MZIMU WA WAUFU (14)
Zephiline F Ezekiel
---
Jina: MZIMU WA WAUFU
Mtunzi: Maundu Mwingizi
SEHEMU YA KUMI NA NNE
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Masu/Ng’ombe alilia kwa sauti kubwa ya uchungu ambayo iliotoka kama ilivyo kwa Ng’ombe wengine wanaokua machinjioni, Hunudu akasogea na kisu chake kisha akamshika kichwa na kuibinua shingo kwa juu, Koromeo likawa liko mbele likisubiri kisu
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
Wakati Hunudu ndo ananyanyua kisu achinje ghafla kikazuka kimbunga kikubwa sana, Kimbuka kilichoambatana na upepo mkali kupita kiasi, vumbi likatinga vilivyo eneo lile, watu wakainuka na kujificha sura zao kuhofia mchanga kuwaingia machoni, wengine walijigeuzia kwenye kuta za nyumba ili kuupisha upepo huo mkali upite, Kimbuka hiki hakikua cha kawaida kabisa maana kilichukua muda mrefu eneo moja tu pale pale msibani, mpaka baada ya dakika kama tano kimbunga kikaisha na kutoweka kabisa, vumbi likapungua, watu wakawa wanajifuta mchanga machoni, Vijana waliokua wameinama kumshika Ngo’ombe nao walikua wamesambaratika kwa Kimbunga kile kilichoacha gumzo pale msibani, baada ya hali kutulia watu wakarudi kukaa kwenye majamvi na wachinjaji nao wakarudi kuchinja, Hunudu alionekana kubadilika sura yake kwa jazba, ni kama vile ameshagundua kua hali haikua ya kawaida kabisa, Vijana wakasogea na kumshika Ng’ombe tena kwa mara nyingine ili achinjwe, sasa awamu hii
hata kabla Hunudu hajainama na kisu chake Kikazuka tena Kimbunga kikali kuliko kile cha awali, watu wakataharuki tena, kama ilivyo kawaida ya Vimbunga hua vinazunguka kwa mtindo wa duara huku kikihama sehemu moja kwenda nyingine, basi Kimbunga hiki kikahama na kusogea mpaka kule anapotaka kuchinjwa Ng’ombe/Masu kikazunguka eneo lile mpaka wachinjaji wakasambaana kisha Kikafuatiwa na Tetemeko kubwa sana la ardhi, baada ya sekunde kadhaa kimbunga kikasambaa kwa kuelekea juu!!!
TOBAA!!
Kimbunga kikampita Ng’ombe na kupeperuka nae juu ya anga, baadhi ya watu waliokua wamefumbua macho yao walishuhudia tukio lilela ajabu na la kuogofya sana, wakajaribu kuoneshana juu kabisa jinsi Kimbunga kinavyoondoka na Ng’ombe mzima, watu wakaanza kukimbia kwa woga, hakuna alieamini tukio lile la kustaajabisha, na baada ya sekunde chache hali ikatulia na upepo ukapoa na kurudi kama ilivyokua mwanzo, Kina mama wengi walitoka uani mpaka barabarani kuja kushuhudia kilichotokea kufuatia kelele zilizokua zikiendelea huku Barabarani
“Imetokea nini?” Aliuliza Bi mkbwa mmoja wa makamo hivi
“Tangu nizaliwe mpaka natoka mvi zote hizi sijawahi kushuhudia muujiza kama huu” alijibu mzee Kabango huku akiwa bado anaangalia juu ambako Kimbunga kimepotelea huko
“Nini hasa kimetokea sasa?”
“Ng’ombe amebebwa na kimbunga kimemchukua na kupotelea nae juu”
“Maajabu haya jamani” kila mtu alieshuhudia tukio lile alikua akiwasimulia vijana wenzie alichokiona
“Hapa kuna kitu tu sio bure, haiwezekani kila tukianza tu kumchinja Yule Ng’ombe kinazuka kimbunga, mara kimeibuka na kumpitia kabisa ng’ombe” alisema mmoja kati ya wale viajana waliokua wameinama kwa ajili ya kumshika vizuri Yule ng’ombe
“Halafu jamani si mnakumbuka Yule mtoto aliekua analia anasema tusimchinje baba yake, sasa ndo naanza kupata picha kamili”
“Halafu baba yake na huyo mtoto ni Masu huyu aliekua na marehemu huko porini na amepotea hukohuko”
“Jamani hapana, hili sio jambo la kufumbia macho”
Judith, mke wa Masu alikuwepo pale nje akisikiliza mkasa mzima hivyo akawa analia kwa uchungu mkubwa baada ya kuanza kupata picha kuwa inawezekana ni Mume wake huyo aliekua anataka kuchinjwa
“Kwani huyo Ng’ombe mlimnunua wapi?”
“Mimi hata sijui alinunuliwa wapi, itakua ni machinjioni tu” Watu walizidi kumiminika pale msibani, wengine walikua wanatokea maeneo ya mbali sana, nao walifika kufuatia kusambaa kwa taarifa hiyo ya ajabu kua Ng’ombe amebebwa na Kimbunga, Wazee wenye hekma walijitahidi kuwatuliza watu na kujaribu kuwafanya walichukulie lile jambo ni la kawaida tu ukizingatia pale ni msibani na hata maiti angali hajahifadhiwa bado, japo ilikua ngumu kueleweka ila kwa kiwango kidogo walijitahidi kuituliza hali ile na watu wakarudi kwenye utulivu uliokuwepo, japo stori zilizoendelea kutawala ni hizo tu
*****
Nje ya kituo cha Polisi cha Msimbazi alikua amesimama Sheikh Jabu akiwa amefanikiwa kumuwekea dhamana mke wa Mzee Kikoko, na sasa alikua akimpa habari zote za Mkasa wa Masu na kifo cha Mzee Kishindo, Japo mama huyu hakuonesha kushtuka kabisa kutokana na habari hizo, zaidi mama huyu alikua akiulizia hali ya mumewe tu
“Kwahiyo huko Ddodoma unaenda na nani?”
“Ninaenda peke yangu, we nakuchukulia bodaboda uende nyumbani ukaoge halafu uwahi msibani”
“Hapana mimi sitakwenda huko msibani kabisa”
“Shemeji kwanini usiende, hivi hauoni utaleta picha mbaya sana kwa jamii?”
“Hapana Sheikh Jabu, kumbuka kwamba ni majuzi tu marehemu aligombana na mume wangu nasikia mpaka wakapigana na mikia ya taa, halafu Mzee Kishindo ameng’ang’ania kumlaghai Masu, na sasa amefariki katika mazingira ya utata hivyo naweza kufika pale nikaonekana mimi ndio muhusika”
“Kwanini ujishuku kua umehusika, Shemeji jaribu kujifikiria mara mbili” Baada ya majibizano hayo wakaagana Sheikh Jabu akaenda kutafuta gari ya kumpeleka Dodoma kumuangalia swahiba wake na huku mke wa Kikoko akachukua bodaboda iliyompeleka moja kwa moja mpaka nyumbani kwa Sheikh Jabu ambako ndiko alikofikia
*****
AKIWA njiani kuelekea stand ya mabasi ya UBUNGO kwa ajili ya kuangalia kama ataweza kupata usafiri wa gari ndogo inayokwenda Dodoma, simu yake ikaita, kwakua alikua barabarani na anaendesha pikipiki hivyo hakujishughulisha kuipokea wala kuingalia, lakini mtetemesho aliouweka kwenye simu yake hiyo wakati wa muito ulimtoa katika umakini wa uendeshaji akajikuta anakosa utulivu kabisa, na kwakuhofia kusababisha ajali ikabidi apaki pembezoni mwa barabara ili aiangalia simu yake apate kumtambua huyo anaempigia simu, alipoitoa simu yake na kuiangalia ilikua ni namba mpya, akabonyezo kitufe cha kupokelea kishaakai lengesha spika ya simu hiyo katikati ya sikio lake la kushoto
“Hallo..”
“Sheikh Jabu?...” ilikua sauti ngeni kidogo kwake, hakuweza kuitambua vema
“Naam, ni mimi, we nani?”
“Mzee Kabango hapa naongea”
“Ndio Bwana mkubwa, kuna usalama?”
“Hakuna usalama, uko wapi sasa hivi?”
“Mie niko njiani naelekea Stand ya mkoa, mbona unanitisha?”
“Fanya hima urudi kaka, mambo yameharibika huku”
“Bwana Kabango, nilikuambia tangu mwanzo kua jukumu la hapo nyumbani ni la kwako sasa mimi nije kufanya nini tena! Hapa najitahidi kumuwahi Bwana Kikoko hali yake ni mbaya huko”
“Najua hilo, lakini mpaka nimekupigia ujue maji ya yametufika shingoni, Chondechonde fanya hima uje kila mtu anakusubiri wewe hapa” Simu ikakatwa ghafla na kumuacha Sheikh Jabu akibaki njiapanda asiejua pa kwenda, Hali ya Kikoko ilizidi kumtia hofu, huku msibani nako kuna umuhimu sana, alitafakari kwa kina mwishowe akaamua kurudi tu kule msibani ili akapate taarifa ya kilichotokea
*****
Huko msibani watu sasa walikua wametulia kidogo, utulivu ulirudi katika hali yake, na sasa watu wote waiofurika kuja kuangalia ule muujiza wa Ng’ombe kubebwa na Kimbunga walianza kusambaa na kuifanya idadi ile ya mwanzo ya wafiwa kurudi kama ilivyokua awali, Hunudu alitoweka katika mazingira ya ajabu sana kiasi cha kuacha maswali kwa watu wengi pale msibani maana kila walipomuangaza hawakumuona tena, na hata hivyo hakuna aliekua akimjua pale msibani. Pikipiki ya Sheikh Jabu iliingia pale msibani na haraka haraka akaigesha chini ya uga uliosukwa vizuri kwa nyasi kisha akajongea mpaka pale kwenye Jamvi kubwa la rangi ya kijivu, Baada ya kuwasalimu aliketi chini na kumfanya sasa Mzee Kabango aliekua amejilaza kama mtu aliekimbia kilometa kadhaa ainuke na kuketi huku wakiwa wametazamana
“Naam bwana mkubwa nimetika wito..” Baada ya Sheikh Jabu kufungua mazungumzo mzee Kabango alikohoa kidogo nae akaanza kushusha mtiririko wa kisa kizima kilivyokua mpaka mwisho, Kisa hiki kilimuacha mdomo wazi Sheikh Jabu, licha ya ujasiri ambao hua ndio vazi lake kuu lakini kwa hili aliingiwa na baridi ya hofu, watu kadhaa walijisogeza karibu pale kujaribu kuchangia mada
“Huyo aliyekua mchinjaji yuko wapi?”
“Ametoweka tu na hakuna aliemuona wakati anaondoka”
“Mnajua kweli huyo?”
“Hapana ila cha ajabu wakati tunataja wajih wake kuna Binti mmoja alishutuka sana akasema kua anahisi kumjua huyo mtu”
“Ni nani huyo binti?”
“Wanamuita Mama Zani..”
“Mmh Judith? Mke wa Masu?, Amemjuaje?”
“Anadai kua mumewe alikua akisumbuliwa sana kwenye Ndoto ya ajabu, na katika sifa za huyo mtu aliekua akimuota kila siku ndo huyo kijana mwenye Jicho bovu, sasa ukijumlisha na utata wa hili tukio la leo ndo kabisa ameamini” Kisa hiki hakika kilizidi kuacha maswali mengi yasiyo na majibu, Lakini kwa Hekma na Busara ikabidi Sheikh Jabu awatulize watu pale msibani kwa kuwanasihi kwa maneno ya busara sana mpaka wakatulia, akawaomba kwanza washirikiane kulimaliza suala la mazishi halafu hayo mengine yatapata muda wa kutosha wa kuyajadili, watu walimuelewa na sasa Shughuli za kuandaa mazishi zikaendelea kama kawaida, Ikabidi sasa bila ya kupenda Sheikh Jabu asisafiri tena na badala yake abaki pale nyumbani ili kukabiliana na matatizo yatakayojitokeza
Ilipotimu saa tisa alasiri watu walikusanyika nje ya nyumba ya Mzee Kishindo kwa ajili ya kufanya Ibada ya visomo maalum kama dua ya mwisho kwa marehemu wao, hakika watu walikua wengi kuliko kawaida, bila shaka wapo waliohudhuria kutokana na uvumi tu uliojitokeza wakati wa tukio lile, Naam Dua zilifanyika kwa ukimya na utulivu mkubwa tofauti na misiba mingine, Hatimae Mwili wa marehemu ukawekwa ndani ya Jeneza tayari kwa ajili ya kuswaliwa kisha kwenda malaloni kumuhifadhi.. Ikafanyika Sala ya Maiti iliyoongozwa na Sheikh Jabu mwenyewe, mbali ya ukaribu wake na marehemu pia Sheikh jabu alikua ni msomi mzuri tu na mjuvi wa masuala dini, Baada ya kumaliza swala hapakua na cha ziada tena maana hata chakula hakukuandaliwa tena tangu Ngo’mbe apotee ghafla, hivyo wanaume wakanyanyua Jeneza na kuliweka katikati ya mabega na shingo zao kama ilivyo kanuni na taratibu za ubebaji wa Jeneza, na safari ya mwisho ya hayati Kishindo ikawa inakaribia kufikia tamati
Makaburini hapakua mbali sana na nyumbani hivyo safari ya mwendo wa miguu tu ilitosha kuwafikisha katika viwanja hivyo vya makaburi ndani ya muda wa kama nusu saa hivi, na taratibu zote za mazishi zikafanyika na hatimae Kishindo akazikwa, ilikua ni huzuni na vilio kila kona, vijana kwa wazee walishindwa kuzificha huzuni zao na kuangua vilio hukohuko makaburini
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni