Mtunzi: Denis Benard
SEHEMU YA KUMI
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Mama aligeuka na kumuangalia Faluu kwa macho Fulani ya kutisha,hali ambayo ilimpelekea Faluu kuogopa na kisha mama alicheka na katika mazingira yasiyotarajiwa alipotea na ule mwili wa marehemu.Ilikuwa ni siku ya historia kwa Faluu kwani hakuyategemea mambo yote yaliyotokea usiku kucha na hivyo kumpelekea kuishiwa nguvu na kupoteza fahamu palepale.
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
Alilala pale kwa muda mrefu sana na kwa kuwa pale ndani hakukuwa na mtu yeyote,ilikuwa ngumu sana kwa Faluu kupata msaada.Masaa yalizidi kwenda,wakati Faluu akiwa usingizini,alianza kuota akiwa mkubwa na pia yuko kwenye hiyo nyumba ya mjomba wake na watu wengi wakiwa wanamuabudu yeye, lakini wakati akiendelea na maisha hayo kwenye ndoto,siku moja alikuwa ametoka nyumbani yeye na mfanya kazi wake wakiwa wameenda kutafuta dawa katika msitu mmoja mkubwa sana,alikutana na bibi mmoja mzee sana akiwa hajiwezi,huyo bibi alianza kuomba msaada kutoka kwao..
‘’wajukuu zangu naomba mnisaidie bibi yenu’’Huyo bibi aliongea.
Faluu alimuonea huruma na kutokea kuvutika kumsaidia yule bibi,Lakini lile swala la kutoa msaada yule mfanya kazi wake hakulihafiki kabisa.
‘’Sikia mzee,moyo wangu hauko tayali kabisa wewe kumsaidia hyo bibi,ni vyema ukamwacha tukaendelea na shughuli zetu’’Yule mfanya kazi aliongea.
Yale maneno ya mfanya kazi wake yalimuingia kidogo kichwani na hivyo kufanya wao waendelee na safari yao,lakini walipokuwa wakiondoka yule bibi alianza kulalamika huku akionesha kushindwa kufanya kitu chochote pale..
‘’eeeh,mweeeeh!nisaidieni jamani,nakufa…ooooh”alilalamika yule bibi huku akipiga kelele katika msitu ule.
Baada ya yule bibi kulalamika sana,Faluu alishindwa kuivumilia ile sauti na hivyo akajikuta anarudi nyuma ili aende kumsaidia yule bibi,wakati akigeuka nyuma ili aende kumsaidia,yule mfanya kazi wake alimshika mkono na kumzuia asiende..
‘’Sikia mzee,tafadhali sana usiende kumsaidia yule bibi,acha tuendelee na kazi iliyotuleta huku muache huyo bibi aendeleee na biashara yake’’Mfanya kazi wake alimsihi sana Faluu asifanye vile,lakini ilikuwa ngumu sana kwa Faluu kuvumilia ile sauti ya yule bibi na hivyo ilibidi aende kumsaidia.
Kwa bahati mbaya alipomsogelea karibu yake lilitumwa kombora mithili ya moto na kumuingia Tumboni na hapo hapo Faluu alijikuta akishtuka baada ya kupoteza fahamu kwa muda mrefu,baada ya kufumbua macho tu,mtu wa kwanza kumuona alikuwa ni mama yake..
‘’Mama nimeota ndoto hapa….’’ Aliongea Faluu huku akiwa anathema kwa nguvu sana,lakini kabla hajamalizia mama yake aliongeaa..
‘’Najua,lakini usipoangalia huruma yako itakupeleka pabayaa” Mama yake aliongea.
Yale maneno yalimfanya Faluu habaki mdomo wazi huku akijikuta anakosa kitu cha kumueleza mama yake.Baada ya muda wa dakika kadhaa alitabasamu na kuongea maneno kwa mama yake..
‘’Mama naomba nikuulize kitu’’ Faluu aliongea.
‘’Wewe uliza tu’’ Mama alijibu.
‘’Kwanini umeniambia hivyo? Na umeijuaje ndoto yangu ?’’ Faluu alimuuliza mama yake.
(Mama alicheka sana )
‘’Sikia mwanangu,kwanza nikueleze kitu hivi,mimi mama yako ninauwezo mkubwa sana saa hizi,ninaweza kukuona na kutambua kitu unachokifikiria wewe au mtu yeyote na pia nikikuona wewe naijua tabia yako kwasababu mimi ndiye niliyekuzaa,hivyo nakujua zaidi ya mtu yeyote anavyokujua,jaribu kubadirika kwa maisha unayoyaendea’’Mama aliongea.
‘’Nijaribu kubadirika? unamaanisha nini?” Faluu aliuliza.
‘’Mwanangu nikikuona wewe,nakuona mtu Fulani mkubwa sana katika maisha yako ya baadaye,lakini naona maisha Fulani magumu kwako na yenye maumivu usipo badirika, kwasababu
ya mwenendo wa eneo hili na watu wake,unatakiwa usiwe na huruma sana na wakati mwingine ili uende vizuri jaribu kuangalia sana maisha yako kuliko kitu chochote kile katika dunia hii’’Mama
alijibu.
‘’Mama yangu nahitaji sana kukuelewa lakini bado naona kama unazunguka tu, naomba uniambie tu mama yangu ili nikuelewe’’Faluu aliongea.
‘’Haya mwanangu,ndoto yako si umeifatilia ,yale ndiyo maisha halisi yanayokuja kwako na kile ulichofanyiwa ndicho kitakacho tokea kwenye maisha yako usipokuwa msikivu nakuangalia maisha yako,kwasababu siyo kila mtu anayekuja katika maisha yako anahitaji sana msaada wako,lakini wengine wanafanya hivyo ili wapate nafasi ya kuharibu maisha yako mwanangu,Siyo kila anayekuchekea anakufurahia,wengine wanakuwa wanakusanifu tu’’mama yake Faluu aliongea kwa ukubwa.
‘’Mama nimekuelewa sana,enhe! Neno la mwisho kwangu nini?’’Faluu alimuuliza mama yake.
(Mama alitabasamu, kutokana na mwanaye kuelewa maneno yake)
‘’Vizuri sana mwanangu, kitu cha wewe kufanya ni hivi,angalia sana na uwe makini mtu asiutambue udhaifu wako, kwa sababu udhaifu wako utakapo julikana watu wengine wanaweza kuutumia ili wakuangushe wewe hapo’’Aliongea mama na baadaye alipotea katika mazingira yale.
‘’Kwa hiyo…aaaah, sasa mbona unaondoka tena! Ila siyo mbaya asante kwa maneno yako mazuri mama yangu’’ Faluu aliongea huku sura yake ikitawaliwa na furaha.
Wakati Faluu akiwa amaezubaa anayafikiria yale maneno amabyo mama yake limueleza Hali ya hewa ilibadirika na mawingu yalitanda katika kile kijiji na kijiji chote kilionekena kuwa na utulivu sana.
‘’Eeeh, hii hali vipi sasa mbona imekuwa ghafla sana’’ Faluu aliongea huku akionekana kustahajabika, Wakati akiwa katika mshangao huo,kwa mbali alisikia sauti kama mtu anaongea,hali ambayo ilimfanya kutega sikio na kusikiliza kwa makini ili ajue kinachoongelewa.
‘’Haya jamani leo kutakuwa na kikao pale nyumbani kwa mwenyekiti wetu wa kijiji, hivyo watu wote mnatakiwa kufika bila kukosa,tutaongelea mambo yote yaliyotokea katika kijiji chetu na matatizo yote yanayokikabili kijiji’’ Huyo mtu aliongea na baada ya ile sauti kusikika, ile hali ilipotea ..
(Faluu alishtuka)
‘’Heeee! Hii hali vipi tena, halafu kwa huyu mwenyekiti ndiyo wapi?” Faluu alikuwa akijiuliza maswali tu.
Masaa yalienda na ilipofika saa kumi na moja(11) jioni watu walianza kukusanyika katika eneo la tukio huku Faluu akiwa ametulia nyumbani kwao akitafakari kikao hicho na eneo ambalo hicho kikao kitafanyika.Baada ya watu kuwa wengi, watu wengine walianza kujiuliza baadhi ya maswali..
‘’Mbona huyu mzee wa mtaa wa juu hapo hatumuoni? Au hata yule kijana wake’’ Mtu mmoja aliongea.
‘’Mzee wa hapo mtaa wa nyuma? Mzee nani huyo” Aliuliza mtu mwingine.
‘’Nazungumzia mzee Kachali’’ Yule mtu alijibu.
‘’Aaah,mzee Kachali! Kwani mzee Kachali anaishi na kijana pale nyumbani kwake saa hizi?”Yule mtu aliuliza.
‘’Ndio yupo’’ Yule mtu alijibu,
‘’Mmmh,sijawahi kusikia,wala kumuona labda atakuja’’huyo mtu aliongea huku akionekana kutoyaamini yale maneno.Baada ya mazungumzo yao kwa dakika kadhaa,waliachana nayo na kila mtu aliendelea na mambo yake huku wakisubilia kuona kitakachoendelea.
Wakati huo Faluu alikuwa akiendelea kuyafikiria maisha maisha yake,hali iliyopo na hicho kikao,mawazo yake yalionekana kutokuwa na maamuzi sahihi juu ya nini afanye kwa wakati huo hususa ni kifo cha mjomba wake na mambo mengine. Kipindi hicho Faluu akiwa katika msongo wa mawazo aliisikia sauti ikimueleza…
‘’Fanya unayoweza lakini hakikisha haukosi kwenda katika hicho kikao sawa’’
(Faluu alishtuka na kujikuta akigeuka geuka ili amuone huyo anayeongea)
‘’Kwanini unasema hivyo?’’ Faluu aliuliza.
‘’Hakikisha unaenda usikose maana huko ndiko kwenye ushindi wa maisha yako’’ hiyo sauti iliongea na wakati huo mama alijitokeza.
‘’Ndio ushindi wa maisha yangu? Na pia kwanini unapenda kupingana na mawazo yangu?’’ Faluu aliongea, huku akionekana kulaumu sana.
‘’Sikiliza mwanangu sina la ziada,ila kubwa kwa sasa ni hilo tu,wewe nenda eneo la kikao ni mtaa wa mbele hapo,simama uende sasa hivi’’ mama aliongea, huku akijivuta Faluu alisimama na bila kufanya chochote katika mwili wake,alianza safari ya kwenda kwenye kikao hicho,alipokaria katika mazingira yale,watu wote waligeuka kumshangaa huku wakimshangilia na kuongea..
‘’Huyu Ndiye…’’ watu waliokuwepo pale waliongea…Tukio lile la watu kumshangaa yeye,lilimfanya abaki akiwashangaa wale watu pia, kwasababu hakuwaelewa nini wanamaanisha kuongea vile,hata yule mwenyekiti aliyekuwa anasimamia kikao kile alibaki akiwashangaa piaa.
‘’Jamani mbona kama siwaelewi mnachomaanisha kusema hivyo?’’Faluu aliwauliza.
‘’Ni kweli hata mimi mmeniacha njia panda,nini maana yenu,kuzungumza hivyo?’’Mwenyekiti aliongea.Walijikuta wakikaa dakika tano bila kusema chochote,muda kidogo alisimama kijana mmoja nakuongea.
‘’Samahani mwenyekiti,sisi tunataka huyu kijana ndiye awe kiongozi wa hiki kijiji chetu’’aliongea yule kijana.Faluu baada ya kusikia hivyo alijikuta akipigwa na butwaa na kutokana na mshtuko ule alianguka na kupoteza fahamu,watu hawakujali walimpa huduma ya kwanza na baada ya kupata nafuu na fahamu kurudi,aliongea
‘’Jamani samahani mimi siwezi kazi zenu’’Faluu aliongea.Watu walizidi kumsihi na kumtaka hakubali kulivaa jukumu hilo,baada mvutanao wa muda mrefu,alikubali na kuwa kiongozi,yaani mwenyekiti wa kijiji hicho na ndiye alivunja rekodi ya kiongozi mdogo kuliko wote waliowahi kuwa katika kijiji kile.
MWISHO
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi