KITABU CHA SHETANI (5) Jina: KITABU CHA SHETANI Mtunzi: Aziz Hashim SEHEMU YA TANO TULIPOISHIA... Kwa bahati nzuri, alfajiri hiyo hakukuwa na foleni, dakika kadhaa baadaye wakawa tayari wameshawasili kwenye Hospitali ya Mwananyamala , akapokelewa na wahudumu waliokuwa zamu na kumlaza juu ya kitanda chenye magurudumu, IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI 👉INSTALL👈 TUENDELEE... harakaharaka akakimbizwa wodini. “Amepatwa na nini?” aliuliza daktari kwa mshangao baada ya kuona hali isiyokuwa ya kawaida kwenye mwili wa Edmund. “Hata hatuelewi, tumeshtukia akianguka na kupoteza fahamu.” “Mungu wangu! Hebu nipisheni kwanza, tokeni nje,” alisema daktari huku akiinua simu ya mezani iliyokuwa ndani ya wodi hiyo na kupiga namba fulani, wale wapangaji wenzake Edmund na baba mwenye nyumba wakatoka huku nao wakiendelea kuulizana maswali yaliyokosa majibu. Mshtuko aliouonesha daktari ulizidi kuwachanganya, wakawa wanasubiri miujiza tu kwani kwa hali aliyokuwa nayo Edmund, chochote kingeweza ku…