Mwandishi: Juma Hiza
SEHEMU YA TATU
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Mapenzi yangu na Sesilia yalizidi kupamba moto kila siku na hakukuwa na tatizo lolote, niliendelea kufanya kazi yangu ya bodaboda huku ulipofika wakati wa kuwa na Sesilia niliweza kuwa naye.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA CnZ Media APP INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
Lilipofika suala la kwenda kunitambulisha nyumbani kwao maeneo ya Keko alipokuwa akiishi na Dada yake ambaye ndiye alikuwa akimsomesha chuo nilionekana kusita kidogo, sikuwa na ndoto za kuja kumuoa Sesilia katika maisha yangu hivyo kile alichokuwa akinieleza kilichukua sura mpya katika ufahamu wangu.
“Unasemaje?” nilimuuliza.
“Nataka nikakutambulishe kwa Dada yangu halafu tayari nimeshamueleza kila kitu kuhusu wewe anataka akufahamu,” aliniambia Sesilia maneno ambayo yalinishangaza sana.
“Mbona imekuwa mapema sana!” nilimuuliza huku nikiwa nimekumbwa na bumbuwazi.
Nilizidi kushangazwa na maneno ya Sesilia aliyokuwa akinieleza kwa wakati ule, alionekana kumaanisha kila kitu na hakuwa katika utani kama nilivyokuwa nikihisi.
Nilitafuta mada nyingine ya kumpotezea lakini kabla ya kukolea alinirudisha katika mada ile ile ya mwanzo, aliniambia anataka nikajitambulishe kwa dada yake.
“Sesilia lakini si ungesubiri kwanza?” nilimuuliza.
“Nisubiri nini Metu wakati sisi tayari ni wapenzi,” alinijibu.
“Hata kama lakini suala la kwenda kujitambulisha sio la kukurupuka kama unavyodhani,” nilimwambia.
“Tatizo kwani liko wapi?” aliniuliza.
“Wewe hulioni?”
“Metu au huna mpango wa kuishi na mimi ndiyo maana unakataa kwenda kujitambulisha niambie au una mwanamke mwingine umempata?” aliniuliza kisha nikakaa kimya, sikutaka kumjibu kwa maana nilianza kupandwa na hasira.
Kwa muda ambao nilikuwa nimekaa kimya akarudia kuniuliza swali hilohilo, nikazidi kupandwa na hasira za ajabu hata sikujua zilitoka wapi. Nilijikuta nikifyatuka na kwenda kumpiga kofi moja upande wa shavu la kushoto halafu nikaanza kumtolea maneno makali ya kumkaripia, haikuchukua hata muda machozi yakawa tayari yameshatawala mashavuni mwake, alikuwa akilia.
“Tena naomba unyamaze kwani kuna ulazima wa mimi kwenda kujitambulisha kwa dada yako,” nilimwambia kwa sauti ya ukali kisha nikamtukana tusi moja la nguoni. Akanyamaza kisha akayafuta machozi yake. Akaniomba msamaha kwa kosa ambalo hata halijulikani, nikamsamehe maisha yakaendelea.
****
Nilijikuta nikianza kumchukia Sesilia kutokana na itikadi alizokuwa akiniletea. Katika kumbukumbu zangu sikumbuki kama kuna siku niliwahi kupanga au kuwaza siku moja nitakuja kuishi na mwanamke ambaye nitamuoa na mwisho wa siku nitatengeneza naye maisha. Huo nakumbuka ulikuwa ni ugomvi mkubwa na Mama yangu, kila siku alikuwa ni mtu wa kuniambia nitafute msichana mmoja wa kumuoa lakini maneno yake naweza kusema yaliingilia sikio la kushoto na kutokea la kulia. Nakumbuka kesi za wanawake niliyokuwa natembea nao zilipozidi kuwa nyingi Mama yangu aliniambia nihame nyumbani nikapange chumba changu na hiki ndiyo kilikuwa chanzo cha mimi kupanga chumba Tandika Azimio huku nikimuacha Mama yangu ambaye alikuwa akiishi Mbagala Kizuiani. Alichoka na aina ya maisha ambayo nilikuwa nikiishi.
Furaha yangu ilikuwa ni kuona nakuwa na msichana katika mapenzi ambaye mwisho wa siku nafanikiwa kumvua nguo yake ya ndani na kisha kufanya naye mapenzi. Hiyo ndiyo ilikuewa furaha yangu wala hakukuwa na kingine ambacho nilikuwa nakipenda katika mapenzi, ni kufanya ngono na kuhakikisha namteka mwanamke kimapenzi ili asifikirie kuniacha katika maisha yake.
Baada ya kumfanyia visa na mikasa mpaka kufikia hatua ya kumpiga, niliamini mpango wangu ulikuwa umetimia. Licha ya kuwa nilimchukia ghafla! na kumkinai kwa mapenzi yake lakini nilizidi kujiona kidume ambaye sikutumia pesa, dawa wala kitu chochote katika kumteka kimapenzi Sesilia. Ufundi wangu wa kitandani pamoja na ahadi zangu za kufikirika ndizo zilizomteka Sesilia, akabaki akiamini kuwa mimi ndiye mwanaume wa maisha yake, hakutaka kunipoteza na kila baya nililokuwa namfanyia aliweza kulipokea kwa mikono miwili na kwa uvumilivu huku akiamini kuwa kuna siku nitaweza kubadilika.
Chuoni alipokuwa akisoma wanaume hawakuacha kumsumbua na kila mwanaume ambaye alikuwa akimtongoza hakuacha kuniambia, aliniambia huku akiniaminisha kuwa alikuwa akijiheshimu na kujilinda hivyo nisijali kuhusu yeye.
“Sasa kama anakutongoza unaniambia ya kazi gani?” nilimuuliza kwa ukali wakati aliponipigia simu na kunieleza juu ya Lecture ambaye alikuwa akimsumbua.
“Metu mbona hivyo lakini?” aliniuliza.
“Mkubalie sasa unamwachaje kwa mfano,” nilimwambia.
“Hivi nitaanzaje kumkubalia wakati mimi nipo na wewe.”
“Kwahiyo.”
“Kwahiyo nini?”
“Wewe unaniigizia upendo, huko chuo najua una wanaume wako.”
“Metu huniamini?”
“Siwezi kumuamini mwanamke katika maisha yangu,” nilimwambia kisha nikamsikia akianza kulia, sikutaka kukisikiliza kilio chake, niliamua kukata simu.
Kesi za kila siku juu ya wanaume waliyokuwa wakimsumbua ndizo nilizozitumia kama fimbo ya kumuadhibu, nilimwambia kuwa simuamini hivyo asiendelee kuniaminisha upendo wake niliyoufananisha na gazeti kila mtu anasoma.
Kuna muda nilijisikia kufanya mapenzi, nilimtafuta na kumuigizia upendo, alipokuja nilimfungia ghetto siku hiyo na hakukuwa na kitu kingine tulichokifanya zaidi ya kufanya mapenzi, nilifanya naye kila aina ya staili unazozijua na nyingine usizozijua.
Baada ya kumtumia sana kimapenzi nilianza kumuacha kimya kimya. Nilikuwa simtafuti tena kama ilivyokuwa hapo awali, alipokuwa akinipigia simu na kunitumia ujumbe mfupi sikuweza kumjibu kwa wakati na nilipokuja kumjibu nilisingizia kazi yangu ya bodaboda ndiyo iliyokuwa ikinifanya nikose muda wa kuwasiliana na yeye wakati, hilo hakujali na kama haitoshi akawa ananitumia ujumbe kila siku, sikutaka kumjibu kwa maana tayari nilikuwa nimeshamchoka.
Katika kipindi hicho ambacho alikuwa akinitumia ujumbe mfupi na kunipigia simu bila kuchoka nilikuwa tayari nimeshakutana na Samira msichana ambaye nilikuwa nimempenda, kazi yangu ilikuwa ni kumpeleka kila siku kazini kwake Posta na kumrudisha.
Nilichokuwa nimekipanga kwa wakati huo ni kufanya mabadiliko makubwa sana ya kimapenzi, nilipanga kuachana na Sesilia na kuanza kumfukizia Samira.
Ingawa Sesilia aliendelea kunitumia ujumbe mfupi na kunipigia simu kila wakati lakini sikutaka kujali hilo, nilikuwa nimepanga kuyapeleka majeshi kwa Samira ambaye alikuwa akinichanganya kwa wakati huo.
“Mbona hujibu lolote Metu?” alinitumia ujumbe Sesilia.
“Nipo bize,” nilimjibu.
“Upo bize unafanya nini?”
“Sitaki maswali mengi wewe elewa kuwa nipo bize.”
“Metu.”
“Nini?”
“Mbona unanijibu hivyo lakini?”
“Ulitaka nikujibu vipi sasa?”
“Basi mpenzi ukishamaliza huo ubize utaniambia.”
“Poa,” nilimjibu.
Niliendelea kumfikiria Samira pale kitandani nilipokuwa nimejilaza, akili yangu ilikuwa imetawala jina lake, nilipokuwa nikiitazama picha yake aliyokuwa ameiweka Profile WhatsApp ukichanganya na baridi kali iliyokuwa ikinitafuna nilizidi kumtamani vilivyo.
Kuendelea kuishi na ndoto au mawazo ambayo hutaki kuyafanyia kazi kamwe ni vigumu kubadilika na kuwa kama unavyowaza. Sikutaka kubaki kuishi na ndoto za kumpata Samira ambazo sikutaka kuzifanyia kazi, niliamua kumtumia ujumbe mfupi WhatsApp na kama bahati alikuwa online kwa muda huo.
“Mrembo,” nilimtumia.
“Abee Metu niambie,” alinijibu.
“Picha yako nzuri sana.”
“Ipi hiyo.”
“Hiyo uliyoiweka Profile.”
“Asante mwaya.”
“Usijali unafanyaje?”
“Nimelala, nahisi baridi ya hatari.”
“Pole ila umevaa sweta?”
“Ndiyo nimevaa lakini bado nahisi baridi.”
“Pole vipi nije?”
“Uje wapi?”
“Hapo ulipo?”
“Weee naogopaa.”
“Unaogopa nini sasa?”
“Tuachane na hizo habari niambie mambo mengine.”
“Mambo yako poa kabisa.”
“Nisamehe kwa kukusumbua leo.”
“Usijali hiyo ni kazi yangu wala usijali mrembo.”
“Sawa,” alinijibu.
Nilishindwa kumuingizia mada za kimapenzi kwasababu tayari alionekana kuzikwepa, hakutaka kuwasiliana na mimi kwa njia hiyo, sijui ni kwanini ila hakutaka kufanya hivyo.
Nikajikuta nikikosa maneno ya kumuandikia baada ya kunijibu ujumbe wake wa mwisho aliyouambatanisha na emoji ya mikono miwili iliyojikunja kuashiria kushukuru.
Nikaendelea kubaki online huku nisiwe na cha kumuandikia Samira.
“Nakupenda,” niliandika maneno haya kisha nikawahi kuyafuta, nilihisi kukosea kumuandikia.
“Sawa,” nilimuandikia na kumtumia kisha hapo hapo zikatiki tiki mbili za rangi ya blue kuashiria ujumbe tayari umeshapokelewa na kusomwa.
Nikamuona akiniandikia, nikasubiri jibu lake, wakati huo Sesilia alikuwa ameshaanza tena kunipigia simu, nikawa namkatia simu yake maana nilihisi usumbufu.
“Usiku mwema ila usisahau kesho mapema kuja kunichukua kuna sehemu nataka unipeleke,” alinitumia Samira.
“Sawa haina tatizo,” nilimjibu kisha hazikupita sekunde akawa tayari ameshatoka online.
Kama walivyosema wahenga kuwa siku zote pole pole ndiyo mwendo, sikutaka kuwapinga hata kidogo, niliamini katika msemo huo na ndiyo nilikuwa nikiutumia katika kumfukuzia Samira, sikutaka kuweka papara nyingi maana mwisho wa siku ningeweza kumpoteza.
Sesilia hakuchoka kunipigia simu, aliendelea kunipigia simu mfululizo, mwisho nikaamua kupokea.
“Mpenzi wangu kwanini unanifanyia hivi lakini?”
“Kitu gani kibaya nilichokufanyia?”
“Hupokei simu yangu.”
“ Nilikuambiaje?”
“Hata kama yani ndiyo uko bize muda wote huo halafu nakuona online WhatsApp kwani unafanyaje?”
“Sifanyi kitu.”
“Mmmh! Kweli Metu?”
“Sasa mbona unaguna au unataka nikudanganye?”
“Sio hivyo lakini unavyonifanyia sio vizuri, naumia mwenzako sina amani.”
“Umemaliza?”
“Unasemaje Metu?”
“Nakuuliza umemaliza kuongea?”
“Metusela una nini lakini mpenzi wangu mbona umebadilika sana?”
“Sesilia wewe ni mtu mzima halafu tena ni msomi hivi hata picha unayoiona bado tu hujui ni nini kinachoendelea au unataka mpaka uambiwe kuwa umechokwa hupendwi tena ndiyo utaelewa?”
“Unasemaje?”
“Sikupendi nimekuchoka,” nilimjibu kisha nikakata simu.
Yalikuwa ni maneno machache niliyomwambia Sesilia ambayo niliamini yangeweza kumuumiza sana huko alipo lakini sikutaka kuyawazia sana, kwanza niliamini alikuwa ni msichana na muda wowote angeweza kupendwa na kunisahau katika maisha yake.
“Kwanini umenifanyia hivyo Metu kwanini hukuniambia mapema kwamba hilo ndiyo lilikuwa lengo lako. Ziko wapi zile ahadi zako za kwamba utanioa na kunithamini kama mwanamke wako. Umenichoka baada ya kukupa mapenzi sawa Metu nashukuru sana ila sitaki kuamini kama kweli nimeachana na wewe,” alinitumia ujumbe mfupi Sesilia.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi