa gari, na simu ya chidi nayo ilikuwa ikiita, na mpigaji alikuwa ni mke wake,.. "MY WIFE" ndio jina lilioseviwa katika laini, Sarah alishika kifua chake kama vile anazuia presha kwa kuliona hilo jina,.. Sasa akawa anajiuliza, aipokee au aiache.. Lakini mwisho akaipokea na kutega skio ili kujua kweli ni mke wake au kaandika jina tu…

"haloo, mume wangu umefika salama??.. Mume wangu nijibu basi, umefika salama huko??"

Sarah alikuwa tayari keshampenda kijana mwenye mke, tena wawili hao wanapendana sana, ila sarah hakuwa akilijua hilo, kuwa anapoingia palishaingiliwa na wenyewe,.. Unaambiwa mapebzi ni kikohozi lazima ukohoe uifurahishe hisia zako, lakini kwakuwa maadili au tamaduni zetu za Kiafrika ni ngumu mwanamke kumwambia mwanaume kuwa anampenda, hua wanaonyesha vitendo kisha mwanaume humalizia kipande kilichobaki,… Hivyo kama wewe ni ziro basi utaendelea kuwa ziro tu…

Sarah mwanzo alipokuwa akimuuliza aonyeshwe supermarket hakuwa na hisia zozote za mtu huyo, na pia sarah alikuwa ni mtu mcheshi na muongeaji sana,.. Hivyo alijikuta akifurahiwa na rafudhi ya kitanga aliokuwa akiiongea kijana chidi,.. Mwisho wa siku mwanga unammulika kijana chidi na kusababisha Sarah kuona majeraha yalio katika mwili wake, hususan usoni mikononi na hata kichwani pia alikuwa na ngeu kubwa na ilikuwa ikitoka damu. … Sarah ni mtu aliependa sana kuseidia watu bila kujali uwepo wake, awe hamjui au anamjua lakini ilimradi tu amemseidia kwa namna moja hadi nyingine,… Unaambiwa ukipata pesa usizitumie peke yako..

UKIONA UMEPEWA,… JUA KUNA MWENZAKO KANYANG'ANYWA… HIVYO ALIPONYANG'ANYWA YULE NDIO UKAPEWA WEWE, ALAFU WEWE BADO WAZITUMIA VIBAYA HIVYO ULIVYOPEWA

Hivyo sarah alikuwa ni mschana mwenye hofu ya Mungu, licha ya kujiona wanazo.. Kijana chidi anaseidiwa na kuletwa hospitalini… Lakini sarah anaangukia kumpenda kijana chidi, lakini chidi hajui kama kuna kabahati kanako kuja mbele yake,…..

Sarah aliingia katika gari yake ili kuweza kuichukuwa simu ya kijana chidi, ila aliikuta simu hio inaita, alijishauri mara mbili mbili kuwa apokee au asipokee, "MY WIFE" ndio jina lililoseviwa katika simu ya chidi, lakini sarah hakutaka kuhisi kuwa huyu ni mke wake kweli au aliandika jina tu… Hivyo ili kupata uhakika wa juna lile alibofya kitufe cha kupokelea na kuitegea sikio pasina kutoa sauti yake… Na mke wa chidi nae hakukua kuwa aliopokea hakuwa mumewe, hivyo moja kwa moja alianza kuongea kama ifuatavyo..

"haloo, mume wangu umefika sama??.. Mume wangu nijibu basi umefika salama huko??"

Sarah aliikata simu huku sura yake kuanza kubadirika, Aliiangalia sana ile simu pasina kuipatia jibu, Alichokifanya ni kufuta mised call ambazo alizipiga mwanamke huyo ili chidi asijue kama alitafutwa na mke wake…

Katika swala la mapenzi naweza kusrma wanawake huwa hawana akili kabisa… Kwasababu wewe umempenda leo,… Lakini juwa kuwa kuna mwenzako kampenda jana,.. Lakini yule wa leo anamchukia yule wa jana,.. Wakati yule wa jana ndio alitakiwa amchukie huyu wa leo,.. Basi Sarah aliingia katika chumba alicholazwa kijana chidi na kumpatia simu yake,

"eti nikuulize kitu chidi"

Aliongea sana huku akiwa na shauku ya kuuliza swali alilokuwa akilitaka kuuliza,

"uliza tu usijali"

"Eti, kwani pale stendi ulikuwa unafanya nini"

Aliuliza hivyo na chidi nae hakutaka kumficha kitu chochote

"mimi ni mgeni sana kwenye jiji hili,… Nimetokea tanga, na pale nilikuwa namsubiri kaka yangu aje anichukue"

"ooohhh kumbe ndio hivyo tu"

"huku… Mjini kuna kaka yako na nani yako"

"ni kaka yangu tu basi"

"ok, I see"

"nini"

Sarah aliongea kakingereza kidogo kalikomuacha chidi njiapanda, mana chidi ndio wale wa darasa la saba waliofeli,… Na hakuweza kurudia shule kutokana na mazingira ya maisha yao,..

"nimemaanisha, hivi nimeelewa"

"aaahhh ah nyie wazungu bwana mmhh"

"sa mi mzungu"

"mmhhh sa hivyo ulivyoongea una tofauti gani na yeye"

"Ehe ehe ehe ehe ehe… We chidi we usinchekeshe mie… Sasa ngoja mi niende"

"sawa"

"ila asubuhi nakuletea chai sawa"

"sawa"

Mwanadada sarah hakumwambia kuwa mke wake alimtafuta,…. Kijana chidi hajui hili wala lile alimpigia kaka yake simu na kumwambia mahari alipo,.. Usiku huo huo kaka mtu hakulala, Anachukua toyo ili awahi kule alipoelekezwa,..

Wakati huo huku kwa sarah akiwa ndani ya gari, alikuwa akikumbuka ule muda walipogusana na kijana chidi, inaonekana ile hali imemvutia sana mwanadada sarah,.. Alikuwa akitabasamu tu ndani ya gari huku akikumbuka mambo mengi… Lakini ghafla ananuna baada ya kuikumbuka sauti ya mke wa chidi ikisema mume wangu

"mume wangu…. Mume wangu…. Mume wangu… Mume wangu"

Hilo neno la mume wangu lilikuwa likimuumiza kichwa sana, mana liliganda katika akili yake.. Lakini ghafla anapata wazo na kujisemea mwenye kwa sauti, lakini hakuna mtu alimsikia, mana alikuwa ndani ya gari na kulifungwa vioo

"lakini chidi ni mume wa mtu,… Sasa mimi nafasi yangu itapatikana kweli?… Lakini mimi ni mwanamke, kwanini nimkose,… Kama ni huyo mke wake kamuacha kijijini huko,… So huku haina haja ya kuogopa, I think hii ndio nafasi yangu,… Amjali mke wake lakini mimi simuacha, nitakula nae sahani moja,.. Nitamjali chidi kwa chochote kile atakacho… Kitoto hensam hiv afu nikiangalie, haiwezekani… You Must be Love Me chidi"

Aliongea kisha akawasha gari na kuondoka, ukumbuke kuwa alikuwa bado yupo nnje ya hospitali hio..

Sasa ile anaondoka tu, na Ibrahim nae anaingia,…. Ibrahim ni kaka yake na chidi.. kufika mapokezi aliambiwa kuwa muda wa kuwaona wagonjwa umeshaisha, hivyo haruhusiwi mtu yeyote kuingia ndani, na hata hivyo muda huu wagonjwa wamepumzika… Na mida hio ilikuwa inaendea saa tano usiku

"lakini ni mdogo wangu dokta, naomba hata dakika moja tu"

"hapana njoo umuone kesho"

"dokta, dokta… Nipe hata sekunde tano tu nimuone ndugu yangu"

"anaitwa nani ndugu yako"

"anaitwa rashidi kingazi"

"khaaaa.. Mbona dada yake alikuwa hapa"

"dada yake??"

"ndio… Na tena ndio alimleta hospitalini na hana muda mrefu katoka sasa hivi"

"mmmhhhhh kwenye familia yetu hatuna dada mkubwa kiasi hicho"

"sio mkubwa… Ni mdogo tu hawa wasichana wa mia 19 au 20 hivi"

"mmmhhh… Anaitwa nani uyo dada"

"alijitambulisha kuwa anaitwa sarah"

"hapana,.. Dada yangu mie anaitwa halima na ni bado mduchuuu ana miaka 6"

"ok…sawa, lakini jua kuwa muda wa kuwaona wagonjwa umekwisha"

"sawa dokta… Lakini si anaendelea vizuri"

"usitie shaka, ndugu yako yupo salama kabisa"

Kaka wa chidi alitoka kiunyongee na kuipanda toyo ili kurudi nyumbani, huku akijiuliza kuwa.. Chidi atakuwa kafanyeje usiku huu,….

Tukija huku upande wa Sarah tunaona anafunguliwa geti katika jumba moja la kifahari, yaani mjengo mjengo haswa yaani sijui panaishi raisi hapo ata sijui..

Saa tano sarah ndio anaingia nyumbani kwao,.. Alipaki gari vizuri na kukimbilia ndani mpaka chumbani, ambako chumbani humo kulikuwa na mtu kalala,.. Akamrukia yule mtu

"jamani sarah umenishtua eti"

"am so sorry my friend… But today am very happy more than happy"

Alikuwa ni ndugu yake wa kike, aliokuwa mzuri na mwenye umbo la kipekee, yaan sura ilikuwa murua,… Unajua kila mwanamke hupendezwa na rangi au shepu yake,… Kwa hawa wawili ukisema uchague mmoja, Kiukweli utapatwa na kigugumizi..

"Sarah, kwanza ulikuwa wapi saa hizi usiku huu"

"bwana miriam mi spendi.. Nisikilize kwanza basi"

Huyo ndugu yake alikuwa akiitwa miriam,

"ok.. Haya nakaa vizuri niskilize umbea huo"

Wawili hao walionekana kupendana sana

"Si nilikuwa naenda supermarket eee"

"haswaaa"

"kama unavyojua NAKUMAT SUPERMARKET imebadirika mno hivyo niliisahau mpaka nikaanza kuuliza watu"

"Enheeee"

Nimeuliza weeee… Nikakutana na mtoto huyo"

"mtoto mchanga, alitupwa nini? Mana sisi wasichana kwa kutupa watoto mmhh"

"bwanaaaaa miriiiii mi spendi"

"haya basi sema"

"ni mtoto wa kiume, hensam balaa…. Sasa nikamuuliza kama anajua hio supermarket ilipo… Kumbe na yeye ni mgeni hajui kitu,… Sasa kumuangalia vizuri usoni, kumbe alivamiwa sjui na vibaka, sjui kafanyeje maskini ya mungu… Sikumpita, nilimpeleka hospitali"

"weee nawe si ungeliacha life uko, utakuja kuseidia mijambazi wewe, shauri lako"

"miriam unaniuzi ujue"

"haya endelea… Ila mi sijapenda ivyo"

"Sasa shost kufika hospitalini…. Mtoto ana joto, heeeee we acha tu, yasn alinigusa kidogo tu, mwili ulinisisimka wote… Yaani kila nikimfikiria, natamani kumtongoza eti"

"mschiuuuuuuu (msunyo).. Yaan sarah we akili huna kabisa yan kukutana tu leo leo na kumseidia eti umempenda"

"ndio… Tena asubuhi nampelekea chai"

"hhhmmm utajiju na lijambazi lako"

Miriam alijifunika brangeti na kumpuuza rafiki yake,…

ASUBUHI NA MAPEMA KAKA WA CHIDI YUPO NDANI HOSPITALI

ilikuwa ni mida ya saa moja na nusu asubuhi.. Ibrahim ndio anaingia hospitali na kumkuta mdogo wake akiwa kafungwa mabendeji usoni, mikononi

"rashidi ndugu yangu umefanya nini tena"

"shkamoo kaka"

"marahaba ujambo"

"aahhh sijambo"

"umefanya nini chidi… Ndugu yangu hela zenyewe ndio hizi tena umezua lingine, sasa nitakutoa na nini hapa…. Eti dokta ni kiasi gani matibabu mpaka atoke"

"usijali… Mdogo wako keshalipiwa kila kitu"

"kalipiwa na nani… Na mimi ndio ananitegemea hapa mjini"

"dada yake ndio kamlipia"

"dada yake yupi huyo jamani… We chidi eti nani kakuseidia…. "

Wakati huo huo sarah nae ndio anaingia huku akiwa kashika mfuko mkubwa ulio onekana kujaa chakula..

INAENDELEA...

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni