Mwandishi: Alex Kileo
SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
"naomba polisi yeyote atakaekuuliza kuhusu yale mambo yaliyötokea
kule, mjibu hujui chochote, sawa?" Sajenti Minja aliwasilisha ombi
lake huku akiwa hana uhakika wa kukubaliwa,
"kwanini tufiche ukweli?" Msaidizi wa mganga aliuliza kwa mshangao,
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
"Ukiongea ukweli utakuwa umeniharibia kila kitu katika maisha
yangu, yaani hata kufungwa nitafungwa" Sajenti Minja aliongea kwa
huruma ili kumshawishi Msaidizi wa Mganga akubaliane nae,
"Kwa maana hiyo wewe umependa lile tukio lililotokea siku ile?"
Msaidizi wa Mganga alimuuliza Sajenti Minja,
"Tukio sasa, maana yalikuwa mengi" Sajenti Minja aliuliza,
"La wenzangu kuuawa kinyama?" Msaidizi wa Mganga aliuliza,
"Hapana, nitalifurahia vipi wakati lilikuja kuharibu tiba ya ndugu
yangu na nikampoteza mtu ambaye ndiye nilikuwa nategemea yeye
atamponya ndugu yangu?" Sajenti Minja aliongea kwa upole na machozi
yakimtoka kwa mbali ili kumshawishi tu Msaidizi wa Mganga asiseme
ukweli mbele ya Polisi wengine,
"Sasa kwanini nifiche?" Msaidizi wa Mganga akauliza tena ila
kipindi hiki aliuliza kwa upole,
"Kuwa na utu ndugu yangu, maana unachotaka kukifanya ni kuniharibia
maisha tu" Sajenti Minja aliendelea kumlalamikia Msaidizi wa
Mganga,
"Sio nakuharibia maisha, mbona mimi maisha yangu yameshaharibika?"
Msaidizi wa Mganga aliongea huku anamkodolea macho Sajenti Minja,
"Yameharibikaje sasa wakati upon hai na upon huru?" Sajenti Minja
alimuuliza,
"Hill sio tatizo, tatizo ni kwamba yule Mganga nilimchukulia kama
mkombozi wangu kutokana na maisha yangu" Msaidizi wa Mganga
aliongea,
" kivipi yaani?" Sajenti Minja alimuuliza,
"Yaani nilikuwa sina mbele wala nyuma, ila yule mzee aliniokota tu
mjini na kunichukua kisha akawa ananifundisha uganga na akawa
ananipa kipato kidogo angalau nikajiona mtu" Msaidizi wa Mganga
aliongea,
"Hilo sio tatizo, ngoja upone tutaongea zaidi, mimi nitakusaidia"
Sajenti Minja aliongea kwa huruma huku akichomoa noti nyingi kutoka
katika mfuko wake wa suruali na kumpa msaidizi wa Mganga,
"Za nini hizi?" Msaidizi wa Mganga aliuliza huku akiwa anaziangalia
zile hela akiwa hataki kuzipokea,
"Zitakusaidia kununua vitu vidogo vidogo kipindi upo hapa
Hospitali" Sajenti Minja aliongea huku akiwa bado amezishikilia
zile pesa,
"Wewe ni ndugu yangu bwana, tusaidiane" Sajenti Minja aliongea kwa
upole,
"Ngoja nitoke hospitali tutaongea vizuri ndugu yangu" Msaidizi wa
Mganga aliongea huku akizitia pesa zile mfukoni,
"Nikununulie chakula gani kabla sijaondoka" Sajenti Minja
alimuuliza,
"Chochote tu, mimi mswahili bwana sichaguagi chakula" msaidizi wa
Mganga aliongea,
"Wewe mgonjwa bwana, itabidi ule minyama nyama, ngoja nikakutafutie
kuku bosi" Sajenti Minja aliongea kwa furaha huku akitoka nje na
akiamini tayari ameshamteka hisia yule Msaidizi wa Mganga.
"*
Babu wa monchwari alivyopigwa ule mtama ile asubuhi kumbe aliteguka
mguu maeneo ya nyuma ya paja chini ya kiuno ila alivumilia na
hakuwaambia kitu chochote wale polisi kwa sababu walikuwa na hasira
muda ule, ila ilivyofika jioni maumivu yalimzidia na Babu wa
monchwari akawaambia polisi ila walimpuuza tu, masikini Babu wa
watu maumivu yalimzidia mpaka akawa Amalia kwa sauti kubwa kama
mtoto, kilio kikamfikia mkuu wa polisi na kuja kuangalia kuna nini,
" mbona huyo mzee analia?" Mkuu wa polisi aliwauliza askari
aliowakuta hapo ambayo walibaki wakitazamana bila kutoa jibu,
"Anamaumivu nadhani" Askari mmoja alijibu,
"Babu una tatizo gani?" Mkuu wa Polisi aliamua amuulize mwenyewe,
"Mguu nahisi umevunjika, nawaambia wanisaidie ila wananitukana"
Babu alijibu huku akiendelea kulia,
"Umevunjikaje, umeanguka?" Mkuu wa Polisi aliuliza,
"Hao wenyewe walinipiga asubuhi" Babu alijibu,
"Hata mambo ya kuwapiga watuhumuwa si tulishawakataza?, tena
mnampiga mzee kabisa..ebu chukueni gari ya doria mumpeleke
hospitali" Mkuu wa Polisi aliongea kwa ukali na vijana wake
wakanyanyuka haraka,
"Kwani yupo hapa kwa kosa gani" Mkuu wa polisi akauliza,
"Huyu ndiye yule mlinzi wa monchwari" Askari mmoja akajibu,
"Hata mumpeleke hospitali akapatiwe matibabu na mumrudishe hapa,"
Mkuu wa polisi aliongea na kuondoka huku akiwaacha vijana wake
wakimbeba Babu monchwari na kumpeleka kwenye gari na safari ya
hospitali ikaanza.
Iliwachukua dakika chache kufika hospitali, walimshusha Babu na
kumpeleka kupata matibabu.
Babu akapatiwa huduma kisha kwa Saa nzima na akaonekana ni mfupa tu
ulikuwa umehama eneo lake, madaktari wakafanya jitihada na kumtibu
bila tatizo na kuwaruhusu askari waondoke nae.
Askari walipotoka nje walienda moja kwa moja mpaka kwenye gari yao,
wakapanda gari ili warudi kituoni, kwa bahati mbaya gari yao
ilipata itilafu ikawa haiwaki, ikabidi wapige simu kwa mkuu wao ili
wapate msaada, mkuu wao akawapa namba ya sajenti Minja na kuwaambia
yuko pale hospitali kwa hiyo wampigie awape msaada wa kuwarudisha
kituoni kwa maana Sajenti ana gari.
Sajenti Minja baada ya kupigiwa simu akawaelekeza mahali gari lake
lilipo, wale askari na Babu wa mochwari wakafika mahali gari
lilipo, kisha wakawa wanamsubiri sajenti Minja atoke ndani ili
awarudishe kituoni, na Babu wa monchwari ndio kabisa alikuwa
anaangalia katika mlango wa kutokea hospitali ambayo ndio njia
anayokuja nayo Sajenti Minja..
…Sajenti Minja wakati anatoka ndani ya hospitali, akawaona wale
polisi na yule babu wa mochwari kupitia dirishani, akasita, kisha
akili yake ikafanya kazi haraka.
akarudi kisha akawapigia simu wale askari na kuwaambia kuwa yeye
bado ana shughuli anazifanya katika eneo like la hospitali, kwa
hiyo askari mmoja amfuate ndani ili akampe ufunguo,
mmoja kati ya wale polisi akaenda alipoelekezwa na sajenti Minja,
akapewa ufunguo, kisha akaambiwa arudishe gari pale hospitalini
baada ya kazi zao
Sajenti Minja aliingia katika nyumba ya dada yake saa mbili usiku,
baada ya salamu wakakumbushana mambo yaliyowakuta usiku uliopita,
wakafurahi na kuhuzunika pia,
Ila habari iliyowashtua wote ni kupatikana kwa wale maiti na mtu
mmoja akiwa mzima, pia sajenti Minja akawaambia namna
alivyofundisha yule msaidizi wa mganga kukana kujua lolote.
Mama kayoza kidogo akashusha presha baada ya kusikia hivyo,
"Kitu kingine kibaya ni kwamba hata yule babu wa monchwari
aliyetusaidia kuiba ile maiti nae amekamatwa ila sijajua kwa kesi
gani?" Sajenti Minja aliendelea kutoa habari mbaya,
"Ni hiyo hiyo ya kupotea kwa maiti, asubuhi si nilikuwa hospitali
nilienda kumuona mtu, ndio nikakutana na hizo habari, ila maiti
yenyewe imeshapatikana uko makaburini ilikutwa pamoja na hiyo miili
ya waganga wenu" Mama Kayoza aliwapa habari,
"Kama maiti imepatikana itakuwa afadhali kwa Babu" Kayoza aliongea,
"Hujui sheria mjomba, Babu hawezi kuachiwa mpaka ipatikane au
ijulikane sababu za kuuza ile maiti" Sajenti Minja aliongea huku
akimuangalia Kayoza,
"Sababu iliyomfanye auze si ni pesa?" Kayoza alijibu kiutani na
wenzake wacheke,
"Haya mambo mazito msiyachukulie kiutani utani hivyo" Mama Kayoza
aliongea huku akionekana kutofurahishwa na jibu la Kayoza,
"Mama inabidi tujifurahishe tu, ukisema uegemee sana upande wa
yanayotukuta, tutakuwa watu wa machozi kila siku" Kayoza alimwambia
Mama yake,
"Ujinga huo, badala uangalie namna ya kujisaidia unakalia kuongea
vitu visivyo na kichwa wala miguu" Mama Kayoza aliendelea
kumshambulia mwanaye,
"Vitu vya maana kama vipi?, ngoja nijiandae niende kanisani" Kayoza
aliongea kwa hasira huku akiondoka sebuleni,
"Ana hasira kama babu yake, mzee John Minja" Sajenti Minja aliongea
huku akicheka,
"Mjinga tu, hasira ananiletea Mimi badala ya kumpelekea bibi yake
uko kijijini" Mama Kayoza aliongea,
"Kayoza anaenda kanisani?" Sajenti Minja aliuliza,
"Leo kuna maombi, tena na wewe itabidi uende ili bwana akakupe
wepesi uenda kazi ya kumsaidia mjomba wako itatimia haraka" Mama
Kayoza alimwambia Sajenti Minja,
"Sawa itabidi tuongozane, kwani maombi yataisha saa ngapi?" Sajenti
Minja akauliza,
"Tunakesha" Mama Kayoza alijibu,
"Mh..sasa si itabidi niende nyumbani nikabadili nguo" Sajenti Minja
aliongea,
"Kwani hizo ulizovaa zina ubaya Gani? Mama Kayoza aliuliza,
"Mimi naona sio vizuri kwenda Nazi kwa sababu nimeshinda nazo kutwa
nzima" Sajenti Minja alijibu,
"Hiyo sio sababu, nenda kaoge uende kanisani" Mama Kayoza aliongea,
"Sawa basi, nirudi baada ya muda gani?" Sajenti Minja aliuliza huku
akiinuka,
"Hakuna kuondoka, nilipokwambia ukaoge nilimaanisha uingie bafuni,
sasa unavyotaka kuondoka unadhani bafu lipo kwako tu?" Mama Kayoza
aliuliza,
"Sawa bwana, basi ngoja nikajitayarishe" Sajenti Minja aliongea
huku akielekea vilipo vyumba vya wakina Kayoza,
Baada ya saa moja na nusu wote walikuwa wamejiandaa mpaka Omary
wakaanza kwenda eneo la maombi.
Walienda kwa miguu tu kwa maana ni eneo jirani na wanapoishi.
Walifika na muda ulipofika waumini walikuwa wengi sana kanisani,
walianza kwa kuimba nyimbo mbalimbali za kutukuza.
Baada ya saa zima Mchungaji Wingo aliingia, akakaa katika kiti
anachopaswa kuwepo. Nyimbo ziliimbwa kisha waimbaji wakamaliza,
sala zilianza, walisali muda mrefu sana mpaka kayoza akachoka
kutokana na kwamba yeye sio mtu aliyezoea sana kwenda kanisani,
"oya kaka, tusepe" kayoza alimwambia Omari ambae alikuwa anasinzia
tu muda wote.
"wapi sasa" Omari akauliza kivivu huku akijinyoosha,
"maskani dogo, we unasinzia tu bila ya mpango, usije ukaharibu hewa
bure" Kayoza aliongea kwa utani.
"aah wapi, mimi nina kontroo wewe" Omari akajibu kisha wote
wakacheka.
Wakatoka nje ya kanisa wakawa wanaelekea nyumbani, ilikuwa kama saa
saba usiku hivi, kwa mbali wakaona msichana anawakimbilia, alikuwa
yule binti wa mchungaji,
"habari jamani" Binti akawasalimu.
"nzuri" wakajibu kwa pamoja.
"Kaka unaweza kutupisha kidogo?" Binti Mchungaji aliongea huku
akimuangalia Omary,
"Sawa" Omary alijibu huku akitangulia mbele na kuwaacha Kayoza na
Binti Mchungaji wakiwa wamesimama,
"vipi jibu langu Kayoza" Binti Mchungaji alimuuliza kayoza huku
akiwa hana chembe ya aibu.
"kesho nitakujibu" Kayoza akajibu kwa ufupi.
"jamani mbona unanifanyia hivyo, au kwa kuwa nimekwambia
nakupenda?" Binti Mchungaji alilalamika kwa huruma.
"sikia binti, hapa unapoteza muda wako bure, kiukweli kabisa mi
siwezi kukubalia ombi lako" Kayoza aliongea kwa ujasili kwa maana
aliona bora amueleze ukweli tu kuliko kumpotezea muda,
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi