SHETANI ALINIITA KUZIMU (6)

0

SEHEMU YA SITA
TULIPOISHIA...
Nikiwa katika ungo wangu niuendesha kwa kasi ili kukwepa kufika nyumbani kukiwa kumepambazuka. Kukufafanulia hapo ni kwamba, hakuna kitu ambacho wachawi wanakuwa makini kama kuchelewa kurejea nyumbani wanapotoka kwenye mikutano yao au kuwawangia watu.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA CnZ Media APP INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO

SASA TUENDELEE...
Siku iliyofuata asubuhi na mapema nilichukua jembe na kuelekea shambani, jambo la kushangaza nilipofika nilikuta shamba lote likiwa limelimwa.

Kwa kuwa nilikwenda shambani kwa nia ya kulima, sikuwa na kazi ya kufanya nikaamua kurudi nyumbani huku nikijiuliza ni mtu gani alifanya kazi hiyo. Baada ya

kufika nyumbani nilimkuta yule dogo ambaye alikuwa kiongozi wetu akinisubiri, tuliposalimiana alinipa hongera kukuta shamba langu limelimwa. Alipotoa kauli

hiyo nilimwambia kwamba jambo hilo lilinishangaza ndipo alisema kazi hiyo aliifanya yeye, nikamuuliza aliwezaji kulima shamba lote peke yake?

Dogo alitabasamu na kunifahamisha kwamba alikuwa na watu wake aliokuwa akiwatumia kufanya kazi mbalimbali. Kutokana na furaha niliyokuwa nayo kukuta shamba

langu limelimwa lote kwa siku moja, nilimuuliza aliwalipa kiasi gani cha fedha, akacheka. Dogo huyo aliniambia kwamba watu wake hawakuwa na gharama zaidi ya

kuwapa chakula tu, nikamsisitiza anipeleke nikafahamiane nao. Kufuatia ombi langu hilo, yule dogo aliniambia atanipeleka usiku kisha akaniaga na kuondoka.

Siku hiyo nilishinda nyumbani nikifanya kazi ndogogo hadi usiku ndipo yule dogo kiongozi wetu alifika na kuniambia muda wa kwenda kuwaona watu wake uliwadia.

Tuliondoka hadi sehemu iliyokuwa na kichaka na pagale akaniambia nisubiri awaite, nikiwa nashangaa alianza kuwaita kwa kusema; “Nyie misukule yangu amkeni na

kuja hapa sasa hivi kuna mtu anataka kuwasalimia.” Hazikupita dakika mbili niliona kichaka kikitikisika kisha walitokea watu wa kutisha waliokuwa na nywele

ndefu, kucha ndefu, walikuwa weusi tii kama walijipaka mkaa na walikuwa wananuka sana.

??Kwa kuwa ilikuwa mara yangu ya kwanza kuwaona watu wa namna hiyo nilistaajabu na kumuuliza dogo kama ndiyo walikuwa watu wake! Dogo alicheka na

kunifahamisha kwamba ndiyo watu waliokuwa wakimsaidia kufanya kazi za kilimo na nyingine kisha akaniambia kama niliwahitaji nimwambie aniuzie wangapi.

Kabla sijamjibu, alinieleza kuwa kama sitapenda aniuzie anaweza kunisaidia kunitafutia misukule nitakaokuwa nawamiliki mwenyewe. “Haya chagua unatakaje kati ya hayo mawili, nikuuzie au nikusaidie kuwapata wako?”

dogo aliniuuliza. Kwa kuwa niliwahitaji sana watu wa kunisaidia kufanya kazi zangu nilimwambia aniuzie wanne, akasema sawa. Nilipowaangalia kwa karibu

misukule hao niliweza kuwatambua wawili, mmoja alikuwa kijana aliyekufa miaka saba iliyopita na mwingine alikufa ghafla baada ya kuumwa kichwa. Nilimuuliza

yule dogo kwa misukule wanne niliowahitaji nimlipe shilingi ngapi, akasema hakuhitaji fedha ila nitakapovuna mahindi nimpatie magunia mawili, nikamwambia sawa.

Baada ya kukubaliana, aliniambia niwachague misukule niliowahitaji, nikawachagua ambao niliwaona walikuwa na nguvu. Nikiwa nimesimama na watu hao waliouawa

kichawi, dogo aliniambia niwe nawapa chakula chochote lakini unga na pumba ndicho chakula walichokuwa wakikipenda sana. Aliponipa maelezo hayo, nikaondoka

nao na kwenda kuwaficha kwenye kichaka kilichokuwa karibu na shamba langu.

Sehemu nilipowahifadhi nilipaamini sana kwani watu walikuwa hawafiki na hata kama wangefika kwa macho yao ya kawaida wasingeweza kuwaona. Kukufafanua hapo ni

kwamba mtu akiwekwa msukule siyo rahisi mtu ambaye siyo mchawi au hajachanjiwa dawa kumuona hata kama atakuwa karibu kiasi gani. Kwa upande wa misukule, wao

huwaona watu lakini hushindwa kuwaita kwa sababu hukatwa ndimi zao na kupumbazwa ufahamu kwa ndumba.

Baada ya kuwaficha pale kichakani, nilirudi nyumbani nikalala hadi asubuhi niliposhtuka usingizini kufuatia mtu kugonga mlango. Nilipofungua nilimuona yule

dada mpangaji wangu ambaye hakuwa na mume, baada ya kusalimiana naye tuliketi sebuleni ili kujua alikuwa na shida gani. Dada huyo aliniomba msamaha kwa

kuniamsha na kuniuliza; “Hivi wewe kaka unafanya kazi gani?” Kufuatia swali hilo nilimuuliza kwa nini alinihoji hivyo wakati alikuwa anajua nilikuwa

najishughulisha na kilimo. Yule dada alinijia juu na kuniambia kwamba mimi nilikuwa mchawi niliyekuwa nawasumbua usiku na kuwakosesha usingizi.

Kauli ya yule dada ilinichefua sana na kuhoji kwa nini alisema nilikuwa mchawi, bila woga alinieleza kwamba alikwenda kupiga lamri kwa mganga na kuelezwa

nilikuwa mchawi na nilikuwa nawawangia usiku kucha. “Hivi kaka kwa nini unatufanyia hivyo tumekukosea nini?”

yule dada aliniuuliza huku akipaza sauti kiasi cha kusikiwa na watu wengine. Kauli ya yule dada ilinichefua sana na kuhoji kwa nini alisema nilikuwa mchawi,

bila woga alinieleza kwamba alikwenda kupiga lamri kwa mganga na kuelezwa nilikuwa mchawi na nilikuwa nawawangia usiku kucha. Kwa kuwa alikuwa amenitibua

sana nilimwuliza kwa nini yeye kama mwanamke aliacha kufanya mambo yake na kuamua kunifuatafuata. Yule dada alinijibu kwamba alichoshwa na kuwawangiwa usiku

ndiyo maana aliamua kwenda kwa mganga na siyo alikuwa akifuatilia mambo yangu.

Kwa jinsi alivyonidhalilisha nilimwambia mdomo wake ulimponza na asingemaliza mwaka, baada ya kumweleza hivyo nilibeba jembe nikaelekea shambani. Siku hiyo

wakati nikilima nilikuwa namfikiria yule dada aliyeamua kunidhalilisha mbele za watu, nikapanga kumkomesha. “Huyu mwanamke anadiriki kunidhadhalilisha namna

ile mbele za watu, huyu lazima nimuondoe duniani, hiyo ndiyo adhabu anayostahili kupewa,” niliwaza. Baada ya kulima nilirejea nyumbani ambapo nilichukua maji

na kwenda kuoga kisha nilibadili nguo nikaamua kwenda kutembea mtaani kwa ajili ya kunyosha miguu.

Nilipotoka kwangu kila mtu niliyekutana naye alikuwa akinikata jicho na baadhi niliwasikia wakisema; “Jamani huyu kaka kumbe mchawi mkubwa!” Kauli hizo

ziliniumiza sana na kunizidishia hasira dhidi ya yule mpangaji wangu, hata hivyo kujisafisha na kashfa hiyo niliamua kuigiza kama nimeokoka. Jambo la kwanza

kulifanya siku iliyofuata nilinunua Biblia na kila ilipofika Jumapili nilikuwa nakwenda kusali, lakini siyo kwenye makanisa ya kilokole ambayo wanakemea

nguvu za giza. Nilijua nikienda huko nitaumbuliwa na maombi nikawa nahudhuria ibada kwenye makanisa ya kawaida.

Baada ya kununua Biblia kila Jumapili nilikuwa nakwenda kusali lakini siyo kwenye makanisa ya kilokole ambayo wanakemea nguvu za giza. Nilijua nikienda huko

nitaumbuliwa na maombi, nikawa nakwenda kusali kwenye makanisa ya kawaida. Kufuatia kila siku kwenda kanisani, majirani zangu waliamini kwamba sikuwa mchawi

na yule dada alinisingizia tu. Kwa kuwa nilipanga kumuua yule mpangaji wangu, niliamua kumpa roho ya mauti ndipo siku moja niliporejea nyumbani kutoka shambani nilitengeneza uchawi kisha nilinuiza afe ghafla.

Hata hivyo, nilihisi rafiki yake mmoja aliyekuwa akiishi naye ndiye aliyemshawishi aende kupiga ramli kwa mganga wa kienyeji ili kumjua mtu aliyekuwa

akiwawangia. Awali nilitaka naye nimtie roho ya mauti lakini niliamua kuachana naye na ‘kudili’ na aliyenidhalilisha hadharani. Baada ya kuandaa uchawi

wangu, siku iliyofuata saa mbili usiku ndipo niliiamuru ile roho ya mauti ikamuingie yule dada na akifa maiti yake ipelekwe hospitali na si kwa mganga wa kienyeji.

Kukufafanulia hapo ni kwamba, mtu aliyekufa ghafla kwa kurogwa, ndugu zake wakimshtukia kwamba karogwa wakimpeleka kwa mganga wa kienyehi huzinduka lakini

akipelekwa hospitali anakufa moja kwa moja. Kulitambua hilo, wakati nanuiza ile roho ya mauti kwenda kwa yule dada sikusahau kuiambia ndugu zake wasipate

ufahamu wa kumpeleka kwa mganga ila hospitali. Baada ya kunuiza nilijifanya naumwa nikalala chumbani kwangu kwani nilijua muda si mrefu yule dada angefariki dunia.

Nikiwa chumbani kwangu nilisikia yule dada akilia na kusema kwamba rafiki yake alianguka ghafla na kufariki dunia, kilio cha dada huyo kiliwashtua wapangaji

wengine. Kutohisiwa mimi ndiye nilimuua yule dada, niliamka huku nikijikongoja na kujifanya naumwa nikatoka na kuanza kuhoji kimetokea nini, wakaniambia yule

dada kafariki. Nilijifanya nimehuzunishwa sana na kifo hicho ndipo nilishangaa kumuona yule rafiki wa marehemu ametoka mbio.

Hakutumia muda mrefu huko alikokwenda akarejea na gari akiwa na mganga ambaye nilibaini ndiye waliyekwenda kupiga ramli na kuambiwa mimi nilikuwa nawaroga.

Jamaa huyo nilikuwa namfahamu kwani tulikuwa tukiishi eneo moja na alisifika sana kwamba alikuwa mganga mahiri. Baada ya kufika waliingia ndani, kwa kuwa

chumba hakikuwa na silingibodi juu nilimsikia mganga huyo akisema yule dada alirogwa na alikuwa na uwezo wa kumzindua kwa sababu hakufa.

Hakuishia hapo, alisema inatakiwa wamtoe pale na kumpeleka nyumbani kwake ambako atamfanyia dawa. Niliposikia kauli hiyo, moyo ulinipiga paa! Kwa kuwa

sikutaka kabisa dada huyo azinduke niliwafuata na kuwaambia wampeleke hospitali kwa sababu alipoteza fahamu kwa tatizo la kuishiwa damu. Jambo la kushangaza

ni kwamba licha ya kusisitiza sana wampeleke hospitali na kuwaambia huko nyuma niliwahi kuwa daktari lakini yule mganga alipinga.

Alichokifanya aliwasihi watu waliofika pale nyumbani wakiwemo ndugu wa yule dada kwamba, wasihuzunike kwani hakufa bali alirogwa na atamzindua kisha

akaondoka naye. Kitendo hicho kiliniumiza sana kwani yule mganga alikuwa na nguvu nyingi hivyo nisingeweza kupambana naye ili aniachie mtu wangu niliyetaka

kumfanya msukule. Baada ya kutafakari sana, ilipofika saa sita usiku niliuita ungo wangu nikaamua kumfuata yule dogo mchawi ili akanisaidie.

Nilipofika nilimsimulia kila kitu kuhusu yule dada na mganga na kumuomba anisaidie ili asimzindue kwani nilitaka kumfanya msukule. Yule dogo akashauri kesi

hiyo tuipeleke kwa malkia ndipo tulipanda ungo na kumfuata malkia ambaye ndiye alikuwa mkuu wetu katika ulimwengu wa kichawi. Baada ya kunishauri hivyo

tuliondoka hadi kwa malkia, tukiwa kwenye makazi ya mkuu wetu huyo tulimuona akiwa ameketi nje ndipo dogo akaniambia nimfuate kwa unyenyekevu nikamwambie tatizo langu.

Nilipomfikia nilimsujudia mara kumi na sita kisha nikamweleza shida yangu ndipo malkia akatikisa kichwa na kusema; “Huyo mganga anataka kumfufua mtu wako si ndiyo?” Nikamwambia ndiyo. Baada ya kumweleza hivyo, akaniuliza nilikuwa nataka msaada gani, nikamwambia aniongezee nguvu ili nikamshinde mganga na kumgomboa mtu wangu, akasema sawa.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)