MY DIARY (45)

0
Jina: MY DIARY
Mtunzi: __

SEHEMU YA AROBAINI NA TANO
TULIPOISHIA...
Ndio niliona hipo haja ya kuokoka na kuishi maisha ya utakatifu kwa maana nishaishi maisha yote ya kuwa mbali na mungu. Nakumbuka nilipokuwa mdogo kipindi hicho naujua mlango wa kanisani tuisahawahi kufundishwa kuwa mtetezi wa kweli wa maisha ya mwanadamu ni Mungu.

Na siku zote alaaniwe mtu yule amtegemeaye mwanadamu.

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI

TUENDELEE...
Sio kazi ya mwanadamu kuhukumu lakini kama watazamaji wa shindano hilo watanihukumu kwa video hizo za uchafu ambazo sikuwa na uhakika kuwa zilishasambazwa mtandaoni au zilikuwa pale tu kwa Biggie ambaye ni Father House and Mother house wa jumba hilo.Haya mawazo yote yalikuwa ni yangu na niliumia na kujutia maisha yote mabaya ambayo nilishawahi kupitia.Lakini baadaye nilijipa moyo na kusema kuwa yote yaliyotokea yalikuwa ni mapito ya dunia hii kwa sababu huwezi kuwa imara kama hujapitia majaribu.

Hata dhahabu hupita kwenye moto ili iweze kung’ara.Wakati naendelea kuwaza mambo hayo yote nilisikia kengele kuhashiria kuwa tunatakiwa tukaongee na Biggie. Roho iliingiwa na hofu nikajua labda ndo safari yangu ya mwisho ya kutoka.Sikuelewa lakini nakumbuka jana yake tuliambiwa kuwa hakuna mshiriki yoyote atakayetolewa kwa sababu kura zetu zilikuwa zinalingana.

Tulitega masikio kwa umakini sana ili tujue nini kiongozi huyo wa jumba hilo anataka kutuambia. Hakuwa na jipya sana zaidi ya kutukumbusaha kanuni na taratibu za hapo. Alitueleza mchuano umekuwa mkali sana hivyo wameamua kuongeza siku moja ili kupata mshindi wa ukweli.

Nilifurahi maana nilihisi kuwa siku hiyo moja inatosha kabisa kubadilisha matokeo na mimi kutangazwa mshindi.Nilijua kabisa wiki hiyo moja inatosha kabisa team Leah kufanya yake.Nilijua kabisa Mark atakuwa anaendelea kunipigania kwa hali na mali kwa upande wa Tanzana pia Lilian atakuwa akinipigania kwa hali na mali kwa upande wa Zambia.

Siku hiyo moja iliyobaki ilikuwa kama mwaka mzima maana kila mtu alikuwa na hamu kubwa sana ya kutangazwa mshindi.Ilibidi wote tuungane na kuwa kitu kimoja. Mda wote tulikuwa pamoja na kulikuwa hakuna namna yeyeote zaidi ya kuwa kitu kimoja kila mtu alitamani yeye atangazwe kuwa mshindi lakini pia kila mtu alikubali ukweli kwamba mtu yeyote baina yetu anaweza kutangazwa kuwa mshindi. Mda mwingi tulikuwa tumekumbatiana kama vifaranga ambavyo vina njaa a vinaamini vitanyonya kesho.

Waswahili wanasema siku hazigandi na kama ipi ipo tu, riziki iiyopangwa na Mungu hakuna mwanadamu anayeweza kuiziba.

Huku tukiwa tumeshikana na kukumbatiana na kusubiri mshindi kutangazwa Biggie alianza kwa mbwembwe kwa kuita jina langu.Nikasogea mbele huku machozi yakinitoka nikijua kuwa nilikuwa nimeshika nafasi ya tatu.Niliambiwa nikae upande wa kulia. Alafu akaitwa mwingine akaambiwa akae uapande wa kushoto. Vivyo hivyo akaitwa na mwingine na yeye akakaa katikati.

Baada ya hapo host wa show akasema kwa bahati mbaya mwaka huu hatutakuwa na mshindi wa tatu bali……….. kabla hajamalizia kelele za shangwe zilipigwa na kuniacha nikishangaa nisijue alisema nini mpaka watu wote walioalikwa kupiga kelele za shangwe kiasi hicho.Mimi binafsi sikuelewa au alimaanisha wote kuwa ni washindi bado sikuelewa nikabaki tu nmeshangaaa. Akasema sijamaaanisha kuwa watu wote ni washindi ila nimemaanisha kuwa Mshiriki wa kushoto na katikati wote kwa pamoja ni washindi namba mbili kwa sababu kura zao zimegongana hivyo watapata kitika sawa.

Kauli hiyo iliwafanya washiriki wale wawili waende kukumbatiana.Nilibaki mimi nimesimama na kushangaa kama mtu aliyepigwa na butwaa sikujua nini kinaendelea na nihisi nilipatwa na ugonjwa wa mshangaooo.Hivyo ma bibi na mabwana napenda kumtangaza Leah kuwa ndiye mshindi wetu wa shindano hili hiyo ilikuwa ni sauti ya aliyepewa kazi hiyo..Niliendelea kusimama pale pale kabla ya machozi kuanza kunitirika sikuamini macho yangu na masiko yangu kama kweli mimi nimetangazwa kuwa mshindi wa shindano hilo.

Kelele za shangwe ziliendela huku mimi nikapiga magoti na kuinua mikono juu na kumwambia mungu asante kwa sababu ameniunua kutoka kwenye dimbwi la mkato wa tamaa mpaka kwenye bonde la Baraka.Nikiwa hapo chini nilishangaa kuona watu wawili wakiniinua kwa furaha na so wengine bali ni Mark na Lilian.NilifurahI sana tukakumbatiana kwa furaha na kuruhusu watu wangu wote wa karibu kuja kunipa pongezi na kunikumbatia.Wengine waliambiwa wasogee ili nipigwe picha za ukumbusho.Kulikuwa na wawakilishi kutoka Zambai na pia kulikuwa na wawakilishi kutoka nchini Tanzania

Nazani sasa wote kwa pamoja walishakubaliana na ukweli kuwa mimi nilikuwa na uraia wa nchi mbili.Niliweka mapozi ya kila aina ili mradi tu nipigwe picha za kutosha za kuuza kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari.Nilikua na furaha ambayo naweza kusema kuwa haikuwahi kutokea maishani mwangu.

Nilimshukuru Mungu kwa kila lililotokea mpaka nikafikia hapo na nilikuwa na furaha kwa sababu ndoto yangu moja na kubwa ya kuja kuwa superstar mkubwa sana ilikuwa imefanikiwa.

Hapo sasa wasanii maarufu wa Zambia waliapanda na kutoa burudani na pia sio hao tu bali pia wasanii kutoka Tanzania na wao walipanda na kutoa burudani.Mashabiki wote waliomba nipande na kuwapa burudani ile ambayo nilikuwa nawapa kipindi nikitafuata kura zao.Kwa kweli sikusita nilipanda na kuanza kukatika mauno.Yaani naweza kusema siku hiyo nilitoa burudani kuliko siku yoyote maishani mwangu.

Nilifanya kila kitu hapo jukwaani na kuacha watu wote wakinishangaa.Sijui na Dj alijuaje nyimbo zangu maana alikuwa anapita mule mule. Nilicheza nyimbo kama tano mfulizo za kutoka nchi mbali mbali.Nilicheza kwanza staili za nyumbani kwetu yaani Tanzania, pili nilicheza za Zambia, nikapiga za South afrka, Nigeria na Jamaika.Nia yangu ni kuwathibitishia kuwa tu hawakukosea kunipa kura zao pamoja na skendo zote zilizovumbuliwa kwa ajili ya kunichafua na kuhakikisha kuwa si shindi shindano hilo.

Hapo nilishia mike na kuruhusu mtu yeyote anajiamini kuwa anajua kucheza basi aje kunibambia. Nilifanya vitu ambavyo kwa kweli mpaka leo nashindwa kuvieleza kwa maana viliweka historia kubwa sana tofauti na mashindano yoyote ya big brother yaliyotokea.Ujue walikuwa wamezoea kwamba burudani nyingi zilikuwa zinatolewaga kabla ya mshindi kutangazwa na baada ya hapo mshindi huwa anatoweka mara moja na kupotea.Sasa siku hiyo burudani ndo zilikuwa zimeenza maana watu wote walikuwa wakinishangaaa jinsi nilivyokuwa na uwezo mkubwa wa kutoa burudani.

Naweza kusema niliwachanganya na kuwavuruga maana wengine walinichukulia mimi kama ni mpole sana na huwa nacheza tu kwa sababu tuliambiwa tuoneshe vipaji ndani ya jumba hilo.Kwa hiyo kitendo changu cha kutoa burudani ambayo hawakuiwahi kuiona wala kutegemea kuwa naweza kuifanya ilikuwa ni bonge la surprise kwao. Its enough its enough its enough(inatosha, inatosha, inatosha) hayo yalikuwa ni maneno ya Biggie mara baada ya kuona jukwaa limejaa na kila mtu akitaka kucheza na mimi mabausa walizidiwa na burudani ikabadilika na kuwa fujo.

Watu wote walishuka na nikabaki mimi na Biggie na host wa show hiyo.Nilikabiziwa zawadi yangu na kupewa cheque ya dola 300,000. Kabla sijashuka jukwaani host wa show alisema one more thing please, I have one more big surprise hapo(kitu kimoja tafadhali na pia nina surprise ingine). Hapo alifanya kila mtu awe kimya na kusikiliza ni surprise gani ilikuwa ikifuata mimi mwenyewe nilikuwa kimya kujua ni surprise gani inafuata.

Badala ya kusema nini kinafuata mtangazaji huyo maarufu alikaa kimya kama dakika nzima na kusababisha sintofahamu kwangu na kwa wageni wengine.Alikuwa ni kama mtu aliyetafakari jambo kabla ya kusema ni surprise gani hiyo aliyokuwa nayo.Nilitamnai nimsogelee na kumwambia kuwa si aseme tu hicho kitu watu tutawanyike maana tulishazidisha mda wa kuwepo hapo.Nilivyoona ameeendelea kukaa kimya nilimfuata na kabla sijamfikia alisema nawakaribisha wageni maalumu kutoka Dubai waje watuambie ni surprise gani waliyokuwa nayo.

Kabla ya hao wa Dubai kuna kijana ambaye alikuwa amekaa mbali sana naweza kusema mwisho wa ukumbia alipiga kelele na kuanza kukimbia kuja mbele ya jukwaaa.Kila mtu alishindwa kuelewa ni nini kilikuwa kinaendelea na kijana huyo alikuwa ni nani.Hata mimi ilinibidi niangalie kwa umakini kupitia screen kubwa ambazo zilikuwa zikionesha kila tukio ambalo lilikuwa likiendelea hapo ukumbini.Ilikuwa haina haja sana ya kungalia nyuma bali kila meza kulikuwa na kamera maalumu zilizoonesha kuona kila kitu ambacho kilikuwa kikiendelea.Kijana huyo hakuwa pekee yake bali alikuwa na binti ambaye alikuwa ni mrembo sana.

Nilikaza macho vizuri ili niweze kumtambua kijana huyo alikuwa ni nani.Sura yake haikuwa mbali sana na kumbukumbu za macho yangu. Ni mtu ambaye nilikua namjua kabisa.Kilichonichosha zaidi ni mkononi alikuwa na picha.Sasa sikujua ile picha ilikuwa ni ya nini.Mabausa waliweka ulinzi mkali ili kumzuia asipande jukwaani maana angeweza kuleta majanga.Ilikuwa ni lazima wamzuie kwa sababu hawakujua kuwa nia yake ni nzuri au mbaya.

Wakati wakiendelea kumzuia niliona tena wale wageni iliosemekana kuwa wanatoka Dubai kuwa walizuiliwa kidogo ili kupata ufumbuzi wa hilo ambalo lilikuwa likiendelea.Mabausa walimzuia na nilivyovuta kumbukumbu vizuri niligundua kuwa yule alikuwa ni James kaka yangu ambaye alipoteaga na ambaye alichnganyikiwa kutokana na ugonjwa aliokuwa akiugua ugonjwa wa U-Social.Yule dada aliyekuwa nyumma yake bado sikuweza kumtambua.Nilimuona host naye ameshuka kwenda sehemu ambayo mabausa walikuwa wamewazuia watu hao wasipande kwenye jukwaaaa. Niliona wamesogea pembeni na kuwa wanasahurina.Ilichukua kama dakika tano hivi kabla ya Mtangazaji huyo na mwendesha show hiyo kupanda na kuanza mbwembwe zake….

“Naomba tusikilizane jamani mambo yamekuwa mambo na sasa kama nilivyosema mwanzo kuna surprise ilikuwa ikifuata na sasa sio suprize moja bali ni surprise tano.Nazani hizi zote zitaweka historia mpya kwa wafuatiliaji wa Big brother na pia kwa mshindi wetu Leah.Sasa naomba watu wote mpige kelele kwa surprise namba moja.Watu wote walishangilia isipokuwa mimi maana nilishindwa kuelewa nini kilikuwa kinaendelea.

Surprise namba moja ilikuwa ni kupanda jukwaani kwa yule kijana ambaye alikuwa akizuiliwa kupanda. Aliruhusiwa kupanda na hapo sasa ndo nikamuona vizuri na kumtambua. Nilikuwa kama niliyepigwa butwaa nisiamini nilichokuwa nakiona mbele yangu. Oooooh my God hold me on yalikuwa ni maneno yaliyonitoka kutoka kwenye uvungu wa moyo wangu mara baada ya kumuona James kwa uzuri zaidi na kuamini kuwa yule kweli alikuwa ni kaka yangu.

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)