KIJIJINI KWA BIBI (3)

0
Mwandishi: Alex Kileo

SEHEMU YA TATU
TULIPOISHIA...
Tausi akasema, Kayoza akakimbilia suruali

ya stellah akaikota kisha akaisachi,

"mh..hamna kitu'' Kayoza akajisemea peke yake, kisha akasogea

mlangoni

"kasema hana" Kayoza aliongea kwa sauti ya juu kidogo,

KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO

SASA TUENDELEE...
"khaa jamani hela

zote zile za kwenye pochi kazimaliza jana!?, Tausi aliuliza kwa

mshangao.

Kayoza ndio akagutuka na kupepesa macho mule chumbani, ghafla

akainama chini ya meza ilipokuwa pochi ya Stellah, akaichukua pochi

akatoa noti ya shilingi elfu kumi, akaenda hadi mlangoni,

akaufungua mlango kidogo,

"mambo" Kayoza

akamsalimia Tausi,

"safi, vipi stellah

bado kalala?" Tausi aliuliza baada ya kujibu

salamu huku nafsi yake ikiwa na amani,

"yuko macho ila anaona

uvivu kuinuka kitandani" Kayoza alijibu huku akitabasamu.

"Na wewe uko poa?" Tausi alimuuliza Kayoza,

"Niko Poa, unaweza kuniambia nini kiliendelea baada ya mimi kunywa

pombe jana?" Kayoza alimuuliza Tausi,

"Jana ndio nimejua kuna watu wana vichwa vibovu" Tausi aliongea

huku akicheka,

"Unamaanisha nini?" Kayoza aliuliza,

"Yaani wewe ulikunywa bia moja tú na ukazima kabisa. Yaani kabia

kamoja tu?" Tausi aliongea huku akiendelea kumcheka Kayoza,

"Baada ya hapo?" Kayoza aliuliza,

"Sisi tuliondoka na kuwaachia chumba. Sasa labda wewe ndio uniambie

baada ya hapo mlifanya nini?" Tausi aliuliza ila kiutani,

"Na wakina Omary walielekea wapi?" Kayoza aliuliza,

"Jana tulichukua chumba kingine baada ya wewe kuzidiwa" Tausi

alijibu,

"Kwa hiyo wewe ulilala na wakina Denis?" Kayoza aliuliza,

"Ndio, ila hatukufanya kitu" Tausi alijibu huku akijisikia aibu,

"Poa, Acha mimi nirudi kulala kidogo" Kayoza aliongea,

"Inaelekea mlikuwa na shughuli nzito jana usiku" Tausi aliongea

huku akicheka,

"Ebu fuata kilichokuleta, kama huna cha kuongea ni bora uondoke"

Kayoza aliongea huku akifunga mlango na kumuacha Tausi akiendelea

kucheka.

"Hutaki kusifiwa?" Tausi aliuliza huku akiwa amefungiwa mlango kwa

nje,

"Kwanini usijisifie wewe uliyelala na wanaume wawili?" Kayoza

aliuliza huku akiwa ndani,

"Acha maneno yako ya kipuuzi" Tausi aliongea kwa hasira,

"Kwani yako ndio ya maana?" Kayoza nae aliuliza,

"Ebu muamshe Stellah nimsalimie shoga yangu" Tausi aliamua kubadili

mada,

"Nimekwambia amelala, Kwanini huelewagi wewe?" Kayoza aliuliza kwa

hasira huku akiwa ndani,

"Nilijua amelala na ndio maana nikakwambia muamshe, au mtu

anayeamshwa ni wa aina gani?" Tausi alihoji huku akiwa nje,

"Ebu nenda bwana, mtaongea baadae akiamka" Kayoza aliongea,

"Ujue mimi ni shoga yake?, ebu muamshe nimuulize kitu" Tausi

alikazania utasema alikuwa anajua kuwa Stellah hayupo tena duniani,

"Mimi boyfriend wake, nimesema muache apumzike" Kayoza aliongea kwa

mamlaka,

"Umesema wewe nani wake?" Tausi aliuliza,

"Boyfriend wake" Kayoza alijibu,

"Leo ndio umekubali kujiita boyfriend wake, si ulikuwa unajifanya

humtaki?" Tausi aliuliza huku anacheka,

"Hayakuhusu" Kayoza alijibu na kufanya kuwa kama wanasutana,

"Kwa hiyo ndio umegoma kumuamsha?" Tausi aliuliza huku akimcheka

Kayoza,

"Nenda dukani, ukirudi utakuta nimemuamsha" Kayoza alijibu ili tu

Tausi aondoke.

Baada ya tausi kuridhika na majibu ya Kayoza aliondoka na kuelekea

dukani.

Kayoza akaona hiyo ni nafasi nzuri ya kuuficha mwili wa

Stellah,Akauchukua mwili wa

stellah na kuuingiza chini ya kitanda, na kisha akaenda bafuni na

kukuta kuna taulo zimetundikwa ukutani, akaichukua moja kwa ajili

ya kwenda kufutia damu iliyomwagikia sakafuni.

Akaichukua na kurudi nayo chumbani, sasa wakati anaangaika

kufuta damu sakafuni mara mlango

ukafunguliwa ghafla, alikua ni Tausi, alipoziona zile damu sakafuni

alionekana kushtuka sana,

"vipi kuna usalama kweli?" Tausi aliuliza,

"upo shem" Kayoza alijibu huku akizuia hasira zake kutokana na

Tausi kuingia bila hodi,

"Hizo damu za nini sasa?" Tausi aliuliza,

"Stellah alijigonga kidogo ukutani ndio damu zikawa zinamtoka

puani"

Kayoza akatumia uongo kujibu,

"stellah mwenyewe kaenda wapi?" Tausi akauliza tena,

"kaenda kuoga" Kayoza akadanganya tena.

"Acha na mimi nikaoge" Tausi aliongea huku akinyanyuka ili aondoke,

wakati ananyanyuka akadondosha dawa ya

meno, ikabidi ainame ili aiokote, ile kuinama tu, kwa ajili ya

uchovu pia

na hangover alizoamka nazo akajikuta anapiga mweleka mtakatifu

puh, hadi chini, sasa akawa anajigeuza geuza pale chini, mara

macho yake yakagota chini ya uvungu wa kitanda,

"khaa naota au?" Tausi akajikuta amelopoka.

Ni kitendo bila

kuchelewa, Kayoza akaruka hadi

shingoni kwa tausi, ila hapa hakumnyonya damu ila alimkaba

shingoni kisawa sawa mpaka binti wa

watu akatoa shuzi zito alafu akatulia

kimya, hakutaka kumuua ila alitaka kumzuia tú asipige kelele na

matokeo yake yakawa ni kuua bila kukusudia. Kayoza akazidi

kuchanganyikiwa, Akauchukua mwili wa

Tausi nao akauingiza chini ya kitanda, Kayoza akawa kama chizi kwa

maana alikuwa anazunguka tú ndani bila kujua anachofanya.

Baada kama ya dakika ilisikika hodi nyingine,

"Nani?" Kayoza aliuliza huku jasho la uoga likimtoka,

"Mimi muhudumu" Sauti ya kike ilijibu kutoka nje,

"Unasemaje?" Kayoza aliuliza,

"Nauliza kama mnajitaji kufanyiwa usafi chumbani kwenu" Mhudumu

aliongea huku akiwa nje,

"Hapana hatuhitaji" Kayoza alijibu,

"Pia kama mtahitaji supu au chai vinapatikana pia" Mhudumu alizidi

kuongea,

"Tukihitaji tutakuja wenyewe kuagiza" Kayoza alijibu huku akikereka

kutokana na maswali ya huyo muhudumu,

"Alafu pia kama chupa za soda au bia chumbani kwenu, naziomba"

Mhudumu aliongea pale nje ya mlango,

"Acha ujinga msichana, ujue huo ni usumbufu unatufanyia katika

starehe zetu, au ndio mmefundishwa hivyo na bosi wenu ili nikitoka

nikamuulize?" Kayoza aliongea kwa hasira baada ya kuchoshwa na

maswali ya Mhudumu,

"Basi samahani kaka yangu, usiende kumwambia bosi wangu" Mhudumu

aliongea huku akiondoka haraka haraka mlangoni mwa chumba

alichokuwamo Kayoza.

Mhudumu wakati anaondoka, koridoni akapishana na Denis na Omary

ambao nao walikuwa wanaelekea katika chumba alichokuwepo Kayoza,

walifika mlangoni na kuingia bila hata kupiga hodi.

"bishoo vipi unambonji paka saa tano,

au binti kakupa vitu hadimu?" Omary

aliingia kwa staili hyo, ila kayoza hakujibu, alionekana ana mawazo

sana,

"vipi kaka mbona hivyo? Sie tuliechangia demu tuko poa hatuna

mawazo, we uliejilia mzigo wa peke

yako umeshika tama" Denis akaongeza neno tena, pia kayoza

hakujibu na wenzie wakawa wanaishangaa hiyo hali na mwisho wote

wakakaa kimya. Mwishowe baada ya

ukimya mrefu,

"tunaweza kwenda au kuna kitu mnangoja?" Kayoza aliuliza,

"warembo wako wapi?" Denis nae akauliza,

"nimeua" Kayoza akajibu kwa kifupi,

"tunajua umeua Stellah, Tausi tumeua sisi"

Denis akasema uku neno kuua akijua kayoza kamaanisha ni kitendo cha

kufanya mapenzi,

"au wameenda kupata supu moto?" Omary akatupia swali tena,

"wako chini ya kitanda" kayoza akajibu huku dhahiri uso wake

ulionesha amechanganyikiwa.

Kwa kuwa Omary alikaa kwenye kochi, yeye

ndio akawa wa kwanza kutupia macho chini ya kitanda, aliona Stellah

na Tausi wakiwa chini ya kitanda, ila hakuamini alichokiona,

ilibidi asogee mpaka ilipo miili ya wakina Stellah na kuhakikisha

mwenyewe kwa macho yake kuwa wale wanawake wawili tayari ni

marehemu.

"Mungu wangu, umeua kweli" Omary aliuliza huku akiwa anasimama,

Kayoza kuona hivyo nae allisimama na kwenda alipokuwa Omary na

kumkaba shingo….

Denis akanyanyuka haraka mithili

ya gari inayowaisha mgonjwa

mahututi hospitalini, lakini kayoza

alikua na kasi mara mbili, akawai

mlangoni.."please Denis na Ommy, nawaomba

mtulie rafiki zangu, nahitaji msahada

wenu" kayoza aliongea kwa upole,

Denis ikabidi arudi na kufunua godoro na

kuziangalia zile maiti, huku akionekana ni mtu mwenye maswali

mengi kichwani, baada ya muda

kidogo akagutuka,

"imekuaje kaka?" Denis

akauliza huku akiwa bado anaziangalia zile maiti,

"Kwanza kubalini kuwa upande wangu, alafu nitawaambia ukweli" Kayoza aliongea huku akiwatazama wenzake kwa zamu,

"Tuambie kwanza nini tatizo?" Omary aliongea huku akijishika shingo kutokana na kabali alipigwa na Kayoza muda mchache uliopita,

"Mimi niko upande wako, na nitakuwa upande wako" Denis aliongea huku akimuangalia Kayoza aliyeonekana kuchanganyikiwa,

"Hata mimi niko upande wako, haya tuambie ilikuwaje?" Omary aliuliza,

"jamani nitawaambia tu,

cha muhimu tuondoke eneo hili haraka iwezekanavyo" Kayoza

akaongea kwa kuwasisitizia wenzake,

"Ok, fasta basi" Omari

akawaharakisha wenzake huku akionekana mwenye wasiwasi.

Wakavaa haraka, na wakawa wanaelekea nje. Wakanyoosha moja kwa moja mpaka mapokezi,

"Mbona Mpo peke yenu, wenzenu wako wapi?" Dada wa mapokezi aliwatania,

"Bado wanajipodoa, si unajua tena mambo ya wanawake?" Omary alijibu huku akicheka,

"Haya, nawasikiliza" Dada wa mapokezi aliongea,

"Tumekuja kulipia chumba" Omary aliongea huku akimkabidhi pesa Mhudumu,

"Sasa mbona ya chumba kimoja?" Dada wa mapokezi aliuliza baada ya kuzihesabu zile pesa,

"Hicho kingine watalipia wadada" Denis alijibu,

"Na wakikataa?" Dada wa mapokezi aliuliza ila kwa utani,

"Wakikataa itabidi muwazuie na wawasaidie kufua mashuka" Omary nae alitania huku wakianza kuondoka na kumuacha yule dada wa mapokezi akicheka.

Njiani kila mmoja

alikua anafikiria lake,

"Tunaenda wapi sasa?" Kayoza aliuliza huku akiwa hana muelekeo,

"Itabidi turudi kwanza chuo" Denis alitoa jibu lililomfanya Kayoza asimame ghafla,

"Hamuoni hatari iliyopo mbele yetu? Sasa tukirudi chuo si naweza kukamatwa?" Kayoza aliuliza huku akiwa bado amesimama,

"Acha ujinga wewe, hakuna hata mmoja atayetuhisi sisi tunahusika na vifo vile" Denis alimwambia Kayoza,

"Kwa hiyo?" Kayoza aliuliza,

"Kwa hiyo turudi chuo, alafu tuangalie upepo unaendaje na tukiona mambo yanaweza kuharibika basi ndio tutaangalia namna ya kupambana" Denis alimueleza Kayoza,

"Alafu hili suala ni letu sote, sio lako peke yako" Omary nae akaongezea maneno yalimpa nguvu kidogo Kayoza na kukubali kurudi kwanza chuo.

Walienda mpaka jamatini ambapo ndipo zilikuwa coaster za kuwapeleka chuo, wakatafuta usafiri ambao ulikuwa upo tayari kuondoka na wakaingia, baada ya muda mchache gari iliondoka.

Walipofika eneo la chuo wakaingia kwenye chumba chao, Denis na Omari wakaingia kuoga,

Kayoza akajitupa kitandani ila sio kwamba alitaka kulala, hapana, mawazo ndio yaliutawala ubongo wake muda wote.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)