Mtunzi: Maundu Mwingizi
SEHEMU YA SITA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Huku Buguruni nako Judith alikua peke yake Chumbani analia tu kama mwehu, alikua akiuumizwa sana na matatizo yanayoendelea kutokea ndani ya familia yake na Masu, alikua hata hajui Masu atakua wapi muda ule wa usiku, kama atakua mzima au Laa, na zaidi kila alipowafikiria wazazi wa Masu walivyomzushia kua kamroga mtoto wao ndio kabisa alihisi kuchizi lakini hakua na Jinsi zaidi ya kumuomba Mungu amuoneshe njia, nae alilala tu bila matumaini huku akitia nia kesho yake kwenda kumtafuta hovyo hovyo mumewe
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
Saa kumi na moja alfajir Mzee Kikoko aliamka kwa ajili ya kusali kama ilivyo kawaida yake, akatoka nje kwa ajili ya kuoga na kujiandaa na swala, hakutaka kwenda msikitini aliamua tu kua ataswali pale pale nyumbani, Alipomaliza kuoga akatoka mpaka pale uani ndipo akamuonaSheikh Jabu akipigwa mswaki akamsogelea na kumsabahi
“Assalamu alaykum”
“Owhoo bwana Kikoko waalaykum salaam, habari za Shinyanga?”
“Nzuri tu Sheikh, nawe za Tabora huko?”
“Huko hawajambo, poleni tu na matatizo?”
“Aaah bwana hivyo hivyo tupo nayo”
“Nasikia umekuja na mama Masu..”
“Ndio, yuko ndani humo bado amelala”
“Vizuri nitamsalimia kukipambazuka, Enhee nasikia tena ikawa mambo ya aibu huko Amana hospital… kunani tena mzee mwenzangu?”
“Unajua Yule mwanamke wake na huyo Masu ni mpuuzi sana, pamoja na Kishindo nae ndo wale wale, hapa hata mwanangu sijui yuko wapi” Kikoko alianza kufunguka sasa, Sheikh Jabu akaona yatakua makubwa ikabidi amkatishe
“Sasa mi nadhani tukaswali kwanza halafu we ukapumzike tu kasha tutaonana kule Dukani ndo tutaongea vizuri”
“Haya hakuna tabu” Kikoko akaingiachumbanikwake, huku nyuma Sheikh Jabu alikua amechia tabasamu la mamba huku akimuangali alwatan Kikoko akiingia chumbani kwake
Baada ya swala tu Shekhe Jabu hakukaa tena akaondoka zake nakuelekea mjini alikua na miadi na mtu maeneo ya dukani kwake Kariakoo, lakini Kikoko yeye alirudi kulala akivuta muda kupambazuke vizuri ili baada ya kupata ‘Istiftahi’ yaani kifungua kinywa ndipo nae aende kwanza dukani akaongee na Sheikh Jabu halafu zoezi la kumsaka Masu lianze
*****
Majira ya saa nne asubuhi tu tayari duka la Sheikh Jabu lilikua limefurika, wengi walikua wameenda kuzungumza juu ya balaa liliotokea jana yake kule Amana hospital maana tayari taarifa zilkua zimeshafika pale, na kwakua Jabu hakuwepo Dar hivyo kila mmoja alifurahi kuonana na kuzungumza na Sheikh Jabu, muda si mrefu Mzee Kishindo nae aliwasili pale dukani akapokelewa vizuri na Sheikh Jabu na baada ya kuketi tu nae akaanza kuwapa mchapo kuhusu mikwara aliyopigwa na Mzee Kikoko juzi yake kupitia simu, Sheikh Jabu alikua akicheka mpaka machozi
“Unajua Yule Bwana Kikoko hua simuelewi kabisa yaani anazeeka na upuuzi wake ha ha ha..” alichombeza sheikh jabu
“Nakwambia jana ungemuona alivyoingia hapa na ule mustache wake kama AmrishPul ungepasuka mbavu” wakati wadau wakiendelea kupashana habari za udaku na ufyetere ghafla kwa mbaali akaonekana Alwatan Kikoko akivuka barabara na kuja usawa wa dukani
“Jamani Kikoko huyo anakuja..”
“Hebu badilisheni mada msije kutuletea songombingo hapa” wadau wakajifanya wanajadili suala la Katiba mpya anayoendelea kuandikwa huko Bungeni, Naam Kikoko akawasili
“Karibu Alwatan Kikoko..” Sheikh Jabu alimpokea
“Shukrani.. Assalamu alaykum”
“Waaleykum salaam, karibu uketi hapo kwenye kiti chako cha uvivu” wakati anasogea kwenye kiti akakutanisha macho na Mzee Kishindo
“Hapana nimeghairi, wala sikai tena kuna Mchawi humu ndani”
“Acha mambo yako bwana Kikoko mchawi gani tena?”
“Si huyu Kishindo, ninyi hamjamjua tu kua ndie anaemroga mwanangu huyu?”hapohapo Mzee Kishindo uzalendo ukamshinda akajibu
“Tafadhali bwana Kikoko naomba heshma iendelee kujizungusha katika mhimili wake”
“Kwahiyo we ni kidume sana? Haya inuke tupambane”
“Naam mie ni Kidume tena Rijali haswaa, na ni baba wa Watoto watato”
“Mpuuzi mkubwa wewe mwanaume mzima unajisifia kua na watoto watano, njoo kwangu uone timu ya mpira, na leo bora nimekukuta hapa unieleze sababu za kumroga mwanangu halafu wewe huyo huyo unajifanya eti utamsaidia”
“Mie nimroge mwanao kwa lipi? Leo unajifanya humjui mchawiwako eeeh?Au nimwage mchele kwenye kuku wengi?”
“Mwaga huo mchele, Kuku wakiula basi nawao usiku tutawala kwa wali, mzandiki mkubwa wewe”
“Sikia bwana Kikoko, mie ni mtu mzima sasa hizo hila na shari unazonitafuta nimeshazijua kitambo kirefu tu ila kaa utambue kua Chiriku mzee hakamatwi kwa makapi..”
“Unajifanya muungwana sasa baada ya kulikoroga, kwahiyo ulizikaanga Bisi halafu unataka kuwaachia wenye meno watafune si ndio? Sasa nakwambia hivi utanionesha alipokwenda mwanangu mwanga mkubwa wewe, Laa sivyo humu leo hatoki mtu kama Airtel money”
“Tafadhali bwana mkubwa chunga ulimi wako, Kumbuka kua Cheche huchoma msitu na ulimi uliponzakichwa, jambo dogo sana unalolidharau lizaweza kukuletea madhara makubwa katikamaishayako..”
“Utanifanya nini wewe? Mie ndio Alwatan Kikoko nitakuhamisha mji huu”
“Debe tupu halichikutika, najua siku zote debe likiwa halina kitu ndani yake basi hata likidondokewa nakitu kidogo kamap punje ya haradani litapiga kelele tu ila debe lililojaa hata unga laini wa azam halitotoa kelele hata ulipige teke, sasa we Debe tupu endelea kupiga kelele tu”
“Unaleta dharau sio? Ngoja nikuoneshe..” Kikoko akavua mfuko mdogo aliokua ameuning’iniza begani ili amvae sasa Mzee Kishindo, yaani Kikoko alikua amejawa shari mwili mzima, watu wote dukani walikua kimya ikabidi sasa Sheikh Jabu aingile kati
Jamani wazee wenzangu hebu muogopeni mungu, angalieni sasa mnajenga picha gani kwa vijana wadogo hawa mbele yenu!!” Kwakua Kikoko hua anamuheshimu sana Sheikh Jabu akashusha pumzi kidogo kasha Seikh Jabu akaendelea
“Wahenga wanasema Chungu kidogo huwahi kuchemka wakati chungukikubwa huchelewa kuchemka wakiwa na maana kua Kichwa kidogo kwa maana ya uchachewa hekma , busara, na maarifa huwahi kuchemka hata kwa mambo madogo tu, sasa wazee wenzangu mnashindwa kutumia hekma zenu kulimaliza jambo hili bila tafrani ukizingatia umri wenu umekwenda sana na wanasemakua ukimuona NyaniMzee ujue kakwepa mishale mingi sana”
“Kwahiyo Sheikh Jabu unamaanisha haya mambo ni madogo wakati mie mwanangu amerogwa na tayari nimeshambamba mchawi wangu ukizingatia mpaka sasa sijui mwanangu amepotelea wapi” alidakia tena Kikoko
“Hapana sina maana hiyo, nina maana ya kwamba kwa tatizo hili ilikua vema mkakaa kama watu wazima nakulimaliza, naamini katika maisha mmeshakutana na changamoto nyingi kuliko hii”
“Mie siwezi Kukaa na huyu fatani na hasidiwa maisha yangu”
“Usiseme hivyo bwana Kikoko kumbuka kua Dhoruba iliko ndiko shwari iliko bimaana kua wagombanao ndio wapatanao, lazima tuliongee na limalizike kwa salama jambo hili”
wakati Sheikh Jabu akiendelea kuwanasihi wazee wenzie kwa mbali wakasikia wimbo wa Mwanameka ukitokea katika Mfukowa Koti wa Mzee Kikoko, ilikua ni simu yake ikiita alipoitoa akaona ni namba ya Masu, mojakwa moja akajua ni Mke wa Masu tu huyo
“Enheee hongea upese na wewe mchawi namba mbili”
“Baba shikamoo” Ilikua ni sauti ya Masu
“Marahaba, we Masu uko wapi?”
“Niko kwangu”
“Ulikua wapi tangu jana sie tunakutafuta”
“Nililala nyumbani kwa Boss wangu”
“Nakuja huko sasa hivi” Mzee Kikoko akakata simu kasha akatoka bila hata ya kumuuaga mtu yeyote na kuanza kuelekea kwa Masu,
Huku nyuma aliacha gumzo kubwa na vicheko vya hali ya juu kwa wadau pale dukani japo Mzee Kishindo alionekana kutokuana furaha kutoka na majibizano yale
****
BUGURUNI KWA MNYAMANI
Masu alikua amejilaza kitandani akionekana ni mwenye mchoko wa hali ya juu huku kichwa chake akiwa amekilaza juu ya miguu Mkewe Judith, halafu kwa pembeni walikua wamekaa watoto wao wawili mapacha Zani na Fani ambao hawakuelewa chochote kinachoendelea kutokana na udogo wa umri wao,
“Yaanimimi nahangaika hivi na wewe halafu wazazi wako wananitukana na kunidhalilisha mbele za watu kiasi kile..”
“Nisamehe mimi mke wangu, wala usiwalaumu wale, uzee umeshawaingia”
“Hapana ni bora nikakuacha uendelee kuishi na wazazi wako kwa amani kuliko haya mateso nayoanza kuyapata, yaani wananiita mimi mchawi”
“Judith yaani uondoke kisa Baba yangu? Kama mimi na wewe tumependana hakuna wakututenganisha zaidi ya Mungu, kumbuka mwanzo wakati tunataka kufunga ndoa ya kiserekali alinikataza na kunitishia kunitolea radhi lakini niliongea nae na yakaisha sembuse hili”
“Haya kwanini na jana ukakimbia hovyo a ukenda kulala kusikojulikana? Una jua mie nilibaki katika hali gani?..” wakati wanaendelea na mazunngumzo wakasikia sauti ya mlango ukigongwa
“Ngo! Ngo! Ngo!..”
“Ngo! Ngo! Ngo!..”
Judith akainuka kitandani na kwenda kufungua mlango, alipofungua tu akakutana na Sura ya Alwatan Kikoko akiwa amenuna vibaya
“Karibu baba” Kikoko hakujibu kitu akaingia mpaka ndani na kumkuta Masu akiwa amejilaza pale kitandani
“Karibu mzee”
“Ahsante” Kikoko akavuta kistuli karibu na kitanda alichojilaza Masu halafu akakaa nae, hapo hapo Zani na Fani wakamsogelea Babu yao na kumkalia miguuni. Mazungumzo yakaendelea
“Enhee unajisikiaje?
‘Naendelea vizuri kiasi”
“Mwanangu umeamini kinywa cha mzazi hakitoi harufu mbaya bali kinatoa maneno ya Baraka?”
“kivipi Baba?”
“Wakati unataka kumuoa huyu mwanamke mie na mama yako si tulikukataza wewe hukusikia sasa si unaona mabalaa hayo?”
“Sasa baba lakini haya matatizo yanahusiana nini Judith?”
“We umesharogwa huwezi kujitambua, tuulize sisi tulioko pembeni, sasa sikiliza mimi sitaki tena kukuona ukiwa na huyu mwanamke, hawa wanao nitaondoka nao nitaenda kuwalea Shinyanga..”
“Lakini baba…”
“Lakini nini? Nimeshamaliza, kwanza Hebu amka ukaoge tuondoke mara moja nikupeleke kwa sheikh Jabu”
Masu akainuka akatoka mpaka nje akamuambia Mkewe ampelekee maji bafuni akaoge, Judith akachukua ndoo ya maji mpaka bafuni kisha Masu akafuata, Masu akaanza kuoga kama kawaida,
Wakati huo huku chumbani Mzee Kikoko akiendelea kucheza cheza na wajukuu zake, lakini Judith akaamua tu kukaa zake nje maana aliona sasa tayari bwawa limeshaingia Ruba. Akiwa Bafuni Masu akijipaka sabuni, tayari alikiwa na mapovu mwili mzima ghafla alisikia mlango akigongwa, akajiuliza huyu nani tena?!
Ikabidi ajimwagie haraka maji usoni ili atoe mapovu, alipomaliza akafumbua macho HAMAD!! Alipigwa na butwaa, alijiona yuko katika Bafu, zuri na la kisasa tofauti na kule alikokua akioga, akawa hajitambui kua yuko wapi, akaanza kutetemeka, alipojiangalia vizuri akajigunduakua alikua sio Masu tena, alikua amebadilika kabisa maumbile yake na sasa alionekana kama mwanamke mzuri na mrembo hasa, Masu alizidi kuchanganyikiwa, akajiangalia zaidi ya mara mbili, vile vile akiwa ni mwanamke kabisa tena alieumbika kike
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi