MTU WA UFUKWENI (19)

0
Mwandishi: Andrew Mhina

SEHEMU YA KUMI NA TISA
ILIPOISHIA...
Baada tu ya kuondoka Dr. Jackson alipiga simu nyumbani kwa msichana wake wa kazi aitwaye Magreth: “Halo mage mama ameshatoka au bado yupo?” Aliuliza ili kuhakikisha. “Ametoka na gari Muda si mrefu.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Kwani hukumpata kwenye simu yake?” Aliuliza Mage. “Simpati sijui kuna tatizo gani kwenye simu yake alijibu Dr.Jackson kisha akakata simu na kuingia kwenye gari tayari kwa safari ya nyumbani. Aliporudi nyumbani aliingia kwa haraka chumbani na kumchukuwa mtoto Lameck na kuingia naye kwenye gari hatimaye kuliondoa kwa mwendo wa kasi sana. Hali hiyo ilimchanganya sana Mage kwa sababu ndio alikuwa anamwandalia mtoto uji wake.

Alikosa la kusema kwa sababu hakupata hata nafasi ya kuuliza, kutokana ana haraka aliyokuwa nayo bosi wake. Njiani watu walishangaa mwendo huo wa gari ilikuwa kama gari ya mashindano. Kwa mwendo huo aliwahi kufika maana kwa mbali aliona gari ya Mary ikiingia kwenye kibarabara kidogo ufukweni hapo.

Baada ya Mary kupaki gari yake alitoka kwa haraka na kuelekea ilipo nyumba ya Ramson na wakati huo huo Dr. Jackson aliipeleka gari yake na kuipaki kando ya gari la mkewe. Taratibu alitoka ndani ya gari na kunyata huku akiwa amejawa na hasira kubwa sana. Alimwona mkewe akikumbatiana na Ramson baada ya Ramson kutoka kwenye nyumba yake. Ni ajabu kuwa hawakumwona kwa haraka Dr. Jackson akija labda ilikuwa ni kwa sababu ya shauku yao ya kuonana.

Mfuko wa hela ulikuwa kwenye kiti wakati wao walipokuwa wakisalimiana. Kabla hawajamaliza kusalimiana walisikia sauti: “Hapo hapo mlipo msifanye jambo lolote wala kukimbia! Nataka maelezo ya kutosha kila mmoja ajieleze kwa zamu juu ya ubaya huu mnaonitendea.”Alisema Dr. Jackson kwa sauti nzito isiyo na mzaha hata kidogo. Mary na Ramson walipatwa na mshituko usio wa kawaida! Baada ya kugeuka walikutana na mtutu wa bastola! Mary alitamani ardhi ipasuke na kuingia! Alifedheheka sana kubambwa na mumewe katika hali ile akiwa na Ramson. Pamoja na kuiona bastola bado Ramson hakuvumilia aliamua kukimbia. “Simama hapo hapo kabla sijakumaliza!” Alisema Dr.Jackson kwa sauti kali lakini Ramson aliendelea kukimbia. Dr. Jackson alikasirika zaidi na kufyatua risasi iliyompata Ramson mguuni na kuanguka chini na kuachia kelele za maumivu.

Baada ya kuanguka Dr. Jackson alimfuata kwa mwendo wa haraka akiwa na hasira kali, huku akiwa amemlenga na mtutu wa bastola yake. Ufukwe huo ulikuwa umetulia sana ila kelele za Ramson tu za maumivu. Wafanyakazi wote wa Ramson walitawanyika kwenda kufungasha mahitaji muhimu kwa ajili ya wateja. Kwa hiyo ufukweni hapo alikuwepo Ramson peke yake na wageni wake hao. Unafikiri unaweza kuniharibia familia yangu kisha unikimbie? Umefanya kosa kubwa sana.

Heri ungesimama tu tukayaongea kuliko kunikimbia.”Alisema Dr. Jackson kwa hasira huku akimsogelea Ramson kwa hatua imara. Kuona vile Mary aliamua kuingilia kati na kwenda kumzuia mumewe. “Tafadhali usimuue Ramson hana kosa mimi ndio mwenye makosa yote mwache tafadhali.” Mary aliyasema hayo huku akimnyang’anya Dr. Jackson bastola yake.

Wakati wakinyang’anyana kwa bahati mbaya risasi ikatoka kwenye bastola na kumpiga Mary kifuani, mara hiyo akaanguka chini! Jackson alihamaki sana na kuiweka bastola yak echini na kumwinania mkewe huku akipiga kelele.“Mary mke wangu usife! Mke wangu Mary Usife!! Nisamehe kwa hili lililotokea ni hasira tu. Na mimi nimekusamehe kwa yote uliyonitendea.

Lakini Mary alikuwa tayari amekata roho. Uchungu wake uliongezeka na kutokwa na machozi mengi, huku moyo ukimwuma sana. Hakutaka kufanya hivyo tangu mwanzo; ni jambo lililotokea kwa bahati mbaya tu. Mary alikuwa kila kitu katika maisha yake. Kosa lile alikuwa tayari kumsamehe mkewe na kuendelea kuishi naye. Alizingatia sana maneno ya rafiki yake Mudy alipomwambia:

“Moyo uliniuma pindi nilipokumbuka jinsi mama alivyokuwa akimsema vibaya mkeo kuwa ni mgumba. Hali hii ikanipa kuona kuwa labda shemeji alifikia mahali akapimwa na kuonekana kuwa hakuwa na matatizo hivyo akaamua kuzaa nje ya ndoa na kuificha siri hiyo japo kwa fedha ili kuficha aibu yake na yako katika ndoa yenu. Ndio maana akagharimika kufanya ujanja ili atoe fedha zote hizo!”

Maneno hayo yalijirudia rudia katika akili zake huku akilia machozi mengi. Baadaye alikumbuka tena maneno ya mwisho aliyoambiwa na Dr. Mudy wakati wakiagana kuwa:

“Ninakuamini sana kuwa wewe ni mtu jasiri unayeweza kuvumilia mambo magumu sana katika maisha. Sitaamini macho yangu kama utaonyesha kubadilika katika tabia yako ya mwanzoni. Jikaze na uendelee kuwa jasiri na mvumilivu ili mambo haya yamalizike kwa usalama. Naamini baada ya hapo amani itakuwa kubwa katika maisha yenu.”

Maneno haya yalikuja kwa nguvu ya aina yake huku yakimsuta sana, kwa sababu tayari ameshafanya mambo ya ajabu kinyume na ushauri huo. Maisha yake aliyaona bure kabisa bila Mary mke wake. Mara hiyo hiyo akaamka na kuchukuwa bastola yake na kumsogelea Ramson aliyekuwa amejisogeza sana akitaka kutoroka. Alipomwona Dr. Jackson anakuja alipiga kelele za kuomba msamaha: “Nisamehe kaka, usiniue tafadhali! Ni ushawishi tu na ibilisi, nisamehe mkubwa wangu!”Sauti yake ilikuwa ya kutetemeka na macho alikuwa ameyatoa kwa woga akiogopa kifo!

“Ukweli unastahili kufa tena kifo kigumu zaidi ya mtu yeyote, kumbuka makosa yako yote! Umenichukulia mke wangu na kuzaa naye, na ni wewe umesababisha kifo chake. Lakini Mimi sitakuua kama ulivyofikiri, Moyo wangu unauma sana kwa hukumu jinsi nilivyomwua mke wangu japo sikudhamiria!”Alitulia kidogo akiwa anatafakari jambo! Kisha kama aliyeshtuka akamwambia kwa sauti: “Nipe kalamu na karatasi upesi kabla sijageuza mawazo yangu!” Alifoka kwa hasira kali. “Viko pale mezani kwenye kibanda changu kaka!” Alisema Ramson huku akiendelea kutetemeka kwa hofu.

“Subiri hapo usiondoke ukiondoka nitakuadhibu.” Alisema hivyo Dr.Jackson wakati akikimbilia kibandani. alikaa baada ya kukuta karatasi na kalamu, kisha akaandika mambo mengi sana kwenye karatasi kama mbili hivi. Baada ya hapo alinyanyuka na kwenda aliko Ramson na kumpa zikiwa zimekunjwa.

“Chukuwa karatasi hizi na ufuate maelekezo yote yaliyopo humo!” Alisema Dr Jackson huku akiwa katika hali mbaya sana iliyotawaliwa na huzuni na hasira. Ramson alizipokea kwa mashaka huku akiwa anaendelea kusihi asamehewe. Hakujua maana ya karatasi hizo.“Ramson Mtoto wako uliyezaa na mke wangu yuko ndani ya gari yangu pale. Nimegundua mambo yote yaliyofanyika na ushahidi wote upo ndani ya dashboad kwenye gari. Sina tena thamani ya kuishi katika dunia hii bila mke wangu Mary!” Dr. Jackson aliyasema hayo huku akimwacha Ramson na kumsogelea mkewe.

Alipofika ilipo maiti ya Mary alipiga magoti na kuishika huku akiongea maneno ambayo Ramson hakuyasikia kwa sababu ya umbali. Ghafla Ramson alimwona Dr. Jackson akinyanyua bastola kujielekezea kichwani! Alipiga kelele “Usifanye hivyo Brother!” Alijikongoja kujaribu kwenda kumzuia asijiue, lakini maumivu ya mguu yalikuwa makali sana kiasi cha kushindwa kusogeza hatua hata tatu mbele.

Kelele zake za kutaka kumzuia asijiue hazikufua dafu, mlio wa bastola ulisikiika na mara hiyo Dr. Jackson alianguka kando ya mkewe na kufa hapohapo. Mshituko alioupata Ramson ulikuwa ni mkubwa sana, hivyo alipiga kelele za mfululizo kama kichaa! Ilikuwa wazimu hasa maana mambo yenyewe yalikuwa hayachukuliki katika akili za kawaida!

Ilikuwa ni kesi ambayo ilikosa mahali pa kusimamia. Kesi Isiyo na ushahidi wowote wala mwelekeo hasa. Baadaye uchunguzi ulifanywa na Polisi haukuona kuwa Ramson alihusika kwa lolote. Ilionekana kwamba muuaji ni Dr. Jackson ambaye alimpiga risasi mkewe na kutaka kumuua Ramson badala yake risasi ikampiga ya mguuni. Baadaye alijipiga risasi ya kichwa mwenyewe. Uchunguzi wa alama za vidole kwenye bastola ile uliona kuwa mtumiaji wa silaha hiyo alikuwa ni Jackson mwenyewe.

Wakati upelelezi wa haya yote unafanyika, Ramson alikuwa Hospitali akitibiwa akiwa chini ya ulinzi. Mpaka anapata nafuu kubwa kwenye jeraha lake la mguu, upelelezi ulimwondoa kwenye shutuma na baadaye walimwachia huru. Ramson alitoka Hospital asijue la kufanya. Ila alikumbuka kuwa karatasi zile alizificha sana baada ya kukabidhiwa na marehemu Dr Jackson.

Alipoingia kwenye gari la Jackson aligundua picha na vyeti. Picha zile zilimwonyesha yeye akiwa na mke wa Dr. Jackson wakiogelea na nyingine zilizokuwa na ushahidi pia vitu vte hivyo alivificha pamoja na zile hela. Alifanya hivyo kusudi kuondoa ushahidi wa yeye kuhusishwa na vifo vya Dr. Jackson na mkewe.

Hii pekee ndiyo iliyomweka mbali na kesi ya mauaji hayo. Baada ya yote hayo Wafanya kazi wake walipokuja aliwaaagiza wampeleke mtoto kwa mmoja wa rafiki zake. Simu aliyompigia rafiki yake huyo ilimfanya akubali kumtunza mtoto huyo, hadi hapo mambo yatakapotulia. Katika maficho alikozificha karatasi zile na fedha alizokabidhiwa na Marehemu Mary palikuwa salama. Baada ya kurudi akiwa huru alikuta vitu vikiwa vile vile kama alivyoweka.

Alikaa na kuamua kusoma makaratasi yale aliyopewa na Dr. Jackson, maana tangu apewe hajawahi kuyapitia na hakujua kuwa yalihusu nini! Mwili ulimsisimka sana baada yakusoma kichwa cha habari! Maneno yaliyofuata yalimfanya apanue mdomo kwa mshangao! Kila hatua aliyoipiga katika kusoma maneno yaliyopo pale, vilimfanya aduwae! Ilikuwa ni zaidi ya habari! Ilimshangaza na kumshtusha kwani ndani ya karatasi zile Dr.Jackson alirudia kusema kuwa, hakuwa na budi kufa kwa sababu hataweza kustahimili kuishi bila Mary mkewe!

Na pia asingevumilia kupata hukumu ya mauaji ya mkewe ambayo mwenyewe hakukusudia kufanya hivyo. Lakini jambo la msingi ni kwamba hakuwa na ndugu hata mmoja, ila wazazi wake tu ambao wako kijijini nao ni wazee sana. Kwa hiyo ameamua kumrithisha Ramson mali zake zote, ambazo ni pamoja na mahotel mawili ya kitalii yaliyopo Lushoto mjini.

Makampuni ya usafirishaji iliyopo jijini Dar es Salaam. Mashamba mawili yenye heka kumi kila moja, moja likiwa Lushoto na jingine likiwa Korogwe Pia kulikuwa na nyumba tatu; Moja ikiwa hapo mjini Tanga na nyingine ikiwa Arusha na nyingine ilikuwa Ostabay Dar es Salaam.

Fedha zilizoko Bank zilikuwa ni Shilingi milioni mia sita na hamsini. Mwisho wa yote akamwambia atafute wakili kwa sababu yeye pamoja na mali zote hizo hakuwahi kuweka wakili binafsi. Wakili atakayemweka amsimamie katika kubadilisha hati za umiliki wa mali zake, kutoka jina la Dr. Jackson Kigoi kwenda jina lake yaani Ramson. Hakujua aanzie wapi baada ya kuona mambo hayo.

USIKOSE SEHEMU IYOFUATA

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)