Mtunzi: __
SEHEMU YA AROBAINI
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Alikuwa akinyata kwa kweli. Kweli hata mimi nilimkubali tu siku ya kwanza ingawa bado nilikuwa sijajua ufanisi wake wa kazi.
Nilikaa nae hapo kwangu kwa mda wa siki tatu huku asubuhi tukiamka na kuendelea na kazi.
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI
TUENDELEE...
Ndani ya mda huo nikagundua kuwa alikuwa na uzorfu mkubwasana hivyo kazi hiyo alikuwa akiimudu kabisa.Hapo sasa nilimkubali sana Mark na ile kauli yake kuwa yeye huwa hafanyi makosa katika kufanikisha jambo alilodhamiria.
Basi nilitumia mda huo vizuri kuweka mambo yangu sawa ili nikienda Dar niyaache yakiwa shwari kabisa.Niliamua kwenda Arusha kumsalimia yule mtoto wa
Joyce ambaye alikuwa akisoma shule ya boding.Pia nilimtafuta baba yake nikamsalimia na kwa kuwa niliongozana na Mark basi nilimtambulisha kuwa huyo ni mume wangu.Tulimaliza shughuli za huko na tulirudi zetu moshi tayari kwa kuondoka na kuelekea Dar es salaa. Sikusita pia kwenda kumsalimia mama yake mdogo na Joyce ambaye kwa sasa ndo nilikuwa namchukulia kama mama yangu na kila mwezi nilikuwa nikimtumia hela ya kula.Na yeye nilimtambulisha kwa Mark na kumuelezea nia yetu ya kutaka kuona
Tupo ndani ya Dar es salaama jiji la maraha na karahaa. Maisha mapya yameanza huku mimi na Mark tukiishia kama mke na mume lakini kamwe alikataa kushiriki tendo la ndoa.Kila siku alisisitiza kuwa tutaenda kupima afya lakini ikifika siku hiyo Mark huwa anajifanya yupo bize hivyo tuliendelea na maisha ya kila siku ya kutafuta hela.Mark alitumia mda wake mwingi sana kunitambulisha mimi kwa marafiki zake na ndugu zake. Mark alinifanyia tena kipart cha kunivalisha pete kama kile alichonifanyia Dar es Salaam na safari hii licha ya marafiki zake pia walikuwepo ndugu zake na wazazi wake.Hii sasa ndo naweza kusema kuwa ndo ilikuwa ni Engagement Day kwa sababu hata mama mdogo wa Moshi tulimtumia nauli kuja kushuhudia swala hilo.
Pia Waridi yule dada wa saloon alikuja na Marry pia yule mdogo wake Joyce hivyo hao ndo walitambulishwa kuwa ni ndugu wangu.Sikuwa na jinsi kwa sababu kwa kweli nilikuwa sina ndugu zaidi ya hao hivyo nilikubaliana na matokeo.Baadaye wote hao walirudi Moshi tenalkwandege hivyo kuwatengenezea historia maana hakuna hata mmoja aliyewahi kupanda ndege.Hapo sasa nikawa na uhakika kuwa Marka atanioa.
Tulianza kufanya kilichotupelaka Dar es salaam si unakumbuka pia pamoja na mambo ya kuwajua ndugu jamaa na marafikia lakini pia ilikuwa ni kwa ajili kucheza ile movie ya LET ME LOVE YOU.Mark alianza kunifundisha vitu muhimu ninavyotakiwa kuvijua kabla ya kuiingia kwenye tasnia hiyo ya filamu ikiwa ni pamoja na kunipeleka kwa mwalimu wa wa chuo cha sanaa cha kaole ambacho kipo bagamoyo. Mwalimu huyo nilikutanishwa naye ili aweze kuniambia vitu muhimu vya kuvijua na kuvifanya kabla sijaingia kwenye tasnia hiyo ya filamu.Nakumbuka swali la kwanza aliloniuliza mwalimu huyo ni je nilishawahi kuwa a ndoto ya kuigiza fialmu hapo kabla?Nilijibu swali hilo kwa harakaharaka kuwa ndio nilishawahi kuwa na ndoto hiyo na ndoto hiyo imechagizwa na kutiwa chachu na Mark.
Kama kweli una ndoto hiyo kitu cha kwanza na cha muhimu kukijua ni kwamba ndoto hiyo ili ifanikiwe na kuwa kweli ni lazima niwe tayari kujitoa, kujifunza na kutenga mda mwingi kwa ajili ya kazi hiyo na pia niwe na shauku ya kujua mambo muhimu yanayohusu tasnia ya filamu. Akanambia kuwa wapo watu wengi wanaifanya kazi hiyo lakini hawahifanyi kwa ufanisi kwa sababu hawana mafunzo na hawataki kujifunza. Ujue kipaji ni asilimia chache sana zinazomfanya mtu awe muigizaaji bora aliendela kusema mwalimu huyo. Aliongeza kuwa juhudi na bidii ya kujifunza na kujua mazingira yanayokuzunguka ili kuweza kucheza filamu ambayo itagusa maisha ya jamii inayokuzunguka ni jambo la muhimu sana.
Nilitega sikio kwa umakini ili kumsiliza mtaalamu huyo amabye alikuwa pia ni professor wa mambo ya sanaa. Basi akaendelea kunielezea vitu vichache vya kuzingatia labla ya kuwa muuigizaji. Hatua muhimu aliyoniambia ni “Learn How to Act”(jifunze jinsi ya kuigiza).Siku zote ni muhimu kujifunza kama unataka kufanikiwa kiurahisi.Kwa hiyo alinishauri kama nina mda basi niende kusomea fani hiyo iwe kwa kozi fupi au kwa semina.Kitu cha pili alichokisisitiza ni location. Alinambia kwa kimombo kuwa “if you hope to work in film as an actor you need to go where the work is. Hapa alikuwa na maana kwamba kama napenda kuwa muigizaji wa filamu ni vizuri nikaenda kuishi sehemu ambapo kazi hizo zinafanyika kwa urahisi.Alinitolea mfano kuwa filamu nyingi za Canada na miji mingine ya Marekani zote zinachezwa Los Angles na New York.Kwa hiyo alisisitiza kwa Tanzania Dar es salaam tayari imepiga hatua katika tasnia hiyo na filamu nyingi zinafanyika Dar es salaam.
Hatua muhimu aliyoniambia ni “Learn How to Act”(jifunze jinsi ya kuigiza).Siku zote ni muhimu kujifunza kama unataka kufanikiwa kiurahisi.Kwa hiyo alinishauri kama nina mda basi niende kusomea fani hiyo iwe kwa kozi fupi au kwa semina.Kitu cha pili alichokisisitiza ni location. Alinambia kwa kimombo kuwa “if you hope to work in film as an actor you need to go where the work is. Hapa alikuwa na maana kwamba kama napenda kuwa muigizaji wa filamu ni vizuri nikaenda kuishi sehemu ambapo kazi hizo zinafanyika kwa urahisi.Alinitolea mfano kuwa filamu nyingi za Canada na miji mingine ya Marekani zote zinachezwa Los Angles na New York.Kwa hiyo alisisitiza kwa Tanzania Dar es salaam tayari imepiga hatua katika tasnia hiyo na filamu nyingi zinafanyika Dar es salaam.
Kitu kingine cha muhimu alichonambia ni kwamba niwe tayari kujitoa kwa ajili ya kazi hiyo na niwe tayari kupoteza hata marafiki ili mradi tu nifanikiwe. Hapa alisisitiza kuwa lazima nifanye kazi kwa bidii sana kwa sababu hata wacheza filamu maaraufu ambao wanalipwa vizuri sana kwenye matangazo lakini bado hawalali na kubweteka.Alimaliza kwa maneno machache ya kiingereza kuwa kama nataka kufanikiwa basi nahitaji time(mda), training(mafunzo). Dedication (kujitoa), passion and patience( shauku na uvumilivu).Basi niliagana na mwalimu huyo ambaye kwa kweli alinijenga kisaikolojia na kujiona ni mtu ambaye niyaweza yote aliyosema kwa uwezo wa Mungu muumba mbinu na vyote vilivyomo.
Baada ya hapo Mark akaendelea kunifundisha jinsi ya kucheza na kamera pindi tunapochukua picha za filamu.Uzuri kichwa changu kilikuwa ni chepesi sana ambacho kilikuwa kinauwezo wa kushika mambo kwa urahisi zaidi.Katika mda mchache nilikuwa nimeshapiga hatua kubwa sana na nilishaweza kuigiza baadhi ya matukio ambayo nilikuwa napewa kama majaribio.Mark alitumia filamu zake zilizopita kunifundisha na alikuwa akijaribu kunipa sehemu zile ngumu niingize. Neno lake kubwa lilikuwa leo nataka ugize kama fulani kwenye filamu fulani, kisha ananipa hiyo part na naiangalia kisha naifanya.Mark alifurahishwa sana na uwezo wangu hasa kwenye vile sehemu za burudani na kuwafurahsha watu.Kwa hiyo kipaji changu cha kucheza mziki kipaji changu cha kucheza na hadhira jukwaani vyote vilinisaidia kuimudu sanaa fani hii ya filamu.
Lilian Muchuma disgner na mwanamitindo maarufu wa nchini Zambia naye alitokea kunikubali sana na alijitolea kuwa ananivalisha mavazi yake na kutengeneza brand mpya ya biashara ambayo iliendelea kunipa umaarufu sana kupitia mitandao ya kijamii. Jamii ya Watanzaia ikaanza kunikubali na umaarufu ukaanza kuja.Magazeti ya udaku nayo hayakuchoka kumuandama Mark wangu kwa madai kuwa anatoka na mzambia. Watanzania wengi hawakujua kuwa mimi ni mtanzania kwa sababu ya Lilian Muchuma, wao walijua kuwa mimi ni mzambia ambaye tupo share na mwanamitindo huyo ambapo eti mimi niliamua kujikita kutafuata masoko upande wa Tanzania.
Mark naye alitumia nafasi hiyo vizuri kwani aliniambia kamwe nisiweke ukweli wowote kuwa mimi ni mtanzania au ni mzambia.Maisha yakaendelea huku tukiwa kwenye mikakatai ya kuitoa ile filamu yetu ya “LET ME LOVE YOU”.Katika filamu hiyo pia tuliamua kumuweka Lilian Muchuma ili tupate pia wateja wengi kutoka nchini Zambia. Lilian yeye alicheza kama mwanamke wa kwanza kuolewa na Mark tena kwa ndoa kubwa. Lilian kwenye filamu hiyo alionekana kama msichana ambaye Mark alimpenda sana pengine kuliko kitu chochote duniani.Lakini filamu hiyo ilionesha kuwa Lilian ni binti ambaye Mark alimtoa kijijini akiwa ni mshamba kupindukia.Utamu wa fiamu hii ni kwamba matukio mengi yalichukuliwa nchini Zambia ambapo tulikwenda kwa mwaliko wa mwanamitindo huyo.
Filamu hii inaonesha mara baada ya Lilian kutolewa kijijini kwao na kupelekwa Lusaka kwa ajili ya kuishi na Mark hapo ndipo kasheshe za binti huyo zinapoanzia.Binti huyo anabadilika na kulijua jiji na kuanza kumsaliti Mark.Baadaye Lilian anaanza kutoka na mapedeshee na watu maarufu nchini Zambia. Filamu inafafanua kuwa kipindi hicho Mark alikuwa ni mtu wa maisha ya kawaida sana hivyo alizidiwa nguvu na watu wenye uwezo.Dhuluma hiyo ya mapenzi ndo inamfanya Mark kuyachukia mapenzi na kuanza kutafuta hela kwa nguvu huku akiaamini kuwa ndo kitu pekee kinachoweza kurudisha furaha yake iliyopotea.Katika harakati zake hizo za kutafuta hela ndipo anapata dili la kuja Tanzania kufanya biashara.Mark anaonekana mkoani mbeya ambapo alikuwa akitoa vitu nchini Zambia na kuleta hapo Mbeya. Akiwa mkoani Mbeya anakutana na msichana mwingine ambaye anatokea kumepnda sana na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi.
Filamu hiyo inaendelea kuonesha kuwa mara baada ya Mark kukolea na penzi la binti huyo na kuanza kusahau maisha aliyopitia akiwa na Lilian hapo tena anapatwa na Majanga mazito mara baada ya binti huyo kumuibia mamilioni ya hela na kutoroka. Kitendo hicho cha kuibiwa fedha zake za biashara zinamrudisha sana nyuma Mark kimaendeleo na kujikuta akianza upya.Baadaye anapata taarifa kuwa binti yule yupo Dar es salaam na amekuwa tajiri sana. Mark anaamua kufanya utafiti juu ya taaarifa hizo na kuamua kwenda Dar es salaam. Anaamua kuhama mji kutoka mbeya na kwenda Dar es Salaam mara baada ya kujua mwanamke huyo mahali anapoishi.Mark anafanikiwa kuonana na mwanamke huyo lakini mwanamke huyo anamwambia hakuna haja ya kulipa kisasi anampa mara mbili ya hela alizomuibia. Mark anashangaazwa sana na mwanamke huyo lakini kwa kuwa shida yake ilikuwa ni hela anaamua kuachana nae na kuanza maisha mapya hapo jijiini Dar es salaam
Maisha yanaendela lakini Mark amekuwa tajiri na mtu mwenye mafanikio sana kiuchumi.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO